Video ya kilichojiri leo baada ya uchaguzi mkuu wa TZUK jijini London
Naibu balozi wa Tanzania Uingereza Mh. Chabaka Kilumanga (wa nne toka shoto) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi mpya wa jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza (TZ UK Association) mara baada ya uchaguzi Mkuu leo jijini London. Kushoto kwake ni Mwenyekiti mpya wa TZ UK Bw. John Lusingu wakati Katibu Mkuu Hassan Hafidh ameketi wa kwanza shoto akifuatiwa na Makamu mwenyekiti Nellie Nsemwa, Mratibu wa Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa kimataifa Bi. Bertha Somi, Naibu Balozi, Mwenyekiti Lusungu, Mama Grace Adel Shangali (Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya), Katibu Mkuu Msaidizi Dessa Makoko na Mtunza hazina Dk. Evans Mella. Katibu mwenezi Goodluck Mboya ni wa kwanza shoto nyuma na wajumbe.Abdul Dau
Chama cha watanzania nchini Uingereza leo jumamosi ya tarehe 27 mwezi wa tatu kimechagua viongozi wapya watakao kiongoza chama hicho kwa muda wa miaka miwili.
Akizungumza kwenye mkutano huo Mwenyekiti mpya wa chama hicho Bw. Lusingu amesema atashirikia na watanzania wote ili kuweza kufanikiwa kukiendelendeleza chama hicho. Katika uchaguzi huo Bw. John Lusingu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Bi. Nellie Nsemwa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Msaidizi, Bw. Hassan Hafidh amechaguliwa kuwa Katibu, D Makoko amechaguliwa kuwa kuwa Katibu Msaidizi, Bw. Goodluck Mbuya amechaguliwa kuwa Katibu Mwenezi na Dr. Evans Mella amechaguliwa kuwa Mweka Hazina.
Picha zaidi www.tz-one.blogspot.com



Lusingu, Hongera.
ReplyDeleteUjumbe:
Tekeleza wajibu wako wa kuwaunganisha watanzania wote na si kuwatenganisha katika misingi ya kisiasa!
Angalizo: Jina lake ni John Lusingu na siyo Lusungu.
ReplyDeleteHongera:
Naupongeza uongozi mpya wa UK TZ...Nawatakia mafanikio mema katika kazi ya kutujumuisha watanzania hapa ughaibuni. Mungu aendelee kuwapa uwezo wa kuona mbali ili tuandae maisha ya vizazi vijavyo. Tuwe na sustainable concepts, sustainable visions na sustainable strategic plans zitakazotuelekeza katika maendeleo.
Mdau mwenzenu katika libeneke.
Nani kawachagua? Watanzania walio uingereza? Ni wangapi hao watanzania? Uchaguzi ulikuwa wa aina gani na umefanyika lini? Mlitoa tangazo la uchaguzi ili watu wajitokeze ktk kupiga kura au kugombea hizo nafasi?
ReplyDeleteAu mmepeana Uongozi?
Tunaomba Majibu.
Michuzi, katika jamii yenye kuheshimu demokrasia na uhuru wa kuzungumza, ningekuomba utoe haya maoni yangu.
KWELI SASA NAAMINI CHAMA (CCM - UK) KIMESHIKA HATAMU ZA UONGOZI
ReplyDelete"KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI"
Watu wa Reading leo mlitaka kuharibu uchaguzi mkihofia mtu wenu hatapata nafasi.
ReplyDeleteama hakika mmejidhalilisha sana.
kuweni wastaarabu kila kitu mnataka nyinyi.
baada ya mtu wenu kupata mmeshangilia sana.mbona hajalalamika tena kuhusu Demokrasia?
ni unafiki wa wazi mlitaka kuharibu kazi nzuri ya balozi na anaondoke na doa la uchaguzi.
lakini mama kwa hekima zake aliweza kuweka mambo sawa ila leo mmemfanya awajue kweli nyinyi ni Opportunist.
Hongera mama maajar kwa kazi kubwa na nzuri hatiamye jahazi umelivusha salama.
balozi anayekuja awe makini na watu wa Reading.
uchaguzi wa leo umedhihirisha kuwa wenzetu ni chui na si kondoo kama alivyoweza kumuhadaa Balozi kwa muda mrefu.
walikuwa tayari kuvuruga uchaguzi kwa gaharama yeyote kama mtu wao hatapita.shame on you.
Mtu anakaribishwa anaanza na 'Bwana asifiwe'?
ReplyDeleteHii ni jumuiya ya Watz Uingereza au Pathfinders wa makambi ya SDA?
Aggggghk!!!
Jifunzeni, mualike viongozi wa jumuiya zingine kutoka nchi nyingine ili wawape challenges za kuachana na matawi ya akina Mahina na makundi yasiyo na faida.
Bwana asifiwe tunaikubali lakini ina mahala pake si hapo? Siku nyingine mtajazua mtafaruku usiozimika kwa salamu kama hizo pasipo husika?