Video ya tukio hilo leo

kuna kila dalili leo mishahara ya kina nanihii itachelewa....
Umati wausanyika Bank House ambayo inafuka moshi mweupe toka ghorofa la pili

moshi mweupe ukifuka Bank House

wanahabari wakiwa kazini

wateja na wafanyakazi wakiwa nje

lango kuu limefungwa
wadau wakiwahi chao...

HABARI ZIMETUFIKIA SASA HIVI KWAMBA JENGO LA BENKI YA NMB KWENYE MAKUTANO YA BARABARA ZA PAMBA NA SAMORA AVENUE MAARUFU KAMA BANK HOUSE LIMESHIKA MOTO KWENYE GHOROFA YA KWANZA NA KUZUA KIZAAZAA KWA WATEJA KUTOKA NJE MKUKU KUOKOA MAISHA YAO MARA KING'ORA CHA MOTO KILIPAONZA KUPIGA KELELE.

RIPOTA WA GLOBU YA JAMII ALIYE SEHEMU YA TUKIO ANASEMA MOTO HUO UNASADIKIWA ULISABABISHWA NA CHECHE ZA WELDING INAYOFANYIKA SEHEMU MOJA YA GHOROFA HILO AMBALO LIKO KATIKA UKARABATI MKUBWA.

RIPOTA WETU ANASEMA SHUGHULI ZA BENKI ZIMESIMAMA KWA MUDA NA WATEJA WANAOTAKA HUDUMA WAMEGANDA NJE NA GARI YA ZIMAMOTO IMEWASILI MUDA SI MREFU ULIOPITA, INGAWA MOTO UMEWEZA KUZIMWA NA WALINZI NA WAFANYAKAZI WA BENKI NA HAMNA MADHARA YALIYORIPOTIWA HADI SASA. TASWIRA ZAJA PUNDE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kaka hayo ni mazoezi kwa ya ajili ya kupima uharaka katika majanga ya moto kwa vikosi vya zimamoto na wafanyakazi wa maeneo husika.Hakuna hatari kihivyo.

    ReplyDelete
  2. Sasa huyo mwanahabari anaandika kwenye viganja!!!!??

    ReplyDelete
  3. we anon.02:37:00 sasa unataka kuwa kama Tomaso mpaka ushuhudie wewe mwenyewe ndiyo uamini jengo lilikuwa linaunguaa?

    ReplyDelete
  4. Very poor safety coordination. imagine if this was the real tragedy, despite all sign of fire hazard, wadau were allowed to go inside the building. There were no Firemarshall been seen to help in evacuation. Plain cloth Policeman is seen standing there doing nothing! Very long way to learn

    ReplyDelete
  5. Jamani jamani watanzania wenzangu tujifunze kukaa mbali na ajali kama hizi siyo kuzikaribia namna hiyo. watu hajajua kwamba chanzo cha moto nini lakini bado wanashangaa shangaa hapo hapo, je kama kuna bomu linafukuta? au kuna mitambo ya gesi imepitishwa kwenye jengo kama hilo atapona mtu kweli mara tu likilipuka lote? Let be careful people. And always take cautions.

    ReplyDelete
  6. Jamani, how many fires are you going to experience hadi mjue there is an arsonist on the loose!? Kila kona moto, kila kona moto, hivi hao polisi hawawezi kufikiri kuwa labda kuna mtu ameamua kuwa anaanzisha moto kila kona. I think its an arsonist, Michuzi washauri hao wakubwa wa jiji la Dar hapo mjini waanze uchunguzi zaidi. This is beginning to look like planned fires not mere technical defaults!

    ReplyDelete
  7. Uwiiii jamani watanzania pole zetu sana. Kila kukicha yaani kama sio moto ni ajali kama sio hivyo ni majambazi tutafika kweli?

    Mungu ibariki Tanzania na watu wake!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...