Edward Moringe Sokoine (1938-1984)
Ni miaka ishirini na sita iliyopita. Siku ya Alhamisi, majira ya jioni kama saa kumi na moja. Anga la jiji la Dar es Salaam lilikuwa jeusi likihanikizwa na mawingu madogo madogo yaliyojikusanya kuashiria kamvua kalikokuwa kametawala siku hiyo.
Hizi ni nyakati za masika katika sehemu kubwa ya nchi. Ndo kwanza nimerudi toka shule, tayari nimeshajipakia ugali wangu wa njano (Yanga) na maharage ya Iringa. Nipo mtaani nikicheza na wenzangu chandimu. Hatuna viatu, tupo pekupeku lakini hatujali kitu.
Maisha yalikuwa mazuri bila kujua adha na masumbufu ambayo wazazi walikuwa wanayapitia ili kutufanya watoto wao tuweze kwenda chooni. Nikiangalia pembeni, akina mama walikuwa wamekaa wakisukana na wengine walikuwa kwenye vibustani vyao wakipalilia matuta ya viazi vitamu.
Hakika hatukujua lililokuwa limetokea masaa machache yaliyopita hapa nchini kwetu. Lakini ghafla redio zikaanza kupiga wimbo wa taifa. Si aghalabu kusikia wimbo wa taifa mida kama ile tena kipindi kile kisichokuwa na sikukuu wala mgeni yeyote wa kitaifa.
Haiyumkiniki kuna jambo kuu limetkea. Katika utoto wangu, ghafla nikaacha kucheza, akina mama waliokuwa wakisogoa nao wakapigwa na ubaridi wa ghafla. Katika mshawasha wangu wa kitoto nikaijongelea redio kutaka kujua kilichojiri jioni hiyo ya Alhamisi nyeusi. Dakika kadhaa zilipita kabla ya wimbo wa taifa kuisha. Sauti iliyojaa huzuni ikasikika.
Hata katika utoto wangu, naweza kusema kwa hakika kuwa sauti ile ilikuwa katika huzuni na majonzi na ilionesha ni ya mtu aliyekuwa katika kilio muda si mrefu uliopita. Naam, ilikuwa ni sauti ya hayati baba wa Taifa.
Nayakumbuka maneno yake mpaka sasa. Hivi ndivyo alivyosema: "Ndugu wananchi, leo mnamo majira ya saba mchana, ndugu yetu, mwenzetu, Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais, Edward Moringe Sokoine amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea huko Morogoro wakati akilejea Dar es Salaam kutoka Dodoma kwenye mkutano wa Bunge" Naam, hiyo ndiyo sababu ya kupigwa kwa wimbo wa Taifa jioni ile.
Utando mweusi ukatanda. Simanzi ikatawala. Vilio vikasikika, furaha ikatoweka. Giza la mawingu meusi likaongezea upotevu wa furaha. Nikausikia ukelele mkuu kutoka kwa mama mmoja aliyekuwa ameshika jembe akipalilia bustani yake "Mama wee mkombozi wetu amekufa, nani atatutetea sisi wanyonge?" Hakika ndivyo aliomboleza mama yule.
Huzuni kuu ikaniingia ghafla. Nikajiwazia "Sokoine kafa? Hapana, amekufa?" Nafsi ilikataa kuamini, akili ya utoto ikaniambia haiwezekani. Ghafla machozi yakaanza kunitiririka. Naam nililia. Nilimlilia mzalendo wa kweli. Wazazi walilia, wananchi walilia, hata Nyerere alilia tena hadharani, hakulia kiunafiki alilia kweli. Watanzania wapenda haki tulilia, tulimlilia mpenda haki mwenzetu. Sokione mzalendo wa kweli.
Mwana wa Kitanzania asilia, mtetezi wa kweli wa wanyonge, mchapakazi, mpigania mema ya nchi. Naam, yawezekana kwa wengine ameshafutika lakini kwa wapenda haki, Sokoine atabaki kuwa kioo chetu daima.
Huyu ndiye mtu aliyekuwa na sifa nilizozitaja wakati ule kwenye ile ndoto yangu ya "Namuona mtu huyu". Yawezekana alikuwa na kasoro zake kama mwanadamu na hata kiutendaji lakini daima nia yake njema kwa watu wake iliyafunika makosa yake hayo.
Alipendwa na wanyonge na kuchukiwa na wezi, wabadhiifu wa mali ya umma na wahujumu uchumi (leo tunawaita mafisadi). Huyu ndiye aina ya mtu tuliyemuhitaji Tanzania ya leo.
Nimemkumbuka Sokoine, mtanzania mzalendo mwana mpenda nchi aliyenifanya nihisi msiba wake kuwa unanihusu kwa ukaribu mno. Naam, wajamaa kama kina Subi lazima watamkumbuka mtu huyu na kumuomboleza daima.Mungu alipenda kumchukua ingawa tuliona amemchukua mapema mno. Pumzika kwa amani Baba Sokoine, mtanzania na mzalendo wa kweli.
Amina!
Dk. F. Mghanga, MD

Umenikumbusha mbalki sana. Mimi nilikyuwa Temeke siku hiyo saa kumi jioni.
ReplyDeleteNi kweli,,,,umenigusa juu ya huyu Mtanzania mzalendo mpenda nchi..! lah,,hakika umentia huzuni upya,,,maana siku hiyo mimi nilkuwa barabarani nikielekea kijiji kingine kwenda kulala huko ili alfajiri niweze kupanda basi kwenda Chuoni,nikiwa na mzee mmoja aliyekuwa m/kiti wa kijiji chetu,,mzee Timotheo Mabula,,ndipo akaniambia,,kijana umesikia hayo....? SOKOINE kafa,,Lo,niliishiwa nguvu nikakaa chini...yaliyofuata nitakuambia baadaye..kweli NAMKUMBUKA MPIGANIA WANYONGE.
ReplyDeleteI was a young boy by then but I still remember everything too. No one is perfect. But, at least He was Patriotic and considerate for the majority poor Tanzanians. RIP
ReplyDeleteUmetukumbusha wengi, ilikuwa ni siku ya majonzi kupoteta kiongozi wa kweli na mtetezi wa wanyonge, ili kumkumbuka nawakumbusha Watanzania mwaka huu tuna uchaguzi, tuchague viongozi kama Sokoine.
ReplyDeleteMdau,
Houston, TX, U.S.A
Umenikumbusha mbali. Nafikiri wengi wanakumbuka siku ya tukio hilo kutokana na msiba ulivyotokea. na uzuri wa wakati huo kila mtu alikuwa anasikiliza Radio Tanzania. Mimi nilikuwa Moshi nasoma darasa la nne. Moshi enzi hizo sisi tulikuwa tunatoka madarasani saa kumi jioni, wakati nimefika mtaani kwetu nikaona watu wamesimama kila mahali vikundi vikundi wanasikiliza Radio tena wamesimama bararabani enzi hizo hakuna magari mengi mitaa ya Moshi. Nikamuuliza mtoto mmoja kuna nini? Akaniambia Sokoine kafa, walahi hata watoto wa enzi hizo tuliguswa na kifo chake ukizingatia habari zake zote tulikuwa tukizipata kutoka Radio tanzania, na magazeti ya Uhuru na Mzalendo enzi hizo hatusomi Daily news maana darasa la nne lugha bado.
ReplyDeleteNa tulimfahamu vizuri maana usipojua siasa za ndani kama waziri mkuu nani, vita vya ulanguzi na hata tarehe ya kufa kwake, ina maana somo la Siasa lingekupiga chenga.
mwenyezi Mungu amlaze pema. Amina
Umeikosea kidogo hotuba ya Mwalimu alipokuwa anatangaza msiba kwani Hayati Sokoine hakuwa Makamu wa pili wa Rais. Hotuba ilikuwa hivi "Ndugu wananchi leo mnamo saa saba mchana ndugu yetu, kijana wetu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndg. Edward Moringe Sokoine wakati akirejea kutoka Dodoma gari yake ilipata ajali. Amefariki Dunia." Baada ya hapo ni wimbo wa Taifa na nyimbo za maombolezi. Ni siku ambayo sitaisahau nakumbuka nilikuwa std. 7 kesho yake shule kila mmoja alikuwa na hadithi yake
ReplyDeleteNilikuwa niko Lusaka,mama akanipigia simu na siku iliyofuata akanitumia magazeti mawili tofauti kuhusu kifo cha Sokoine.Ukweli ni kwamba umaarufu wa Sokoine siku hizo ulianza hata kuupita umaarufu wa Mzee Nyerere,kwani Mzee Nyerere alimpa Sokoine madaraka mengi na alimuamini na kumpenda sana.Ndiyo maana Nyerere alihuzunika sana na kifo chake.ASANTE KWA NAKALA NZURI YENYE KUMBUKUMBU NYINGI YA WAKATI HUO.VERY PROFFESSIONALLY WRITTEN!
ReplyDeleteAMA HAKIKA UMENIKUMBUSHA MSIBA MZITO NA KUNITIA MACHOZI MOYONI. SOKOINE ANALIKUWA KIONGOZI MZALENDO, MPENDA NCHI, MPIGANIA WANYONGE, NA MKALI KAMA SIMBA KWA WALE WOTE WALIOHUJUMU NCHI.
ReplyDeleteUKO WAPI MUNGU? TAZAMA TANZANIA YETU YA LEO. TUNAOMBA KIONGOZI MPYA MWENYE SIFA KAMA SOKOINE. AJE AKAMBOE NCHI YETU ILI BADALA YA WACHACHE KUNUFAIKA WATANZANIA WOTE WANUFAIKE NA NCHI YAO.
MIAKA MINGI IMEPITA SASA LAKINI SOKOINE TUNAKUKUMBUKA. PUMZIKA SALAMA MZALENDO WA TANZANIA.
Nakumbuka wakati huo nilikuwa JKT Maramba (baada ya kumaliza ukuruta pale Mgambo JKT). Baada ya habari kutangazwa pale kambini za kifo cha Sokoine, kikosini iliamuliwa kambi ishiriki kwenye maombolezo kwa shunguli maalum. Nilikuwa kwenye kikundi cha 'unembo" pale kambini. Wanembo tukaitwa ili kuandaa nyimbo na mashairi wakati ma-servicemen wengine wanaenda kupalilia mikokoa. Nakumbuka hata mazoezi yalitaka kutushinda maana jinsi nyimbo/mashairi vilivyotungwa vilituongezea masikitiko na huzuni. Siku ilipofika ya maonyesho (kama sikosei ilikuwa ile siku ya mazishi), tuliingia ukumbini, tukaimba shairi tukiwa tumeshika mashavu mara ukumbi ukarindima kwa vilio, machozi yalidondoka sio kwa sisi tuliomba tu bali hata watazamaji. Kwa kweli kazi yake ilionekana na ilikubalika ndio maana huzuni ilitanda na itaendelea kutanda.
ReplyDeleteNikiwa chuo kikuu (UDSM), kikundi cha Theatre Art pale chuo (1985), kilikuja na igizo ambalo lilikuwa linaeleza namna “dongo” lilivyoshushwa toka juu, na jinsi ambavyo “dongo” halikujulikana limeenda wapi…... nakumbuka jinsi wasanii walivyomuweka muigizaji anaefanana na Sokoine… akitoka na kuingia kwenye jeneza....kidogo igizo likikuwa linatisha!
Dr fabian mghanga vipi mambo umenikumbusha mambo mengi sana ya zamani mimi mzee wa shaaban robert
ReplyDeleteDuh....umenikumbushaa mbali sana huu msiba wa SOKOINE....nilikuwa mdogo sana about 10years old but msiba wake uliniuma sana..he will be missed daima...duh RIP
ReplyDeleteUmenikumbusha mbali saana. Nilikua mdogo lakini nakumbuka aunt yangu alikua anaimba kwanya kuu ya kanisa la Lutheran Arusha mjini walichaguliwa kwenda kuimba kwenye mazishi. Walifundishwa wimbo kwa sijui siku mbili walifanya mazoezi kweli tulikua tunakwenda kumchukua usiku...ule wimbo wao ulivuma sana ...hata siukumbuki tena.
ReplyDeleteLakini mpaka leo nakumbuka mama yangu alikua analia...halafu baada ya hapo ilikuja miaka mingi tu kila siku watu wanasema wamemwona mahali hapa mara kwenye ng'ombe zake...nadhani alichukua muda kucross.....
Hivi hebu tujiulize kama angekua mpaka leo Tanzania ingekuaje?
Manake nakumbuka rafiki za baba yangu walikua matajiri wakawekwa jela ili waonyeshe hela zao wamezipataje...
HIVI KUNA SIKU YA SOKOINE?
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteFanya mambo tupate wale tu-picha tuwili au tutatu twa hili tukio. Maana hii tribute imewagusa wengi naomba tusogee mbele ili kumuenzi shujaa huyu. wengine tulikuwa wadogo sana kukumbuka chochote hii leo lakini habari zake tulizisoma kwenye somo la siasa shule ya msingi (enzi za Chama na serikali)
Ombi hili si kwa michuzi peke yake, Mdau yoyote yule aliyeguswa ruksa kumtumia picha Ankal ili atuwekee ktk Globu yetu ya Jamii
Dk umenikumbusha mbali sana nilikuwa darasa la pili nikiwa Rusumo mpaka wa Tanzania na Rwanda kifo kile kilileta majonzi katika kimji kile na Wanyarwanda walitufariji kwa kifo hiki maana hata wao walimfahamu Edward Moringe Sokoine naamini huyu kiongozi asingelikufa Tanzania ingekuwa tofauti iliyo na haki na tusingesikia mambo ya mafisadi hata kidogo. RIP EDWARD MORINGE SOKOINE.
ReplyDeleteNakumbuka kauli yake ya mwisho kuaga Kikao kuwa "tutakutana tena hapa hapa (dodoma)". Ama kweli hatujui siku wala saa ya kuiaga hii dunia. Laiti tungejua sijui ingekuwaje?? Asante Fabby kwa kutukumbusha.
ReplyDeleteMum, Mafinga
I am crying right now reading this. Amam kweli umetonesa kidonda. Nilikuwa mdogo lakini kama alivyosema mdau mmoja hapo juu, hata watoto enzi hizo walijua Sokoine ni nani. Nilikwa darasa la tatu, lakini nilienda kuaga maiti pale diomond na wanafunzi wengine. Enzi hizo nilikuwa Chipukizi Kinondoni tawi la Kabangwa! Wooh! What will he say about Tanzania now. Mpenda wa Haki na mtetezi wa wanyonge. The Martin Luther King of Tanzania! May he rest in Peace!
ReplyDeleteIF TEARS COULD BUILD A STAIR CASES AND MEMORISE THE LANE I WOULD WALK RIGHT UP TO THE HEAVEN AND BRING YOU BACK AGAIN,TANZANIANS ARE CRYING FOR YOU COZ THOSE WHO GOT CHANCE LIKE YOURS DID US WRONG.....THEY ALWAYS CHEET,LIE AND STEEL,NO BODY CAN DO THEM ANYTHING,THEY GOT POWER AND THEY ARE SELFISH.
ReplyDeleteTHANKS FOR WHAT YOU HAVE DONE FOR US
THERE IS ONLY ONE EDWARD MORINGE SOKOINE.
NILIKUWA MAZENGO HIGH SCHOOL FORM SIX, KWA KWELI ILKUWA SIKU YA HUZUNI NCHI NZIMA.ALIKUWA MTU WA WATU. NAKUMBUKA WATU WA LINDI NA MTWARA MWAKA HUO WALIKUJA JUU NA KUANZA KUCHANGA PESA ILI WAJENGE BARABARA YAO TOKA DAR HADI MTWARA, SOKOINE AKAJA JUU AKASEMA ACHENI MCHANGO RUDISHENI PESA ZOTE KWA WATU WALIOCHANGA MIMI NI WAZIRI MKUU NA NITAHAKIKISHA BVARABARA HIYO INAJENGWA KWA NINI MUJENGE WENYEWE KWANI NYIE SI WATANZANIA, KWANI HAMLIPI KODI NA HAO WENGINE WALIOJENGEWE NA SERIKALI NI NANI SO LONG AS I AM A PRIME MINISTER OF THIS COUNTRY NITAIJENGA. BAHATI MBAYA AKAFARIKI HAIKUJENGWA HADI MKAPA ALIPOINGIA MADARAKANI, NA YEYE KAJENGE KWA KUONA AIBU ATAKAPOMALIZA MADARAKA WATAMUULIZA HATA NA WEWE WA HUKO UMESHINDWA KUJENGA NDO IMEJENGWA NA SINA UHAKIKA KAMA IMEISHA MAANA NILISIKI YA NDUNDU KUKWAMA MAGARI MWAKA HUU, WA KUSINI VIBANENI VYAMA JUU YA ROAD HIYO UCHAGUZI HUU, NA TUCHAGUWE VIONGOZI WA AINA YA SOKOINE NA KAMA HAWAPO BASI WAJARIBU KUMSOMA NA KUMUIGIZA BASI
ReplyDeleteHabari na kumbukumbu ya kifo cha Sokoine ni huzuni kubwa sana mioyoni mwa watanzania walio na msimamo na mapenzi ya dhati juu ya haki na usawa kwa taifa lao. Wakati huo nilikuwa na miaka kama sita hivi, ila meseji niliipata. Wazazi wangu na ndugu na jamaa wengine tukiwa huko Kahama walikuwa wamejipumzisha kibarazani baada ya shughuli za siku hiyo (I think)huku wakisikiliza redio, na sisi watoto wao tulikuwa tukicheza cheza tu. Ghafla nikasikia "what!", "mama yangu", "uuuwwwiiiii" n.k. and we all rushed to the verandah to learn what just happenned. Nadhani ilikuwa mara yangu ya kwanza kusikia jina Sokoine na kujua kuwa tuna waziri mkuu. Ila tangu siku ile nilizidi kujua mengi sana kuhusu Sokoine maana alikuwa gumnzo kubwa sana ambalo sikulidharau kamwe, kama ilivyo sasa.
ReplyDeleteIla dunia hii imejaa wanafiki sana. Naamini wakati ule hata hawa mafisadi wa sasa walilia sana, ila leo wanashangilia kwa vile watu kama Sokoine ni kama vile hawapo kabisa, na kwao hilo ni jambo jema. Laana iwe kwao!