TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkutano wa kumi na tisa wa Bunge umeana leo Jumanne
tarehe 13 Aprili na unatarajiwa kumalizika tarehe 23 Aprili 2010 mjini Dodoma.
Katika mkutano huu wa Bunge, shughuli za Mkutano mzima zitakuwa
kama ifuatavyo:
1.0 SHUGHULI ZA SERIKALI
A. MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI:
(Kusomwa mara ya kwanza na hatua zake zote)
katika Mkutano huu wa Kumi na tisa wa Bunge, Jumla ya
Miswada mipya nane (8) itasomwa kwa mara ya kwanza
na kupitia hatua zake zote. Miswada hiyo ni :-
1. Muswada wa Sheria ya Watu wenye Ulemavu wa
Mwaka 2010, [The Persons with Disabilities Bill, 2010].
2. Muswada wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji
wa Mifugo wa Mwaka 2010 [The Livestock
Identification, Registration and Traceability Bill, 2010].
3. Muswada wa Sheria ya Kusimamia na Kudhibiti
maeneo ya Malisho na vyakula vya Mifugo wa Mwaka
2010 [The Grazing-Land and Animal Feed Resources
Bill, 2010]
4. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria
Mbalimbali za Fedha wa Mwaka 2010 [The Financial
Laws [Miscellaneous Amendments) Bill, 2010].
5. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya
Masoko na Mitaji na Dhamana wa Mwaka 2010 [The
Capital Markets and Securities (Amendments) Bill,
2010].
6. Muswada wa Sheria ya Madini wa mwaka 2010 [The
Mining Act, 2010]
7. Muswada wa Sheria ya Madawa wa mwaka 2010
[The Pharmacy Act, 2010]
8. Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa
mwaka 2010 [The Written Laws (Miscellaneous
Amendments ) Act, 2010]
B. MAAZIMIO YA BUNGE:
Halikadharika, Bunge linatarajia kutoa Azimio
litakalowasilishwa na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika
Mashariki ambalo ni Azimio la Kuridhiwa kwa Itifaki ya
Soko la pamoja la Afrika Mashariki
Halikadharika, Bunge linatarajia kutoa Azimio
litakalowasilishwa na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika
Mashariki ambalo ni Azimio la Kuridhiwa kwa Itifaki ya
Soko la pamoja la Afrika Mashariki
2.0 MASWALI:
Aidha, katika Mkutano huu wa Kumi na Tisa, Jumla ya Maswali
125 yanatarajiwa kuulizwa na Kujibiwa ambapo
Maswali 14 yanategemewa kuulizwa kwa Mheshimiwa
Waziri Mkuu.
Aidha, katika Mkutano huu wa Kumi na Tisa, Jumla ya Maswali
125 yanatarajiwa kuulizwa na Kujibiwa ambapo
Maswali 14 yanategemewa kuulizwa kwa Mheshimiwa
Waziri Mkuu.
3.0 TAARIFA ZA KAMATI:
Kwa Mujibu wa Kanuni ya 114 (15) ya Kanuni za Bunge, Toleo
la 2007, Kamati zote za Kudumu za Bunge zitawasilisha
Mezani Taarifa za Mwaka, na kwamba taarifa hizi zitapangiwa
muda wa kujadiliwa katika Mkutano ujao wa Ishirini wa Bunge.
KAMATI YA MIUNDOMBINU:
(i) Taarifa ya Kamati ya Miundombinu kuhusu Taarifa ya
Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge kuhusu
Uendeshaji Usioridhisha wa Shirika la Reli Tanzania.
uliofanywa na Kampuni ya RITES ya India.
(ii) Taarifa ya Kamati ya Miundombinu kuhusu Taarifa ya
Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge kuhusu
utendaji wa kazi usioridhisha wa Kampuni ya Tanzania
International Container Terminal Services (TICTS).

4.0 SEMINA ZA WABUNGE WOTE:
Katika mkutano huu wa Kumi na Tisa, Ofisi ya Bunge imepokea
maombi ya kufanyika kwa semina zifuatazo:
i. Semina kwa Wabunge wote kuhusu Mapitio ya
MKUKUTA - I na mwelekeo wa MKUKUTA – II
itakayotolewa na Wizara ya Fedha na Uchumi tarehe
15/4/2010
ii. Semina kwa Wabunge wote kuhusu Soko la Pamoja la
Afrika Mashariki, itakayotolewa na Wizara ya Ushirikiano
wa Afrika Mashariki. Semina hii imepangiwa tarehe
17/4/2010 siku ya Jumapili.

Imetolewa na
Owen Mwandumbya
Kny: KATIBU WA BUNGE
Owen Mwandumbya
Kny: KATIBU WA BUNGE
basi hapo utasikia mtaalam katoka UK na kachukua madola kibao kitu cha kufanywa hata na muheshimiwa spika mwenyewe kama mafundi wapo dar, na akija mtaalaam utasikia alichomeka waya wa spiker akaulegeza kidogo tu basi na kuchukua mshiko wake, kazi ya kufanywa na mtoto wa 3yrs old, basi watu wale bunge la mwisho kuelekea uchaguzi,yaani bongo tulikuwa kila mtu msanii siku hizi fisadi, fundi mitambo wa mjengoni kakorofisha upate zuga inaitajika transister ya bei mbaya apige panga. bongo tambarare
ReplyDeleteDu huyo Askari wa kike ni maarufu sana Dodoma!! yaani wee acha tu ..mitaa ya Air Port, Equator Bar, CNC, NK....KUMBUKUMBU KALI SANA MICHUZI!!
ReplyDelete