Habari Kaka Michuzi.
Nilikuwa naomba kama mtu yeyote anayo au anajua sehemu ambayo ninaweza kupata CD inayoonyesha culture za watanzania kama music, ngoma na mambo ya tourism Tanzania. Kama unaweza kunipatia nitashukuru sana.
Ninataka kuonyesha hapa kwaajili ya kuweza kukuza na kuonyesha utamaduni wetu. Nikipata majibu upesi nitashukuru zaidi kwani muda umebaki kidogo.Sasa nafikiri majirani zetu wataonyesha vitu vya kwao basi nasisi tusiwe mbali.

Natanguliza shukurani.
Wasiliana na mimi kwenye email ifuatayo:
Kimandolu@hotmail.com.
Mdau California

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nimefurahishwa sana na huyu bwana anayeipenda nchi yake na utamaduni wake.Hili limenigusa ni vema nikamjulisha huyu bwana kuwa aende makumbusho pale njiani kuelekea mwenge atapata kila kitu cha kila kabila ngoma, nyimbo, mavazi, nyumba, unyago na jando vyakula nk,ukihitaji msaada zaidi tutakusaidia

    Mama Bishanga
    Washington
    DC

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...