
Familia ya Mzee Augostino Lissu Mughwai wa Mahambe, Singida inasikitika kutangaza kifo cha mama yao mpendwa,Martha Alu Alute kilichotokea tarehe 30 Machi, 2010 huko Dar es Salaam, Tanzania.
Maandalizi yanafanywa kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Mahambe, Singida kwa mazishi.
Marehemu alizaliwa mwaka 1932 Ighuka, Singida. Ameacha mume na watoto nane: Alute Mughwai wa Arusha, Tundu Lissu, Mjengi Lissu na Christina Lissu wa Dar es Salaam, Rose Masesa wa Songea, Peter Muro Mughwai wa Kondoa, Mateo Mughwai wa Singida na Vincent Lissu Mughwai wa Connecticut, Marekani.
Vile vile marehemu ameacha wajukuu 20, na vitukuu 6.
Kwa marafiki wa wafiwa wanaokaa nje ya Tanzania (Marekani, Uingereza n.k) unaweza kutuma rambirambi zako kwenye
accnt # 1259458568,
routing #221172610.
Au
kwenye anwani ifuatayo:
Vincent Mughwai
370 Huntington Road
2F Bridgeport
CT 06608
Poleni kaka na dada zangu. Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.Alex na Familia, Maryland, USA
ReplyDeleteLissu Mghwai poleni kwa msiba mlioupata, mlimpenda mama sana lakini mungu amempenda zaidi, BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE AMEN. Alcard Mumwi& Family, Dar, Tanzania.
ReplyDeletePoleni,kwani Bwana ametoa na ametwaa. Ila rambi rambi lazima tuweke kwa hizo akaunti??
ReplyDeleteMungu awasaidie sana katika kipindi hiki kigumu cha msiba,poleni sana kwa msiba,D.Mwashumbe
ReplyDeleteNdugu ALUTE na TUNDU namuomba Mungu awatie nguvu na moyo wa subira wakati huu ambapo mumefikwa na msiba wa kufiwa na mama yenu. Poleni sana. May Her Soul Rest in Eternal Peace. Amen
ReplyDelete