Na John Kitime
Hatimae inataka kuwa. Kama ambavyo wapenzi wengi wa Blog ya www.mwakitime.blogspot.com
wamekuwa wanaomba, mwanga umeanza kuonekana kuwa itawezekana.
Wenye afro zao wazitimue au wakachome tena nywele hahahaha, wenye raizon zao, wenye slimfit zao,(kama zitawatosha na hivyo vitambi hahaha), wenye mashati ya ndege, wenye superfly, pekos, maxi, midi, mini, raizoni (sio Yanga) wazitoe vumbi maana wanamuziki wa zamani wameamua kuwa watafanya show moja kubwa ambapo wanamuziki wa muziki wa dansi na disko toka enzi za buggy watapanda tena stejeni na kujikumbusha mambozzz yalivyokuwa.
Onyesho hilo ambalo pia litahusisha Madjs wa enzi hizo linategemea kufanyika mwezi July, hususan siku ya SabaSaba, kama mambo yakienda mswano.
Tayari Kilimanjaro bendi wana Njenje wametoa vyombo na eneo la mazoezi na wanamuziki kadhaa wamekwisha jitokeza kukubali kushiriki. Fuatilia katika blog hii upate kujua nani na nani watakuwepo. Mapato ya onyesho hilo yataenda kwenye huduma ambayo itatajwa baada ya siku chache.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kwa hiyo kandambili watakuwa mashakani. Tunaomba Raizon ya kweli irudi kama zamani yaani chama la maboni nalo lirudi kama zamani - kwani tumechoka kuvaa kandambili. PAN HOYEE

    ReplyDelete
  2. kwa sisi wakazi watandale itakuwa kazi kuvaa hiyo midundo kutokana na barabara zetu nakiza cha usiku mbona mnataka kutuvunja miguu

    ReplyDelete
  3. Kaaa wanjameni, hizi ngoma zinajina lake maalumu, teremka tuzoze, ha ha ha ha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...