JK akiongea kwenye hafla hiyo
JK akiwa na Kiongozi wa KKKT Askofu Dk. Alex Malasusa (kulia kwake), Waziri wa Elimu ya Juu Profesa Maghembe (kuume) na Askofu wa KKKT Dayosisi Kuu ya Magharibi, Elisa Buberwa (shoto kwa JK) wakati wa hafla hiyo
JK akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh. Milioni kumi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha mahusiano wa benki ya NMB, Shy-Rose Bhanji kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu kishiriki cha Josiah Kibira (JOKUCO) kinachotarajiwa kuanzishwa mwishoni mwa mwaka huu mkoani Kagera. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall jijini Dar wikiendi hii.
JK akimkabidhi picha ya kuchora Mkurugenzi Mkuu wa Cargo Stars, Bw. Jamal Malinzi, baada ya (Bw. Malinzi) kuinunua kwa shilingi milioni kumi katika mnada wa kuchangia Chuo Kikuu cha Josiah Kibira (JOKUCO) kilichopo mkoani Kagera. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Diamond jubilee hall wikiendi hii. Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii

KKKT YAUSIFU UONGOZI WA JK

Kiongozi wa Kanisa la Kikristo la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dk. Alex Malasusa ameusifia na kuupongeza uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa dhamira, vitendo na mafanikio makubwa katika sekta ya elimu yaliyopatikana chini ya uongozi huo.

“Tunaipongeza sana Serikali yako, Mheshimiwa Rais, inavyojali umuhimu wa Watanzania wengi zaidi kuzidi kupata elimu. Ni nia ya KKKT kuendelea kushirikiana na Serikali yako katika kuendelea kutoa huduma za elimu nchini,”Askofu Malasusa amemwambia Rais
Kikwete.

Askofu Malasusa alikuwa anazungumza kwenye chakula cha jioni cha kuchangisha fedha za kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Josiah Kibira mjini Bukoba, shughuli iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond mjini Dar Es Salaam, usiku wa jana, Ijumaa, Machi 13, 2010.

Rais Kikwete aliongoza uchangishaji fedha wakati wa chakula hicho na kiasi cha sh 706, 560, 000 zilichangwa kwa ajili ya uanzishaji wa chuo hicho kitachokuwa chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini kinachomilikiwa na KKKT.

Akizungumza kabla ya kuanza uchagishaji, Rais Kikwete naye alilipongeza Kanisa la KKKT kwa mchango wake katika elimu, na kulihakikishia kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana nalo katika kutoa huduma ya elimu.

“Tunathamini sana mchango mkubwa wa KKKT katika utoaji wa huduma mbali mbali za jamii kwa wananchi, na hasa elimu.”

Rais Kikwete pia alirudia ahadi ya Serikali yake kuwa itamwajiri kila mwalimu, na hasa walimu wa masomo ya sayansi, wanaohitimu elimu ya ualimu kutoka vyuo mbali mbali, ili kukabiliana na tatizo la walimu katika shule nchini, hasa za sekondari.

“Sisi katika Serikali tutamwajiri kila mwalimu…yoyote atakayehitimu elimu ya ualimu anaweza kujihesabu kuwa tayari ameajiriwa. Hii ndiyo ahadi yetu. Ninayo ahadi na walimu katika kuwapatia ajira. Yoyote anayehitimu tutamchukua,”alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete pia alilipongeza Kanisa hilo kwa kuamua kukipa chuo hicho kikuu jina la Josiah Kibira ambaye alikuwa Mwafrika na Mtanzania wa kwanza kuongoza shirika la makanisa duniani la World Federation of Churches.

“Wote tumesikia habari kuhusu mwana-Kagera na mzalendo huyu. Alikuwa mwalimu, mchungaji, askofu na mwanaharakati wa elimu na maendeleo ya jamii. Habari zake zinatuhamasisha kufuata nyazo zake,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“ Askofu Kibira alikuwa schoolmate wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere shuleni Tabora mnamo miaka ya 1940. Wanafanana. Na fikra zake za kizalendo, hasa kuhusu elimu na ukombozi wa kiroho na kiuchumi, zinashabihiana na za Mwalimu Nyerere. Yeye, kama Mwalimu Nyerere, hata kama hatunao sasa, tutaendelea kuwakumbuka kwa mchango wao katika kuijenga na kuiendeleza nchi yetu.”

Wakati wa mnada wa picha kwenye uchagishaji huo wa fedha za kujenga chuo hicho, picha ya Rais Kikwete ilinunuliwa kwa kiasi cha sh milioni 16.5, picha ya Askofu Kibira ilinunuliwa kwa sh milioni 6.3, picha ya Mwalimu Nyerere ilinunuliwa kwa sh milioni tatu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. HAYO NDIO MAENDELEO SIO KILA SIKU KUGOMBANA NA UDINI KAMA NIGERIA TUANZISHE VYUO WATU WASOME

    ReplyDelete
  2. kwanza boresheni vyuo mlivyonavyo si kufungua utititli bila vifaa na walimu. period

    ReplyDelete
  3. Lutheran hongereni sana,sema mnaenda polepole sana. Kweli mnashindwa kufungua vyuo vikuu kila mkoa? Mnashindwa kutafuta waalimu wanaotosha na wenye viwango vya kutoa elimu nzuri na kwa bei nafuu kwa watanzania mpaka wanauawa huko India?
    Je mmesahau kuwa biblia,inasema mshike sana elimu na wala usije ukamwacha aende zake?

    Tunataka vyuo vikuu vya kutosha kutoka kwa mashirika yote ya dini na hatutaki vita.

    Mdau,
    Pigaboksi,Norway

    ReplyDelete
  4. hongera JK kwa kuwa mstari wa mbele katika kuchangisha pesa kwenye sekta ya elimu

    ReplyDelete
  5. Mkurugenzi wa Tanzania House Of Talent (T.H.T) Bw. Ruge Mutahaba amemtaka Mkurugenzi wa Deiwaka Production Bw. Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II a.k.a Sugu amwombe msamaha dhidi ya tuhuma zilizotolewa juu yake kuhusiana na kampeni ya Malaria No More.

    Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mchana Mikocheni jijini Dar,Ruge Mutahaba amesema kuwa amempa Mr II masaa 72 ili aweze kumuomba msamaha/radhi dhidi ya shutuma ambazo amezisambaza dhidi yake kuhusiana na sakata hilo la Malaria No More


    "Kiukweli nimeamua kuwaita waandishi wa habari ili niweke sawa haya mambo, mimi nilipewa tenda na kampuni ya Roundtrip kusimamia upande wa wasanii, jukwaa pamoja na`kusimamia mambo mengine hilo ndiyo lilikuwa jukumu langu mimi kama mimi,haya mambo mengine yanazungumzwa juu yangu sijui yanatoka wapi,hivyo namuomba Mr II aniombe radhi/msamaha kwa vyombo vile vile vya habari alivyovitumia kunidhalilisha mimi na kunivunjia uaminifu kwa jamii ninayoiongoza"alisema Ruge Mutahaba.

    ReplyDelete
  6. Malinzi bado upo? Duuu...kila mahali hukosekani?

    ReplyDelete
  7. Kaka Michuzi

    Asante kwa habari njema za University mpya mkoani Kagera. Tunaomba picha nyingine pamoja na events nyingine zilizotokea usiku huo.

    Denmark

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...