Sisi ni wabeba Box huku ughaibuni na idara yetu ya maboksi inamiliki ndege ya mizigo (pichani) yenye uwezo wa kubeba Tani 49 kwa mpigo. Tumefanya kazi nyingi za Ministry of Defence MOD kule Basra (Iraq) pamoja na Disaster emergency Committee DEC kule Haiti. Na sasa hivi tuna kazi ya FIFA 2010 kwenda Africa Kusini kutoka Ulaya.

Kwa sasa tunapeleka farasi South Africa halafu tukirudi tutabeba Machungwa na mihogo kutokea Nairobi. Tunajua kabisa kuna machungwa na vitu vingi sana vya ku-export vipo Tanzania. Hata kama itashindikana mtakuwa mashahidi kwamba nilijaribu na kuweka hii tenda
Maelezo zaidi nimeweka kwenye attachnent

MAOMBI YETU NI MAWILI TU

KUTUUNGANISHA NA WATU WANATAKA KUEXPORT FLOWERS AND ORGANIC PRODUCE OR ANYTHING FOR EXPORT ILI KU UTILIZE CARGO SPACES KWENYE NDEGE INAPORUDI ULAYA.


As it stands now, tutashuka Nairobi kuchukua Mizigo. tunadhani Tanzania pia kuna vitu vingi sana vya ku-export. Hivyo shime kwa wenye mwamko tuwasiliane tuangalie namna tutavyoweza kushirikiana.

PIA TUNATAKA KUWEKA MATANGAZO YA

KUVUTIA UWEKEZAJI NA UTALII TANZANIA

Kwa maelezo zaidi tunaweza kuwasiliana
Email: info@swahilitravel.co.uk
Tel: +44 7932 088 488
Tel: +44 7896 702 705

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. hii mbona haijakawa sawa? weka tovuti yako.

    ReplyDelete
  2. Anon wa Mon Apr 05, 01:09:00 PM

    Tovuti ya nini?, huyu jamaa ni mbeba box kaajiriwa na wenye ndege hiyo kutafuta tenda ili apate commission yake. Kwa taarifa yako bongo hupati kitu mpaka ujitambulishe kwa wshika mafaili na uwaeleze wao watanufaika vipi na kukupa wewe tenda?

    ReplyDelete
  3. Good idea

    ReplyDelete
  4. hi inaweza kusaidia sana kama itakuwa endelevu maana sisi wadau wa kilimo kanda ya kaskazini tunapata shida sana kutegemea ndege za manati ha KIA na kucross border kwenda Jomo Kenyata ni cost, muda, na usumbufu wa mpakani, in brief hebu wasiliana na chama cha exporters TAHA ( just google their website) arusha watakupa in detailled information. asante

    ReplyDelete
  5. Nimeona tovuti yao inajengwa....ila nawapongeza sana hata hapo mlipo duu!!naupenda sana ujasirimali kama huoo...kupitia blog jamii aah mtapata kazi nyingi tu hasa arusha maua design...ingawa nasikia wana ushuru mkubwa sana heri muwe mnapakilia hk hk nairobi...kia noma

    ReplyDelete
  6. Anonym 01:09 wa April 05. Unapoona info@swahilitravei.co.uk inaashiria kuwa kuna tovuti fulani hapo hapo...nakushauri ujaribu www.swahilitravel.co.uk utaona kuwa wako katika kazi ya kutengeneza hiyo tovuti unayoulizia...nadhani nimekusaidia kwa kadri niwezavyo. Ikiwa bado, basi wasiliana na hao swahili travel katika anuani ya barua pepe waliyotupatia katika tangazo lao.

    ReplyDelete
  7. Tovuti ya nini mbona watz wabishi. Amekupa email inayoeleweka na namba za simu. What else do you people need? Kama huna cha ku-export kaa kimya wajanja wachape kazi.

    ReplyDelete
  8. WADAU WA UK TUELEZENI. HIZI SIMU NI ZA MOBILE AU LANDLINE?? TUWEKANE SAWA KWANZA..

    Mimi

    ReplyDelete
  9. Web sawa lakini hiyo Website mbona kama inahusu mambo ya Tours tu ya Tanzania,?? mi nahisi kuna jambo hapo huyu anajidai tu, yaani wazungu nao akili zao ni matope au?

    ReplyDelete
  10. Anon 08:49 sasa huko kujidai unamaanisha nini
    Hao wazungu unaowatukana wamukosa nini ?
    Kama wangekuwa na akili za matope wangewatawala ?
    Labda nyie ndio wenye akili za matope hata umeme wa uhakika unawashinda

    ReplyDelete
  11. Watu wengine bwana sasa hao wazungu wanahusika na nini mpaka kutukanwa
    Jamaa wameacha contact zao kama una hoja au wazo si bora uwasiliane nao

    ReplyDelete
  12. April fools day!!!!!!!!

    ReplyDelete
  13. hizo ni mobile sio landline
    landline zinaanzia 01,02 ukipiga from tz ni +441....au +442...

    ReplyDelete
  14. wangesema makaburu mngekimbilia haraka haraka.hongereni ndugu zangu watanzania.

    ReplyDelete
  15. Hili ni wazo zuri sana kukumbuka Tanzania kwni matunda bado yanaozea shambani ila sasa jinsi tusivyopendana
    Ushauri wangu bora endelea huko huko kenya Bongo watakufitini tuu

    ReplyDelete
  16. GOOD IDEA,NGOJA TULIFANYIE KAZI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...