Home
Unlabelled
Mbunge wa vunjo apata nafuu baada ya kupatwa na kiharusi bungeni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
hayupo hospitali ya taifa muhimbili, amelazwa MOI ni vitu viwili tofauti!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteHELP HELP HELP
ReplyDeleteThis is a lost in translation
How can a person kuugua kiharusi ghafla? au you mean kuanguka kifafa ghafla
Wataalam nielimisheni
Kiharusi ni ugonjwa gani?
ReplyDeleteKiharusi ni ugonjwa ambao ukiupata unajisikia kama mwali anayetaka kufanyiwa afanyiwayo mwali usiku wa harusi yake, hence the name Kiharusi.
ReplyDeleteKiharusi aka stroke. Kimsingi ugonjwa huu hutokea pale ubongo unapokosa damu kutokana na tatizo kwenye mishipa inayosambaza damu ubongoni.Mara nyingi hii hutokea ghafla ingawa wakati mwingine kuna dalili unazoweza kuona. Ziko aina mbili kuu, moja ni mshipa wa damu kuziba ama kukaza na kusababisha sehemu ya ubongo isipate damu(ischemic) na nyingine ni mshipa kupasuka na kusababisha damu kuvuja kwenye ubongo (hemorrhagic). Kisha aina ya kwanza huagawanywa tena kwenye makundi matatu. kundi la kwanza ni kiharusi kipitaji(transient ischemic attack/TIA) yaani kwamba mshipa unaziba kwa muda kidogo kisha unaachia. Hii huonyesha madhara kwa muda yakiwemo mdomo kupinda, kupoteza fahamu, kiungo kulegea nk hupona katika muda wa masaa 24 hadi 72. Kundi la pili ni kiharusi kinachojirudi (reversible) hiki kinaweza kutokea sawa tu na aina hiyo ya kwanza lakini pia hupona baada ya muda na mtu kurejea nguvu na matumizi yote ya viungo kama kawaida. Tofauti ni kwamba hiki kinakaa zaidi ya masaa 72. Na aina ya tatu ni kiharusi kikuu (major stroke) athari ya hiki ni za kudumu na humuacha mtu na ulemavu kutegemeana na sehemu ya ubongo iliyopatwa na madhara. Maelezo ni marefu kuhusu mada hii lakini nadhani nimejibu baadhi ya maswali likiwemo la kiharusi kinapatikana ghafla ama la. Kikubwa chunga afya yako.
ReplyDeleteDakta G
Kiharusi ni Kupooza au Kuparalaizi, Nijuavyo mimi Kiharusi kikikupiga inachukua muda kidogo kupona, nashangaa mweshimiwa fasta kaamka...kweli Mungu Mkubwa!
ReplyDeleteNapenda kutoa pole kwa Mheshimiwa mbunge ambaye pia imetokea kuwa ni jirani yetu pale kijijini kwetu Marangu. Wadau, kuna mambo mengi tunaweza kutania lakini inapokuwa ni kuhusu afya ya mwenzetu sioni kunautani wowote wa kutufurahisha. Hebu fikiria kama unapata taarifa kama hii ambayo inamuhusu mzazi wako au ndugu yako yoyote au rafiki halafu unaona wana jamii wanafanya ni sehemu ya kutafuta cha kuchekea. Je, ungefurahi? Tutumie glob ya jamii kimuafaka tafadhalini...wakati wa utani na viburudisho tufanye hivyo, na wakati wa tatizo basi tutowe ushirikiano mzuri hata wa kusema pole mzee mungu atakusaidia.
ReplyDelete-Mdau
Mpaka uchaguzi ufike, tutaona na kusikia mengi miongoni mwa wabunge!
ReplyDeleteNaungana kabisa na wadau wengine kumpa pole mh. mbunge, mungu atakujalia utapona.
ReplyDeleteLakini pia naungana na huyu aliyelaani tabia ya watu kuleta utani mahali ambapo apastahili utani.mtu anayefananisha kiharusi na jambo kama ngono ama kufanya mapenzi hatufai kabisa. inawezekana kuna baadhi ya wenzetu wana matatizo makubwa sana vichwani maana si kitu chepesi kwa mtu kuja na maoni ya kukejeli mgonjwa ama magonjwa.
Dakta G
ReplyDeleteNakushukuru, ni dhahiri waelewa matatizo ya neurolojia. Mimi kinachonipumbaza ni majina ya magonjwa hayo.Ukiangalia kamusi nyingi za kiswahili zasema kiharusi ni stroke, mimi siku zote tangu utoto tuliambiwa ukisema ua ukiimba chooni utapata kiharusi, na kiharusi hicho ni kile kitu waganga waita parkinsonism ua parkinsons disease.Hakika kuna tofauti kubwa sana baina ya maradhi hayo,tafadhal niambie parkinsons disease yaitwaje kiswahili
Astaghfiru lah, Mungu atupitishie mbali matatizo hayo
Mdau hapo juu. Kuna magonjwa mengi yaliyo na tafsiri ya kiswahili lakini inapokuja kwenye magonjwa yanayohusisha majina ya watu hayabadiliki. Parkinson ni jina la mtaalamu aliyeuelezea ugonjwa huo kwa kinagaubaga hivyo kwa heshima ugonjwa huo ukapewa jina lake. Kwa hivyo kwa lugha yoyote ile unabaki kuitwa hivyo pengine kwa kiswahili utaitwa pakinsoni.
ReplyDeleteMheshimiwa Dakta G
ReplyDeleteNakushukuru katika jitihada yako ya kunielimisha lakini mimi ni mwanafunzi mkorofi kidogo.Nakubaliana nawe kuwa magonjwa mengine yana majina ya wataalam waliofufunua maradhi hayo lakini sio kusema kuwa magonjwa hayo yalikuwa hayana majina mengine au kuwa dunia nzima yajulikana kwa majina ya wataalam hao tu
Mfano HANSENS DISEASE
Kiingereza.....Leprosy
Kiswahili......Ukoma
Kiarabu........Sara"ath
Nimekupa mfano wa ukoma kwa sababu ugonjwa huo binadam alikuwa nao tangu enzi za nabii Isa,umetajwa kwenye Matthew 8.2-4,Luke 4:27.Leviticus,Exodus etc
Kwenye Hadithi umetajwa
Ni dhahir basi kuwa Hansens disease was well known before Hansen and Parkinsons disease was well known before Parkinson
Samahani kwa ubishi
muheshimiwa kapatwa na TIA achunge afya sasa la sivyo itarudi kwa hasira.
ReplyDelete