Makamu Mwenyekiti wa Bunge la China Mhe. Yan Junqi ambaye yupo Dodoma kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine, akifurahia zawadi ya vinyago toka kwa Spika Mh. Samwel Sitta. Ziara yake inakusudia kuimarisha ushirikiano kati ya Bunge la China na Tanzania.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge la china Mhe. Yan Junqi akitambuliswa kwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda mara alipowasili bungeni Dodoma
Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta (wa tatu kulia) akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mazungumzo baina ya Ujumbe wa makamu Mwenyekiti wa Bunge la china Mhe. Yan Junqi ( Mwenye Nyeupe Kushoto) katika kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Spika Bungeni Dodoma . Makamu Mwenyekiti huyo wa Bunge la china , yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine, ziara yake inakusudia kuimarisha ushirikiano kati ya Bunge la China na Tanzania.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge la china Mhe. Yan Junqi akisisitiza jambo katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika Ofisi ya Spika Bungeni kati ya Ujumbe wa Tanzania kwa kuongozwa na Mhe. Spika. Kulia ni Balozi wa China nchini Mhe. Liu Xinsheng na kushoto ni Mkalimani wa ujumbe huo Bi. Shi Meiqi. Makamu Mwenyekiti huyo wa Bunge la china , yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine, ziara yake inakusudia kuimarisha ushirikiano kati ya Bunge la China na Tanzania
Makamu Mwenyekiti wa Bunge la watu wa China Mhe. Yan Junqi akifurahia picha ya jingo la Bunge mara baada ya kukabidhiwa na Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta Dodoma leo. Kulia ni kaimu katibu wa Bunge John Joel. Mhe. Junqi yupo katika ziara ya siku Moja nchini ambapo anatembelea Bunge la Tanzania ikiwa ni njia ya kuimarisha ushirikiano kati ya Bunge la China na Tanzania.
Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, akifurahia mojawapo ya Kompyuta ndogo nne ( Laptops) alizokabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la China Mhe. Yan Junqi ambaye yupo Dodoma kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine, ziara yake inakusudia kuimarisha ushirikiano kati ya Bunge la China na Tanzania
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda, akimpokea katika viwanja vya Bunge, Makamu mwenyeki wa Bunge la China ( National Peoples Congress) Mhe. Yan Junqi mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Bunge. Makamu Mwenyekiti huyo pamoja na ujumbe wake wapo katika ziara ya siku moja nchini ambapo anatembelea Bunge la Tanzania.
Makamu mwenyeki wa Bunge la China ( National Peoples Congress) Mhe. Yan Junqi (kulia) akisindikizwa kuingia katika ukumbi wa Bunge mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Bunge.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge la watu wa China Mhe. Yan Junqi ( wa pili kushoto) akifuatilia kipindi cha maswali na majibu katika ukumbi wa Bunge Dodoma. Mhe. Junqi alikuwa katika ziara ya siku Moja nchini ambapo anatembelea Bunge la Tanzania kujionea mambo mbalimbali.
Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. tehe..tehe...tehe..tihii! tofauti ya zawadi ya vinyago na kompyuta!

    ReplyDelete
  2. nani kakwambia wachina wanaitana "MHESHIMIWA" wewee?aya ni mambo ya kujitukuza kwa wabongo tu km mungu...inakera na eti usipomwita ivo anaona umemtukana na kumshisha hadhi,,lifutwe ili jina la MHESHIMIWA muitwe tu bwana/bi ful stop

    ovyo kabisa eti mheshimiwa

    ReplyDelete
  3. Yaani sisi tumekuwa watu wa vinyago tu....Nenda Marekani vinyago, Ulaya vinyago, China vinyago...Tangu zama za kale hadi enzi za sasa! Hii kitu vipi!?

    ReplyDelete
  4. sasa mnaponda nini vinyagoio ndo mnavyoweza tengeneza tu kuna lipi lingine.lazima ukubali asili yako wewe ni kinyago na ngoma tu. computer za waupe.

    ReplyDelete
  5. mzee wa bunjuApril 21, 2010

    Chonhe chinde Mh, wa china usituletee mambo ya kung fu bungeni sisi wenzenu tuna vitambi, manbo ya kuumizana kabla ya mswada kupita hatuyawezi

    ReplyDelete
  6. Chinese are true hustlers.They fake it till they make.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...