Rais Wa Namibia Hifikepunye Pohamba akimkabidhi Nishani ya Juu ya Ushujaa ya Taifa la Namibia, Mama Maria Nyerere kwa niaba ya Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kutambua juhudi za Mwalimu katika ukombozi wa bara la Afrika ikiwemo Namibia katika hafla maalumu iliyofayika katika mji mkuu wa nchi hiyo Windhoek jana jioni.Katika hafla hiyo viongozi Mbalimbali wa Afrika waliokuwa mstari wa mbele katika harakati za ukombozi kusini mwa Afrika nao walitunukiwa nishani hiyo akiwemo Rais wa Zamani wa Zambia Keneth Kaunda ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, Marehemu Agostino Neto wa Angola, Marehemu Oliver Tambo wa Afrika ya Kusini, Rais Denis Sassou Nguesso wa Kongo Brazaville, pamoja na watu wengine mashuhuri waliokuwa msari mbele katika ukombozi wa bara la Afrika.Pembeni ya Mama Maria kushoto ni Mtoto wa Mwalimu,Bwana Makongoro Nyerere ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mara.
Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia akimtunuku Nishani ya Juu ya Ushujaa ya Taifa la Namibia Rais Mstaafu wa Zambia Kenneth Kaunda kwa kutambua mchango wake katika ukombozi wa nchi za kusini Mwa Afrika ikiwemo taifa la Namibia. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais wa Namibia Hifikepunye Pohamba katika hafla maalumu kuadhimisha miaka 20 ya Uhuru wa Namibia na pia kushinda uchaguzi mkuu ambapo ataendelea kuiongoza Namibia kwa muhula wa pili.Sherehe hizo zilifanyika katika mji mkuu wa Namibia Windhoek.
Juu na chini ni baadhi ya Watanzania waishio Namibia wakimlaki kwa furaha Rais Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili mji mkuu wa nchi hiyo Windhoek kuhudhuria sherehe za miaka 20 ya Uhuru wa nchi hiyo ambapo pia Rais wa nchi hiyo Hifikepunye Pohamba ataapishwa kuendelea kuingoza nchi hiyo katika muhula wa pili kama Rais. Picha na Freddy Maro






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Kila leo mnaenda sehemu tofauti ila kuja kwetu hatuwaoni, ndio nini hivyo? wakati sie ndio tungetakiwa kupewa kipaumbele manake ndio tutakaokuwa maraisi wa baadae, njooni na huku tunawaona tu kwenye picha ila hamji.
    Mdau north america

    ReplyDelete
  2. Tupo tuliosema mambo ya kuleta uchamachama ughaibuni yanaweza kuleta aibu mkatuona wapuuzi nk.
    Angalia picha hiyo ya kanga ya kampeni huko Namibia. Kama kuna Mtanzania mwenye kuamini sera za chama cha upinzani hapo kuna mawili: ama awaache CCM na Rais wa CCM au aibuke na yeye na kanga yake nyekundu inayosema 'Chagua Kalumanzira'.
    TANZANIA KWANZA!!!

    ReplyDelete
  3. Mbona kampeni za uchaguzi hazijaaanza rasmi, lakini kuna haya makundi ya ccM yanaanza kizazaa?? Au ndio tuseme ccM inakwenda kinyume na sheria za nji?

    ReplyDelete
  4. Wengine hawajui kutofautisha Utaifa na mambo ya Chama, sasa hilo likanga la nini hapo!

    ReplyDelete
  5. Nimeamini waTZ wa USA ni kiboko. Mambo ya dizaini hii hayafanyiki jamaa akijaga USA. Ha ha ha!!!!

    ReplyDelete
  6. Watanzania wanaoishi Marekani bwana wanajua kuandaa hoja. Watanzania wanaokaa nchi nyingine (UK, pamoja na nchi nyingine za Afrika - India Ikiwemo) wamekaa kiuoga-uoga. Ndio maana wanapewaga ruksa za kumwaga ma-kanga na mabendera. Watu wa US wanajiandaa na hoja na kuomba wakutane na Rais akija huku lakini sijui kuna tatizo gani kwenye jambo hilo. Mhhhh..........

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...