Inaripotiwa kuwa ajali mbaya ya basi ya Kampuni ya AM Coach aina ya Scania lenye namba za usajili T316 AZR limepinduka na kusababisha vifo vya watu ishirini na nne (24) na kuacha majeruhi hamsini na sita (56).

Basi hilo lilikuwa likisaifiri kutoka mkoani Arusha kuelekea Mwanza na kupatwa na ajali hiyo baada ya kupasuka tairi na kisha kupinduka lilipokuwa wilayani Nzega mkoani Tabora, takriban kilomita kumi na mbili (12) toka mjini Nzega.

Inasadikiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi uliochangia kushindwa kuhimili kusimamisha basi hilo punde tairi lilipopasuka.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Liberatus Barlow amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na mganga katika hospitali ya wilaya ya Nzega, John Mwombeki amethibitish vifo hivyo. Mungu awapumzishe pema marehemu wote. Amin.

Ajali za magari zimekuwa zikitokea mara kwa mara nchi ni Tanzania na vyanzo vingi vya ajali hizo ni pamoja na mwendo kasi, barabara chakavu na vyombo vya usafiri vibovu.
chanzo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Hivi ndiyo kusema tatizo hili limetushinda kabisa utatuzi??

    Mimi bado lawama zote kwa serikali kushindwa kudhibiti Road safety. Mdereva wahuni, wamilikiwa mabasi wahuni, Trafiki police rushwa, Mabasi mabovu basi ili mradi tu. Mpaka lini tutaendelea kupoteza roho za watu zisizo na hatia??????

    ReplyDelete
  2. Ankal mi nashindwa kuelewa,wamekufa watu 24, alafu 56 majeruhi ! ina maana hilo basi lilikuwa na abiria 80 ! mi nnavojua mabasi maximum yanakuwa na siti 65 kama ni 3 by 2,kama ni 2 by 2 zinapungua zaidi,na siku hizi mabasi hayaruhusiwi kusimamisha abiria,tena hao ni ambao wamekuwa affected,kama kuna ambao hawakufa au kujeruhiwa ina maana gari lilikuwa na abiria zaidi ya 80 ! mi napenda Traffic wote ambao walikuwa ktk vituo ambavyo hili basi lilipita na wakaliruhusu kuendelea wachukuliwe hatua kali sana ili iwe fundisho.
    asante.

    ReplyDelete
  3. JAMANI HIVI TUTAENDELEA KUONA NDUGU ZETU WANATEKETEA KWA HIZI AJALI ZA KIJINGA HADI LINI!!!!!
    HIVI VYOMBO VINAVYOSIMAMIA USAFIRI VINA KAZI GANI? KWANINI KILA SIKU AJALI TUUU!!! NA MARA ZOTE CHANZO NI KILEKILE...MARA MWENDO KASI, MARA MATAIRI FEKI!!! MARA MAGARI YANAWEKWA INJINI ZA MARORI!!!.... NINA AMINI HAYA YOTE VYOMBO VYA USALAMA VINAYAJUA!!

    EE MUNGU TUNAHITAJI SASA UONGOZI WAKO
    NA UTUOKOE NA HAYA MAJANGA

    KWELI NI AIBU JAMANI!!! KHAAAAAAA!!!

    ReplyDelete
  4. Kama tunavyoona usalama barabarani uneshindikana ni katika taasisi zote. Hakuna anayejali kila mtu na maslahi yake binafsi. Siku hizi mtu akipata uongozi zi kwa taifa bal kwake yeye na familia yake basi. Nyie mkifa haya, mkipata vilema haya,n.k. Angalia waliohamishwa kipawa wanavyotaabika sasa. Je! na hao ni uzembe wa trafiki? ni uzembe wa TABOA? ni uzembe wa barabara? Nyie acha tu ,hiki ni kiama viongozi wanatuletea kwa kukilazimisha. Lakini mwisho wake upo kwa kila mmoja ambaye kwa sabb yake vifo, shida, n.k vimetokea. Vyote vitahamia kwao

    ReplyDelete
  5. PETER NALITOLELAMarch 02, 2010

    WHY PEOPLE IS DYING WITH ACCIDENT AND NO BODY ARE CONCERNING WITH THE DYING PEOPLE ON THE STREETS, WHY WHY ARE THIS HAPPENG TO US, THE DRIVER IS SO SPEEDING FAST AND LET THE CAR RUN OVER TO THE INDIVIDUAL PASSENGERS AND ITS FAMILY SO THAT THERE ARE SO DYING INDIVIDUAL LIKE OUR COUNTRY HAVE NO ACCIDENT LAW ON THE ROAD AND SPEEDING DRIVERS. I AM SICK OF THIS MESS I AM CAUSING PEOPLE TO DYING LIKE CHICKENS NO BODY ARE GOING TO JAIL ANY HOW. MICHUZI ARE DOING FANTASTIC JOB TO ANNOUNCE THIS HABIT ON ITS BLOG OF FAMILY GIVE ITS UP MICHUZI NO BODY CAN LET HE DOWN. YOU KNOW HOW IS HARD HIS JOB ARE TO JAMII AND ALLIES OF THIS BLOGS. I SUB MEETS MY COMMENTS. THANKS YOU ALL OF YOU.

    ReplyDelete
  6. Inasikitisha sana, Mungu azilaze roho zao mahali pema. Na majeruhi tunawaombea Mungu awasimamie wapone.
    Serikali lazima iweke mikakati mipya ya kuwabana hawa madereva wazembe, mikakati hii ianzie kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri, kuwaka watu dhamana. Wanaajiri watu wahuni wahuni tu, wasiojali maisha ya wenzao.

    Lakini kuna abiria pia wakorofi?
    Huchangia katika kumlazimisha dereva aendeshe mwendo kasi ili wawahi katika mambo yao.
    Pia Magari yanakuwa mabovu, unakuta mmiliki kila akishauriwa arekebishe vifaa yeye anataka waendelee kidogo atabadili baadaye.

    Makosa haya yako kila upande, ni suala la kukaa pamoja na kujua nini kinafanyika.


    disminder.

    ReplyDelete
  7. MTAJUA WENYEWE NA UPUMBAVU WENU,KILA SIKU TATIZO MOJA,KUSOMA HAMJUI HATA PICHA HAMUIONI?MNAJUA KABISA KWAMBA UZEMBE NI MKUBWA SANA KWA MADEREVA WA BONGO NA SIO TU HILO HATA HIZO LESENI MNAZOTOA NI ZA DILI DILI TU HAKUNA DEREVA ALIYEENDA SHULE HAPO,HAMTAMBUI HAYO?SUBIRINI SASA MCHINJWE WOTE MUISHE SHENZI ZENU NDIO MTAREKEBISHA SYSTEM ZENU NA SIRUDI BONGO NG'OO HATA HAPA NILIPO NIKITIMULIWA NATAFUTA KIWANJA KINGINE CHA KWENDA KUDADEKI

    ReplyDelete
  8. Mafisadi wanataka kuongeza idadi ya wabunge badalaya kununua Vizalisha umeme kwenye Hospital zetu.

    ReplyDelete
  9. Anony no moja kwani tatizo gani ambalo tumeweza kutatua mpaka sasa?Imefika mahali kwa watanzania hata yale mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu tunamwachia Mungu. Binafsi huwa sikati tamaa lakini kwa namna tunavyoyaendesha maisha yetu kama sinema naelekea kukata tamaa.Ajali kila siku zinaua hakuna hatua zozote madhubuti zinazochukuliwa from top to bottom.

    ReplyDelete
  10. wewe mdau wa 02,10:29:00 AM, PETER NALITOLELA, kwa nini usiwasilishe mawazo yako kwa kiswahili ili ueleweke, hicho kiingilishi chako bwana haaa...inaonyesha mwalimu wako alikuwa wa vodafaster.

    ReplyDelete
  11. PETER NALITOLELAMarch 02, 2010

    ANOY 02,10;29 AM
    I AM A PEOPLE LIKE YOU SO YOU DIDN`T NOT UNDERSTAND YOUR ENGLISH THAT IS MY NOT MY BUSINESS I DOESN`T HELP YOU ANY THING. I AM FINISHED MUZUMBE AND WITH HONORS WITH ALL THE SUBJECTS OF MY CLASS, I AM PASSED AND I AM SMART KID, FROM ST. ANTONY MBAGALA UNTIL MUZUMBE UNIVERSITY EVERY ONE I AM KNOW SO MUCH WHY DO YOU NOT WRITE ON ENGLISH IF YOU ARE KNOWING IT. YOU ARE HATER AND SELFISH, IAM NOT STOPING TO WRITE ALL IN ENGLISH.

    ReplyDelete
  12. Poleni wote ambao mmepotelewa na ndugu na jamaa zenu mwenyezi Mungu azipokee Roho za marehem kwa Amani!!
    Tukirudi ktk ukweli Tanzania Rushwa kwa watu wa Usalama barabarabi itatumalila sie tusio na hatia! Ajali hii ni ushahidi tosha kuwa hilo basi lilibeba idadi kubwa ya abiria kuliko unavyotakiwa!Lakini askari (Trafik) wote waliokagua gari hilo hawakuliona hilo !!!
    Nimewahi kusafiri njia ya kigoma - Mwanza kupitia Geita ndani ya basi tulikuwa zaidi ya abiria 100+!! Abiria kama 30 hivi walikuwa wamesimama toka Kigoma(toka saa 12asubuhi mpaka 4usiku)mpaka mwanza! Nilitoa machozi jinsi wananchi wa maeneo hayo wanavyopata shida ya usafiri. Cha kushangaza kila kituo cha trafiki dereva na kondakta waliteremka na bila kificho tulishuhudia rushwa ikitolewa ili safari iendelee na mpaka tunafika gari hilo halikukamatwa!!!!!
    Kwa hakika hii pamoja na nyingina nyingi ni sababu kubwa zinazochangia roho za watu wasio na hatia kupotea bila huruma!!
    Chonde chonde Serikali inahitaji nguvu za ziada kukomesha mambo haya la tutazidi kuangamia kila kukicha!
    Inasikitisha sana!!

    ReplyDelete
  13. hii inasikitisha sana kwa sisi tunaotumia mabasi.rushwa itatumaliza,na serikali wameshindwa kabisa kuidhibiti.speed ya magari ni kubwa mno.zamani mabasi kutoka bukoba yalikuwa yanalala dodoma,lakini sasa hivi basi linaingia ubungo terminal saa nane usiku njia nzima wanaonga mapolisi.BABA MUNGU TUSAIDIE kwa nguvu za kibinadamu imeshindikana

    ReplyDelete
  14. Wakati umefika matatizo madogo kama ya matairi mabovu abiria wenyewe tunaweza kukwagua kabla ya kuchagua basi la kusafiria.

    ni rahisi sana kuchunguza kama matairi yameisha au ni mazima na yanafaa kusafiria.

    kupasuka kwa tairi mara nyingi inatokea kwa tairi kuwa la mda mrefu na limefika wakati wa kubarishwa ndio inaposhindwa kumudu mwendo wa kasi wa madereva wetu.

    kwahio angalieni abiria matairi manake naona tunakufa kwenye hizi ajali kama kuku bila sababu.

    ReplyDelete
  15. Have lost two cousins. May God rest their souls in peace. Amen

    ReplyDelete
  16. Bwana Michuzi nimesikitika sana kusikia habari za ajali hiyo iliyotokea Nzega ya basi la AM Coach. Mimi ni mwenyeji wa Arusha sasa hivi ninaishi Mwanza. Kwa hiyo mimi ni shuhuda wa mwendo kasi na ubora usioridhisha wa mabasi hususani ya njia hiyo ya Mwanza-Arusha-Moshi.

    Kwa sababu hizo toka mwezi Julai, 2009 ilinilazimu kwa usalama wa maisha yangu nihamie njia ya Mwanza-Musoma-Serengeti-Arusha, amabyo inauhakika wa safari salama kwa mabasi ya KIMOTCO na COAST LINE, naomba niwapongeze wamiliki, wafanyakazi wa mabasi hayo pamoja na uongozi wa Hifadhi za Serengeti na Ngorongoro kwa kudhibiti mwendo kasi kila wakati.

    Katika ajali hiyo ya AM Coach huko Nzega, imeelezwa kwamba ilisababishwa na pancha.Kwa akili zetu za kawaida tukubaliane kwamba chanzo namba moja cha ajali hiyo ni mwendo kasi na ubovu wa mabasi hayo kwa ujumla. Mimi ni dereva, lakini utashangaa mnasafiri kwenye basi kama abiria mara likipata pancha tairi lililopata pancha ni kipara na lile litakalobadilishwa pia nikipara tene cha kutisha zaidi bado wakimaliza kubadilisha tairi dereva anaendesha gari kwa mwendo kasi.

    Lakini kwa hili la ajali za mabasi lawama wanazistahili wafuatao. Kwanza; wamiliki wa mabasi kwa kukubali mabasi mabovu kubeba abiria na kutokuwa na madereva wa kuajiliwa bali wa mikataba isiyo rasmi.Pili; madereva wa mabasi hayo kwa kukuendesha mabasi mabovu, yaliyojaa abiria na kwa mwendo kasi( rejea ajali ya AM Coach; waliofariki 26, majeruhi 54, ukijumlisha walikuwa abiria 80) hiyo ni sawa? tatu; kikosi cha usalama barabarani, trafiki, kwa kuruhusu mabasi mabovu kutembea barabarani ya kiwa yamejaa abiria kupita kiasi na bila kuzingatia ratiba na muda wa kutembea kati ya kituo na kituo au wilaya na wilaya, nne; lawama ni kwa SUMATRA kwa kutochunguza sababu za ajali za mara kwa mara na kuzitafutia ufumbuzi, tano; lawama ni kwa abiria ambao wanakosa ushirikiano na ushupavu wa kukemea vitendo vibovu vya madereva,matingo na matrafiki wakati wa safari za mara kwa mara za mabasi.

    Bwana Michuzi kwa sisi wachumi na wazalendo wa taifa letu, inatusikitisha sana kuona tunapoteza lasilimali watu kwa vifo na ulemavu vinavyowapata watanzania kwa njia ya ajali za barabarani za mara kwa mara. Kwa sababu ya ajali hizo familia na taifa kwa ujumla wanakuwa masikini kwa sababu ya vifo na ulemavu wa kudumu wa ndugu zao. Taifa linaingia gharama zisizotarajiwa kwa ajili ya matibabu na huduma zingine za dharula.

    Kwa hili la ajali za barabarani na hususani za mabasi, kama ingekuwa kwa nchi zilizokomaa kidemokrasia, Afande Kombe angekuwa tayari amejiuzuru cheo chake kwa sababu ya kushindwa kusimamia askari wa chini yake amabo wanakumbatia vitendo vibovu barabarani kwa sababu wanazozijua wao( sizizo na manufaa kwa taifa) pia boss wa SUMATRA angeshajiuzuru kwa kushindwa kubaini sababu za ajali na kutafuta ufumbuzi wake na hukumu za wasababishi wa ajari za barabarani zitungiwe sheria kali itakayo wapa fundisho wakosaji.

    Kwa hiyo kama vile tunavyoogopa Malaria na magonjwa na majanga mengine ni wakati muafaka tuzione ajali za barabarani kama janga tena lililo kubwa lakini lenye tiba. Tuseme "AJALI ZA MABASI HAZIKUBALIKI"

    Na shauri Speed governor zirudishwe pia kwa usimamizi wa karibu sana, ratiba za mabasi zizingatiwe kwa karibu sana, kama basi inatakiwa kusafiri kwa masaa 18 au 20 toka Moshi hadi Mwanza inakuwaje basi litoke Moshi lifike Mwanza saa 12 jioni?
    Zaidi ya yoye tuwaombee kupona majeruhi wa ajali ya AM Coach huko Nzega na Mungu azilaze pema peponi roho za waliokufa katika ajali hiyo Amen. Pia tumuombe Mungu awape matumaini ndugu waliofiwa na wapendwa wao katika ajali hiyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...