Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Omari Chambo akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi za Jamii na Maendeleo ya Makazi wa Msumbiji Bi. Maria Luisa Mathe(mwenye shati jeupe) na Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Bi. Fatma Salum Ally wakielekea sehemu ya juu ya Daraja la Umoja kukagua maandalizi ya sherehe za Uzinduzi wa Daraja hilo tarehe 12 mwezi ujao jana katika eneo la Mtambaswala wilayani Nanyumbu mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Omari Chambo (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi za Jamii na Maendeleo ya Makazi wa Msumbiji (Mwenye shati jeupe) Bi. Maria Luisa Mathe na Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Bi. Fatma Salum Ally(kushoto) wakikagua Daraja la Umoja eneo la Mtambaswala mpakani mwa Tanzania na Msumbiji katika maandalizi ya sherehe za Uzinduzi wa Daraja hilo mwezi ujao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Omari Chambo akiwaongoza viongozi mbalimbali kutoka wilayani Nanyumbu na Msumbiji kukagua maandalizi ya sherehe za uzinduzi wa daraja hilo katika eneo la chini ya Daraja la Umoja lililojengwa kwa Ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji katika eneo la Mtambaswala wilayani Nanyumbu leo.
Picha cha Aron Msigwa -MAELEZO



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Wachumi naomba mnisaidie, Hivi hilo daraja lina any postive impact kwenye economy ? Ama ndo mambo ya kisiasa tu

    ReplyDelete
  2. This is what we should be doing. Building bridges and forging alliances.

    ReplyDelete
  3. labda pica hapa zinadanganya, kwa hivyo tuelezeni mliona kwa macho hivi hilo daraja lina lanes ngapi? mbona naona kama ni lane mbili tu?

    ReplyDelete
  4. nyie watu wa kaskazini na kwingineko acheni hizo dalaja kujengwa kusini kufungua border na nchi za kusini mshaona nogwa hampendi wezenu tuendelee siku si nyingi mambo yetu yatakuwa poa kuanzia barabara,umeme,elimu nk kusini hoyeeee
    by chingas in doha

    ReplyDelete
  5. Anno wa Fri Apr 23, 11:31:00 AM,
    Hilo daraja ni 2 lanes. Nafikiri ni kutokana na funds na studies.
    Newburgh–Beacon Bridge ilifunguliwa November 2, 1963 as a two-lane (one in each direction) bridge, although original plans called for a four-lane bridge, funding difficulties resulted in the reduction in lanes.
    Capacity ilipokuwa ndogo decision was taken by authorities to add a second parallel span south of the original.

    ReplyDelete
  6. we michuzi kwa kubana meseji haujambo hivi huwa unajisikiaje?? angalia usije ukabana na hizo nanihii zako hapo chini ya kitovu!

    ReplyDelete
  7. Umoja Bridge lina faida sana za kiuchumi na ushirikiano kwa nchi za kusini. Bridge ni part ya Mtwara Corridor project.Wakimalizia kutengeneza barabara ya Somanga-Ndundu na masasi Tunduru mpaka Songea mambo yatakua mwake!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...