katika pitapita zake ankal baada ya kuchota advansi mgodini alipitia supamaket moja na kukuta maboxi kibao ambayo baada ya kuulizia akaambiwa ni vilaji vipya visivyo na kilevi kutoka Ujerumani kwa jina la Holsten. Pamoja na kuelezwa kwamba ni moja ya vilaji bomba ughaibuni aliambiwa pia vinakuja vya kila aina kama vile vya tofaa (epo), embe (mengo), limau (lemoni), Stauberi, clasik na komamanga (pomegranate). Akaomba kuonja hiyo ya komamanga na akakoma ubishi. alipouliza vinapatikana hapo tu akaambiwa la hasha, karibu supamaketi zote vipo. akajitwika boxi moja la komamanga na kuondoka nalo...bei karibu na bure
kilaji kisicho kilevi cha komamanga.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. TITO kasema gonga tu gonga hahahahaah. Seif.

    ReplyDelete
  2. Pesa bwana wamekulipa bei gani lol! kumbe Sheikh michuzi naye anashusha maji.

    ReplyDelete
  3. Hahaa.. Michuzi kumbe na wewe ni MODEL wa kwenye matangazo!!?

    Haya mzee.. Baelezee!! Baelezee!!

    ReplyDelete
  4. ankal una visa, eti stauberi

    ankal inaonesha mikwanja haikusumbui manake kila kitu kwako bei ni kama bure...

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  5. Ankal huu ndo mwanzo wa kupata utamu wa ngano! itaanza kidogo kidogo kisha utataka kujaribu ngano yenyewe wala usikizoee kikinywaji hiki kwani kimetengenezwa na ngano!

    ReplyDelete
  6. Mimi sina mazoea yakuandika katika blog hii ya Michuzi. Lakini huwa nakerwa sana na matumizi ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kwa mfano kama kinatumika maneno ya Kiswahili au Kiingereza basi maneno yaeleweke. Kwa mfano Tofaa (epo),embe (mengo)na limao (lemoni). Sasa hayo kwenye mabano ni kwamba mwandishi alikosea au alikuwa anataka kuchekesha? Blog ya michuzi inazidi kuwa juu na inaangaliwa na watu wengi kwa hiyo tujaribu kuandika lugha inayoeleweka kama ni Kiswahili au Kiingereza kieleweke.Dictionary zipo tuzitumie. Ukisoma hii message ni wazi kwamba alieandika possibly hana elimu yakutosha. Lugha lazima uielewe vizuri na uwe very fluent kabla yakuweka jokes ambazo hazifurahishi kama zilivyo ila zinamfanya mwandishi asieleweke. Na message zingine zinakosa hata ladha ya kusoma.

    ReplyDelete
  7. DUUUH KUMBE KOMAMANGA INAITWA POMEGRANATE!!! HAYA BWANA ANKAL AHSANTE KUNIPA NENO JIPYA LEO. KOMAMANGA NALIJUA NA NI TUNDA LENYE DAWA NYINGI KWA BINAADAMU, NGOJA NITAONJA NA MIMI NIONE UTAMU WA HOLSTEN. OLE WAKO NILEWEEE!!!

    ReplyDelete
  8. Samahani sana kuingilia kwenye blog yenu. Kwakweli sikujua blog ina wenyewe wala sitarudia tena ku comment. Naomba tu nifahamishe hizo blogs zingine zinazotumia kiswahili sanifu nizitembelee. Ni swala lakuelewesha tu. Narudia samahani sana.

    Asanteni.

    ReplyDelete
  9. Wewe mwenye kutaka lugha sanifu hebu toka bana, na usisahau kufunga mlango utatuingizia nzi maana wenzio twanywa HOLSTEN huku...HOLSTEN OYEEE!

    ReplyDelete
  10. Kutumia Kiswahili sanifu au Kiingereza sanifu kwa mtu aliyeenda shule ni vizuri. Hata kuchanganya hizo lugha mbili kwa pamoja pia sio tatizo mradi iwe SANIFU. Nadhani blog hii inatumia slang au "swanglish" kama ndio lugha sanifu na imeshazoeleka hivyo. Kwa mtu mgeni unaweza usielewe kwa sababu lugha zote zina slang lakini sio wote wanaweza kuzielewa. Eg mtu anapoandika ANKAL AU ANKO hicho sio Kiswahili na sio Kiingereza lakini kwa sisi wa blog hii inabidi tuelewe tu hivyo na message ifike. Ukiangalia West Africans kuna lugha inaitwa pigeon English ambayo hata wakiandika ni wachache wataelewa maana ni lazima uelewe 'accent' ya West Africans ili kujua wanacho kisema. Huwa hakitumiki kwenye maandishi ni kwa ajili yakuongea tu.

    ReplyDelete
  11. Ndugu Mdau wa Thu Apr 22, 09:05:00 AM, pole sana kwa kukwazwa na lugha za hapa! Hata hivyo nashukuru kwamba umejitetea kuwa wewe si mwandikaji sana hapa globuni! Hizo lugha alizoandika Ankal Michuzi ndizo zinazotumika hapa na ndizo zinazotuleta sisi wengine kuondoa boredom ya kazi!
    Kuna sisi wengine siku haipiti bila kuja hapa kucheka (ikiwamo kucheka lugha kama hiyo), hivyo tuache wenyewe na globu yetu!Hii globu ina wenyewe, na ndio sisi!

    Mdau wa Mwenge

    ReplyDelete
  12. ANONI WA 22, 09:05:00 AM, Mbona unatuharibia mudi? sisi tunaelewana vizuri tuu. na ndo maana hakuna stekholda hata mmoja aliyelalamika kutoelewa lugha ya blogu yetu. Sasa ndugu yangu naomba nisaidie kitu kimoja. mimi baada ya kusoma komenti yako nimejisikia kukutukana tusi zito kidogo hata mimi sijalipenda, naomba namba zako za simu nikutukanie pembeni maana hilo tusi halijakaa vizuri.

    ReplyDelete
  13. Duh yani hapo jamaa mumempiga na Buti la warehouse kudadadeki hahahahaahahha Mzaramo anauwa.

    ReplyDelete
  14. Sh. ngapi?!
    mi nataka ya epo na stauberi!

    ReplyDelete
  15. teh teh teh teh! ooh mbavu zangu! nimecheka mpaka basi! kweli watu mmedata! hivi huu msadifu kiswahili hajui km wabeba box tukiwa hapa kwa ankal ni kama tupo Majengo Mbeya! ala! hapa ndo nyumbani! so hakuna kitu mtu utashindwa kukielewa nyumbani kwenu au kwako!Ankal ana busara anajua akitumia hicho kiswahili unachotaka wewe bloguni hapatanoga!

    ReplyDelete
  16. Hayaa mjadala wa Luga umeishaa, ameshaelewa huyu mgeni. haya turudi kwenye HOLSTEN EPO, HOLSTEN MANGO, HOLSTEN LEMON, HOLSTEN STORBERI NA HOLSTEN KOMAMANGA.
    Hebu tukazitafute Tuzinyweeeeeeeeeeeee. wadau hoyeeee.

    ReplyDelete
  17. ANKAL WEWE HATA USIOGOPE HATA IKIWA NI YENYE ALCOHOL KWANI TITO KASEMA GONGA GONGA

    TITO NOMA SANA ANASEMA KAGUNDUA KUWA DAWA YA UKIMWI NI KUGONGA GONGA LAGA

    YULE JAMAA KIBOKO ETI MKIPATA WANAKE GONGENI BILA KUVAA SOKS KAAZI KWELI KWELI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...