Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark Mwandosya akizungumza na wataalam wa sekta ya maji (hawapo pichani) kutoka Halmashauri mbalimbali nchini wakati wa hafla ya kukabidhi magari 61 na Mashine za kudurufu 61 kwa halmashauri za mikoa 11 kusaidia Programu ya Maji na usafi wa mazingira vijijini leo jijini Dar
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark Mwandosya akikagua moja ya gari aina ya “Land Cruser hard Top New Model “ ambayo yametolewa kusaidia Programu ya Maji na usafi wa mazingira vijijini leo jijini Dar
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark Mwandosya akiendesha moja ya gari alilokabidhi kwa Halmashauri ya Rorya akiwa na Mbunge wa jimbo hilo Prof. Philemon Sarungi .
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark Mwandosya akimkabidhi funguo za gari Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Mpanda Injinia Godfrey Mbabaye.Takribani magari 61 na mashine 61 za kudurufu zimetolewa kwa Halmashauri za mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera,Kigoma, Mara,Tabora, Rukwa, Manyara, Mtwara, Arusha na Mbeya leo jijini Dar


NA MAGRETH KINABO – MAELEZO.
SERIKALI imewatahadharisha Wakurugenzi wa Halimashauri nchini kutotumia magari yaliyotolewa kwa ajili ya Programu ya Maji na usafi wa Mazingira vijijini katika shughuli nyingine nje ya utaratibu uliowekwa.
Hayo yalisemwa jana (leo) na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya wakati wa hafla fupi ya kukabidhi baadhi ya halmashauri magari 61, kati ya 125 na mashine za kudurufu 56 kati ya 171 iliyofanyika jijini Dar leo.
Magari hayo kila moja lina thamani ya sh. milioni 63.5 na mashine hizo sh. 460,000 kila moja yamekabidhiwa kwa halimashauri hizo ,kwa ajili ya kusaidia kutekeleza programu hiyo ili kuboresha huduma za maji nchini na kuinua maisha ya wananchi. Magari mengine yanatarajiwa kuwasili mwisho mwa Machi.
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwasihi mchukue dhamana ya kuyatunza magari haya. Mhakikishe yanatumika kwa malengo yaliyokusudiwa .Yasitumike kwa shughuli nyingine au shughuli binafsi. Msiuziane magari haya,”alisema Profesa Mwandosya.
Waziri Mwandosya aliwaagiza kuwa wahakikishe wanayafanyia ukaguzi wa kiufundi magari hayo mara kwa mara na kwa wakati kama inavyotakiwa kupitia maelekezo yaliyomo kwenye vitabu husika.
Aliongeza kuwa katika matengenezo na ukaguzi watumie karakana za halmashauri na kuwasiliana na kampuni ya Toyota wanapohitaji ushaur au maelezo ya kiufundi, huku watumie madereva wenye ujuzi na kuwataka wasiwadilishe mara kwa mara isipokuwa pale inapobidi.
"Tutawapatia nyezo za kufanyia kazi hakikisheni wananchi wanapata maji,” alisisitiza. Katika hafla hiyo Waziri Mwandosya alikabidhi magari manne kwa ajili ya Biharamulo, Longido, Mpanda na Rorya.
Waziri Mwandosya alizitaka mamlaka za maji kubaini vyanzo vya maji na kuvitunza, na kuongeza kuwa idadi ya watu wanaopata majisafi na salama kwa upande wa vijijini imeongezeka kutoka asilimia 53.5 mwaka 2004/05 hadi kufikia asilimia 61 kwa mujibu wa twakimu za Desemba mwaka 2009.
Amesema serikali inatarajia mwishoni mwa mwaka huu itakuwa ni asilimia 63, wakati malengo ya Millinea ya kuwapatia maji safi na salama wananchi wa vijijini ni asilimia 65 ifikapo mwaka 2010.
Kwa upande wa miji ya mikoa makuu ya mikoa alisema idadi ya watu wanaopata maji hayo imefikia asilimia 84, lakini changamoto ipo Dar es Salaam ambapo wameweza kufikisha asilimia 68, wakati lengo la millinea ni kuongeza kutoka asilimia 73 hadi asilimia 90 ifikapo mwaka 2010.
Waziri Mwandosya alisema ili kukabiliana na changomoto ni vema mipangomiji iende sambamba na huduma za maji na umeme.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. wasije kuyauza tu au kuuza vifaa !!kwani wabongo sijuhi tumeumbwaje kwani tunajua kuua tu siyo kutunza.

    ReplyDelete
  2. Gari zimechukua pesa nyingi kuliko pesa zinazohitajika kuweka hayo maji kwa wananchi,cha ajabu utakuta zinatumika kubeba maboss na wake zao kwenye vikao visivyokuwa na mwisho na posho,kwenye maskini hujiongezea umaskini.

    ReplyDelete
  3. 2010 hiyo old boys network tutaona picha nyingi sana kama hivi. I wish Tanzania kila mwaka ungekuwa wa uchaguzi tungekuwa tumeendelea sana. Maana hawa jamaa wasingelala wangekuwa wanafanya kazi za wananchi

    ReplyDelete
  4. jamani sasa na sisi huku kisarawe tumechoka kila siku mikoa hiyo hiyo na wilaya hizo hizo vipi huku kisarawe ama akuishi watu?

    ReplyDelete
  5. nifuraha kwetu wa tz kuona hayo yanatendeka.lakini mwishowake mbaya
    kinachotakiwa umewakabidhi maliyetu sie wananchi. usisahau kuwapitia kazi zao. ujue wewe waziri ni muajiriwa wetu watanzania.isiwe utendaji mbovu kilasiku hamfatili

    ReplyDelete
  6. aagh! mwaka wa uchaguzi huo!!!mwaka huu picha na takwimu kama hizi zitakuwa nyingi sana..lakini ikifika tu january kimyaaaaa!!!
    Hakuna watu rahisi kuwaongoza duniani kama wabongo..hakyamungu!

    ReplyDelete
  7. haya magari msiyauze kimagendo...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...