Mkuu habari..Kuna malipo ya beach parking ambayo tumeana kulipishwa kwa upande wa Coco Beach al-maaruf kama Coco ya wahindi. Yaani siku hizi kuna malipo ya beach parking kwa kila weekend tu.
Ningependa kupata msaada wa kujua kama ni kweli au la wadau wanaibiwa. Kama ni sheria imewekwa na manispaa ya Kinondoni au ni mradi wa wajanja flani. Kama ingekuwa ni sheria ya manispaa mbona beach zote za public hazina parking fees? Na hizo fees zinatumikaje kwani hatuoni lolote linalofanywa hapo mahali kama vile ujenzi wa vyoo na sehemu za kutupa taka na huduma zingine za msingi kwa jamii. Hii imekaaje?
Mdau Ostabei


aiiseh......!hapo ni ulaji tu! recsiti haina anwani wala muhuri, ulaji wa nguvu. wahusika wakishtuka.....aaah watu wamesha toka. ahsante mdau kwa kutushtua, mie siwezi kulipa katika staili hiyo, kwangu itakua zogo tu...bora nisiende...wizi mtupu mbele ya "waziri mkuu"
ReplyDeletemimi naona kitu hiki ni uongo wa kutupwa... maana hizo risti ni feki feki feki.. hata mimi naweza nikatengeneza.. pili mabango ya kuuza mihogo ndio iliyo tumiwa kuweka matangazo... je hii ni ukweli???
ReplyDeleteMradi wa wajanja huwo.Walio kwenye nafasi wataendelea kula na wanyonge wataendelea kuwa maskini.Taasisi na wizara,halmashauri za serikali zimejaa mafisadi kwhiyo hamna fisadi hatakaemshughulikia fisadi mwenzake.Sijuhi tumelaaniwa!!!!!!!!?
ReplyDeleteKiuhasibu na kiutaratibu hii is just a piece of paper, sio document halali ya kuthibitisha malipo. Haina anuani ya mpokeaji, haina 'title' kwamba ni 'receipt' au stakabadhi ya malipo, haina muhuri au logo ya mpokeaji, ina mapungufu mengi kwa kweli. Kuna uwezekano mkubwa kwamba huu ni wizi tu kama ulivyosema mradi wa mjanja fulani fisadi. Kuna wakati hapo mimi niliwahi kukamatwa na 'polisi'ambaye baadae nilihisi kwamba alikuwa feki kwa kosa la ku-park pasiporuhusiwa wakati hakuna kibao cha 'no parking'. Kuna uhuni mwingi tu unafanyika maeneo hayo wajanja wanajichukulia pesa. Naamini wanakula na wakubwa ndio maana hatua hazichukuliwi. Kama ni kweli 'serikali ya mtaa wa Oysterbay' inatoza hizo pesa then shame on them kwa kutokuwa na standard office documents za kutozitumia fedha hizo kwa ajili ya kuendeleza hizo beach na kuweka huduma muhimu kwa watumiaji.
ReplyDeletemradi wa mtu huo.oh shauri yenu.
ReplyDeleteOhhhh wiziiiiii mtupuuuuuuuuu!!!
ReplyDeleteanother fiasco, another UFISADI,
Miradi ya wakubwa, miradi ya uchaguzi bana wewe pana juwa, some more miradi coming.
Mtoto wa Mkulima..
Hao wanahitaji kukamatwa, viboko na kupewa adhabu ya kulima eka 30 kila mmoja kwa jembe la mkono ili dhana ya kilimo kwanza ifanikiwe.
ReplyDeleteLukuviiiiii ....
ReplyDeleteona hii sasa
mimi sisemi mengi leo
Jamani kuna kibao nitakipiga picha leo jioni alafu nimtumie ankal akiweke hewani
ReplyDeletebalaa hili .......
sioni taabu kulipa parking ili mradi kuwe pasafi, kuna mmasai anayelinda gari wakati napunga upepo.
ReplyDeletekama hivyo havitendeki basi ni haki kufoward malalamiko kwa mkuu wa wilaya kwenda mbele
wewe uliye-post hii risiti una akili kweli???
ReplyDeleteKwa nini unataka kutuharibia biashara yetu?
Unajua hii nchi ni ya akina nani?
Kwa taarifa yenu, sisi ndio wenye nchi, ndio tunaokula nchi.
Tahadhari kwenu msio na hata feni nyumbani kwenu halafu mnajifanya kuja kupunga upepo huko bichi! Kaeni mkao wa kuliwa zaidi.
Kwa taarifa yenu bichi zote mtakuwa mnazisikia kwetu sisi watoto wa kidosi tu. Ngoja uchaguzi mkuu upite tuanzishe kiingilio cha shilingi mia tano kwa kiila kichwa kinachokwenda bichi.
Wikiendi (jumamosi na jumapili) shs 500/=
siku za kawaida shs 300/=
sikukuu shs 1000/=
Kwanza kuna taarifa nimepata kuwa kuna masikini bado wanaishi karibu na bichi. kufikia mwaka 2020 tutahakikisha hakuna masikini anayeishi ndani ya kilomita 10 kutoka bichi.
hakuna masikini atakayeenda bichi bila kulipia.
mtu huna uhakika wa kula halafu unakuja bichi???
kwanza inakuwaje mnakuja bichi??? watu hamjui aa wala bee mnakuja bichi???
halafu mnajifanya kulalamikia vitu vidogo vidogo kama malipo ya parking bichi??
mbona mnalipa kodi nyingi namna hiyo na barabara nimbovu, hsipitalini mnalipa na bado huduma ni mbovu, mbona umeme unakatika katika na mvua zinanyesha hadi mafuriko na bili za umeme mnalipa halafu hamlalamiki???
hivi mpaka mlipishwe kitu direct ndo mlalamike???
Mnajua kodi mnazolipa???
amakweli yaliyomo yamo!
yaliyomo yamo!
Pia kuna wajanja wnakusanya 5000 au 10,000 tena kwa makelele, matusi na vitisho. Wanasema ni fedha za kukusanya takataka Bonde la Mpunga.
ReplyDeleteUkweli hakuna usafi, au ukusanyaji taka unaofanywa. Sasa, baada ya siku ya kulipwa hizo 10,000 huchukua takataka na kuzirundika kwa mfano Namanga kwenye open space ambayo wajanja (fulani) wanataka kuibifsisha. Hapo sasa ni dampo. dampo lingine limefunguliwa Maandazi Road yote, la tatu lipo dimbwini kwa Mzee Mzima. Pia kuna lingine lipo mbele ya Simona.
Kuna serikali ya Mtaa ya wajanja - Msasani na Oysterbay. Wengine wamejipya vyeo vya Reverend lakini wanajulikana kuwa sio waadilifu ila ni mafisadi tu.
Mushi aiseee mangi lakini miradi ya wapi hii arawa? toka umekuja obey imekuwa shida tu kila kitu wafanya mradi ati. tukurudishe buguruni kule ulikokuwa?
ReplyDeleteJK alishasema kukaa bichi ni bu bure kweli we unachaji na vijana wenye filimbi. nawenyewe wanakula upepo.
acha wisi aisee fanya kasi kwabidii ati ili uondoke nakupita pale wami kwa he shi, heshima kweli.
jamani ivi kuna mtaa wa oysterbay? coco beach iko Toure Drive...mtaa wa oysterbay uko wapi?
ReplyDelete