Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Maendeleo Dr. Komba (Mwenye mwamvuli) akijiandaa kumlaki Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samuel Sitta Chuo Kikuu cha University of Dar es salaam kampasi ya Mlimani leo kabla ya kuzindua rasmi mpango wa KUREJESHA MAADILI KWA WATUMISHI WA UMMA kwa lugha ya wenzetu Public Integrity Restoration Initiative (PIRI). Mpango unaanza na vijana 4000 wanaomaliza vyuo vikuu vya umma. Changamoto aliyoitoa ni kwamba mpango huu uenee vyuo binafsi, vya kati vinavyotoa vyeti na diploma maana huko pia kuna wahitimu wengi, lakini pia uenee kwa wote, hasa waliopo kwenye utumishi hivi sasa inapasa elimu hii ya maadili ya utumishi wa umma iwafikie.
Mh. Sitta akilakiwa
Kaimu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Yunus Mgaya akimuongoza Mgeni rasmi kuelekea ukumbini. 




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...