Habari zilizotufikia punde: Imetaarifiwa kutoka Jijini Brussels nchini Ubelgiji kuwa bia ya Ndovu Special Malt imepata Medali ya Juu ya Dhahabu ya Viwango mwaka huu 2010 kutoka katika Taasisi ya Monde Selection iliyopo nchini Ubelgiji. Hii ni mara ya kwanza kwa bidhaa iliyozalishwa hapa nchini Tanzania kuwahi kupata medali ya juu ya kiwango hiki. Jopo maalum la majaji walioteuliwa na Taasisi ya Monde Selection huonja kwa nyakati tofauti tofauti vinywaji vya bia kutoka nchi mbalimbali duniani. Ili kuweza kupata tuzo ya medali hii ya hali ya juu ya Grand Gold Quality Award, bia husika lazima ipate matokeo ya wastani wa jumla usiopunga kati ya alama 90 – 100 %. Kitu ambacho kwa hali ya kawaida si rahisi kufikiwa lakini haikuwa hivyo kwa bia ya Ndovu Special Malt.
Hii yote imeweza kufikiwa kutokana na utaalam na uzoefu kwa kupika bia yenye kimea maridhawa kilichoiva kinachoipa bia hii harufu nzuri, rangi ya dhahabu iliyokolea na ladha tamu ya kimea, huku ikiwa haijaongezwa kemikali za kuhifadhia.
Kufuatia uchunguzi juu ya unywaji wa bia katika soko la hapa nchini Tanzania, wataalam wanasema kuwa wapenzi wengi wa bia wameiweka Ndovu Special Malt katika kundi la aina yake la ‘Beyond the Ordinary, na ya kipekee, hapa nchini hata kimataifa.
Akitoa hisia zake za furaha kufuatia tuzo hii iliyopata bia ya Ndovu Special Malt, Mpishi Mkuu wa bia katika kiwanda cha bia cha TBL, Bw. Gaudence Mkolwe alisema, “Sisi hapa TBL tupo kutimiza lengo moja tu ambalo ni kuendelea kutengeneza bidhaa za hali ya juu ambazo zinatambulika kimataifa na ushahidi ni hii tuzo ya medali ya juu ya dhahabu iliyopata bia yetu ya Ndovu Special Malt. Hii kweli ni bia halisi ya Kitanzania yenye viwango vya juu”.
Kwa Taarifa zaidi wasiliana na:
Oscar Shelukindo, Ndovu Special Malt Brand Manager,
Client Service Manager-Media,
+255 754 319019,
frank@ayr.co.tz
Kuhusu TBL
Tanzania Breweries Limited (TBL) inatengeneza, kuuza na kusambaza bia, vinywaji vyenye ladha ya matunda vilivyo na kilevi na vinywaji visivyo na kilevi hapa Tanzania. TBL pia ndiyo kampuni mama ya Tanzania Distilleries Limited pamoja na kampuni shiriki ya Mountainside Farms Limited.
Bia zinazotengenezwa na kampuni ya TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Pilsner Ice na Pilsner Lager. Bia nyingine kubwa zinazotengenezwa na kundi la makampuni ya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redd’s Premium Cold na Konyagi Ice.
Kundi la makampuni ya TBL limeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam, limeajiri watu wapatao 1,300 na linawakilishwa nchi nzima na viwanda vitatu vya bia, kiwanda kimoja cha kutoneshea, kimoja cha kutengenezea kimea pamoja na bohari 9 za kusambazia bia.
Kuhusu SABMiller
SABMiller plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabar matano. Bia zake ni pamoja na zila za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji nchini India.
SABMiller imeorodheshwa kwenye

masoko ya hisa ya London na Johannesburg.

Ni katika jitihada za kutufanya ma-native tukubali uwekezaji, kwa maana ya kwamba, hao waliotoa hiyo tuzo ni damdam na hao waliopewa hiyo tuzo, then wao wanapeana 10% baadae. Ni mojawapo ya Marketing Stratergy.
ReplyDeleteNdani ya siku mbili tatu utasikia imepandishwa bei, looh wametuponza wapenzi wa kinywaji hiki.
ReplyDeleteWengine wanaamini kuwa baia ni bia tu. Lakini kuna tofauti kati ya malt, ale na lager!
ReplyDelete