Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam Afande Suleiman Kova (kushoto) akionyesha zana mbalimbali zilizokamatwa kutoka kwa majambazi 6 waliokamatwa na polisi wakati wakijiandaa kwenda kufanya uhalifu katika maeneo ya Tegeta, Dar. Vitu walivyokamatwa navyo ni pamoja na mitungi ya gesi, funguo 73, mitarimbo na plasta moja kubwa.
Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kushoto) akionyesha gari yenye namba za usajili STK 1739 mali ya Wizara ya maliasili na Utalii ambalo liliibiwa na majambazi katika eneo la Mabibo, Dar es Salaam na kukutwa Mbagala.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. sasa kova tunataka umkamate AFANDE SELE aeleze kwanini alimpiga MABUSU MADEE raisi wa manzese mbele ya waziri shamsa mwangunga wakati anajua fika maelfu ya watanzania walikuwa wanaangalia fainali ya maisha plus

    ReplyDelete
  2. mmhh majambazi bwana hayakomi, hayajui hata soda walizokuwa wanakunywa zitaonyeshwa hadharani sijui dawa ni nini maana hata hiyo ya kuonyesha vifaa vyao haisaidii

    ReplyDelete
  3. HAHAHAHA AFANDE KAAMUWA HII SASA NDIO KESI SASA, KUMBE UKIAMUWAU NAFANYA KAZI BILA WADAU USINGEFANYA KAZI. KHAMIS.

    ReplyDelete
  4. wewe wa kwanza hacha bangi kwenye jamii rais wa manzese aende akatishe serikali yake uko uko uswahili kwao mambo sele na madee wapi na wapi.

    ReplyDelete
  5. UHEJEJEJJEJEJEJE

    ReplyDelete
  6. hivi kwa nini hiyo mifuko ya police nimikubwa hivyo??

    ReplyDelete
  7. longa longa tu mnaditia wachapakazi hivi sasa lakini mnasahau mnapowababikia watu keshi na halafu kuwachafulia majina yao na kuwakurupukia tuu na kutaka kuwatia ndani bila ya uthibitisho kamili.
    hamna lenu jambo nyinyi njangu njangu kina kovu

    ReplyDelete
  8. Vipi walikuwa na pingu ?

    ReplyDelete
  9. nilipoona picha ya pili nikajua heh matapeli wengine wanatambulishwa, mwingine ataambiwa sogea huko ili mwenziwe atambulishwe na vifaa vyao na sifa zao kibao, kumbe sio safari hii

    ReplyDelete
  10. Hahaha naona Afande leo leo meno nje anafurahia kurudi kwenye ngoma yake anayoipenda. Ile ya last time ilikuwa ngumu kuicheza na mapigo yake yalikuwa hayaeleweki kama ni mdumange, mganda, mnanda, taarab au bongo flava. akajikuta hajui acheze vipi.

    By the way hongera kwa kuzuia uhalifu japo ninajua hawa mliowakamata walikuwa hawajapata vibali vya vijana wako katika kufanya kazi waliyotaka kuifanya.

    ReplyDelete
  11. huyo picha ya kwanza anaechungulia mlangoni sijui ataka ahakikishe kila kifaa kinatamkwa sawasawa isije ikawa electoniki ya muro

    ReplyDelete
  12. MAGARI YA AINA HIYO YANAPENDWA NA WEZI KWANI YANA SOKO HUKO ARUSHA, MOSHI NA MWANZA. NAKUMBUKA TULINYANG'ANYWA GARI KAMA HILO MWANANYAMALA USIKU TUKITOKA KAZINI NBC HEAD OFISI. TULIKUWA TUNARUDISHWA MAJUMBANI NA GARI KAMA HIZO USIKU TUKIMALIZA KAZI BASI ILE TUNAMSHUSHA MFANYAKAZI MMOJA WAKATOKEA WATU NA MAPANGA, BUNDUKI NA RUNGU WAKATUAMURU KUSHUKA NJE YA GARI NA ATAKAYE BISHA ATAULIWA NA MAGUMI NA MAKOFI YALITEMBEA KIDOGO TUKAPIGWA CHINI WAKAINGIA NDANI YA GARI HAO WAKACHICHIA NALO, NA YOTE YA NBC HQ YALIIBIWA HUO ULIKUWA MWAKA 1999 HADI 2001 YOTE YALIIBIWA

    ReplyDelete
  13. majambawazi wa magari wana yapenda sana hayo malandcruiser wenyewe wanayaita mkonge nafikuri wnaita mkonge kwa ajili ya hilo dude jeusi mbele ya gari hayo magari na sukari huku rwanda na burundi wanpata hela nzuri sana vile hapy magari ni imara sana na ya bei nzuri sana kwa biashara yao ya uchori
    mdau former bibi wa jambazi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...