MCHAKATO WA MIAKA MINNE (2006 -2010) WA KUTAFUTA MAREKEBISHO YA SHERIA ZINAZOHUSU HAKI YA KUPATA HABARI USIPUUZWE NA SERIKALI
Mnamo Aprili 14, 2010 katika kikao cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma, Mheshimiwa Damas P. Nakei, Mbunge wa Babati Vijijini aliuliza swali bungeni akitaka kujua kuna mipaka gani katika kupata taarifa kutoka serikalini na kuna taarifa gani ambazo mbunge anaweza kukataliwa akiziomba.
Swali hilo na lile la nyongeza la Mhe. Nakei na lingine lililoulizwa na Mhe. Zitto Kabwe (Mb) yalijibiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mhe. Phillip Marmo (Mb) ambaye alibainisha haki na mipaka ya mbunge kupata taarifa kutoka serikalini akinukuu fungu la 10 la Sheria la Kinga, Madaraka na Haki za Bunge sura ya 296, toleo la mwaka 2002.
Mhe. Marmo wakati akijibu swali la nyongeza la Mhe. Kabwe alitoa kauli ambayo sisi kwenye Umoja wa Wadau wa Kutetea Haki ya Kupata Habari tumeona ni bora tuitolee tamko na ufafanuzi. Alisema:
“Masharti ni pamoja na hayo ambayo niliyataja katika majibu ya nyongeza, lakini pia ikumbukwe kama kuna mahitaji makubwa na duniani kote pale ambapo kuna mahitaji makubwa ya wananchi ikiwa ni pamoja na Wabunge kupata taarifa Serikalini kumekuwa na michakato ya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria ambayo inatoa maelekezo kwa ndani zaidi. Sheria hii inaitwa Freedom of Information Act kwa kawaida.
Katika nchi yetu, muda huu wote hatujapata msukumo wowote kutoka kwa jamii, kutoka kwa Wabunge hata vyombo vya habari. Kwa hiyo, ndio maana tumeendelea kutumia utaratibu huu ambao unatumika sasa.”
Mheshimiwa Samuel Sitta (Mb), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia alichangia kwa kutoa changamoto kwa wabunge kutumia Kanuni ya 81 ambayo inawaruhusu kupeleka miswada binafsi au kamati ya Bunge kupeleka muswada bungeni kwa kujadiliwa na kupitishwa.
Maswali ya Mhe. Nakei na lile la nyongeza la Mhe. Zitto na majibu ya Mhe. Marmo na mchango wa Mhe. Sitta katika mjadala huo yapo kwenye kumbukumbu za Bunge, yaani Hansard.
Umoja wa Wadau wa Kutetea Haki ya Kupata Habari umestaajabishwa sana na kauli ya Mhe. Marmo kuwa hapa nchini hapajakuwa na msukumo wowote kutoka kwenye jamii, wanahabari na hata wabunge katika kudai sheria ambayo itawapa haki wananchi kudai na kupata habari na taarifa mbalimbali ambazo zipo mikononi mwa serikali na taasisi na wakala wake.
MCHAKATO WA UMOJA WA WADAU WA HABARI
2006 - 2010
Mnamo mwezi Februari 2005, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ilifanyiwa marekebisho ya kumi na nne ambayo yalifuta na kutunga kifungu kipya cha ibara ya 18 ambacho kinatoa haki kamili ya kutafuta, kupata na kusambaza habari bila ya kujali mipaka ya nchi.
Hatua hiyo ya kimapinduzi imeonyesha kuridhia kwa serikali kutoa haki ya kupata habari kwa raia wake.
Hatua mbalimbali zimefuatia mabadiliko hayo ikiwa ni pamoja na kuandaa Sera ya Mawasiliano Serikalini ambayo, kwa mujibu wa taarifa za kuaminiwa, iliridhiwa na Baraza la Mawaziri la serikali ya awamu ya nne.

Mnamo mwezi Oktoba 2006, tukio jingine la kihistoria lilitokea kwa serikali kuchapisha rasimu ya Muswada wa Sheria ya Uhuru wa Habari, 2006 kwa njia ya tovuti.
Rasimu hiyo ya serikali ilifungua milango kwa wadau mbalimbali kuanzisha mjadala wa kitaifa kuhusu sheria hiyo ambayo kiutaalam na kwa kuzingatia kanuni na misingi ya kimataifa iliyojadiliwa hapo juu, ilibainika kuwa rasimu hiyo ya muswada inakiuka kanuni na misingi ya uhuru wa habari badala ya kuitekeleza.
Upatikanaji wa habari zilizomo katika asasi za umma na ulinzi wa wapiga filimbi (whistleblowers) ni miongoni mwa mambo yaliyopewa nafasi ndogo sana katika rasimu hiyo na vilevile habari nyingi zimeendelea kuwekewa kinga ya usiri. Alimradi rasimu hiyo ilionekana kuwa na mapungufu mengi na wadau waliikataa na kuiomba Serikali itoe muda wa kutosha ili waweze kukusanya mawazo ya wadau na kutoa mapendekezo yao. Maombi hayo yaliridhiwa na serikali.
Umoja wa Wadau wa Haki ya Kupata Habari unaojumuisha asasi kumi na moja za kiraia (mbili zikiwa nje ya Tanzania) ulifanya mikutano na midahalo mbalimbali nchi nzima ili kutekeleza mchakato wa upatikanaji wa sheria bora ya uhuru wa habari hapa nchini.
Mapendekezo ya wadau juu ya Sheria ya Haki ya Kupata Habari yaliandaliwa na kukabidhiwa kwa Serikali mnamo mwezi Agosti 2007 na nakala kusambazwa kwa wabunge wote ikiwa ni pamoja na Baraza la Mawaziri, Idara na Taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali nchini. Mapendekezo hayo yaliyowekwa rasmi yamejumuisha maslahi ya Taifa kwa ujumla wake ikiwa ni pamoja na kuweka misingi bayana ya namna gani raia wa kawaida anaweza akadai haki yake ya kupata habari. Takriban zaidi ya nakala 7,000 zilisambazwa kwa wadau mbalimbali na magazeti tofauti yalichapisha mapendekezo ya wadau ili wananchi waweze kuendelea kuyasoma na kuyaboresha.
Aidha, masuala ya huduma za vyombo vya habari, kama yalivyoainishwa na wataalam mbalimbali, yalitenganishwa katika mapendekezo hayo ya Umoja wa Wadau wa Habari na mapendekezo tofauti ya Muswada wa Huduma za Vyombo vya Habari yaliandaliwa na kukabidhiwa kwa Serikali mnamo mwezi Oktoba 2008. Nakala za mapendekezo hayo pia zilisambazwa kwa wabunge wote, Baraza la Mawaziri na idara na taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali.
Pia, Umoja wa Wadau umekuwa na mikutano miwili rasmi na Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Jenista Mhagama ambaye yeye na Kamati yake yote imetoa ushirikiano mkubwa katika kujadili na kuchambua mapendekezo hayo ya wadau na kuyaboresha zaidi.
Hata hivyo mpaka sasa, kumekuwa na ushirikiano mdogo mno kutoka Serikalini kufanikisha azma hii kubwa ya kupata sheria nzuri ya Haki ya Kupata Habari na sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari. Kwa mfano, hakuna jibu rasmi lililotolewa na Serikali kuhusu hatua zilizochukuliwa kuhusiana na mapendekezo hayo ya wadau.
Haijulikani kama mpaka sasa Serikali imeyakataa ama imeyakubali mapendekezo hayo ya wadau. Juhudi za Umoja wa Wadau kuweza kuwa na mkutano wa pamoja kati ya wataalamu wa serikali na kutoka kwa wadau ili kupata muafaka wa mapendekezo, zimegonga mwamba. Umoja wa Wadau ulimwandikia barua tatu rasmi Mhe. George Mkuchika (Mb), Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo mwaka jana yaani barua ya Februari 2, 2009 ; barua ya Septemba 8, 2009 na barua ya Novemba 30, 2009 ili kuweza kuwa na mkutano huo wa pamoja. Hata hivyo, hadi leo hakuna barua hata mmoja iliyojibiwa hata kusema tu imepokelewa !
Katika kikao cha pamoja kati ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Umoja wa wadau na Serkali kilichofanyika Januari 20, 2010, jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Joel Bendera(Mb) alisisitiza kuwa machakato wa sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari unaendelea na unaandikiwa hati uende kwenye Baraza la Mawaziri kauli ambayo imetamkwa pia na Waziri Mkuchika. Lakini wote wawili hawana maelezo juu ya sheria ya Haki ya Kupata Habari. Inaelekea imewekwa kando.
Inasikitisha sana na kukatisha tamaa kusikia kauli ya Waziri Marmo kuwa hapajakuwa na msukumo wowote kutoka kwenye jamii, wabunge au vyombo vya habari kutaka kuwepo kwa sheria nzuri ya kumwezesha kila mwananchi kuweza kupata habari anazohitaji. Juhudi ambazo zimefanyika hadi sasa ni kubwa lakini ni dhahiri kuwa serikali yetu haitaki kusikiliza mawazo ya wananchi katika jambo hili.
Haki ya kupata habari ni haki ya msingi ya kila mtu ambayo imelindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.
Ni jukumu la serikali kutunga sheria nzuri ya kuwezesha upatikanaji wa habari muhimu zinazomuwezesha kila mtu kutekeleza haki zake za msingi. Lakini kama haipo tayari kufanya hivyo, basi tunatoa wito kwa Bunge kufuata wito wa Mhe. Spika kutumia vyema kanuni ya 81 inayowezesha wabunge au Kamati ya Bunge kupeleka hoja binafsi ya sheria ya Haki ya Kupata Habari. Bila shaka Umoja wa Wadau utakuwa tayari kushirikiana na mbunge binafsi na pia na Kamati ya Bunge husika kufanikisha azma hii.
Kuwepo kwa sheria inayotekelezeka ya haki ya kupata habari kutawezesha Tanzania kupiga hatua katika duru za kimataifa na hivyo kufanikisha malengo ya milenia ikiwa ni pamoja na kupunguza/kutokomeza umaskini uliokithiri, kutokomeza vitendo vya jinai na kupiga vita rushwa, kuondoa ubadhirifu katika asasi za umma na za binafsi, na kuleta maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Umoja wa Wadau wa Habari unajivunia kuwa Watanzania walio wengi wameshiriki katika kufanikisha kuandaa mapendekezo ambayo yamewasilishwa Serikalini ya Muswada wa Sheria ya Haki ya Kupata Habari na Muswada wa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari. Pamoja na hayo, Umoja huo tayari umeshaandaa mapendekezo ya kanuni zitakazowezesha utekelezaji wa sheria hizo mbili kwa urahisi na bila kusababisha utata.
Ili kuhakikisha sheria hizo hazikinzani na sheria nyingine za nchi, mapendekezo ya wadau yametoa mwongozo kuhusu sheria zitakapokinzana. Aidha, inapendekezwa pia kuwa baadhi ya vifungu vya sheria pamoja na baadhi ya sheria nzima zifutwe ili kuwezesha utekelezaji rahisi wa sheria hizi mbili zitakapopitishwa na Bunge.
Umoja huo wa wadau unaogozwa na Baraza la Habari la Tanzania (MCT); na kuhusisha Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-Tan); Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA); Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS); Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC); Shirika la Elimu ya Sheria Tanzania (TANLET); Shirika la Msaada wa Sheria (nola); Chama cha Wamiliki wa Vyombo Vya Habari (MOAT) na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TNGP). Washiriki wengine wa Umoja huo ambao wamekuwa wakitoa mchango wa kitaalamu ni Commonwealth Human Rights Initiative (CHRI) ya India and Article XIX ya Uingereza.
Kajubi D. Mukajanga
Katibu Mtendaji
Baraza la Habari Tanzania na
Mwenyekiti wa Umoja wa Wadau
wa Haki ya Kupata Habari
April 20, 2010

Mhh! siamini ninachokisoma. Ina maana Waziri Marmo alikuwa nje ya nchi tangu 2005/06? Hapa inadhihirisha wazi kwamba hata huko ndani ya Govt hakuna haki ya Kupata/kupashana Habari. Ina maana Cabinet ikukutana wengine wanabania habari? Hongereni wadau na kamati ya Mh. Jenister Mhagama hakikisheni sheria hii inapita ili wa TZ wasiendelee ku-EPWA kodi zao.
ReplyDeleteBinafsi napata tabu sana kutafsri baadhi ya maneno yanayotumiwa na vingozi wetu huko serikalini kukwepa wajibu kama "Mchakato Unaendelea, imefikia katika hatua nzuri tu, muwe wavumilivu tu tutatatua tatizo hivi karibuni nk nk...Hakukuwa na sababu ya kuchelewesha Mswaada wa Habari kwa sasa kwa kuwa karibia hatua zote ulikwisha pitia.
ReplyDeleteLabda Serikali yetu inaona utakuwa ni kikwazo au hauna maslahi kwa Taifa.Lakini hilo litakuwa ni Kitendawili cha kale na Hadithi za "Alfulelaule"...Kwa nini Miswaada ambayo inasura ya maslahi ya viongozi zaidi imepitishwa haraka sana Bungeni Kama ule wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, Baraza La Usalama la Taifa; nk na huu wa Habari wanasema "mchahato bado haujakamilika??"..Huyo Mchakato anauchakata nani kama si hiyo hiyo Serikali? Na kama Bajeti ya Wizara ya Habari ilitaja kutumia Fedha za Umma katika kukamilisha Sheria hii ya Habari miaka miwili iliyopita, Je, Fedha hizo zilizotengwa zimetumika kufanya nini kama Muswaada wa Sheria haujaweza kwenda Bungeni mpaka leo?.
Ni hatua nzuri lakini tunapaswa kuwa makini kama tunahitaji Freedom of Information Act au Access to Information Act au Freedom of Speech Act. Sheria hizi zinafanana sana lakini si sawa. Tufanye upembuzi yakinifu. Haki ya kupata, kutoa na kusumbaza habari ni haki ya kikatiba. Ni budi kuwe na sheria inayotekeleza haki hiyo. Haya yote ni sawa na haki ya kuwa na faragha, haki hii iko kwenye katiba lakini hatuna Privacy Act. Huu ni mwanzo mzuri. Tuendeleze michakato hii kwa faida ya Tanzania yetu.
ReplyDelete