Na Mohammed Rama Mhina,
wa Jeshi la Polisi

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kuratibu Silaha ndogondogo hapa nchini, kesho Jumanne Aprili 27, 2010 saa 2.00 asubuhi itakutana ili kupitia maazimio ya mapendekezo ya mswaada wa kurekebishaji sheria za kumiliki silaha hapa nchini.

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika, amesema kuwa Mkutano huo ambao utafanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kuanzia saa 2.00 asubuhi, utawashirikisha baadhi ya Maafisa wa Wizara na Idara za Serikili zinazojihusisha na masuala ya kiusalama pamoja na baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mkutano huo ambao pia utahudhuriwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai utafunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Lawrence Masha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...