.jpg)


Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini
Kijiji cha Masaera, Kamati ya Maji ya Kijiji.
Kijiji cha Masaera, Kamati ya Maji ya Kijiji.
TANGAZO
Kutoka kwa: Mratibu wa Ukarabati wa Mfereji wa Masaera
Kwa: WAMASAERA WOTE
Wahandisi Wasio na Mipaka kutoka Chuo Kikuu cha Valparaiso, Marekani {Engineers Without Borders -USA, Valparaiso University} ambao wanashirikiana na wanakijiji katika kukarabati mfereji wa Masaera wameshafanya yafuatayo:
1. Wameshirikiana na wanakiji kukarabati maeneo yaliyoharibika kwa kutoa vifaa na ufundi.2. Wameshiriki kuweka geti katika chanzo
3. Wanaendelea kushiriki katika kuweka vibanio katika kigawe cha pili kwa simony mikaeli temu na mianzini kwa Marseli Sandi.
4. Wamesaidia vifaa vya thamani ya shs 600,000 [laki sita] paa la jiko la shule ya msingi ya Mandaka mazoezi. Paa limeshawekwa na mafundi seremala wa Masaera bila kulipwa [yaani kwa kujitolea]
6. Watakutana na wanakijiji wote Jumanne sokoni Kiano, mchana saa nane, kwa marejesho na kuagana.
7. Wataondoka Jumatano asubuhi.
Kutoka kwa: Mratibu wa Ukarabati wa Mfereji wa Masaera
Kwa: WAMASAERA WOTE
Wahandisi Wasio na Mipaka kutoka Chuo Kikuu cha Valparaiso, Marekani {Engineers Without Borders -USA, Valparaiso University} ambao wanashirikiana na wanakijiji katika kukarabati mfereji wa Masaera wameshafanya yafuatayo:
1. Wameshirikiana na wanakiji kukarabati maeneo yaliyoharibika kwa kutoa vifaa na ufundi.2. Wameshiriki kuweka geti katika chanzo
3. Wanaendelea kushiriki katika kuweka vibanio katika kigawe cha pili kwa simony mikaeli temu na mianzini kwa Marseli Sandi.
4. Wamesaidia vifaa vya thamani ya shs 600,000 [laki sita] paa la jiko la shule ya msingi ya Mandaka mazoezi. Paa limeshawekwa na mafundi seremala wa Masaera bila kulipwa [yaani kwa kujitolea]
6. Watakutana na wanakijiji wote Jumanne sokoni Kiano, mchana saa nane, kwa marejesho na kuagana.
7. Wataondoka Jumatano asubuhi.
Canute W Temu,
Mwenyekiti wa Kamati ya Maji Kijiji na
Mratibu wa Ukarabati wa Mfereji.
Masaera
unataka kimaro achanganyikiwe! anyway nice job,
ReplyDeleteIts so sad tunavyosubiri mpaka watu waje watuwekee vigate etc. Hao makandarasi wanafuzi wao practical field zao wanazifanyia wapi? Ni aibu sana kwa vile vitu vya kufanyia majaribio kwa wanafunzi wetu ili wakimaliza waweze kujenga ma flyover (lol)viko kila kona lakini hatuvitumii. Mwishow wakimaliza college hata chochote hawajui na hawajui waanzie wapi.
ReplyDeleteasante kwa hao waliojitolea kutengeneza hiyo mfereji manake kama sio hao hata bata wetu wangechukuliwa na mafuriko ya mifereji.....
Kazi nzuri ndugu mwenyekiti kwani kilimo pekee ndiyo kimbilio la mwanakijiji. Sisi wana kijiji wa Masaera tuko pamoja nawe.
ReplyDelete......Kazi nzuri, vijiji vingine viige mfano, kwa kasi hii sera ya kilimo kwanza itakuwa juu...
ReplyDeleteAnony wa 03:00:00am nakubaliana na wewe 100%
ReplyDeleteERB, CRB na NCC wapo lakini zimekaa kisiasa zaidi! Hizi Bodi na Baraza hazifanyi upembuzi yakinifu (Feasibility study) wa kumsaidia mkulima (na Tanzania asilimia 80% ni wakulima)aondokane na umaskini. Hata majengo ya K/Koo yanayosimamiwa na STD VII sidhani kama wamefanya juhudi za kutosha. Hivi majanga kama ya Haiti, Chile na Uturuki (Mungu aepushie mbali) yakitokea hapa Dar, kweli litabaki tofali juu ya tofali??!!
Nimependa, jinsi huo ushirikiano ulivyoweza kufanikiwa. Hapo Masaera ni pazuri na ardhi yake ina rutuba sana. Kwa kweli Mzee Temu na team yako hongereni. Ningevutiwa kama vijana wa kitanzania wataweza kuwezeshwa na kusaidia sehemu mbali mbali za maendeleo kupitia NGO an vikundi vya ujasiriamali, hata kutumia jeshi la kujenga taifa. Tungeweza kuelimisha jamii madhara, hatua za kuzuia magonjwa na kampeni za usafi, hata namna ya kukabiliana na majanga i.e mafuriko.Tupigishe harambee wajukuu zako, vanilla na kilimo viweze kuleta maisha bora masaera na Ngangu, Marawe,Kilema kwa ujumla.
ReplyDeleteTanzania ni rushwa tu kwenda mbele hakuna kingine... vijana wetu wapo wa kufanya kazi hizi, lakini hawawezeshi wanatafuta atakayewapa cha juu.
ReplyDeleteAnkal
ReplyDeleteHao Engineers Without Borders ni watu makini ambao wana mengi ya kutufundisha. Ingawa taaluma yao ni uhandisi, wanafanya juu chini kuwa sambamba na wataalaam wa fani zingine, hasa kwa kuzingatia hali halisi ya utandawazi katika dunia ya leo. Wanafahamu kuwa kufanikisha miradi mbali mbali duniani kunaendana na kufahamu na kuzingatia hali halisi ya kila jamii, ikiwemo saikolojia, mila, desturi, lugha na utamaduni kwa ujumla.
Kwa msingi huo, wamenikaribisha niwasaidie mawazo, kutokana na uzoefu wangu katika kutafiti na kuandika kuhusu masuala ya tofauti za tamaduni, hasa baina ya utamaduni wa Mmarekani na ule wa Mwafrika. Hayo ndio baadhi ya mambo nitakayoongelea kwenye warsha zangu Tanzania mwaka huu: Meeting Point Tanga, 12 Juni, na Arusha Community Church, Julai 3. Mipango mingine inaendelea.
Ni muhimu nasi tukajifunza kuangalia masuala kwa mtazamo mpana kama wa hao Engineers Without Borders. Bofya hapa.
Thank you all for your sincere comments. But why are people uncomfortable in giving their names? their identity? even in such a straightforward issue? Only MBELE gave his name?
ReplyDeleteAs long as we give sincere comments we should be bold enough to reveal our true names! Tuandike maoni yetu na tutoe majina yetu ili tuweze kufahamiana na kubadilishana mawazo kwa tukijuana. Kwa mtindo huu tutaelewana kwa dhati nani wadau wa maendeleo ya kweli ndani ya demokrasia ya kweli.
Asanteni sana kwa maoni yenu mazuri,
Canute Temu , Mdau wa Maendeleo ya dhati vijijini, Mkalimani, na mwanaelimu.
Sipendi Kimaro achanganyikiwe, la hasha, nataka aelewe kuwa katika jimbo kuna wadau wengi wa maendeleo na ingekuwa jambo la busara kutafuta njia za kuunganisha nguvu zao na kuleta msukumo wa usasa [modernisation] katika nyanja zao mahsusi. Sikuwahi kusikia habari za mkutano ulioitishwa kijimbo kuhusu maendeleo ya kiuchumi wala ya kijamii, au nilipitiwa? C Temu.
ReplyDeleteNaomba mtu yeyete anayejua sera ya KILIMO KWANZA imechapishwa wapi na nani anijulishe nijipatie nakala yangu. Niko kijijini na nahisi KILIMO KWANZA ni Kauli Mbiu [SLOGAN?] tu?
ReplyDeleteNaomba msaada.Tunachofanya sisi kijijini mwetu ni kujiendeleza kiuchumi kwa kukarabai mfereji wetu bila msukumo wa kauli mbiu hiyo.
Canute Temu.