Amani akiwajibika vilivyo
Mwimbaji maarufu nchi Kenya, Amani kwa mara nyingine tena aliwafurahisha wapenzi wa muziki jijini London baada ya kuangusha shoo moja matata sana. Amani ambaye yupo nchini uingereza kwa ziara ya mwezi mmoja, alifanya show yake ya tatu katika ukumbi wa Club Africa iliyopo Canning Town, London. Show hiyo ilionekana kumefana sana kwani wapenzi wengi walionekana kuridhika na minenguo na kipaji cha uimbaji cha mwanadada huyo. Mwandishi wa wa Blog ya TZ-ONE, Ally Muhdin alipowahoji wapenzi wa nyimbo za mwanadada huyo, walisema kuwa sauti ya mwanadada huyo na mashahiri ya nyimbo zake zimewafanya waridhike na tamasha hilo. Vilevile unenguwaji wa mwanadada huyo umewaridhisha sana
Wanablog maarufu jijini London, Bi. Jestina George na mhariri wa blog ya TZ-ONE Ally Muhdin wakiwa katika tamasha Amani lililofanyika Club Africa, London




Heko wana-diaspora tunawaona
ReplyDeleteGreat vocal! Ila hizo beats za wakenya zinanikumbusha wali maharage na jua la bongo.
ReplyDelete