manahodha na waamuzi kabla ya mpambano
Simba wakipiga dua kabla ya kuanza mtanange
Benchi la ufundi la simba chini ya kocha Patrick Phiri (shoto), meneja Innocent Njovu (wa pili shoto) na Kocha msaidizi Amri Saidi na wachezaji wa wakiba

simba wakifurahia bao la kwanza
Furaha ya ushindi
Mussa Hassan Mgosi akinyanyasa waarabu
walikuwa wakimkaba mgossi wawili wawili lakini wapi..
Emmanuel Okwi akiandika bao la kwanza dakika ya 53
Mussa Hassan Mgosi akipia la pili dakika ya 71
Goooooaaaaaaal!!!
Picha zote na Francis Dande wa Globu ya Jamii.
WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Simba leo wameibanjua Haras El Hadoud ya Misri bao 2-1 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Simba oye!
----------------------------
Kunradhi wadau. Kutokana nma matatizo yaliyokuwa nje ya Globu ya Jamii taswira hizi zimechelewa kupandishwa. Tunawataka radhi kwa usumbufu wowte uliotokea. Mitambo ya mwenyeji wetu (host) ilikuwa na kwikwi kwa muda ila sasa mambo ni mswano na Libeneke kama kawa.
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Wamebahatisha.

    ReplyDelete
  2. Hongera Simba. Bila ya shaka mechi ya marudiano ndio itakayoamua hatma ya Simba. Nina imani yatajirudia ya 2003 Simba ilipoitoa Zamalek kwa mikwaju ya penalti. Simba ijiandae vizuri.

    ReplyDelete
  3. MARKHABAA!

    ReplyDelete
  4. Tunaomba wasifu wa hiyo timu ya Haras..msaada tutani.

    ReplyDelete
  5. mechi ya marudiano ni simba 0 alhdoooood 1 haaaaaa haaaaaaaa haaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!
    mnoko wa wanoko

    ReplyDelete
  6. Hongereni sana watani, Mungu awaongoze na kuwajalia ushindi mwingine katika mechi ya marudiano!

    ReplyDelete
  7. Hizo taswira haziwekwi tu hapo tuzione jamani,haswa sisi wa ughaibuni,au huo mchezo umechezwa RUKWA nn,mnasubili gari litoke SIMBAWANGA lilete hizo taswira,haaaaaaaa ankal unatuangusha bana

    ReplyDelete
  8. TWAZISUBIRI HIZO TASWIRA JAMAN AU KWA KUWA NI SIMBA,MWATUBANIA ANKAL,UTAZANI HUO MCHEZO UMECHEZWA SUMBAWANGA BWANA

    ReplyDelete
  9. Ankal......nimeona kwenye libeneke la Mohammed Dewji, jamaa ameenda kushuhudia MSimbazi wakifanya mauaji, naona jamaa atarudi SImba....akirdui naona anaweza akatupa furaha ya Zamalek......
    Goli la pili midadi ikawa mingi kwa MO sasa kwa nini asirudi SImba .....

    ReplyDelete
  10. mdau mtoa maoni wa kwanza anaroho mbaya hana hata uzalendo. timu moja nchi nzima inawakirisha kimataifa then unasema wamebahatisha we unataka washinde mangapi ndo uone wanaweza.
    haruuuuuuuuuuuu, kitu kinapaa hicho wacha simba iwape raha mashabiki wake na taifa mwaka huu.
    hongera wekundu wa msimbazi.
    msibweteke misri pachungu sana hasa ukiwa kwao.

    ReplyDelete
  11. uwanja mbona upande huo hakuna watu?
    wabongo kwa kutopenda michezo?ndo maana vitambi nyama-uzembe weee
    hongera simba

    lol

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...