Mwanariadha mwenye ulemavu wa Zanzibar, Amour Ali akichuana na Shukuru Khalfani wa Tanzania Bara (hayupo pichani) wakati wa mashindano ya Pasaka ya Ujirani Mwema kati ya timu za wenye ulemavu za Zanzibar na Bara jijini Dar wikiendi hii. Michezo hii iliandaliwa na Kamati ya Para Olympic ya Tanzania Mwanariadha mwenye ulemavu wa Tanzania Bara Shukuru Khalfani , akichuana na Amour Ali wa Zanzibar (hayupo pichani) wakati wa mashindano ya Pasaka ya Ujirani Mwema kati ya timu za wenye ulemavu za Zanzibar na Bara jijini Dar wikiendi hii. Shukuru alishinda
Mchezaji wa timu ya soka ya wenye ulemavu ya Tanzania Bara Juma Kidevu (kushoto) akichuana na Ali Mkadara wa Zanzibar wakati wa mashindano ya Pasaka ya Ujirani Mwema kati ya timu za wenye ulemavu za Zanzibar na Bara jijini Dar wikiendi hii.
Mchezaji mwenye ulemavu, Rashidi Ali akishindana katika mchezo wa mtupo wakati wa mashindano ya Pasaka ya Ujirani Mwema kati ya timu za wenye ulemavu za Zanzibar na Bara jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Kamati ya Paraolimpiki Tanzania wikiendi hii.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Jambo hili la kuwahusisha ndugu zetu wenye ulemavu ni jambo zuri sana...Hii inawapa kujiamini katika jamii ambayo nyakati fulani wanaonekana kuwa hawana mchango katika jamii... Nimefurahi sana na pia naota shukurani zangu za dhati kwa watayarishaji na watekelezaji wa mpango huu wenye maana sana katika ulimwengu mzima. Endelezeni moyo huohuo hadi vijijini...Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Safi sana hii. Waandalizi tunawapa Hongera sana.

    Tupate hata na miss Tanzania wa wasiosikia, wasioona n.k.

    Hii inawanyanyua sana mioyo hawa wenzetu. Najiuliza leo hii mimi ningekuwa kipofu au kiziwi ningekuaje.

    Eee Mungu asante sana maana ni kwa rehema zako tu. Hatujafa hatujaumbika.


    Utaona ni wachache tutakao comment hapa watu tunapenda mambo ya udaku na siasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...