bwana michuzi na wadau wengine,
kwanza napenda kuchukuwa fursa hii kuwashukuru kwa kuwapatia watanzania taarifa mbali mbali za kila siku.
pili napenda kutoa ufafanuzi kuhusu tangazo la kazi nchini saudi arabia ambalo lilitoka katika blog ya hii ya jamii. mimi ni mtanzania na ni dereva huku saudi arabia na ninayoeleza hapa ni kuwa naendelea kuyapata ikiwa ni pamoja na mateso, manyanyaso na uonevu uliopindukia mipaka katika ubinaadamu.
kwa ujumla hapo dar kuna magenge mawili yanayofanya biashara ya kuandikisha watu kazi na kuwasafirisha kuwaleta huku saudi rabia. mimi ni mmoja wa walioumizwa na genge moja wapo. wanachukuwa fedha kwa waarabu huku saudia na kuwaahidi kuwa watawapatia madereva. kisha wanatangaza nafasi kama hizo huko nyumbani na wanadai kuwa kila anaetaka kazi alipe nauli, viza, ukaguzi wa afya na gharama nyenginezo. jumla huwa baina ya shs laki 8 hadi milioni moja.
aidha wanadanganya watu kuwa mishahara ni riyal 3000. naomba ndugu zangu nikuelezeni ukweli kuwa hakuna dereva anaelipwa riyal 3000. hata sisi tulidanganywa hivyivyo. huku mishahara ya maredeva ni riyal 500 hadi 800. ukibahatika basi ni 900 ijapokuwa kisheria ni riyls 1300 hadi 1500. lakini hakuna mwarabu anayelipa pesa hizo.
baadhi ya uongo wanaodai hao matapeli ni kusema kuwa riyal ni sawa na dola ya marekani wakati wanajua ni uongo. pia hudai kuwa riyal ni shs 350 (angalia tangazo lako) wakati ni shs 300 tu za tanzania. mbali na udanganyifu huo, hawatoi mikataba kwa madereva au kama wanatoa ni feki na wanapofika huku huambiwa mikataba ile si sahihi na kupewa mikataba mipya. pia tunasainishwa mikataba iliyoandikwa kwa kiarabu wakati sisi hatujui kiarabu.
mimi mwenyewe na wenzangtu tulianza kuzusha vurugu tukitaka kurudi nyumbni na baada ya kudai hivyo, waraabu wakatuletea polisi na kupigwa. isitoshe tukaambiwa kama mtu anataka kurudi basi alipie gharama yote iliyotumika kumleta saudia na ajigharamie nauli ya kurudi huko. kwa ujumla tumeshindwa na tunaendelea na kazi mkataba ukiisha tunarudi bongo.
pia ni uongo kusema kuwa madereva wanapewa nyumba. tunaishi katika magari. gari lako ndio nyumba yako na mabegi ya nguo humo humo. kampuni za huku zina madereva 300 hadi 500. jee wataweza kumpatia kila mtu nyumba?
kwanza napenda kuchukuwa fursa hii kuwashukuru kwa kuwapatia watanzania taarifa mbali mbali za kila siku.
pili napenda kutoa ufafanuzi kuhusu tangazo la kazi nchini saudi arabia ambalo lilitoka katika blog ya hii ya jamii. mimi ni mtanzania na ni dereva huku saudi arabia na ninayoeleza hapa ni kuwa naendelea kuyapata ikiwa ni pamoja na mateso, manyanyaso na uonevu uliopindukia mipaka katika ubinaadamu.
kwa ujumla hapo dar kuna magenge mawili yanayofanya biashara ya kuandikisha watu kazi na kuwasafirisha kuwaleta huku saudi rabia. mimi ni mmoja wa walioumizwa na genge moja wapo. wanachukuwa fedha kwa waarabu huku saudia na kuwaahidi kuwa watawapatia madereva. kisha wanatangaza nafasi kama hizo huko nyumbani na wanadai kuwa kila anaetaka kazi alipe nauli, viza, ukaguzi wa afya na gharama nyenginezo. jumla huwa baina ya shs laki 8 hadi milioni moja.
aidha wanadanganya watu kuwa mishahara ni riyal 3000. naomba ndugu zangu nikuelezeni ukweli kuwa hakuna dereva anaelipwa riyal 3000. hata sisi tulidanganywa hivyivyo. huku mishahara ya maredeva ni riyal 500 hadi 800. ukibahatika basi ni 900 ijapokuwa kisheria ni riyls 1300 hadi 1500. lakini hakuna mwarabu anayelipa pesa hizo.
baadhi ya uongo wanaodai hao matapeli ni kusema kuwa riyal ni sawa na dola ya marekani wakati wanajua ni uongo. pia hudai kuwa riyal ni shs 350 (angalia tangazo lako) wakati ni shs 300 tu za tanzania. mbali na udanganyifu huo, hawatoi mikataba kwa madereva au kama wanatoa ni feki na wanapofika huku huambiwa mikataba ile si sahihi na kupewa mikataba mipya. pia tunasainishwa mikataba iliyoandikwa kwa kiarabu wakati sisi hatujui kiarabu.
mimi mwenyewe na wenzangtu tulianza kuzusha vurugu tukitaka kurudi nyumbni na baada ya kudai hivyo, waraabu wakatuletea polisi na kupigwa. isitoshe tukaambiwa kama mtu anataka kurudi basi alipie gharama yote iliyotumika kumleta saudia na ajigharamie nauli ya kurudi huko. kwa ujumla tumeshindwa na tunaendelea na kazi mkataba ukiisha tunarudi bongo.
pia ni uongo kusema kuwa madereva wanapewa nyumba. tunaishi katika magari. gari lako ndio nyumba yako na mabegi ya nguo humo humo. kampuni za huku zina madereva 300 hadi 500. jee wataweza kumpatia kila mtu nyumba?
watu waache kudanganya watanzania. tupo hapa na wapakistan, wahindi, wabengali, waphilipino, wasudan, wanigeria, wakenya na waethiopia. tunaishi maisha magumu sana. sahani ya chaklula ni riyals 45. sasa niambie riyal 800 utaishi vipi? hiyo mishahara huyo jamaa anayodai ni ya wahasibu, madaktari au wahandisi sio madereva.
pia mjue kuwa msaudi katika nchi yake hana kosa. hata ukienda katika vyombo vya sheria huwezi kumshinda. jamaa wana jeuri, kiburi sijapata kuona. tena anakwambia nenda kokote na mwisho utarudi hapa. pia ukufika uwanja wa ndege tu wanakunyanganya pasipoti na huioni tena hadi isku ya kuondoka baada ya kumaliza mkataba. hivyo unakuwa mtumwa huwezi kukimbia wala kufanya lolote.
naomba serikali ituhurumie sisi na hao wanaodanganywa huko tz. ipige marufuku biashara hii ya utumwa maana sisi tunateseka mno. wengine tumeuza viwanja, mafrji, na mali nyenginezo tuje huku lkn maisha sivyo tulivyotarajia. inasikitisha sana.
ubalozi wanajua hali hii, na tukienda kulalamika wanachukua juhudi za kuwasilina na serikali ya saudia lkn waarabu wanateteana. hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na serikali kwa raia wao. tunashukuru juhudi za ubalozi lkn hazizai matunda kwa kuwa saudia serikali inawatetea matajiri wanaonyanyasa sisi wageni..
naomba kama haya ni uongo hao wanaodanganywa wapige simu ubalozini kuulizia wasikie watakayoambiwa.
pia mjue kuwa msaudi katika nchi yake hana kosa. hata ukienda katika vyombo vya sheria huwezi kumshinda. jamaa wana jeuri, kiburi sijapata kuona. tena anakwambia nenda kokote na mwisho utarudi hapa. pia ukufika uwanja wa ndege tu wanakunyanganya pasipoti na huioni tena hadi isku ya kuondoka baada ya kumaliza mkataba. hivyo unakuwa mtumwa huwezi kukimbia wala kufanya lolote.
naomba serikali ituhurumie sisi na hao wanaodanganywa huko tz. ipige marufuku biashara hii ya utumwa maana sisi tunateseka mno. wengine tumeuza viwanja, mafrji, na mali nyenginezo tuje huku lkn maisha sivyo tulivyotarajia. inasikitisha sana.
ubalozi wanajua hali hii, na tukienda kulalamika wanachukua juhudi za kuwasilina na serikali ya saudia lkn waarabu wanateteana. hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na serikali kwa raia wao. tunashukuru juhudi za ubalozi lkn hazizai matunda kwa kuwa saudia serikali inawatetea matajiri wanaonyanyasa sisi wageni..
naomba kama haya ni uongo hao wanaodanganywa wapige simu ubalozini kuulizia wasikie watakayoambiwa.
hapa wapo watz wapo jela mwaka mzima sasa wmeshamaliza vifungo na jamaa hawataki kuwatoa. pia wapo wameletwa siku za karibuni nao sasa wanaanza kualamika. kazi masaa 24 ukipata ajali na gari unakatwa mshahara eti kurepair gari wakati gari zote zina bima. wanatuonea sana hawa waarabu. hatuna jumamosi wala jumapili wala sikukuu.
wapo wenzetu waliopata ajali na kuumia basi hawalipwi mishahra eti hawafanyi kazi wakati ajali mtu hakujitakia. naomba serikali iwakamate hawa jamaa wanaotapeli watu huko bongo na kuwasababishia watz mateso huku uarabuni.
ni mimi mwathirika na kazi ya udereva.
wapo wenzetu waliopata ajali na kuumia basi hawalipwi mishahra eti hawafanyi kazi wakati ajali mtu hakujitakia. naomba serikali iwakamate hawa jamaa wanaotapeli watu huko bongo na kuwasababishia watz mateso huku uarabuni.
ni mimi mwathirika na kazi ya udereva.
Ndugu zangu watanzania ,najua wengi tunamaisha magumu hapa Tanzania lakini ukweli huko nje hali ni mbaya zaidi kama unakwenda bila kujua unakwenda wapi na kufanya nini!!!
ReplyDeleteTanzania tamu jamani....ugali na Kisamvu unakula na maji ya DAwasco siku zinaenda.
sasa si urudi unang'ang'ania nini?!
ReplyDeleteHi All,
ReplyDeleteI have been out of my country, Tanzania for almost four years now. I never been Saudia, but I really agree with this guy.I can strongly feel the sympathy of the whole saga, it is really painful and hurtful.We are facing the racistic situation in here as well, but that is too much...!!.All in all, we will always get proud of our pretty country, pretty kind people of our very own tanzanians.My brother, never give up, born to suffer, keep strungllling, we are all behind you.
Good luck.
Senior Mdau.
USA.
Anonym 11:55, Mdau hawezi kurudi. Passport iko mikononi mwa muarabu hadi siku mkataba aliolaghaiwa akausain utakapokuwa umekwisha... waarabu ni walewale waliokuwa wananunua watumwa na kuwauza jamani msisahau history ndugu zangu....Ni heri kufa masikini katika uhuru kuliko kuteseka utumwani katika utajiri....
ReplyDeleteTusisahau historia ni waarabu na Wazungu waliwauza mababu zetu na mabibi zetu utumwani.Baadaye wakatuletea Uislamu na Ukristo.
ReplyDeleteI've heard before that when you see a racist Arab, he's the worst of all the racists. This suppose to be a muslim country for God's sake. I say it's not about those long beards and Kanzus and Kufis...it's what's inside our hearts that means the most. Hold up muslims, I am muslim too...and Im talking about those we're talking about here, those who treat our brothers and sisters inhumanely....and guess what, I bet most of those workers are muslim brothers too.
ReplyDeleteDo they fear Allah?. Shame on them. Thanks for all the information.
As salaam alaikum.
Bado nashindwa kuelewa kwanini ubalozi wa Tanzania nchini Saudia unashindwa kuwasaidia watanzania hawa wanaodai kuonewa. Kama pasipoti imechukuliwa, hii jukumu la serikali(ubalozi wa tanzania) kuwapatia raia wake pasipoti na kuwalipia nauli ya kurudi nyumbani kama ni kweli wanataka kurudi nyumbani. Na kama hili haliwezekani basi hakuna sababu ya kuendelea kuwa na mahusiano ya kibalozi na saudia.
ReplyDeleteTATIZO NI HALI NGUMU YA MAISHA NYUMBANI,HIVYO MTU UNAONA BORA UTOKE ILI KUPATA UNAFUU WA MAISHA NA KUSAIDIA FAMILIA YAKO,KUTOKANA NA HALI NGUMU WATU IMANI IMEKWISHA NDIO MAANA WANAPANDISHA MIKENGE WENZAO BILA YA HURUMA.WAARABU HANA REKODI NZURI KUHUSU HAKI ZA KIBINADAMU.SISI TUNAOKULA BOX HUKU KWA WAKRISTO ALIHAMBULILAHI,
ReplyDeleteKama kuna anayejiuliza ilikuwwaje kuna Watanzania waliowauza wenzao utumwani enzi za utumwa, hili ndiyo jibu lake. Kaka huyu alivyoeleza ni kama mtumwa mambo leo. Kinachonishangaza ni kuwa imekuwaje serikali hayafuatilii magenge hayo, au inahitajika foreign currency hapo?( kebehi)
ReplyDeletemtoa maada umeonyesha moyo wa kizalendo sana kupenda ndugu zako sio wengine wakiumia wao hawawastui wenzao asante kwa angalizo sasa maadam tumejua atakayeenda kajitakia mateso wewe kazi ya kututahadhalisha ushaifanya
ReplyDeletena wazungu nao si walikuwa wananunua watumwa na kisha kuwauza? vp wao wamebadilika?
ReplyDeletembona hamuwashikilii bango ndo kwanza mnawafata nyuma kwa kila kitu kama mikia?
acheni u-racist wenu hapa sababu katajwa mwarabu mnachoonga au sababu midomo mali yenu?!
kila nchi wana sheria zao na duniani kote kuna watu wana tabia tofauti bila kujali rangi wala itikadi zao, kuna watanzania haoo UK wanakesi kuwatesa watz wenzao waliowachukua kama mahouse gal unawazungumziaje wao?!
au ndo mambo ya chongo kuita kengeza?!
Ankala,wakati blog ya Jamii inavuta time kushehereka mdau wa 8million.Ebu fanya matendo ya huruma ya kuwasaidia hawa wa-TZ wenzetu wanaoteseka umangani.Angalau kuipost kilio cha huju jamaa kwenye media za Bongo..wengine washtuke.
ReplyDeleteUliosema ni kweli kabisa nchi za watu na nakuonea huruma sana .
ReplyDeleteKuna mambo matatu hapa:
Moja, hii kazi haikuwa yako, kwani wewe ulistahili kubaki TZ. Ulikuwwa na kila kitu unachokitaka hapa TZ. Hii kazi ilifaa MTZ aliyetoka Rukwa au Kigoma mwisho wa reli ambaye hata Dar hajafika na ana ujuzi wa udereva magari. Hiyo shida unayoona wewe yeye haitamuumiza.
Pili, nakushauri kumalizia huo mkataba na kuelewa kwamba wenzetu huko nje wanaendelea kutokana na nguvu kazi ya watu wa nchi zingine.Wewe kama unaona shida wahindi, wabangladeshi , wapakistani wapo na kwa mshahara huo watafanya kazi. Tofauti na TZ watu wanaokuja kutoka nje ndio wanaendelea kwa nguvu ya wazawa.
Ukirudi hapa TZ utakuwa umejifunza mambo mengi sana kwamba kuchukua risk sio mara zote zinakuwa na faida. Kusota kwako Saudia tunakuhitaji hapa TZ ukirudi kwani watu wamekaa kugonga debe na kulalamika. Ukirudi anzisha kampuni ya kupelekwa watu huko lakini wawe tu wenye shida na pato lao kwa siku hapa TZ nichini ya riyali 50 kwa mwezi. wakienda Saudia kwao riyali 500 nyingi.
Tatu, waTZ tumezidi kila sehemu tukienda kulalamika tu, utasikia shida na manyanyaso ohh huko Russia, Ukraine,Germany mara ohh..huko UK, au US. kama kwetu TZ kungekuwa kuzuri na uchumi mzuri tusingeenda huko nje bali shida ndo zimetutoa na tuvumilie. Sisi wenyewe hapa TZ tulikuta haya majumba dar na barabara na maendeleo hayaji hivi hivi bila mmoja kuumia.
I LOVE MY COUNTRY TANZANIA!!
ReplyDeletejamani mjue tanzania tuna ukarimu wa ajabu!! hatujui kunyanyasana!!
naishi hapa USA ATLANTA, YAANI huwa napata sifa mbali mbali ila za huyu zinanisikitisha sana!! poleni sana wandugu, God bless yall!!
yaani africa yote TANZANIA NDO NCHI AMBAYO HAWAJUI KUNYANYASA WATU YAANI WAHINDI WAJE TUNAWAPENDA TU, WAZUNGU NA WECHINA ila sisi tukienda kwao ni vingine yaani napata hasira ila poa tu ngoja nimalize shule wiki ijayo narudi HOME kulisaidia NCHI YANGU!
COZI YANGU NINAYOISOMEA NAJUA ITAIVUSHA TANZANIA TO ANOTHER LEVEL!! promise to my pple. love yall!!
Tunaomba wizara ya mambo ya nje Tanzania kupitia ubalozi wake Saudia kutupatia ushauri hapa hapa ktk globu ya jamii kuhusu malalamiko ya raia wa Kitanzania na pia kutoa ushauri nasaha kwa wale wasioamini dhahama wazipatazo watanzania aliosainishwa mikataba ya kazi Saudia.
ReplyDeleteMdau
Mtarajiwa kuwa dereva Saudia.
kwa kweli inasikitisha sana. watu waache kuwadanganya wenzao. poleni mliopatwa na matatizo hayo.
ReplyDeletetatizo watanzania wabishi sana, ukiwaambia kitu, wanakuuliza mbona wewe bado upo huko?na mimi lazima nije, ndugu zangu,ukishaingia umeingia kutoka ngumu.
ReplyDeletena watanzana tulio nje tuache kudanganyana wenzetu kwamba maisa nje mazuri sana ili kuficha aibu zako,kama unalala na njaa waeleze tu ukweli jamaa zako.
Watu wengi ambao wametoka Tanzania yaani wapo nchi nyingine wanaweza kusema mabo haya. Mimi nipo Marekani, raia wa kigeni wanatretiwa kama mavi vile yaani tunanyanyaswa sana si utani, ila hela yao nzuri.Watanzania nyumbani tutawatreat raia wa kigeni vizuri sana kuliko raia wa nyumbani,Mimi nikilrudimtu aniambii chochote kwenye nchi yangu. Brother hang in there maisha ni kuangaika na kujifunza na makosa yetu
ReplyDeleteAnony march 7,11:55,rudi usome mada nzima.inaonekana hujamaliza kusoma alichoandika. jamaa atarudije katika situation hiyo na ndio maana anomba msaada unaowezekana.anaonyesha ni jinsi gani anawish angerudi nyumbani.
ReplyDeleteAnony march 8,02:33,na wewe unaonekana unashiriki na biashara hiyo nini? mbona huna hata huruma.hujaguswa kabisa.wapi na wapi hayo unayosema ,jamaa anaonyesha matatizo ya huko watu tujifunze.
nakupa pole sana ndugu yetu na wengine wote mnaoteseka huko.i hope you will get this situation sorted out soon.
mwisho kabisa naomba bwana michuzi hii uipost kwa vyombo vingine vya habari watu wote waione.na vyombo husika viliangalie swala hili.
nakuunga mkono anony march 8,04:05,
ReplyDeleteni bora tuwe wa wazi na wenzetu tukiwaambia mfanyie kazi,fatilia kwa watu tofauti kama ni kweli.kama alivyosema anony fulani hapo juu usijiendee nje huna mwelekeo wowote,i mean either unaenda shule make sure unasponsor au you have enough income to support yourself wakati ukiwa shule.sio kila mtu hataki kurudi bali wengine ni ile watarudije.at the same time watu wengi tu wapo very succesful huku nje.tazama maisha yako if you are fine at home stay there.nje sio kuzuri kwa kila mtu na sio kubaya kwa kila mtu.
Pole sana mtanzania mwenzetu, pia nakupongeza kwa kuwa muwazi kueleza ukweli ili atayesoma achukue taadhari mapema.
ReplyDeleteKama mmeripoti kwenye ubalozi na hawachukui hatua yoyote basi huyo balozi hatufai kuwa huko sababu naye anahusika kwa mateso yenu. Ni kazi yake kuwasaidia raia wa nchi yake kwenye matatizo kama hayo.
Kwa nini wachukue passiport si mali yao.
Waarabu bado wanamuona mtu mweusi ni mtumwa tu, achaneni nao hao.
Halafu uarabuni wameshaanza mchezo wa kuwatanualia wamarekani. Kila siku wakionyesha nchi yao wanaonyesha sehemu nzuri tu ili kuwavutia wazungu waende huko. Na wanasema 75% ya watu wanaoishi hapo mjini sio wazawa wa hapo. Na nyumba ati huko ni $65,000 kwa mwaka rent. Halafu wamekuja kwa kasi kuwachukua walimu wa shule za chekechea na za msingi ili wakawafundishe watoto wao. Niliona kwenye Tv wanasema walimu wanachukua kutoka USA, Canada, UK na Australia only. Housegirls na drivers ati wanatoka Philipines, India na Africa. Sikujua ni kweli hayo.... Too sad na poleni sana huko
ReplyDeleteIla kila nchi ina ugumu wake na kuna nchi nyingine ugumu unapungua once unapochimbia mizizi yako vizuri chini.....Ni ngumu sana mwanzoni. Kuna wakati nilitaka kuondoka kabla sijamaliza masomo nirudi home. Baada ya kumaliza shule na kuweka vitu vyangu sawa nashukuru Mungu sana na wala siregret for my decision. Kuna nchi nyigine ukishaweka mizizi ni 100% better na kuna zingine hazikaliki no matter what.
Ushauri wangu ni kuwa kama bongo una maisha mazuri don't even bother to get out of there kufanya kazi nje ya nchi....Utakuwa kichaa kama ulizoea kushika briefcase, housegirl na dereva....Huku ni kwa wale ambao hawana maisha bongo...watoto wa baba hawakawii kurudi bongo....watoto waliozoea kutandikiwa vitanda na kuamshwa breakfast ikiwa ready hawakuwezi huku
Lakini kama unakuja kwanza kusoma ni nzuri kwa vile utayajua maisha kabla hujaamua kuishi huku....na kama ni kuja kusoma uwe na miaka chini ya 25, kama ni zaidi ya hapo think twice.
Huku siku hizi hamna kazi hata kwa wenyeji kwa hiyo ukiuza vitu vyako bongo utakuja juta....Na ilikua nursing profession imeboom juzi juzi tu guess what kwavile iliboom wakati uchumi unashuka basi kila mwenyeji keshakimbilia huko na kila mtu kesha kuwa nurse sasa hivi na mahospital kila kukicha yanafungwa kwa hiyo hawawataki tena. Watu wamemaliza nursing hapa mwezi wa kumi na mbili na macho yanawatoka wanarudi kwenye kupangusa vibibi tena na AA zao. Na ilikua wanawatafutia watu paper sasa hivi wanaanza kuchomoa.
Njoo huku bado wewe kijana na njooo kwa ajili ya kusoma kwanza ukimaliza shule ukiamua kukaa huku its okay ukiamua kurudi home its okay too.
Ila ubalozi wa huko kwa nini usiwabail hao watu na hizo contract zao. Si wawalipe hata kidogo hao waajiri ili hao watu wavunje mikataba warudi home.....Ila jikazeni tu kama kuna usalama pambana na maisha tu always kumbukeni there is a ligh at the end of the tunnel
Mdau anasesema Tanzania hamna kunyanyasana, hajasimamishwa na askari wala kwenda mahakamani. Unyanyasaji upo kila kona ya dunia, tusijijanganye hapa na kujipa sifa. Labda umesahau wale wanajeshi wanaopiga wananchi kila siku bila ya kuadhibiwa au labda Azimio la Arusha? Fungua macho. Sisi wengine, tumepoteza mali katika hilo Azimio na ujamaa wa Nyerere, hatutasahau daima unyanyasaji wake hata kama tunaishi Nje na hatutakuya tena Tanzania.
ReplyDeleteMsipende vya rahisi ndugu zangu! Mbona waphilipino,wahindi,wapakistan,wazungu wanaigeria,wakenya nk wapo hapa wanapiga mzigo wala hakuna kelele kama hizo? Tatizo mmezoea vya mkatomkato tu. Dunia ya sasa ni mapambano; pambaneni na muache maneno ya siasa siasa huku si TZ
ReplyDeleteTANGAZO LA KAZI: Mdereva wanahitajika Saudia, uwe leseni C. Macho mazuri yanayoona, Passport na uwe na uvumilivu wa safari. Mshahara ni mzuri na nyumba pia utapewa. Fika ofisini kujaza fomu na ada ni laki tatu...
ReplyDeleteTAPELI
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote. Nchi Nzuri Tanzania ..........
ReplyDeletePole sana kaka. nakutakia siku njema na umalize huo mkataba urudi nyumbani TZ. Hii sio miaka ya utumwa hata kama Tanzania hali ngumu lakini sio unyanyaswe. Nimebahatika kuwa sehemu nzuri huku ughaibuni kwa ajili ya elimu yangu ila sina njia ya kusaidia watanzania wenzangu at the moment lakini I am working towards helping creat more jobs in Tanzania hopefully I will bring a positive change.
ReplyDeleteNASEMAGA SIKU ZOTE KATIKA WATU WALIOKOSA USTAARABU DUNIANI, WAARABU NI WA KWANZA! HAWANA UTAMADUNI WA UBINADAMU. SI NDIO HAOHAO WANAWASUMBUA MÖVENPICK HOTEL? KAA MBALI NA MUARABU
ReplyDeleteMambo vipi? dogo nakukumbuka sana , tulikufanyia mpango wa kwenda SAUDIA mwaka jana, office zetu ziko pale NKURUMAH karibu na intercontinental hotel, wewe bwana ulikuwa umezoea ugali wa kukata na kisu mezani, acha kulalamika jikaze dogo, maisha ya ugaibuni sio lelemama. LAKINI PAMOJA NA HAYO MWARABU SIO BINADAMU na atakae bisha ni mwarabu. ASANTE.
ReplyDeleteHEHEHE KAAZI KWELI KWELI ILIYOBAKI TULIZENI BOLI NYUMBANI JAMANI SIO LAZIMA WATU WOTE KUSAFIRI
ReplyDeleteMAISHA MAGUMU KILA SEHEMU KUMBUKA KUWA HUKO UNAPOTAKA KUKIMBILIA KUNA WATU AMBAO HAWANA KAZI VILE VILE NA KAZI WANAZITAKA
TUPAMBANE HUKOHUKO NYUMBANI MPAKA KIELEWEKE
MBONA ANKAL BADO ANAKAZA BUTI HUKO HUKO NYUMBANI???????? SABABU ANAJUWA KUWA SAFARI ZA NCHI ZA WATU NI UTUMWA MAMBO LEO
IWE MWARABU IWE MZUNGU IWE MWAFRIKA MANYANYASO KILA KONA YA DUNIA YAPO HAO WARABU MNALALAMIKA JE NASISI TUKIANZA KULALAMIKA TUNAVYOTESEKA HUKU KUBEBA MABOKS
FANYA KAZI UKIONA HUWEZI JIKATE ZAKO KWENU HAMNA MTU AMEKUITA KWENYE NCHI YAKE BILA MAKUBALIANO
ndugu watanzania maoni yenu yote hajaangalia utumwa uko wapi. mimi niko hapa oman na haki ya kila mtu inapatikana ikiwa mwananchi au mgeni wote sawa. tena mgeni unasikilizwa zaidi. ama kuhusu utumwa ni viongozi wetu kutojali haki za raiya wake. kisheria ubalozi ni kusimamia haki za wananchi wake. utumwa uko tanzania na siyo mwarabu hiyo ni fikra potovu. maana tanzania ni nchi tajiri ila kutokana na baadhi ya wajanja wachache wanawanyonya wananchi na kuiba mabilion ya pesa sasa huu siyo utumwa haya mtanzania anaua kwa kuiba kuku wakati pengine hajala wiki anapigwa mawe na kuchomwa moto huu sio utumwa. ina maana utumwa unaofanywa na mtanzania mweusi kwa mwenzie huo siyo unyanyasaji. usimlaumu jirani kabla hujaangalia nyumba tako ina matatizo chungu mbovu. leo albino anaogopea maisha yake haya abiria mabasi watu wanashambuliwa na majambazi na kuvuliwa nguo mbele ya wazazi wao huu sio unyama au kwa vile mwafrika mweusi kafanya basi sawa. tusilaumu saudia tujilaumu sisi wenyewe. warabu eti walifanya utumwa mie mwafrika mtanzania mweusi hapa oman sijaona mtumwa kama inavyoeleza kwenye vitabu vya historia utumwa ulifanywa na wazungu. kwanza historia hamujui kabisa mnaropoka tu. saudia haikiwahi hata kutawala ni sawa na kusema zambia ndiyo tanzania. ni muhimu ndugu watanzania tupendane kwa dhati kuanzia chini hadi viongozi tusijigawe magroup haya ccm na haya ya wapinzani. tuwe kitu kimoja watanzania hii italeta baraka. leo tatizo mtanzania madaraka anwasahau wenzake walio chini. machinga wanapigwa na kunyangwa mali zao utafikiri majambazi. tuombe kheri na mapenzi ya vitendo. mohammed manganga
ReplyDeletenitasoma kesho
ReplyDeletemmeandika magazeti sana,pole mdau kaza buti utafanyeje ss!!
UKWELI NDO HUU HAKUNA MAENDELEO BILA KUWAJIBIKA. NCHI ZILIZOENDELEA RAIA ZAO WANAFANYA KAZI KAMA PUNDA, SEMBUSE WE WAKUJA? UTAKUTA MZAWA MSHAHARA WA KAZI MOJA HAUTOSHI INABIDI ATAFUTE KAZI YA PILI. NA HAKUNA UPENDELEO WA MSHAHARA WA WAKUJA NA MZAWA DINARI ILE ILE.
ReplyDeleteUTAMKUTA RAIS WA KAMPUNI KAZI ZIKIZIDI IDARA YA UZALISHAJI ANAFUNGUA TAI YAKE NA KUVAA MAGWANDA YA UZALISHAJI NA KUJITOSHA KUTIA MZIGO, HUYO NI MZAWA. HAKUNA CHA KULALA LAZIMA KILICHOPANGWA KIFANIKIWE.
BONGO TAMBALARE TUMEZOEA LELEMAMA, TUNAFIKIRI UKISHAFIKA MAJUU NI SPEED YAKO KUZOA MAHELA. UKWELI NI SPEED YA UTENDAJI, UAMINIFU NA UWAJIBIKAJI. HUKU HAPENDWI MTU ILA UTENDAJI WAKO NDO SIRI YA MAFANIKIO YAKO.
WATANZANIA MPATAPO DEAL HIZO CHANGAMKIENI KAMA HUNA AJIRA BONGO. NA UKISHAANZA UWE NA MALENGO YA HARAKAHARAKA YA MUDA MFUPI KISHA RUDI BONGO. KAMA WATAKA STAREHE HIZO UTAZIPATA UKISHAMALIZA DEAL YAKO NA SASA UNAFANYA MAMBO YAKO BONGO.
TUMESHUHUDIA MAKAMPUNI YA KIGENI YANAPOFUNGUA MATAWI BONGO NA WANAPOHIMIZA UWAJIBIKAJI UTAKUTA WATANZANIA WANAWAFUNGIA MILANGO NA KUWAITA WATESAJI AU WANYANYASAJI, HII NI SABABU YA KUTOJUA SIRI YA MAFANIKIO KATIKA UWAJIBIKAJI KAZINI. TUWALIOTEMBEA WAMEONA WAMEENDELEA KWA MFUMO HUO VINGINEVYO TUAMUE KURUDIA UJAMAA WA MIAKA YA 70'S KISHA TUMALIZE AKIBA YOTE YA TAIFA TUBAKI NCHI MASKINI YA MWISHO DUNIANI.
KUMBUKENI KILA NCHI INA UTAMADUNI WAKE NA USIFANANISHE BONGO NA NCHI NYINGINE KWANI HATA WAO WANAYO TUNAYOWASHANGAZA KAMA UZEMBE NA UVIVU KATIKA UTENDAJI NDO AIBU YETU. KWANI WENGI WETU WANAOBAHATIKA KUPATA DEAL HEZO NI WALE WALIOSOMA NA WAKAKOSA AJIRA. LAITI WA KIJIJINI ANAYESHIKA JEMBE ANGEPATA NAFASI HIYO AU MACHINGA NA WAKOKOTA MIKOKOTENI UNGESHANGAA WANAVYOCHANGAMKIA TENDA HIYO.
SHERIA ZA KAZI TANZANIA NI ZILE ZILIZOPITISHWA KIPINDI CHA MFUMO WA UJAMAA UPOSHAMIRI AMBAZO ZILIWEKA MISINGI YA KUTETEA MWAJIRIWA ILI KUUA SECTA BINAFSI BAADA YA UTAIFISHAJI, LAKINI LEO INGEBIDI SHERIA HIZO ZIFANYIWE MAREKEBISHO VINGINEVYO UBINAFSISHAJI NA KUKARIBISHA WAWEKEZAJI TOKA NJE WANAPATA TAABU NAZO KWANI NYINGI YA SHERIA HIZO HAZILETI TIJA KWA UKUAJI WA UCHUMI WA TAIFA.
HAYO NI MAONI YANGU BINAFSI
HAKUNA MTU ANAEWEZA KUWAGUSA WASAUDI, SIO WAINGEREZA,WAMAREKANI, WAFARANSA ETC.
ReplyDeleteUNAWEZA UKAANGALIA MATUKIO KIBAO SI KWA WATANZANIA AU WAFRIKA TU HATA WAMAREKANI NA WAINGEREZA WENYEWE YAKIWAKUTA WANAISHIA KUMALIZANA KIMYA KIMYA TU.
MATAIFA YA MAGHARIBI YANAFANYA BIASHARA ZA MABILIONI YA DOLARI NA SAUDI KWA HIYO HAWAWEZI KUFANYA CHOCHOTE HAPO.
NDUGU YANGU MALIZA MKATABA WAKO RUDI BONGO ULE KISAMVU KWA RAHA ZAKO.
MWENYE MASIKIO ASIKIE NA WENGINE TUWE WAANGALIFU NA MAMBO YA KWENDA UGHAIBUNI KICHWA KICHWA, SI UARABUNI TU HATA MAGHARIBI NA KWENGINEKO.
POLENI WOTE MLIOATHIRIKA NA UTAPELI HUO.
K.O.R.
Mdau ningependa kukupa hongera kwa kuwataadharisha watanzania wote kwa ujumla, maan ukiweka jambo kwenye blogu ya jamii basi ujue ujumbe umefika. Pole sana kwa yote yaliyokukuta, hayo uliyoyasema ni ukweli mtupu na nawaonea huruma wadau watao puuza ushauri wako. Waswahili walisema asiyesikia la mkuu, huvunjika guu..Waache tu waende...kwa wale wanaotaka kujua hali halisi ya sehemu kama dubai..soma article hii hapa http://news.bbc.co.uk/2/hi/uk_news/magazine/7985361.stm
ReplyDeletemhmmm aiseee poleni sn kwa kweli inasikitisha sana na inauma kusikia ndugu zetu mnafanyiwa hivi lol hao watu hawana hata chembe ya huruma jamani si binadamu kabisaaa yaani natamani hata na ndugu zao huku sijui tuwafanyaje maana hatari sana na pia ni fundisho kwa wengine waone mfno huu.
ReplyDeletemeggy
Mdau uliyeathirika kwa utapeli wa kazi kwanza pole sana kwa masaibu yaliyokukumba.
ReplyDeletePili nikupe wazo la kutengeneza filamu ya documentary kuonyesha matatizo wanayoyapata watu wanaotapeliwa kwa mtindo huo. Sina utaalamu wa kutengeneza documentary lakini ukipata mtaalamu mkashirikiana unaweza kuwafikia wadau wengi zaidi, wakiwemo wa jumuia ya kimataifa. Kwa kufanya hivyo unaweza ama kusaidia kuondoa tatizo kwa jamaa zenu kujirekebisha au kutahadharisha watu wasiingizwe mkenge.
Nakutakia mafanikio.
Hao wapuuzi wote wanaosema kuwa mbona kuna Wahindi, Wafilipino nk wanapayuka? Just because kuna watu wa nchi nyingine wanateseka haimaanishi Watanzania wakubali tu utumwa. Kitu muhimu ni kuwa hakuna mtu atakayekutoa Tanzania akakupe kazi nzuri nchi za nje. Akikutoza gharama za usafiri ndio ujue kabisa kuwa huo ni utapeli. Kwenda nje kuhangaika mwenyewe au umepelekwa kusoma ni tofauti na kuambiwa kuwa kuna kazi njee huku, njoo
ReplyDeleteKaka nashukuru sana kwa kuwa muwazi, sisi hapa nyumbani tulikua tumeanza kujikusanya kuwashughulikia kina dogo waje huko kwa ajili ya kazi.Nashukuru sana umetuambia ukweli.
ReplyDeleteNdugu zangu
ReplyDeleteMie Nina cousin wangu alichukuliwa kwenda umangani kufanya kazi za ndani, matokeo yake hela waliotumia kumpeleka kule pamoja na passport walimkata kwenye mshahara wake. Kazi kuanzia saa 11 alfajiri mpaka Sita usiku hakuna kukaa ni kusimama tu hata Kama huna kazi. Akaanza kuumwa alijitibu kwa hela zake, mwisho wa siku akaomba kurudi bongo, wakamwambia ajilipie nauli mwenyewe. Sasa hapo kuna ubinaadamu au unyama?
Wewe mdau huko,uliesema kama tunasema coz ni waarabu, wewe ni mwarabu nini? Ndio nyie mnaosoma habari halafu hamuelewi.
ReplyDeleteEti oo huku Uk kuna wananzania wamewatesa wafanyakazi wao wa kitanzania na sasa wana kesi.
sasa jioni ulivyo mpumbavu hao wanakesi sawa, je hao ndugu zako waarabu wnaotawesa watanzania je wana kesi? pumbavuu weeee!! waarabu ndugu zako ndio rasisiti, mgeni huna haki ndani ya chi ya mwarabu ndio zao warabu wabaguzi sana. hapa inayozungumziwa ni haki watanzana amefania mbaya wafana kazi wao wa ndani huko kwenu Uk wana kesi, je hao ndugu zako wanaowafanyia mbaya watanzania wana kesi? usiropokwe km umekunywa maji Snow inayokanywaga na mbwa wa uk.
WAARABU SI WATU MIMI NINA RAFIKI YANGU HAPA WA KISOMALI ALIKUWA HUKO KABLA YA KUJA HAPA UINGEREZA ALIKUWA DEREVA WA TAJIRI MMOJA AMBAYE ALIKUWA NA WAKE WANNE, HUYU BWANA ALIKUWA HARUHUSIWI KUINGIA NDANI YA NYUMBA NA WALA KUONGEA NA FAMILIYA YA KIKE YA HUYU JAMAAA, ALIKUWA ANAMTUMA KAMA MBUZI ALIKUWA ANAMWAMULISHA AENDE MJINI AKAMTAFUTIE VIJANA WA KITHAILAND WA KULAWITIKWENYE MAHOTEL, AKIKOSA ANATAKA KUMLAWITI MWENYEWE, NA SIKU MOJA ALIMLAWITI KWELI KWANI ALIMTISHIA KUMMWITIA POLISI KWA KUMSINGIZIA KUWA AME-RAPE BINTI YAKE NA ADHABU YAKE ALIMWAMBIA NI KIFO NA MATAJIRI WANASIKILIZWA SAUDI, AKAMWAMBIA KAMA HUTAKI NIKUITIE POLISI TOA TIGO CHAMAA AKATOA TIGO, SI WATU HAO, AKUKAA SANA AKATOROKEA UBALOZI WA UK AKALETWA HUKU.
ReplyDeleteTUNAOMBA UBALOZI WA TANZANIA SAUDIA UJIBU HIZO TUHUMA NA WATUELEZE WAMEFANYA JUHUDI GANI KUSAIDIA HAO WATANZANIA NA WAMEKWAMA WAPI MANAKE UBALOZI WA TZ UKO HUKO KWA KODI ZETU NA MOJA WAPO YA KAZI ZAO NI KUSAIDIA WATZ WALIOKO HUKO KUHAKIKISHA HAKI INATENDEKA.
ReplyDelete