
Katika kuendeleza libeneke la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA), Wizara ya Katiba na Sheria imemaliza kuandaa Tovuti yake. Hivi sasa tovuti hiyo inapatikana kwa kupitia address ifuatayo;
Hivo kwa mdau/mwananchi yeyote anayehitaji huduma zinazohusina na sheria, kama vile KATIBA YA NCHI na kadhalika, anaweza kuviona na ku-"download" katika mtandao huo.
Ahsante,
Ni mimi mdau,
Geofrey Chami.
Ahsante,
Ni mimi mdau,
Geofrey Chami.
--------------------------------
Globu ya Jamii inatoa pongezi sana kwa wizara hii kwa libeneke lao ambalo limekaa vyema na kuonesha wizarani kuna viongozi makini wanaojua nini maana ya TEKNOHAMA na matumizi na faida zake. Tunatumai wizara zingine zitaiga mfano ama kuboreza libeneke zao ambazo zimedoda kwa kukosa up-date za mara kwa mara. Hongera sana Wizara ya Sheria na Katiba na mkumbuke kwamba libeneke ni sawa na ndoa. usipoitunza itakufa...
-Michuzi
Kaka Michuzi nakupongeza kwa kuipongeza hiyo Wizara. Kwa bahati mbaya mimi sina la kuwapongeza kwa sababu kubwa zifuatazo 1. Sioni Katiba ya Nchi wanayosema iko kwenye tovuti yao 2. Downloadable Documents ambazo ni .pdf hazifunguki hata moja 3. Policy Document 02 Feb10 inafunguka lakini sijui ni kitu gani kinaonyeshwa. Naomba Msaada wazee wa IT MoCAJ. Muganyizi Philemon
ReplyDeleteNimefungua hizo downloadable documents, hizo PDF zimefunguka na nimezisoma. Ila hiyo POLICY DOCUMENT kilichomo ni kituko, sijui ilikua ni majaribio, sipati picha. Inabidi wahusika walifanyie kazi haraka
ReplyDeleteMAKULILO, Jr.
www.makulilo.blogspot.com
www.scholarshipnetwork.ning.com
San Diego, CA
Muhimu ni kuwa wamepiga hatua, hizo zote zinafunguka ukiwa na subira, haya tuansonga mbele pole pole, GOOD START.
ReplyDeleteNi hatua nzuri kinachotakiwa sasa wawe wanaiupdate at least kila wiki na waiunganishe na mahakama zetu kuu ili tuweze kupata hukumu zinazotolewa kupitia kwenye mtandao.
ReplyDelete