Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akimwelekeza Abdalah Juma namna ya kutumia kompyuta ambae ni mwanafunzi wa sekondari ya Mnolela iliyopo lindi vijijini ambapo Vodcom Foundation ilitoa msaada wa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi milioni 15.

Mkurugenzi wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi wa Mnolela iliyopo lindi vijijini namna ya kutumia kompyuta ambapo Vodacom Foundation ilitoa msaada wa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi milioni 15 katika shule hiyo na ya Mtama zote za lindi vijijini.
Mkuu wa mkoa wa Lindi Said Magalula(katikati)akimkabidhi moja kati ya kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi milioni 15 Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Mnolela Bahia Abbakari(kushoto) mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Mkurugenzi wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba anaeshuhudia.
Baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya Mnolela iliyopo lindi vijijini wakiangalia namna ya kutumia kompyuta mara baada ya kukabidhiwa msaada wa kopyuta 20 zenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Vodacom Foundation. Mkurugenzi wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba akifurahia jambo na baadhi ya wanafunzi wa Mnolela iliyopo lindi vijijini ambapo Vodacom Foundation ilitoa msaada wa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi milioni 15.
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia Mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation, umetoa msaada wa Kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 15 kwa shule mbili za Sekondari Mtama na Mnolela zilizoko Lindi Vijijini ili kuboresha sekta ya Elimu katika shule hizo.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi Saidi Magalula, Mkurugenzi wa Mfuko huo Mwamvita Makamba alisema kwamba msaada huo ni mwendelezo wa awamu ya tatu ya Mradi wa Ugawahi kompyuta kwa shule za sekondari za vijijini. Katila awamu ya kwanza na ya pili jumla ya shule 30 kutoka mikoa tofauti 15 zilifaidika katika mradi huu.

Alisema huu ni mwanzo tu kwani Vodacom Foundation itaendelea kutoa misaada ya kompyuta katika shule za mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwa unalenga kutoa wimbi la uduni wa kompyuta na kuinua elimu na kuisaidia serikali kama sekta binafsi siyo kuiachia serikali pekee lazima tuwe pamoja kuendeleza misingi iliyobora ya elimu.

Naye Mkuu wa Wilaya, akipokea msaada huo aliishukuru kampuni ya Vodacom kupitia mfuko wake huo na kusema sera ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kutoa misaada mbalimbali ya kuiokoa jamii kama Vodacom ni mfano wa kuigwa na mashirika mbalimbali ili waweze kuisaidia serikali na wananchi wanaopatwa na upungufu wa vitu muhimu katika jamii.

“Serikali imeweka sera nzuri za uwekezaji ili kuhakikisha kwamba uwekezaji una kua na wawekezaji pia wanapata fursa ya kuchangia maendeleo ya sekta ya kijamii nchini’

Alisema hivi sasa bila teknolojia ya kisasa amna maendeleo na alichukua frusa hiyo ya kuwaasa wanafunzi wazitunze kompyuta hizo na kuzitumia vizuri kwani wameunganishwa na ulimwengu wa teknolojia ya kisasa na kuwasihi wasitembelee katika tovuti zenye mambo yasiyofaa na ambayo hayana manufaa kwao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. halle berryMarch 21, 2010

    mwamvita umetoka mchicha ndani ya Michelle Obama look! well done vodacom, at least mmeanza kutoa misaada pale inapostahili, ambapo matunda yake ni mema na sio ku obsess na kumwaga mihela kwenye mamiss pageant,.

    ReplyDelete
  2. ANKAL MAMBO YA FULANAZZZZZZ YAMESHIA WAPI? BANDIKA MAJINA BASI TUJUE KAMA TUTAPA FULANAZZZZZ AU PATUPU.
    MDAU
    KISIJU
    PWANI

    ReplyDelete
  3. msimsahau huyo mtoto aliyekaa chini hapo karibu yenu msaidieni viatu jamani, inasikitisha hadi leo tuko tusioweza kununua viatu na kuna wenye magorofa sita na bilioni sijui ngapi

    ReplyDelete
  4. nyinyi Voda sawa mnatoa Computer lakini huko vijijini, mmepeleka waalimu wa hizo computer... ni sawa na kuumpa mkulima Trekta bila Mafuta, si bora abaki na jembe

    ReplyDelete
  5. kwa jinsi ninavyofahamu shule za bongo,hizo computer zitafungiwa na wanafunzi hawatafaidika na chochote.

    ReplyDelete
  6. Hiyo picha ya chini imenisikitisha sana. Hebu angalia huyo mtoto hapo chini aliyekaa. kwanza utajua yuko mbali sijui anawaza nini masikini.

    Tanzania watu wanaishi maisha tofauti sanaaaaa.......

    ReplyDelete
  7. Huyo mtoto ungeli msalimia angalau uka mpatia pesa ya viatu izo Computer azimsaidii kitu chochote uyo mtoto.huyo mtoto anaonyesha ata shule aendi tazama kwanza mwenyewe ajavaa sare zashule wala viatu ana.jamani tusi zielekeze pua zetu juu tazana aliekua chini yako na pembeni yako pia!

    ReplyDelete
  8. watanzania mlivyo wanafiki, mbona sijaona malalmishi ya hiyo sikrini waliyotoa Vodacom kama watu wengi mlivyolalamika skrini namna hiyo ilipotolewa zawadi na Clever Tours Management college? au kwakuwa vodacom jinakubwa! maonai ya leo ndiyo ya busara..kompyuta ni kompyuta hata sie ulaya tunatumia hizo za kisogo na TV za kisogo bila shida..

    ReplyDelete
  9. ....jamani mtanisamehe...kwanza voda wanafanya kazi kubwa sana kuendeleza jamii yetu na hii dili ya kuleta technologia mashuleni ni muhimu mno saaaana...ila jamani bado wanatupa CRT monitors? mnajua kwanini...hizi ndo zinazotolewa Ulaya na Marekani kuja ku dump tanzania/africa sio vizuri hawa wazungu wanaua mazingira yetu kama yao walivoyaua miaka mingi sasa
    SAY NO TO CRT kama wanataka kutuletea computer watupe LCD

    ReplyDelete
  10. Da Mwamvita jama ni mzuri!!. She's a total package....Brains, Body, Heart Mashallah!!, kisha anajua kuvaa sasa. I give her a perfect 100%. Halle Berry ain't got nothin on you Sista.

    ReplyDelete
  11. MAKUBWA YA HALLE BERY NA Mwamvita WAPI NA WAPI?HINA HUU?

    ReplyDelete
  12. Wewe kama unakaa Ulaya hukohuko kwenu sisi tunazungumzia hizo kompyuta hazina maana bila waalimu na nyie mnao zongumzia komputa za vichogo waambieni wahindi na wachina ndo waziondoe maana hao ndo wauzaji msiwasingizie matasha.

    ReplyDelete
  13. Hongera sana dada Mwamvita,Lakini na sisi tunasubiri awamu yetu mtukumbuke. Mwanakijiji - MDIGWA, kijijini Chole Samvula.

    ReplyDelete
  14. Voda asanteni kwa "MISAADA". Ila siku nyingine muangalie hizo zawadi mnazozitoa kama kweli mnazitoa kama zinaendana na teknolojia. Kompyuta-tumbo zimeshapitwa na wakati jamani. Mwamvita umesikia?

    ReplyDelete
  15. HUYU MWANVITA KAOLEWA?JAMANI KUULIZA SI UJINGA KWANI PROBABLY SHE IS UP FOR GRAB i.e AVAILABLE.PLEASE WHOEVER THAT HAS SOME INFO LET ME KNOW COZ I WANNA GO SEE MZEE MAKAMBA...SERIOUSLY OR IF MWANVITA HERSELF IS GONNA READ THIS THEN WIRE ME UP @ gyundad@yahoo.com

    ReplyDelete
  16. Ankal waosha vinywa hawakosi la kusema!!ingekuwa hizo mashine hazijawashawa wangesema hizi skuli hazina stima!Na inasikitisha watanzania wenzetu wa huko ughaibuni hawaamini kabisa kama kuna waalimu vijijini ambao wa basic knowladge ya computer.

    Pia inasikitisha hao hao wa ulaya wanaishia ku criticize juhudi za wadau hapa nchini na wao hawafanyi lolote kuchangia juhudi hizi,wanaishia kutaja LCD tu!!

    Hawa watoto wanahitaji computer ya aina yeyote ile ili wapate furasa ya kujifunza nao waje kubeba mabox huko hulaya jamaniii!!!!!hongereni sana Vodacom Foundation.Hawa waosha vinywa wasiwavunje moyo.

    ReplyDelete
  17. shoshtito umenona!!!

    wee mdau unaetaka kuoa makubwa utayaweza weweee?oohoooo shauriro

    ReplyDelete
  18. IF YOU HAVE DETERMINATION AND FOCUSED ON WHAT YOU WISH YOU COULD GET THEN GO FOR IT,SO MDAU WHO SAID UTAYAWEZA,YES I WILL MDAU,I MEAN IT AND I WANNA PURSUE MY WISH ONLY IF SHE IS SINGLE PLEASE

    ReplyDelete
  19. KAOLEWA TENA NA MTHUNGUUUUUUUUUU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...