Monument De La Renaissence Africaine kwa kifaransa.
Tukitafsiri maneno hayo kwa kiswahili yana maana,
Mnara wa kuzaliwa upya kwa Africa.
bendera zetu

Kaka Michuzi wawekee wadau waone hii ikiwezekana fikisha taarifa kwa wakubwa marekebisho yafanyike.

Mimi ni mmoja wa watanzania wengi tulichomoka bongo kwenda nje kutafuta maisha. Nafanya kazi nchini Mali Africa ya Magharibi. Juzi Jumatatu nilianza safari ya kuja Bongo kupitia Dakar Senegal. Kutokana na mushkeri kidogo sikuweza kusafiri siku hiyo na ikanibidi kubakibaki kidogo hapa Dakar. Basi nikaona wacha nizungukie sehemu za vivutio, sehemu ya kwanza kwenda ilikuwa ni kwenye mnara mpya uliojengwa katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Senegal.

Mnara huo inaitwa "Monument De La Renaissence Africaine" kwa kifaransa. Tukitafsiri maneno hayo kwa kiswahili yana maana, "Mnara wa kuzaliwa upya kwa Africa". Kutokana na maana hiyo nzuri tu, eneo hilo la mnara limepambwa na bendera za inchi zote za Africa. Ila kuna dosari ndio nataka nikueleze hapa kaka, michuzi umakini nimeona una maana sana mtu unaposafiri. Niliona bendera ya Tanzania tu pekee imejitokeza mara mbili, moja imewekwa karibu na bendera ya Liberia na nyingine imewekwa karibu na bendera ya Mali. Isipokuwa ile iliyowekwa karibu na bendera ya Liberia imegeuzwa kichwa chini miguu juu!! Kwa kawaida bendera ya Tanzania rangi ya kijani huwa juu!! na rangi ya bluu huwa chini.

Sasa hapa mkuu nikajiuliza kulikoni!!! Sikupata jibu kazi yangu ikawa ni kupiga picha kama vile mwandishi. Nazituma picha hizo kwako na nimeweka kwenye face book yangu hapo http://www.facebook.com/photo.php?pid=5536411&id=595568447#!/photo.php?pid=5536611&id=595568447&fbid=432484023447

ili wadau muzione na tuone jinsi inavyopasa kuwa makini na kutete uzalendo. Sisemi hawa jamaa walifanya kusudi, inawezekana ni makosa tu ya kibinadamu mtu alipitiwa. Nilituma ujumbe kwa wizara ya utamaduni ya Senegal kuwaeleza juu ya tatizo hilo, hiyo email nitakuforwadia ila usiiweke hewani.

Nikataka nitumie email hiyo hiyo kwa wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania ili wawasilaine na ubalozi wa Senegal uliopo Tanzania kuomba marekebisho. Bongo tambarare kama mnavyosema, nikakuta website ya wizara hiyo haipatikani na kwa hiyo sikupata mawasiliano. Website ya wizara link hiyo hapo kaka jaribu na wewe uone http://www.mfaic.go.tz/

Natumaini wadau mmnenisoma!!
MDAU CNN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. huo ni moja ya ufisadi,wananchi wanalalamika miundombinu mibovu wao wameenda kujenga mnara kwa pesa nyingi sana za walipa kodi.

    ReplyDelete
  2. mdau wa senegal ushukuriwe sana kwa jicho lako la umakini, ila hata mabadiriko yakifanyika ulete hiyo view/taswira

    The Minister Science & Technology 2015

    ReplyDelete
  3. HAO WAMEFANYA UZURI KWA KUWA HAWAKUJUA IPI SAHII KWA HIYO NDO MAANA WAKAWEKA MBILI-HIYO MOJA NI TANZANOS NA NYENGINE NI TANZANIA

    ReplyDelete
  4. We kweli mzalendo,au kwa vile zilikuwa mbili ukagundua tofauti?Mie hata ningekuta imegeuzwa ya Ikulu nsingeshtuka.LOL.

    ReplyDelete
  5. Nchi yenyewe iko miguu juu kichwa chini kwa umasikini, watu wake wako mguu nje mguu ndani kama wewe na diaspora, bendera kijani chini bluu juu, who cares!!

    ReplyDelete
  6. Hata hiyo ambayo ndugu mdau unasema iko sawa nayo imekosewa, Rangi ya Bluu inatakiwa iwe chini upande wa mlingoti.

    ReplyDelete
  7. Ankal, huyu mdau wa Senegal anastahili pongezi kubwa kwa jicho lake. Inahitaji umakini mkubwa sana kugundua blanda iliyofanywa na watu hawa. Inamaana hata balozi wetu kule senegal ameshindwa kubaini pamoja na kuwa huko na ndio moja ya kazi za ofisi yake. Labda watuambie hiyo bendera nyingine ni ya nchi gani, labda kuna nchi tunafanana bendera na kutofautishwa na "turns" za rangi.
    By the way, mdau wa Senegal tunaposema bongo tambarare ni tambarare kweli!! Suala la tovuti ya wizara kutofunguka ni jambo la kawaida sana maana si hiyo tu bali zipo nyingi tu ambazo hazifanyi kazi. Kila kitu bongo take it easy!! Ha ha haaa....
    >>the gr8shuma>>>>>>

    ReplyDelete
  8. AMA KWELI UMEKOSA KAZI......WEWE NJOO BONGO, KULA VACASHIONI YAKO, THEN RUDI HUKO ULIKOAMUA KWENDA KUBEBA BOKSI....SISI HAPA BONGO NI TAMBARARE TU.

    ReplyDelete
  9. Mdau Mbogela tumia akili yako ya darasa la tatu.Hiyo bendera unayodai imekosewa ipo sahihi. Ni upepo umefanya igeuke upande wa kushoto(pichani). Angalia bendera zote zinaelekea upepo unapoelekea.

    ReplyDelete
  10. Nashukuru mdau uliyesaidi kumwelewesha Mbogela, maana nilishangaa maoni yake wakati milingoti inaonekana kwenye picha na mwelekeo wa bendera zote pale inaonyesha upepo unavuma kuelekea upande gani.

    Na ninasifu wote mnaotoa maoni chanya.

    ReplyDelete
  11. Ndugu Mdau wa Thu Apr 22, 03:12:00 PM,Mbogela anaongelea ile bendera ya pili kule kushoto, ile ndogo, sio hii kubwahapa mbele. Ile ndio iliyopinduliwa, bluu iko upande wa juu ilhali inatakiwa iwe upande wa chini mwa bendera yetu.

    ReplyDelete
  12. Mbogela,kwani kamba za kufungia kwenye Bendera zinakuwa upande mmoja au pande zote mbili? Kama ni upande mmoja,basi unachokisema kama ni sahiihi labda yatakuwa makosa ya kiwandani.

    ReplyDelete
  13. Mdau, umechanganya kidogo, uliyosema imekosewa ndio iko sawa, na uliyosema iko sawa ndio imekosewa. blue iko chini siku zote, njano na nyeusi zinaanzia kwachini ya bendera sio juu ya bendera.

    ReplyDelete
  14. Ni nchi gani nyingine inazo bendera mbili katika huo mnara? .... vinginevyo bendera ya Tanzania haijakosewa hata kidogo!!!

    ReplyDelete
  15. Zote zimekosewa ile ya chini ndio Sahihi ila inatakiwa Green iwe juu Blue iwe chini kumbe tukipewa mtihani wa kuchora bendera Asilimia 10 tu ndio watapata naona hatari. Doto.

    ReplyDelete
  16. Hata wewe doto umeshindwa mtihani. iliyokosewa ni moja tu ya chini.

    Bendera ya TZ


    kijani********
    *****o*i******
    ****n*s*o*****
    **a*u*n*******
    *j*e*a********
    n*y*j*********
    n*n*******blue

    hapo juu ni bendera yetu, soma rangi za njano na nyesi diagonally (sijui kwa kiswahili).

    ReplyDelete
  17. Ankal Michuzi nimerudi tena; Bendera ya Taifa huwa Kijani juu na Bluu chini. Rangi ya Bluu huwa upande wa mlingoti hiyo haitegemei upepo.

    ReplyDelete
  18. E bwana eeh mie naona huyu mshkaji wa senegal ni bonge la kichwa. nadhani huyu anayesema amekosa la kufanya yeye ndo kakosa la kufanya maana lait ungejua uthamani wa TZ usingeropoka hivyo. na pole sana maana hata ukiiona bendera ya tanzania inazikwa utashangilia, na hiyo ndo dalili mojawapo ya kuuza uzalendo wako. kwanza inawezekana we mwenyewe hata rangi za bendera umezijua baada ya mskaji kuona makosa yaliyofanyiwa bendera yetu. huo ndo uzalendo wetu wakujivunia popote pale tulipo na usitegemee kutukuza cha mwenzio wewe ni mtumwa wa kuichukia nchi yako yenye amani na inayokupa uhuru uutakao to the max. pole mdau. hongera msenegal

    ReplyDelete
  19. Zungu Wa MbiziApril 23, 2010

    Bw. Mbogela Jackson upo sahihi kabisa, tatizo wadau wameshindwa tu kukuelewa....Rangi ya Bluu inatakiwa iwe chini ikianzia kwenye mlingoti....Wadau jaribuni kutafakari hilo ndipo mtatuelewa mimi na Mbogela tunachokikosoa...hivyo basi kwa mantiki hiyo ni wazi bendera zote hizo mbili za TZ zimekosewa!!!

    ReplyDelete
  20. mdau mtoa mada ndugu clarence ndunguru nimeingia kwenye facebook page yako, aaaaargh kumbe umeoa na watoto juu bwana, kumbe huna ishu mimi nilikuwa ninafikiria jinsi ya kukunasa ili nije tuishi wote huko bamako mali.

    ReplyDelete
  21. ANKAL,Kutokana na maelezo ya Mbogela hapa kumeibuka ubishi mpya kwamba kati ya KIJANI na BLUU ni ipi inatakuwa sehemu yake pana iwe upande wa mlingoti? Hilo la ipi iwe juu halina mjadala tena.Hebu kuwa Jaji kwenye hili la pili

    ReplyDelete
  22. Jamani mimi namshangaa huyu anasema kumbe clarence ameoa na watoto juu anafikiri kwa kutumia ubongo au makalio? maana naona ameingilia afair za watu. habari ya kuoa ni ya mtu binafsi kakangu kama we hujataka kuoa basi usiwaboe wenye ishu zao. na wewe ukitaka oa aalah!

    ReplyDelete
  23. Tukubaliane kwamba mojawapo ya hizo bendera itakuwa imekosewa kupandishwa kwenye mlingoti.

    Sasa hili la bendera mbili wadau limekaaje. Kwamba sisi wakarimu sana tuliombwa moja tumetoa mbili au zimezagaa zagaa tu kote kote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...