Viongozi wa muda wa Jumuiya ya watanzania London inawaomba watanzania wote waishio London kuhudhuria mkutano wa wana-London utakaofanyika ubalozini siku ya jumamosi tarehe 24-April-10 kuanzia saa 1100 asubuhi. Mkutano huu unategemea kuongelea maswala ya chaguzi wa viongozi na muundo mzima wa jumiya ya London.
Uchaguzi wa viongozi wa London unategemewa kufanyika tarehe 01-May-10. Mawazo yako ni mchango mkubwa kwa jumuiya na kama unazo sifa za uongozi na ari ya kuendeleza jumuiya mlango uko wazi kwa kila mmoja.

Asante,
G Mboya - Director of Communication
Viongozi wa jumuiya... inawaomba? Mkutano utaanza asubuhi saa 11? Director of Communications vipi hapa?
ReplyDelete11am au saa tano asubuhi, hii ya saa 11 asubuhi(a.k.a alfajiri)?!ni kali kuliko Director!
ReplyDelete