keki ya maadhimisho miaka 37 ya dojo la Okinawa Karate-Do Tanzania kabla ya kukatwa usiku huu kuadhimisha siku ya Sensei Bomani Day katika ukumbi wa shule ya msingi ya Zanaki Jijini Dar. Dojo hili lilianzishwa rasmi mwaka 1973 na Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika Sensei Nantambu Camara Bomani ambaye sasa ni marehemu. Lilianzia YMCA kabla ya kuhamia (DA) Shule ya sekondari ya wanawake ya Kisutu, baadaye Diamond Jubilee kabla ya kuelekea Zanaki secondary school na sasa lipo Zanaki Primary school. Mamia ya wanafunzi wamepita hapo katika nyakati tofauti. Sifa kuu za dojo hili ni nidhamu ya hali ya juu ambapo hadi sasa hakuna kesi ya vurumai inayomhusisha mwanafunzi wa hapo.
wanafunzi waandamizi katika onesho la 'kumite'

wanafunzi watoto wa chini ya miaka 15 wakicheza kata
wanafunzi watoto katika 'kumite'
wanafunzi wakubwa katika kumite
sehemu ya wageni waalikwa
wageni waalikwa
Mkuu wa dojo Sensei Malekia akitambulisha wanafunzi
pamoja na kukatika umeme sherehe ziliendelea kwa umeme wa jenereta....

Mgeni rasmi Sensei Daudi Magoma Nyamuko (fulana ya rangi ya chungwa) akijiandaa kukata keki. Kulia kwake ni Sensei Heri Kivuli. Wote hawa ni wanafunzi waandamizi enzi za Sensei Bomani ambapo Sensei Magoma alikuwa ndiye mwanafunzi mkuu
Senpai Rashidi Almasi akimlisha keki Sensei Heri Kivuli
Ankal, ambaye pia ni mmoja wa wanafunzi waandamizi hapo dojo, akimlisha keki Sensei Bomani
baadhi ya wanafunzi wa dojo hili
wanafunzi waandamizi wakiwa wamesimama nyuma ya
wanafunzi waliopandishwa daraja usiku huu. wawili walipanda kuwa mkanda wa kijani toka mweupe, wawili wengine walipanda mkanda wa kahawia toka kijani na moja alipata mkanda mweusi toka wa kahawia
wanafunzi waandamizi wakiwa tayari kufanya vitu vyao
mwanadada wa umri wa miaka 15 akipanda ngazi
toka mkanda mweupe kwenda wa kijani
mkanda kahawia toka wa kijani
mkanda mweusi toka wa kahawia
Sensei Malekia akimtambulisha bingwa wa Kick boxing nchini Japhet Kaseba ambaye pia ni mwanafunzi wa dojo hili
shaba lilikuwepo baada ya maonesho....
ubwabwa kwa wageni
nguna
wageni waalikwa wakijichana
wanafunzi wakipata mlo
mpunga baada ya kazi ngumu....



























Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Kwa kumbukumbu zaidi Dojo liliwahi kupita Diamond Jubilee kwenye miaka ya 1974 na 1976.

    ReplyDelete
  2. picha ya muanzalishi ipo wapi?

    ReplyDelete
  3. Hongereni kwa kuendeleza ngoma za Goju Ryu na nidhamu. UJIMA! KUJICHAGULIA!!! Naisikia sauti ya sensei Bomani ikibweka kwa KIAI !!!
    Ankal ahsante kwa picha ya mwanafunzi mkuu wa kwanza kabisa, Sempai Daudi Magoma. Daudi ulikuwa hucheki enzi hizo, hukutaka masihara; naona leo umetabasamu mpaka na keki unasakatia mkuu? Je, akina Sempai Mabruki (1974-75) wako wapi?...
    MOYO JUU!!!

    ReplyDelete
  4. ACHA MKWARA ANKAL

    WEWE MWANAFUNZI WA DOJO?

    HONGERA

    ReplyDelete
  5. Hongera za miaka 37 ya kuzaliwa kwa "Hekalu la Kujilinda"Karate -Do (Mwenendo wa sanaa za mikono mitupu)Tanzania!!Pia ni kumbukumbu kumbwa kwa M-sansei wote hapo katika picha, Sensei Magoma Nyamuko Sarya(salamu nyingi sana), Sensei W. Melkia,Sensei Kheri Kivuli, Sensei Ndaukile, Sensei Mbezi, Sensei Iddi Mzuri, Sensei Rashid Almasi, na Sensei Murudker, hongera kwa juhudi za moyo na nidhamu katika kufundisha Karate.Hongera pia Senpai M.I. Michuzi!!

    Sensei-Rumadha Fundi.

    ReplyDelete
  6. Mimi sikuwa mwanafunzi wa Sensei Bomani Camara, lakini nilipata bahati ya kufahamiana naye miaka ya 70: Alikuwa ni Mmarekani mweusi aliyeamini kuwa bara lake la asili ni Afrika. Aliamini kuwa Waafrika hatuna budi kufanya kazi kwa nia, bidii, umoja, ujima na ujamaa ili tuweze kujitegemea na kuwa karate ilikuwa lazima ichukuliwe katika uhalisi (context). Pia nakumbuka kuwa alioa Zanzibar. We should never forget his spirit and contribution.

    ReplyDelete
  7. Huyo aliripoti hii taarifa inabidi awe Papaa Sensei. Lugha nzuri ya kuripoti.

    ReplyDelete
  8. Tunashukuru kwa kuwezeshwa kuli-kick-ilia mbali Box! Na Lishindwe!

    ReplyDelete
  9. Jamani naupenda sana huu mchezo kwa ajili ya wanangu, ila tatizo naishi mbali na hapo Zanaki Primary ebu mtufikirie sisi wakazi wa Boko.
    Natanguliza shukrani zangu

    Mdau wa Boko

    ReplyDelete
  10. Mr. Bomani began his martial arts training in Africa in the 1906s. By 1968, Mr. Bomani, had traveled to Okinawa and began training with Eiichi Miyazato Sensei at the Jundokan. Mr. Bomani was a student of Miyazato Sensei’s, until Miyazato Sensei passed away in 1999. Since that time he has trained under Koshin Iha Sensei.





    Mr. Bomani was responsible for introducing Jundokan Gojuryu to Tanzania and he founded the Tanzania Okinawa Gojuryu Karate Association. Mr. Bomani was also instrumental in spreading Jundokan Gojuryu through out the United States. He founded many dojos in New York, Washington, Kentucky and Ohio. He has left several yudansha spread across the United States and Africa.





    Mr. Bomani continues his affiliation with the Okinawa Gojuryu Karate-do Kyokai, he continues to visit and train in Okinawa and he spends a great deal of time traveling between his various branch dojo. All of his Gojuryu grades were issued by Eiichi Miyazato Sensei.
    http://gokenkan.com/bomani.aspx

    ReplyDelete
  11. Kwa wale wasiomjua Issa Michuzi waulize pale Zanaki.Issa Michuzi ana Mkanda wa Brown wala msifanye naye mchezo...Kuweni makini

    Michuzi is also an ardent martial arts lover, holding a Brown Belt in Okinawa Goju Ryu Karate attained in 1995 at the Zanaki Dojo under Sensei Nantambu Camara Bomani.

    ReplyDelete
  12. Kwa wale wale ambao waliishi A-Town, naomba kuuliza, Sempai CHOGORO, SEMPAI WILLIAM, SEMPAI MTUMWA WAKO WAPI?

    Hao dio walikuwa wataalamu wetu pale mjini.

    ReplyDelete
  13. Ankal wacha mikwara kwa kutangaza nawe mwanafunzi wa hii kitu.

    Kila siku vekesheni sasa mazoezi saa ngapi?

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  14. Anonymous from Gokenkan. You have written Bomani started training in 1906. That must be an error. Did you mean 1960's???

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 07, 2010

    pongezi kubwa zimuendee sensei rashid almasi,sensei malekia,senpai sefu sudi na namuona yupo na ndugu yake salum sudi,
    kila la heri dojo ndio maisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...