Mkuu sana Heshima kwako.
Ninaomba sana msaada wako ombi langu litoke kwenye blogu yako muhimu sana. Inafikia watu wengi na hasa wahusika na wengine huwa wanajibu.
Kuna bidhaa moja kitafunwa au snack inaitwa CHAMA. Hii kitu inapendwa sana na watoto, vijana wadogo na baadhi ya wenye 18 kwenda juu. Wanangu wanaipenda sana. Kila jioni nisiporudi na chama huwa wanangu wanakosa raha na wananionyesha waziwazi na wanataka niwahakikishie kesho yake kama nitawaletea.
Juzi niliamua kuichunguza kwa makini package ya snacks hizi na nikagundua kwamba haina nembo ya TBS. Ilinitisha kidogo kwa sababu angalau TBS huwa inatupa imani japo kidogo kwamba bidhaa hii inatambulika na watchdog ya viwango.
Sijui kama mamlaka ya vyakula na madawa (TFDA) ina utaratibu nayo wa kuidhinisha matumizi ya vyakula na vitafunwa kama hivi ili kuwahakikishia usalama watumiaji.Naomba kuuliza kwa wadau wote na kama TBS na TFDA wanafikika na pia watengenezaji wa CHAMA snacks, je zinakidhi viwango?
Wamewahi kuzipima na kuzi-certify salama kwa matumizi? Kwanini hazina nembo yoyote inayodhihirisha usalama wake?
Mnaturuhusu watanzania hasa wenye watoto wadogo wanaozipenda sana tuendelee kutumia? Hazijawahi leta madhara yoyote kwa mtumiaji yeyote?Je, mtu binafsi kama mimi nikiamua kuja kuipima TBS au TFDA, kuna gharama yeyote? Nifuate utaratibu gani?
Asante ANKAL nakusihi sana unifikishie ujumbe
Mdau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Siyo bidhaa hiyo tu hata kuna Tomato sauce kwenye chupa kubwa sina uhakika kama ni Dabaga au pia hazina nembo ya TBS. Na ndiyo pia wauza chips wengi hupenda, TBS na sisi walji tuwe makini na kutoa taarifa.

    ReplyDelete
  2. kaka umesema maneno ya maana sana. lakini sheria haikatazi vitu kuuzwa ikiwa hakuna nembo ya tbs. mwenzetu umeshazoea kula na umetokea kuipenda sana . hakuna maumivu yoyote uliyopata katika matumizi yako sasa unaipigia debe? ikiwa TBS na TFDA wanayo wakati wapite mitaani daressalaam nzima usiku ni biashara ya chakula na kuku ukimchunguza sana hotomla.

    ReplyDelete
  3. nilikuwa TZ kwa mapumziko,nilishangaa mtoto wa rafiki yangu neno lake la kwanza kujifunza kulitamka lilikuwa ni chama!kalikuwa kanakula takriban vifuko 2 kwa siku!nvinapendwa mno,vinanini ndani yake?

    ReplyDelete
  4. yaani anko umesema kitu cha maana sana lakini ukumbuke tanzania hamna viwango wala ukaguzi wa vyakula na wala sisi wenyewe hatuna utaratibu wa kuangalia hata expiring date jamani sijui TBS inafanya nini, hayo machama ni uchafu mtupu ni bora uwalatee watoto matunda kwa afya yao, mimi binafsi watoto nilishawaambia wasile huo ni uchafu na wakanielewa.

    ReplyDelete
  5. Chama ni jamii ya product moja ilikuwa maarufu sana in the early 90s inaitwa CORN VITA....sijui wadau mnaikumbuka hiyo?

    ReplyDelete
  6. kwani mkila mapera, mapapai au mihogo mnakuta alama ya tbs? nyinyi kuleni tuu mkitaka kuhoji kila kitu mtakufa njaa shauri yenu!

    ReplyDelete
  7. kwakweli hata mimi ninawatoto wangu wanapenda sana Chama,hata kama analia ukim letea chama tu anayamaza.Nafikiri hiyo ladha iliyomo ni nzuri kwa ulimi wa watoto maana mimi nilijaribu kula wala sikuipenda kabisa.

    ReplyDelete
  8. TBS NI KWA AJILI YA KUONGEZA AJIRA NCHINI HIVYO USIAMINI SANA BIDHAA JENYE NEMBO YAO WEWE TUMIA TU BIDHAA YOYOTE UNAYOTAKA USIJALI. PILI HATA WAO WAFANYAKAZI WA TBS WANATUMIA TU BIDHAA ZISIZO NA NEMBO ZAO. NENDA SHOPRITE UTAKUTA SUKARI WANAYOINUNUA TOKA KILOMBERO IKIWA KWENYE PAKITI ZA KILO MOJA KISHA WANACHANA NA KUZIFUNGA UPYA KWA VIPIMO VYAO NA KUUZA BILA YA NEMBO YA TBS SASA HATUJUI HUWA WANAICHANGANYA NA NINI KUONGEZA UZITO ILI WAPATE FAIDA, UJUE AFUNGAE UPYA BIDHAA HUWA AMEICHEZEA ILI APATE FAIDA.

    ReplyDelete
  9. Mie jamani nakaribia 40 years lakini siwezi kupitisha siku bila kula chama kwa jinsi ninavyozipenda!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...