Ankal akila konozzz na Mh. Balozi Mwanaidi Sinare Maajar wakati wa Diaspora 2 jijini London. Ankal alibahatika kukutana na wadau kibao wa Globu ya Jamii na anawashukuru wote kwa mapokezi mazuri na moyo wa furaha kila aliyekutana naye. Ankal pia anatoa shukrani za dhati kwa Balozi Mama Maajar sio tu kwa kwa kumualika London kuhudhuria Diaspora 2 akiwa kama bloga bali pia anatoa asante sana kwa Balozi huyu mchapakazi kwa kuutambua umuhimu wa libeneke blogs pamoja na social media zingine na kuwa mstari wa mbele kuzifanya zitambulike kama vyombo vingine vya habali. Ankal anamshukuru pia mfadhili wa tiketi yake ya ndege ambaye hakupenda kutajwa, anamwombea abarikiwe na apate zaidi kwa moyo wake wa upendo
Mh. Balozi Mwanaidi Sinare Maajar akiwa na Sakina Datoo (shoto) na Joyce Kisaka, wanahabari waandamizi ambao wako hapa UK kula nondozzzz zaidi
Balozi akiwa na Charles Hilary wa BBC (kulia) na mdau wa Uhamiaji aliyekuja kutoa mada Diaspora 2
wadau wajasiriamali wakiponesha vitu vyao katika Diaspora 2
Toka shoto ni Joyce Kisaka, Sakina Datoo, Charles Hilary, Israel Saria na Vicky Msina
ankal akila pozi na baadhi ya wadau wa ukerewe
wadau wa ubalozini kwetu UK wakiwa tayari kuhudumia wahudhuriaji wa Diaspora 2
Ankal akiwa na Sidi Kikenya (kati) mmoja wa
wachezaji nyota wa basketball enzi hizo na mdau
ankal akiwa na mwasisi wa Bongo Fleva Saleh Jabir ambaye ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza Tanzania kuimba hip hop kwa kiswahili na kuwasha moto kwa wasanii wengine kufanya hivyo na hatimaye Bongo Fleva kushika hatamu.
ankal na mdau wa Birmingham Godwin Kaganda anayekula nondozzz yake ya PhD
ankal na wadau wa libeneke
wadau wakiwa na ankal
ankal na wadau
ankal akiwa na mdau Ralph Godden wa Manchester ambaye ndiye mwanzilishi na mwendeshaji wa libeneke maarufu sana la http://www.babkubwa.com/
ankal na wakongwe wa ukerewe
ankal akiwa na mzee Kishor Thakrar na mdau
ankal akikabidhiwa kitabu cha kujifunza ujasiriamali na mtunzi wake
wadau wakuu wa http://www.ailtv.com/ ikiwa ni pamoja na kaka Freddy Macha (kulia)
mdau Gloria Mtahanamilwa akichangia hoja wakati wa Diaspora 2
wadau wa Diaspora 2 wakiwa na mchezaji nyota wa zamani wa Yanga enzi hizo Yanga Fadhili Bwanga (shoto) aliyetoka Abu Dhabi mahsusi kuhudhuria mkutano huu
Naibu Balozi Mh. Chabaka Kilumanga akiwa na wadau
ankal akiwa na kikosi kazi chote cha Sporah Show.
LIBENEKE OYE!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Mzee wa Libeneke hongera.

    Kitu kimoja cha ajabu hawa watu wote na akili na wider worldview zao walishindwa kulaani kitendo cha kuanzisha matawi ya kisiasa London?

    Basi imekula kwao!

    ReplyDelete
  2. Mpaka Uk, zengwe la uchaguzi wa kajumuiya tu nao ulikuwepo.

    Eti search Commitee!

    kwikwikwi!!!


    Hivi kweli hii diaspora ina lengo gani kwa undani?

    kwa nini wasialikwe na wawakilishi wa nchi nyingine za nje?

    ReplyDelete
  3. Duh!
    Michuzi kweli sikuwezi, yaani konozzzzz mpaka kwa mweshimiwa balozi! Khaah!

    Lakini mbona suti zako zote ni za rangi moja jamani?

    ReplyDelete
  4. Michuzi nasikia uliprizent pepa?

    Uliweza kujibu maswali lakini?
    Au uli prizenti tu na kuingia mitini?

    Maana kuprizenti si kazi, kazi kujibu maswali babake.

    Maana prezenteshen si unakuwa umejiandaa? Lakini maswali ya papo kwa papo unakuwa hujajiandaa.

    Inakuwa ekskyuz mi, padon, kam agein nyingiii!

    Tehe teh tee te!

    ReplyDelete
  5. Mimi nilijua Ile Tshirt ya Uchawi inamwisho wake. Kumbe Anka alivunja sanduku huko ukerewe..Unaona anavyotoka fresh na hii suti yake ya Kwa Fundi Kadago...safi sana,
    Ila pia ankal una bahati umejieleza kuwa ulifadhiliwa tiketi ya ndege mimi nilishaanza kufikiria namna ya kukujumuisha na mafisadi waliochezea hela zetu kutaliii Ukerewe...leo nasitisha mashtaka,
    sasa ukirudi DAR utue ukiwa umetinga hiyo suti.

    Sasa baada ya diaspora 2. diaspora 3,4,5,6... zitafanyika wapi ?? China, Malaysia, Burundi, Rwanda, Kenya, Afrika kusini, Misri, Brazil, Marekani,uganda....Nazo pia mtachoma vidola vyetu kwenda huko!
    Bongo tambarare

    ReplyDelete
  6. kaka uliotuwakilisha tunaomba tuone clip ya hotuba/presentation yako. huko ukerewe

    ReplyDelete
  7. naona Allan Kalinga na mkewe wamevaa mavazi wa wastaarab,acheni basi kuuza pombe mje kwenye dini ya Allah,yeye ni msamehevu na mwenye huruma kwa waja wake.

    Makame umeuza sura,si mbaya kaka,iaonesha watu wa readig mpo pia.

    ReplyDelete
  8. Kudadadeki,kama ni kuuza sura ankal safari hii umeuza,KONOZI pia za kumwaga.

    ReplyDelete
  9. MBONA ANKO HUJAWAPIGIA ZE FULANAZZ? WANGEKUKOMA WENYEWE.KILA MDAU ANGETAKA KUPIGA PICHA NA ZE FULANAZZ

    ReplyDelete
  10. AMANI IDDIMarch 28, 2010

    JAMANI WADAU HEBU JARIBUNI KUJIULIZA HUYU JAMAA MICHUZI VIPI MBONA ANAPENDA SANA KUKUMBATIA KUMBATIA WANAWAKE WA WATU OVYO? AU NDIYO KESHAINGIA ULAYA KWA HALI HIYO MAMBO KIULAYA ULAYA? LAKINI MJANJA MKE WAKE YEYE ANAMFICHA.

    ReplyDelete
  11. Candid ScopeMarch 28, 2010

    Mtindo wa Mavazi ya mchi za magharibi ndo wa kujivunia. Ningekuwepo hapo na kuvaa nguo za uamaduni wa kiafrika ningeonekana si mshamba tu ila nimepungukiwa na kitu fulani kichwani mwangu, hivyo ningelazimika kwenda wanakoazimisha nguo hizo kuondoa aibu, ili mradi kitanzi kinaning'inia shingoni.

    Kati ya wote waonekanao katika picha sijaona mwanaume na akili zake kuonyesha kujivunia ya kiafrika isipo kuwa kunaonekana wanawake kadhaa wamedhamiria kuondoa khofu ya kuona mnukio wa miondoka ya matindo ya mavazi ya kiafrika wamejivunia bila khofu. Walai wanawake wametuzidi kete wanaume kwa mtazamo wangu.
    Mungu Afrika

    ReplyDelete
  12. wazanzibari wako wapi jamani wote machogo chogo au kazi yao kupepeta midomo hawa wazanzibari na kwenda kwenye maharusi makubwa makubwa na umbeya na taaraba kwa sana ndo walicho nacho.

    machogo wanakushindeni kila leo na ndo maana hawataki kukupeni nchi yenu kwa sababu hajui mambo,vichwa vinu vitupuu kama upupu.

    michuzi posti comment yangu mkuu usibaniye

    ReplyDelete
  13. Mdau Godwin Kaganda yuko juu. Tunasubiri nondoz zako darasani IFM na pengineko.

    ReplyDelete
  14. Msaada kwenye tutazz ankal...jamani ningependa kujua maana hasa ya hii diaspora na lengo na madhumuni yake...ningeshukuru kwa kutolewa ushamba.

    mdau Arusha

    ReplyDelete
  15. Ankal amependeza na suti yake hiyo.Je fulana yake kaiacha wapi.Ankal usiivae tena fulana hiyo maana kila sehemu hapa TZ ni fulana hiyohiyo.Ha ha ha aa

    ReplyDelete
  16. DIASPORA NI AINA YA DAWA INAYOTULIZA MAUMIVU.

    ReplyDelete
  17. mdau wa 01:17:00 AM
    mbavu zangu zinauma sana nimecheka kweli watu mmepinda sana lol!

    ReplyDelete
  18. Mbona sioni wahindi? Nakumbuka tulivyokua tunakwenda kubadilisha passiport wahindi walikua wengi kuliko siye wenye asili yetu. Au wao vipaji vyao havihitajiki bongo?

    ReplyDelete
  19. Congrats Mithupuzzz!!!
    Kwanza kwa kuweka pamba kiuhakika, mwisho wa fulanaaaazzzz!!

    Pili, konoozzz unanikosha sana mzee
    na nashukuru kwa bango la Mbeya Highlands

    ReplyDelete
  20. ankal, nimefurahi sana kumuona Saleh Jabir. ile albamu yake ya Swahili Rap ilikuwa moto wa kuotea mbali.

    Nakumbuka enzi hizo dingi mnoko aliposikia swahili rap akasema hili toto litaharibikiwa badala ya kusoma linasikiliza ujinga. Akanipora na kuipondaponda kwa nyundo.

    Lakini kachaa nikaenda kununua nyingine na nikaificha mbali kabisa, dingi akiwa hayupo ndio tunasikiza.

    Ukiweza fanya mahojiano na Saleh Jabir wadau wake tujue kapotelea wapi na anafanya nini kusukuma gurudumu la maendeleo.

    ReplyDelete
  21. Lengo la hiyo dia-kiporo ni matumizi ya pounds za uingereza.
    Kazi kweli kweli!! Watanzania tumelala!

    ReplyDelete
  22. UNCLE MICHUZI SALAAM WALLEHIKUM, NIMETAKA TU KUKUSIFIA JINSI ULIVYOPENDEZA YAANI! UMEPENDEZA KULIKONI HATA HAO WANAOISHI HUKO LONDON, HIYO SUTI YA BROWN NA TAI YA PURPLE UMEIPATIA KWELI NA SHATI LAKO MWENYEWE UKO JUUUU BRO....VERY SMART! GOOD JOB MICHUZI...ASANTE KWA KAZI BORA KAKA...

    ReplyDelete
  23. picha #13 toka juu
    SHOSE????!!!!! mmeo yuko wapi?
    si mchezooo hahahaaaa

    na uyo jamaa wa udsm nani sijui jina limentoka,hahahahaaa picha #2 chini

    akhaaa vijana/wamama mmetulia si haba wal'ahi

    ReplyDelete
  24. konozzzz michu apo mwake umepatia kweli!!

    sina mbavu izi picha:DIASPORA NDO NYIE?

    ReplyDelete
  25. HUYU DOGO SALEH JABIR NAMKUMBUKA... ASIPENDE KUJIKWAZA!!! MUULIZA ANAMKUMBUKA HAYATI ADILI KUMBUKA NA D-ROB (ROBERT) HAO NDIO WAANZILISHI WA BONGO FLAVA KWA KUNDI LA 'KWANZA UNIT' KULIKUWA NA WATU KAMA 'RHYME-SON' ANAWAKUMBUKA HAWA? WALIKULA SHAVU LA KU-PERFORM ZANZIBAR KUIPIGIA DEBE CCM, ENZI HIZO KATIBU MKUU NI HAYATI HORANCE KOLIMBA. MENEJA WA KUNDI ALIKUWA DWEZA!!!! MWAMBIE DOGO YEYE ALIKUWA WA NNE AU WATANO... AWAPE HESHIMA ZAO AKINA ADILI NA D-ROB.

    ReplyDelete
  26. http://www.youtube.com/watch?v=mT2DwfJUD5M

    just watch

    ReplyDelete
  27. aaaaa ankali we ni wewe au yaani hizo suti umetoka ile mbaya na shati la ko la pinki nakufagilia wawawwa,ila mikonozzz imezidi kwa wake za watu wako mmmmmmmmhhh. pia mimi hiyo dispora siielewi naomba ufafanuzi balozi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...