Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Katsuya Okada kabla ya mazungumzo yao kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri huyo, Tokyo akiwa katika ziara ya kiserikali nchini Japan wikiendi hii. Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiongozwa na Waziri Mkuu wa Japan, Yukio Hatoyama kuelekea kwenye ukumbi wa mazungungumzo yao kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu huyo jijini Tokyo Machi 26, 2010 akiwa katika ziara ya kikazi nchini Japan. Waziri Mkuu, Mizengo PInda akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Japan, Yukio Hatoyama (kulia) kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu huyo jijini Tokyo Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akipokea vifaa maalumu 10 vyenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kutoka kwa Mtanzania aishiye Japan Willy Mgoya vyenye uwezo wa kumgundua mtu aliyekunywa pombe katika mkutano kati yake na watanzania waishio Japan uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya New Otani jijini Tokyo. Vifaa hivyo vimetolewa kwa Waziri Mkuu ili avikabidhi kwa Jeshi la Polisi nchini ili livitumie kuwabaini madereva wanaoendesha magari wakiwa wamelewa.
Baadhi ya Watanzania waishio Japan wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza nao kwenye hoteli ya New Otani , Tokyo akiwa katika ziara ya kikazi nchini Japan.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza baadhi ya watanzania waishio Japan kwenye hoteli ya New Otani , Tokyo akiwa katika ziara ya kikazi nchini Japan.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa amembeba mototo, Alisa Charles Kilinda (6) ambaye baba yake alikuwa mmoja wa watanzania waishio Japan waliokutana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya New Otani jijini Tokyo.
SERIKALI ya Japan imelikubali ombi la Serikali ya Tanzania la kutaka
igharimie ujenzi wa nyongeza wa barabara mbili muhimu Kusini na Kaskazini
mwa nchi na hivyo kupanua mtandao wa barabara za zinazounganisha mikoa yote nchini.

Makubaliano hayo yalifikiwa katika mazungumzo rasmi ya kiserikali baina ya
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri Mkuu Yukio Hatoyama wa Japan mjini Tokyo jana (Ijumaa Machi 26, 2010) katika siku ya tatu ya ziara ya siku nne ya
Mhe. Pinda nchini humo.

Baada ya mazungumzo hayo, Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa aliwasilisha ombi kwa Waziri Mkuu wa Japan, Mhe. Yukio Hatoyama, kutaka msaada zaidi wa nchi hiyo kugharimia ujenzi wa Barabara kati ya Mangaka hadi Tunduru na kati ya Dodoma na Babati na Waziri Mkuu wa Japan akakubali.

Barabara ya Mangaka -Tunduru ni kilomita 146 na ya Dodoma Babati ni
kilomita 188. Barabara hizo ni nyongeza katika barabara Tunduru
-Tandahimba (k.m. 186) na Iringa – Dodoma (k.m. 250) ambazo tayari Japan
ilikubali kuchangia ujenzi wake kwa lami pia.

Katika mazungumzo hayo Serikali ya Japan pia imekubali kuisaidia Serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa mradi wa Kilimo Kwanza, hasa kwa
kuwafundisha wahandisi wa kilimo cha umwagiliaji maji ambao ni wachache mno nchini.

Waziri Mkuu Pinda aliwaambia Waandishi wa Habari katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Japan (NHK) kuwa kwa jumla ziara yake ya Japan, kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo, imekuwa ya mafanikio.

“Naona tumefanikiwa sana. Hii ilikuwa ni ziara ya kuendeleza uhusiano na
ushirikiano baina ya nchi zetu na kuja kuwashukuru wenzetu kwa kutuunga
mkono kwa dhati katika jitihada za kujiletea maendeleo na kufuta umasikini,”
Mhe. Pinda alisema.

Mhe. Pinda alisema amemwalika Waziri Mkuu wa Japan kutembelea Tanzania
katika tarehe itakayopangwa baadaye na kwamba Mhe. Hatoyama ameukubali mwaliko huo.

Katika ziara yake hii ya Japan, Waziri Mkuu alitembelea shughuli za ushirika
wa wakulima na taasisi za utafiti wa kilimo na kuwa na mazungumzo na
viongozi wa Japan kuhusu kuendeleza uhusiano na ushirikiao wa maendeleo.

Jana (Ijumaa Machi 26, 2010) usiku, Mhe. Pinda alikutana na Watanzania
wanaoishi kwa kusoma na kufanyakazi Japan katika Hoteli ya Otani mjini Tokyo na kuwaambia kuwa wasikusahau nyumbani pindi wanapomaliza masomo yao au kupata nafasi ya kutoa misaada au kuwekeza.

Umoja wa Watanzania hao ulimkabidhi Waziri Mkuu Dola 2,000 (karibu Sh.
Milioni 3) zikiwa ni msaada kwa waliopatwa na maafa ya mafuriko katika
Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.

Mtanzania mmoja anayeishi Japan, Willy Ngoya pia alimkabidhi Waziri Mkuu
msaada wa vifaa 10 vya kupimia kilevi kwa madereva ili kusaidia jitihada za
Jeshi la Polisi nchini kukabiliana na madareva walevi wanaosababisha ajali
nyingi za barabarani.

.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hongereni wana umoja wa Japan kwa kukumbuka nyumbani. Na huyu aliezaa na mjapan m-kid wake atakuwa raia wa tanzania jina tu.Kwa uzoefu inaonyesha mtu akipata mtoto na wajepu, basi mtoto lazima abobee na kuwa mjapan 100% ukubwani.

    ReplyDelete
  2. Michu--what you forgot to report is what are the Japanese getting back from hiyo misaada. Is it a loan? if yes, is it concessional or? How are they going to guarantee oversight of these miradi? Are this projects strictly for Japanese construction firms au hata mbongo wa kawaida anaweza kubid for a mchongo?

    I love your blog maan, but tuwekee a balanced report/

    Mdau-

    ReplyDelete
  3. now...thats how you use public money on foreign trips by acquiring good deals for the Tanzanians...5 trips, 3 positive 1 leisure 1 failure
    keep up good work pinda and who knows..u can become a savior of the poor(90%)

    ReplyDelete
  4. Anco Michusi mimi nina swali dogo tu kwenye picha ya pili na tatu kutoka chini huyo mdau alivaa scarf ya rangi ya damu ya mzee na koti jeusi je amevaa Helmet kichwani ama ndo kichwa chake real?
    Mdau Maswa Shinyanga

    ReplyDelete
  5. Lete hivyo vipima kilevi ili viwatajirishe 'Trafiki Polisi'. Ajali zitaendelea kama kawa. Mmomonyoko wa fikra za watanzania uliosababishwa na kukata tamaa na maisha iliyosababishwa na serikali ya sisieemmm ndiyo imetuleta hapa tulipo.

    Hata kila polisi akipewa pikipiki mbilimbili hakuna chenjeez zozote pozitiiv tutakazoziona. Itakuwa ni kuwaneemesha polisi tu, na sio kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa. Hivyo vifaa vitatumiwa na polisi katika kuwatisha waendeshaji magari ili watoe elufu mbili (Shs. 200/=) fasta fasta tu.

    Pole inji yangu ya Tanzania inayoangamia.

    Tanzania x 2
    Nakupenda kwa moyo yoteeee
    Inji yangu Tanzania
    Ardhi yako tajiri sanaa!

    Nilalapo nakuota weweee
    Niamkapo Dhahabuuu kwishlinaaaa
    Inji yangu Tanzaniaaa
    Inaporwa kwa kasi sanaaaa
    ....

    Nabata ushungu .... heri niishie sasa. Naingia mitini

    Dayasipora

    ReplyDelete
  6. Mdau Anonym 10:19,
    Nafurahi sana kwa kugundua hilo lakini siyo Michu mwenye hilo tatizo. Mimi ni mzawa wa bongo na kama nikijaribu kuvuta fikra siku za nyuma sana...miaka ya 1970 kuja hadi 2000...sikumbuki wakati wowote Tanzania inakopeshwa. Tanzania inasaidiwa tu haikopeshwi lakini katika taarifa mbalimbali za kiserekali tunaona kuwa tuna madeni...Hilarious...Inafurahisha sana...misaada,misaada, misaada..lakini mwisho inageuka kuwa madeni lakini inakuwa madeni wakati waliokuwa viongozi waliosaidiwa wamestaafu au wametoka madarakani...hakuna wa kumuuliza kuwa hili deni ni lipi na pesa iliokopwa ilifanyia nini....Jamani jamani...tuamke! na tuwe wakweli na tuwe na uwazi! Tumekopeswha kiasi hiki, na tunatarajia kufanyia hili, natunatarajia kurudisha kwa namna hii, kwa kipindi hiki...kwisha...blablablablabla tumesaidiwa...weweeeeeeee....

    ReplyDelete
  7. Wadau wa japan mnaonekana mnamshikamano sana ina reta moyo ila sijuwi na nyinyi mna mpango wa kufungua tawi la ccm ? ila nisinge kushaulini mlete ujinga wa siasa ughaibuni nyinyi fanyeni kazi kama wajepu wenyewe hawa jamaa walio leta siasa EU naona vichwa vyao sio vizuli. mdau wa kabur afughan

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...