Martina wakati huo akiwa na umri wa miaka 4 akiongoza wenzie kuimba wimbo wa 'Tanzania eeee' katika tamasha maalum la watoto liliofahamika kama ZECCHINO D’ORO katika mji wa Bolognia nchini Italia mwaka 1995 Hii ni sehemu ya wimbo maarufu sana ambao ulitokea kupendwa na watu wengi ndani na nje ya nchi katika miaka 1994 na 1995, wakiwemo zaidi watoto, vijana na hata watu wazima.
Nyakati hizo vituo mbalimbali vya Televisheni na Radio vilikuwa vikiupiga wimbo huo na vipo ambavyo vilikuwa vikiutumia wimbo huo kuwavutia watoto ambao walikuwa wakialikwa kushiriki katika vipindi vyao vya redio na Televisheni ambavyo moja kwa moja vilikuwa vikishirikisha watoto.
Mojawapo ni kwamba wimbo huo unasifia kwa uhalisia wake rasilimali zilizopo nchini ambazo pindi watu wakitembelea wanaweza kunufaika kuziona, pamoja na uzuri wa Taifa la Tanzania ambalo limejaaliwa duniani kuwa na vivutio vya kila aina vikiwemo mbuga za wanyama, ardhi zenye rutuba, maliasili kama madini ya thamani na kadhalika.
Tamasha hilo liliwashirikisha watoto wa umri wake kutoka nchi mbalimbali duniani na wimbo huo wa Tanzania ambao yeye alifanikiwa kuuimba ukaingia tano bora na kushika nafasi ya tatu.
Martina akipongezwa na Profesa Philemon Sarungi, Waziri wa Elimu wakati huo ambapo alikwenda kukabidhiwa bendera ya Taifa akiwa mwakilishi wetu katika tamasha la watoto. Hii ndiyo ilikuwa safari yake ya kwanza kati ya tatu alizofanya.‘’nakumbuka tulikuwa shuleni Sista akasema kuna mashindano ya kuimba, hivyo tukashindanishwa wote na mimi pale shuleni nikawa mshindi na hivyo kupata nafasi ya kushiriki katika tamasha hilo’ Anasema.
Anasema anachokumbuka zaidi ni kwamba wimbo huo ulitungwa na mwalimu wa muziki katika shule hiyo aliyekuwa akifahamika kama mwalimu Julius Kapinga, na hatimaye yeye kufanikiwa kuuimba kwa ufasaha.
Anasema wimbo huo aliweza kuuimba kwa lugha mbili yaani Kiitaliano na Kiswahili, ambapo sehemu ya kiitaliano ilitungwa na waandaaji wa shindano hilo wakiongozwa na mama mmoja kwa jina la Mariella ambaye kwa sasa ni Marehemu.
Martina katika mahafali ya kidato cha sita Shule ya sekondari Loyola na mdogo wake Lilian Chambiri (shoto) na ndugu yao. Kidato cha nne alipata daraja la kwanza pointi 14 na anasema wakati huu akisubiri majibu ya kidato cha sita anategemea kufanya vyema. Anasema kabla ya kufanyika kwa tamasha hilo ilibidi aende Italia kwa ajili ya kujifunza na kuchanganyika na washiriki wenzake ikiwa ni pamoja na kuimba kwa kupokezana kwa kuwa alikuwa akiimba Verse na wenzake wakiimba Chorus.
Anasema pia katika safari hiyo ya kwanza alikuwa akifundishwa jinsi ya kulitawala jukwaa wakati anaimba , ikiwa ni pamoja na kuzoea kuimba kwenye umati mkubwa wa watu.
Aidha anasema alitakiwa tena kurudi tena Italia kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha la wanawake lililofahamika kama Women’s Festival ambapo alialikwa kutumbuiza na kwa mara nyingine akafanikiwa kukonga nyoyo za watu wengi.
Anasema alikutanishwa na baba mmoja anayemkumbuka kwa jina la Gideon ambaye alimtungia nyimbo 6 zote zikihusu mazingira na zote zikarekodiwa na kisha kutengeneza album moja.
Kilichogundulika baadaye ni kwamba ulikuwa ni wakati ambao alitakiwa kuanza shule, hivyo mawazo yake mengi ikabidi yahamie shuleni zaidi kuliko kuimba hivyo akaanza shule ya St. Constantine iliyoko Arusha, na kujikuta alipoanza darasa la kwanza akarushwa darasa hadi darasa la tatu.
Martina akiwa na wazazi na mdogo wake LilianAidha baada ya hapo wazazi wake wakaamua kumhamisha shule hiyo na kumuandikisha shule ya St. Mary’s Tabata, na kisha kumalizia darasa la saba katika shule hiyo hiyo eneo la Mbezi Beach.Anasema pamoja na kufaulu vizuri kujiunga na shule za serikali, lakini wazazi wake waliamua afanye usaili katika shule za Marian, Kifungilo na St. Francis, alifanikiwa kupata nafasi katika shule ya Marian na kisha kuanza kidato cha kwanza na kufanikiwa kumaliza kidato cha nne mwaka 2007.
Binti huyo anasema anafurahia kuwa wazazi wake walikuwa hawamlazimishi kusomea masomo ambayo hataki isipokuwa hawakusita kumpa ushauri kwa kile ambacho yeye alikuwa anachagua kukifanya.
‘baba yangu alikuwa akipenda sana niimbe na pia nishiriki kwenye michezo, na mimi napenda sana michezo na hasa kuogelea, ila mama alikuwa akiuliza ni kwa nini nisisome masomo ya Sayansi, ila masomo ambayo nilichagua walikubaliana na mimi kisha wakaniambia niyasome kwa bidii ili niyafaulu vizuri’Anafafanua.
Martina anasema jambo muhimu ambalo anamshukuru mungu ni kumpatia wazazi ambao walishirikiana kumpatia malezi mema, na pia walimjengea misingi ya kumpenda mungu na hivyo kumuwezesha angalau kufikia sehemu ya malengo yake.
Lakini anasema katika maisha yake aliwahi kupatwa na mshituko mkubwa sana alipopata taarifa ya kifo cha baba yake mzazi mwaka jana kilichotokana na ajali ya gari huko Lindi.
‘ulikuwa ni mshituko ambao siwezi kuuelezea, baba yangu alipenda sana maendeleo yangu, na alikuwa anaeleza ni jinsi gani anajisikia fahari kuwa na mtoto kama mimi, lakini hakuna jinsi ni mipango ya mungu. Namuombea mungu ampumzish kwa amani” Anasema.
Ukifanikiwa kukutana na Martina Chambiri hutaweza kuamini kuwa ni yeye alililetea sifa kubwa taifa hili kwa kufanikiwa kupeperusha bendera ya Tanzania nchini Italia na pia alikuwa ni mshiriki pekee kutoka bara la Afrika.




du hongera dada umetoka mbali, all the best for the future and sorry about your Dad, may he RIP.
ReplyDeleteuwiiii jaman huyu mtoto ndo amekua hivyo?aisee miaka inakimbia kweli nshazeeka!anyways baangaa she can still do it.
ReplyDeleteAise ankal, ungetutaftia kijiclip kaule wimbo bwana utuwekeee kidgo. Tanzania eeeee, totomela aaaaa, akupnda fwaiiiii, sijui nininini...
ReplyDeleteAnkal, naomba uwasiliane na mama Chmabiri (mama yake Martina), ikiwezekana watoe CD na DVD ya nyimbo za Martina.. maana nimewahi kuzisikia zikipigwa katika radio..lakini kwa sehemu ndogo tu.. nadhani vema ziwe zinapigwa au kurushwa katika Tv ili watu wajue kipaji cha binti huyu.. nimeona wimbo wa "Tanzania Eh!" katika you tube.. hebu down load na ubandike watu wauangalie..
ReplyDeleteHongera Mungu akulinde akuzidishie, uendelee na juhudi zako.Ila Michuzi inaonekana story yote amesimulia mwenyewe kitu ambacho siamini kama anaweza kukumbuka yote hayo katika umri wa miaka minne, pili hajatumabia Kidato cha sita amefauru kwa kiwango gani. Otherwise kila la kheri dada.
ReplyDeleteWadau,kiukweli ni hivi karibuni tu nilikuwa najiuliza ni wapi alipo huyu binti? na yule kijana aliewahi kushinda tuzo ya muziki marekani? alitunga wimbo kwa jina la My passion.Vibaji vimepotea,je Martina alikuwa na kibaji au zali la kitoto tu?
ReplyDeleteHongera sana Martina ulifanya kazi nzuri sana. Je bado unakumbuka kiitaliano? mana kuna perfomance moja ulikuwa unahojiwa kiitaliano, na ulijibu vizuri mpaka nilishangaa.
ReplyDeleteMmh!huyu sio mdogo wake Elizabeth Chambili kweli?
ReplyDeleteDUH TANZANIA WALAHII, SIJUI CHA KUSEMA, SOMETIMES UNAZALIWA SEHEMU KAMA USINGEZALIWA HAPO, MUNGU BADO YUPO NAWE DADA, KEEP IT UP.
ReplyDeleteHaya hiyo ndiyo tanzania, vijana kama hawa ndiyo serikali ingeweza kuwasaidia na kuwaendeleza vipaji vyao, lakini serikali wala haishtuki na chochote, juu ya kwamba aliiwakilisha nchi na kuiletea sifa, sasa mnategemea kutakuwa na uzalendo wa mtu kuipenda nchi yake?
ReplyDeletehiyo ndiyo Tanzania, fadhila ya punda .......
sujaelewa kashinda tena? au ndo mnamrusha tuu?
ReplyDeleteLMAO...Hahaha!!! Anonymous wa tatu 02:07pm you had me rollin' buoy!!. Automatically siku zote mtu akisikia Jina Martina Chambiri unasikia that song playing in your head!! Amazing!. Tanzania eeeeh!! Tanzania aaaaah!.
ReplyDeleteThat's a special young lady right there....I see a very bright future ahead of you, young lady. I see her winning presidency of Tanzania, if she wants to run for it.
Kitu kingine nakumbuka Mike Mhagama, kwenye DJ Show....Ah Ah A D, Ah D, Ah Dj, Ah DJ Show!!!!
wanaotaka kuangalia video ya wimbo huu hii hapa!! http://www.wavuti.com/19/post/2009/12/tanzania-eeh-tanzania-aah.html
ReplyDeletemdau
Nkya
A town
Ama kweli kamichuzi umeniliza.
ReplyDeletewimbo huu umenikumbusha mengi yaliyonikuta kwenye maisha yangu, wakati huu mwimbo ndio umevuma sana nyumbani mie nilikuwa na matatizo makubwa sana ambayo nikitizama nyuma nacheka na kufurahi hapa nilipo.
wakati wa mwimbo huu bwana ambae aliniambia atanioa ndio alienda kuoa bibi mwingine bila ya kuniambia (kisa anadai eti mie wazazi wake wasingenikubali sababu mie mkristo) nikashtukiziwa tu wakati niko kazini na mwenzangu "hivi unajua?" "B/F wako anaoa wikiendi" nilitamani kuruka kilimanjaro hoteli ila nililia sana, mpaka niliokuwa nao jirani walidhani nitajiua.
mwaka ukapita nikampata mwenzangu mwingine ambae niko nae mpaka sasa lakini mwimbo huu umenitolesha machozi tena.
Afu jamaa mwenyewe hata hawakudumu na mkewe waliachana baada ya muda akarudi kwangu eti tuoane sasa, mie mmmmh saa hizi jioni ndio unaniona??
YAANI BAADA YA KUONA HIZO VIDEO, MACHOZI YAMENITOKA MTU MZIMA, INAUMA SAANA JAMANI, TANZANIA EEEEH, TUNAPIGWA CHINI SAAANA!!!! WHY JAMANI???? KIPI MUHIMU BASI NCHINI KWETU KAMA SIO KUWAENDELEZA TAIFA LA KESHO? KIKO WAPI SASA?!
ReplyDeleteMmmmh!
ReplyDeleteJamani watoto wa siku hizi- wa dot com wanakua haraka!
Khaa!
Hongera sana dada.
ReplyDeleteMungu akubariki sana.Vipi kanisani huwa unaimba kwaya?
Ukifanya hivyo Mungu atakubariki zaidi na zaidi.
Hongereni baba na mama wa Martina,inaonyesha malezi yenu ni safi.
Martina, Mungu akubariki uzidi kukuwa katika kimo na hekima umpendezaye yeye na wanadamu wote wakupende ingawaje ni vigumu, nakutakia heri katika maisha yako. pole kuhusu baba yako.hii dunia ni njia ya kupita tu. uwe na maisha mema.
ReplyDeleteSafi sana! Ni vizuri kuona Martina anaendelea vizuri. Hapa USA wanamwita 'CHILD STAR'.
ReplyDeleteMwaya wasikudanganye dadangu, lile lilikuwa zali la utotoni, bukua mwanetu upate nondo ndo uanze sijui bongo fuleva, so far bado mdogo, ukumbuke hukusoma darasa la II na hata hilo la I ulirushwa tu, usije rudi utotoni kwa kuruka staji moja muhimu. Nasema hivi, soma. Wakware weshakuona, mate nje nje. Utaishia kuuza magazeti ya Udaku sasa hivi.
ReplyDeleteMpg Bx
TeQuann
ReplyDeleteAma kweli wewe ni mswahili sana manake mtu kama Martina Chambiri hata hakukaribishwa na raisi kwa mlo wa ain yoyote lakini alifanya kututangaza sana mie binafsi namshukuru sana.
Haya kaja Hashim hata ushindi hajaleta nyumbani lakini mikiki yote mlimfanyia, sasa ona. Yote hayo ninakushangaa wewe Tequanne kuandika mambo kama hayo wakati Martina alifanya yote haya kwa mapenzi yake sio kutaka kuwa celebrity wala nini.
Go crawl under a rock or something mstzzzzzz shukrani huna.
Martina keep your head up wewe ndio watu tunaokupenda manake unatutangaza bila ya kudai chochote.
Go Martina go
Mdau California.
Kingwedu Jr
ReplyDeleteManeno yako ni ya kweli kabisa manake watu huku wanataka mtu kama vile Hashim, hata kombe hajaleta ila vishindo hivyo mmmh wakati martina anatangaza tu jina bila ya kutaka chochote.
Jamani wadau wenzangu andikeni kwa lugha ya taifa viingereza vyenu havieleweki. Hata kama mnaishi ulaya inayonyesha wazi bado mnahitaji kupolish lugha za wenzetu.
ReplyDeletehuyo mtoto ni talent sana hakuna asiyejua kama alitanga sana tanzania na kusimama kwake jukwani kulichangia kushawishi watalii kuja tanzania kuviona hivyo vivutio,lakini mambo ya TZ jitoe wengine waneemeke, kimtazamo zawadi kubwa ambayo serikali wangempa huyo binti ni offer ya kumsomesha bure tena katika shule yoyote aitakayo any way ndiyo nchi yetu na sijua hata kama mwalimu aliyewashiwishi watoto kuingia katika shindano hilo kama alipewa motisha yoyote au ndiyo iliishia hapo,jamani serikali oneni aibu in my memory huyu mtoto alichangia kushawishi watoto wengi kuonesha vipaji vyao hususani vya uwimbaji,nguzo yake moja imeondoka msaidieni asome.
ReplyDeleteshe was so cute ohhhhhhhhh my Lord look at her now i cant beleave, she is so big and still cute God bless u ma lil sister keep it up and dont give up,sorry about ur dad keep on praying for him its all about god ndio mambo ya dunia alilo panga mungu haliwezi kupanguka but dont give haters chance 2 come near u
ReplyDeleteHuu wimbo sikuujua ...kipindi hicho ndio niliondoka kuja kuanza masomo huku. Hivyo nikapitwa nao...Ila tuwe Simon cowell. Mimi kwa kuusikiliza huu wimbo nimeona mtotot huyu alikua hana haibu na hilo ndio lilimsaidia lakini sauti ya kuimba nyimbo kweli hana. Afadhali uliamua kusoma na huwezi jua hizo nyimbo zingine zilizotungwa na sauti yake kupotelea somewhere ni kwavile huyo producer aliona quality haikua kama alivyotegemea.
ReplyDeleteKazana na elimu na ujasiri wako utakufikisha mbali...Mimi ningekuambia uwe lawyer...Unaonekana kama unaweza kusimama mbele ya watu na kuongea saana
Pole kwa matatizo ya yaliyokukuta. Hata mimi nilipoteza baba yangu miaka michache iliyopita na kila nikiwa nafanya tukio muhimu natamani angekua hapa aone mafanikio yangu. Lakini nahisi ndio yeye anawork upstairs for me....
Mdau wa California
ReplyDeleteKha! we vipi, mbona kunishambulia bila sababu ati?. Hebu rudi juu ukasome comment yangu tena kwanza. That was all praise!. I started with LMAO niki refer comment iliyotolewa mwanzo. Where did Hashim get into this? LOL
Again I say, and I quote what I wrote earlier:
"That's a special young lady right there....I see a very bright future ahead of you, young lady. I see her winning presidency of Tanzania, if she wants to run for it.
"
Nothing but LOVE.
jamani nimekumbuka mbali wakati huo nakula bure kwa baba na mama mambo super cjui kutafuta hata hela. niko shule leo najitafutia maisha mtihani natamani kurudi nyuma kuwa kama mtoto tena nile bure nivae bure nikiumwa nilie baba anikumbatie yaani mpaka nimelia.kip it up martina
ReplyDeleteJamani kweli huyo mtoto ni cku nyingi sana, ila nimepotezana na Aunt yake long time anaitwa Gati Chambiri, ningependa sana nipate namba zake za simu kama itawezekana, mi ni rafiki yake wa cku nyingi sana sema tu tulipotezana....
ReplyDeleteMdau
Kaka michuzi umenikumbusha mbali sana,nilikuwa nataka kujua kwa muda mrefu sasa habari za Martina,wakati huo huu wimbo ukivuma sana nilikuwa form 3 naenda form 4.Nilikuwa naupenda sana.
ReplyDeleteNimefurahikufaham habari za Martina Chambiri tena na jinsi anavyoendelea.Nafikiri kama inawezekana tumwone tena kwenye tv atusalimie watanzania pia atupe au atukumbushe kipaji chake,hata wale ambao hawakumwona wapate kumwona.
Umenikumbusha sana mbali Kaka Michuzi.
Itabidi niwatafute wadau wa FORM4C1 1997 JITEGEMEE SECONDARY tukumbukie zile enzi.