Wadau kunradhi. Leo tumemzika nyanya yetu mpenzi kwenye makaburi ya Nonde, nje kidogo ya jiji la Mbeya. Zifuatazo ni taswira za mazishi hayo (ni nyingi kiasi kwa sababu maalumu) ya nyanya yetu aliyefariki siku nne zilizopoita akiwa na umri wa miaka 92. Ni siku ngumu kwangu ankal binafsi na wanafamilia. Najua wengi wadau mnajiuliza niaje? Huyu nyanya wetu kipenzi ni dada wa nyanya yangu mzaa mama ambaye ni mzawa wa huku Mbeya. Yeye alikuwa Mkatoliki swafi wakati nyanya yangu alikuwa Muislamu kama alivyoturithisha siye wajukuu zake. Huyu nyanya aliolewa na babu mwenye asili ya Ushelisheli.
Nyanya yetu kipenzi akiwa hataki kukaa sawa kwenye taswira hii
Ibada katika Kanisa la Mtakatifu Antoni wa Padua jijini Mbeya
Ma-ankal na wakwe zetu kina Isaak na Edwin Kassanga
Ankal Tony Swai akisoma somo la kwanza
sehemu ya waombolezaji wakiwa kanisani
wakati wa ibada
ndugu, jamaa na marafiki ibadani
ndugu na jamaa
madada
ankal na dada wa ankal
mbele shati jeupe ni mwakilishi wa Vodacom kanda ya kusini
Dada Helena akihakikisha kila kitu kinaenda sawa. Nyanya yetu kipenzi tumemzika ndani ya kaburi la mumewe aliyefariki miaka 25 ilopita kwa matakwa yake marehemu




















Poleni na msiba. Mungu amuweke panapostahili
ReplyDeleteBwana alitowa na bwana ametwaa.....Poleni sana. Anyway, naona Anko mnafanana sana mko kama Wabrazil/Wakorea mnafanana kama vidole.Poleni sana.
ReplyDeletePoleni sana Ankal na wana familia Mwenyeezi Mungu atawapa subira InshaAllah, na amweke Marehemu mahala pema Amin.
ReplyDeleteIlobaki Mumwombee nyanya apumzike kwa amani na mumshukuru Mwenyeezi Mungu mmekuwa na nyanya yenu mpaka vitukuu wamemwona ni jambo la kushukuru sana!
Kaka Michuzi poleni kwa msiba huu mzito. Menyezi Mungu awape Nguvu kwa kipindi hiki kigumu awatie moyo faraja na amani. Sisi wote ni wasafiri hapa duniani na heri ya Bibi Yetu ameishi katika kumpendeza Mwenyezi Mungu maana amepitiliza hata ile miaka iliyoandikwa kwenye Biblia miaka SABINI na yeye kagonga tisini na mbili.Hakuna sababu ya kulia tunachotakiwa kufanya ni kusherehekea Maisha ya Bibi wakati wa uhai wake naamini katuachia mambo mengi mema na mazuri yatakayo tuongoza sisi wajukuu kwa muda mrefu ujao. ASANTE
ReplyDeleteAnkal,
ReplyDeletePoleni sana kwa kuondokewa na Nyanya. Ametimiza wajibu wake hapa duniani, na Mungu amemrejesha kwenye makao ya milele. Tunashukuru kwamba Mungu amewawezesha kusafiri salama hadi kuwahi mazishi. Mimi ni Mkatoliki; nimeguswa sana na ibada ya mazishi ulivyoionesha hapa, ikijumlisha watu wa dini mbali mbali. Mungu awafariji kutokana na msiba huu, na ampokee Nyanya katika pumziko la milele. Amina.
pole ankal kwa kuondokewa na nyanya yenu kipenzi, Mungu ampumzishe kwa amani, amen
ReplyDeletePOLENI SANA ANKALI NA FAMILIA YAKO YOTE SIS TULIMPENDA LAKINI MUNGU ALIMPENDA ZAIDI,JINA LA BWANA LIBARIKIWE,NA MUNGU AMLAZE MAHARI PEMA PEPONI AMEN
ReplyDeleteANKAL MICHU, POLE SANA KWA MSIBA WA NYANYA. MUNGU AILAZE PAHALA PEMA ROHO YAKE, AMINA. MWITA, LONDON
ReplyDeletepoleni sana kwa msiba
ReplyDeletepoleni sana
ReplyDeleteMichuzi umekosea kusema uislam umerithishwa .
ReplyDeleteDini mheshimiwa hairisishwi.
Ankal alikuwa na dhumuni la kuonyesha jinsi dini mbili zinavyoweza kuinteract na mambo yote yakaenda shwari, naona wadau waliotoa comments hapa hakuna hata mmoja aliyeliona hilo!!! Thats from My understanding especially when wrote that he uploaded many pics for a special reason!!!
ReplyDeleteNanjilinji!!!
Poleni sana Ankal kwa kuondokewa na kipenzi.sasa nauliza mbona nyanya anaonekana mzungu kwa umbali?yupo kama africast..halafu hata jina lake...
ReplyDeletePoleni sana. Ikija suala la kurejesha namba kwa Muumba, hapo sisi binadamu hatuna ujanja tena. Tunaomba Muumba ampokee katika ufalme wake.
ReplyDeleteNimefurahishwa na sherehe ya mazishi. Ankal mmedumisha mila za kiTanzania: ninajua kuwa mna uwezo lakini hamkutenganisha waombolezaji kati ya wenye suti za ulaya na khanga kama mtindo ambao umeanza kuibuka jijini dar kutokana na ulimbukeni. mmeruhusu watu wote wachanganyikane bila kuwagawa katika matabaka ya walio nacho na wasio nacho na wote kwa pamoja wanatimiza azma ya kumwombea marehemu. nikiri kuwa ninachukukia ulimbukeni (ambao kwetu hapa umechochewa na ufisadi).
Mungu ampokee katika ufalme wake!
Unkal pole sana kwa kuondokewa na Nyanya yako. kazi ya mola haina makosa. Lakini swali la ufahamu ankal, umesema amezikwa ndani ya kaburi la mumewe? Inaamana wakati wanatengeneza kaburi la Nyanya ilibidi mwili (mifupa) samahani ya Mumewe iwekwe vizuri humo humo ndani ili Bibi naye alale ubavuni mwa mumewe?? Haya ni mapenzi makubwa sana
ReplyDeletepoleni sana wafiwa wote, pole ankal pole sana ila jamani naomba kuuliza mbona sijawahi kumuona or kumsikia japo kwa kutajwa tu mke wa ankal? Nilitegemea sana ankal angekuwa na mkewe kwenye msiba huu mzito kwa ankal, naomba jibu kwa yeyote ajuae tafadhali.
ReplyDeletePoleni sana Mungu amuweke mahali pema peponi, Amin
ReplyDeletePoleni sana ankal.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu awape subira.
(US Blogger)
Poleni uncle na familia.
ReplyDeleteKaka Michuzi pole sana kwa kufiwa na Nyanya. Mungu ailaze pema roho yake peponi.
ReplyDeletepole kaka hila na suggestion sizani kama ni vyema kuweka picha za makaburini na mwili ya marehemu kwenye blog too much pictures ,zina tisha. pole lakini
ReplyDeleteRafiki yangu,
ReplyDeletePoleni sana. Bwana Awe Nasi. Amen.
Fidelis.
Poleni sana.
ReplyDeleteMungu ailaze roho yake pema peponi na awape nyote nguvu.
Asalaam alaykhum ankal
ReplyDeletepoleni sana na msiba mola aiweke mahala pema peponi roho ya mpendwa nyanya yenu amiin.
Chef Issa
pole ankal kwa msiba. ndagha kyala.amen.
ReplyDelete