WIZI WA SIMU HOSPITALI YA AGA KHAN

Morning Ankal pole na shughuli za kila siku za kujenga taifa letu zuri.Ankal mimi ni mpenzi wa blog yako sana,naomba unisaidia kuweka hili jambo ili wadau wengine wasipate tena mkasa ulionikuta mimi.Siku ya tarehe mbili March nilienda hospitali moja maarufu sana hapa mjini iitwayo Aga Khan nadhani kila mtu anaijua.Ankal pale Aga Khan sasa panaanza kuharibika kwa kuwa na wezi wa simu na pochi ndogo zinazojulikana kama wallet za akina mama.
Basi kisanga kilikuwa hivi ankal,nimetoka kumuona daktari wa mwanangu nimekaa pale pharmas nasuburia dawa,nimeweka mkoba wangu pembeni yangu huku nimembeba mwanangu,pale pembeni yangu amekaa mwanamake mmoja ambaye baada ya uchunguzi niliambiwa huwa anauza vitu vya akina mama vya ndani kama brazia na vijinguo vya watoto wachanga.
Basi baada ya muda kama dakika kumi tu hivi nataka kuchukua simu nimpigie mume wangu kuwa aje kutufuata pale hospitali ndo nahamaki kuwa simu zangu zote mbili hakuna moja aina ya nokia na nyingine ni blackberry ambapo thamani yake ankal inafika milioni moja hope unajua bei ya blackberry na Nokia za ukweli izinauzwaje. Ankal yaani niliishiwa nguvu we acha tu.
Sasa yule mama baada ya kuona kama nimeshtuka akanyanyuka akaondoka akazungukia upande wa casuality akaenda kwenye parking za magari hope pale alienda kuzimpa mtu wake kwani muda kidogo tu alitokea kule parking ya mbele ,mimi kuhamaki ikabidi niwaambie askari wa zamu waliokuwa pale basi wakamwita yule mama na kumhoji. Akasema hajachukua basi wale askari wakasema kuna camera ngoja wakaangalie kwenye camera.
Basi muda huo mume wangu alikuwa kashakuja wakaenda nae kitengo cha camera wanafika kule cha kusikitisha ni kwamba hata hizo camera hazijasetiwa na wala hawajui kusetna wala hakuna mtu anayejishughulisha na zo kila mtu anasema hahusiki na camera.
Cha kusikitisha Ankal ni kwamba uongozi haukuona kama lile jambo ni la muhimu au laweza kuwaletea picha mbaya.Nilijaribu kuchunguza nikaambiwa hilo ni jambo la kawaida hapo hospitalini kwao na wala hawaoni kama linaharibu picha ya hospitali yaani ankal mimi na mume wangu tulisikitika kwani hakuna mtu wa utawala aliyeona uzito wa lile jambo.
Yaani ni watu wasiojali kabisa hata ukienda hapo kwao sasa hivi ukauliza staff yeyote atakuambia the same.
Ile siku tuliamua kuondoka kwani ankal tulikuwa na mtoto anaumwa na hakuna ushirikiano wowote tulioupata kutoka kwao.Ila sikukata tamaa baada ya siku nne nilirudi tena pale nikamkuta supervisor mmoja wa reception ninajuana nae na nilifanya nae kazi hapo Aga Khan nikamuuliza akaniambia ile siku hawakupenda tu kunionyesha ngoja yeye ataniangalizia kwenye camera ataniambia baada ya siku mbili nikampigia akanijibu kwamba yule mtaalamu wa mambo ya camera ameacha kazi so hakuna mtu mwingine wa kuweza kuangalia.
Jamani ankal hebu niambie hapo utakasirika kiasi gani?Ankal naomba ushauri kwani mimi nataka kuwashitaki kwani gharama ya simu zangu ni kubwa sana na hasa hiyo blackberry ndio nilikuwa natumia kwa mambo ya ofisini ankal.Niliwapa muda nikidhani hata utawala watalifuatilia ila naona kimya so naona niende mbele.
Ankal ninachotaka kuwaamba wadau ni kwamba wawe macho kwani sio watu wote wanaokuwa pale Aga Khani Hospital ni wagonjwa na wezi wakubwa na akina mama.Naomba unipe mawasiliano na mtu yeyote wa magazeti ili niweze kuliweka watu wajue uozo ulioko hapo hospitali ya Aga Khan.

Ankal nisikuchoshe nakutakia kazi njema na naomba tena chondechonde ankal weka hii hadharani ili watu wasijelizwa kama mimi.
Mdau Konso

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Mdau tunashukuru kwa kutupa tahadhari, ila swala la kuwashitaki utapoteza muda tu, hauna grounds za kuwafanya wawe liable kwa hilo.

    ReplyDelete
  2. Pole sana dada kwa yaliyokukuta, wizi na namna hiyo kwa sasa umeshamiri sana na hasa kwenye mahospitali. mimi mke wangu ameshawai kuibiwa pochi yake yenye fedha pale kinondoni hosp,anasema kuwa ni mama mmoja aliyekuwa naye katika foleni ya kumuona dk.

    Lakini dada!! kama ulimuona huyo mama akimkabidhi kitu mtu fulani kama unavyoelezea mwenyewe kwa nini ukusema ili na huyo mtu akamatwe?hapo ndipo uzembe wa kitanzania ulipofanya kazi yake!! pole sana.

    ReplyDelete
  3. Pole dada kwa yalokukuta, ila Aga khan hilo tatizo lipo, tena si nje tu hadi mawodini, nina ushahidi wa kutosha kabisa, kuna siku baba yangu ambaye ni mchungaji alishaibiwa simu akiwa anatoa huduma ya kiroho kwa mgonjwa ambaye alikuwa taabani, nesi alokuwa nae akampiga bao alipokuja kuulizwa akasema eti siyo yeye, taarifa zikafikishwa kwenye uongozi, wakasema watamwita kumpa feedback lakini cha ajabu hata yule nesi hakuulizwa kitu na badala yake wakamwambia eti 'atakuwa amesahau alipoiweka', lakini kutokana na kwamba ile simu inatumika kwa huduma Mungu alimwezesha mzee akanunuliwa simu nyingine, ila hiyo tabia ipo kabisa agakhan wajirekebishe wote kwa ujumla
    2) Jamani tusimwamini mtu tusiyemjua vitu vya thamani kama hivyo kama ni pochi na vinginevyo iwe kwenye dalax2, hospitali kama hivyo au hata sehemu nyingine, najua kuna mazingira inabidi tu uombe kusaidiwa lakini tuwe macho, nimeshashuhudia kwenye dalax2 dada mmoja kasimama akamwomba mama mmoja amshikie pochi yule mama alikomba kila kitu na vitambulisho vya yule dada akavitupa nje ya dalax2, mwanzo sikuelewa ile picha ila yule mwenye pochi alipokuja kuomba pochi yake ndo nikaelewa na nilimwambia yule dada kuna vitu nimemwona anatupa nje lakini sikuelewa kumbe ni vitambulisho
    Tuwe makini jamani, inauma

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli hili jambo nila kweli mimi nakumbuka mwaka 2008 nililazwa maternity ward, nikawa na simu yangu kitandani baada ya muda ikapotea katika mazingira ya ajabu lakini hisia zangu zilikuwa ni dada mfanya usafi. Baada ya kusema niliambiwa nisome nyuma ya mlango kwamba vitu vyote vya thamani vikabidhiwe kwa nurse mkuu(imagine). Kwa kweli sikutaka kubishana sana kwa sababu nilikua na tumbo la miezi kadhaa nikahisi hapa nikiendelea naweza hata nisipate huduma inavyotakiwa kwa kujenga chuki. Lakini hilo jambo ni kweli kabisa na hiii hosp inatakiwa kuliangalia hili jambo tena. Mama Watoto

    ReplyDelete
  5. Konso pole sana na kulizwa na wakwapuzi. Hoja yangu ni ya jumla. Wizi ama ukwapuzi wa simu za viganjani umeshamiri sana hususan katika jiji la Dar. mnajua ni kwa nini? Ukwapuzi wa simu ni dalili za mfumo wa kifisadi. Mdau wa kwanza ameligusia lakini kwa lugha ya mtaani. Ufisadi husababisha pengo kubwa kati ya walalaheri na walalahoi - kiasi kwamba walalahoi wanaanza kuona ni haki yao kukwapua cho chote kile kikwapuliwacho hata kama hawajui watakitumiaje. Katika mchakato huo wanaoathirika sana si mafisadi wenyewe (kwa sababu wao hawaendi kupiga msitari aga khan), bali ni kundi la akina Konso. Sote, akina Konso na walalahoi tukijiunga kama jeshi kukemea ufisadi, wakwapuzi na vibaka watatoweka. Kwa bahati mbaya hatufanyi hivyo!

    ReplyDelete
  6. Poleni sana watanzania kwa kuendelea kusahau vipaumbele vya maisha binafsi na taifa kwa ujumla.Simu na magari ya mbaya lakini maisha ya watu ni duni kabisa.Pole sana dadangu kwa tukio hilo.

    ReplyDelete
  7. Kutumia mtu nje ya utaratibu (kwa kujuana) kupekura nyaraka za hospitali nao si wizi??? Sasa unalalama nini wakati na wewe mwenyewe huna 'ethics?' Andaa fungu kubwa sana la rushwa kama utafungua kesi dhidi ya hospitali, vinginevyo utaishia kufungwa mwenyewe!

    ReplyDelete
  8. aka khan zamani bwana! siku hizi ni sawa tu na mwananyamala au amana nilienda kupima ngoma wakagoma na majibu yanguati hadi nito cha juu nyoo wakati sijui majibu?? nikawajia ju wee mwishowe nikatoka nje nikwa mlangoni nikawasikia huyu majibu yake poa hatumpi majibu hadi kieleweke lo! nilirudi ndani mbona palichimbika ilibidi wanipe tuu niliapa kutorudi tena pale mkitaka kupima afya zenu nendeni tu muhimbili wana kitengo special pazuriii na kubembelezwa juuu aka khan limebaki jina tuuu huduma mbovuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!

    ReplyDelete
  9. MIMI NAUNGANA NA ANON WA KWANZA, MIMI SIPATWI NA HURUMA KWANI MTU MAKINI AKISOMA HIYO TAARIFA YAKO ATAGUNDUA KWAMBA HAKIJAKUUMA....ETI SI UNAJUA TENA BLACKBERRY NA NOKIA ZA BEI YA JUU? WEWE UNARIPOTI TUKIO LA WIZI AU UNAJITAPA!!!!??? #2@&*!'? .... WEWE!

    ReplyDelete
  10. pole sana dada. Naona mahospitali siku hizi wanalea wezi. We nenda Mission Mikocheni usikie mziki wa wizi. wale hata maiti akifa, kama hakuna ndugu, viatu, simu, vitenge huoni ndani.

    kwa hiyo mahospitalini kuanzia bosi mpaka mfagiaji wote hushirikiana. nnasema hivyo kwa sabb kama si ushirikiano , wezi pale wangekomeshwa

    ReplyDelete
  11. Candid ScopeApril 13, 2010

    KILA MTU ANA HAKI YA KUPATA AU KUWA NA ANACHOKIPENDA. ILA KUNA KASUMBA FULANI KWA WAAFRIKA.
    TUNAPENDA KUJIONYESHA KWA MAMBO YA JUU SANA AU KUWA NA VIFAA VYA THAMANI KULIKO MATUMIZI YAKE YANAVYOHITAJIKA. KUNA ULAZIMA GANI KUWA NA mobile phone MBILI ZA GHARAMA WAKATI ZOTE KAZI NI MOJA TU? INAPOTOKEA MAKASA KAMA HUO SASA UNAJUTIA KUPOTEZA MALAKI YA PESA KWA MKUPUO. NIPO NABEBA BOX HUKU NA NILIPOKUJA LIKIZO WASWAHILI WALINIAMBIA LIKIZO YANGU NAJARIBU TO ECONOMIZE KAMA WAZUNGU WAFANYAVYO, NIKAWAULIZA KWA NINI WAKANIAMBIA ETI WABONGO WANAPORUDI LIKIIZO UTADHANI MAJUU PESA NI CHA KUMWAGA. LAKINI WAZUNGU WENYEWE HAWAFANYI HIVYO. WAKANIELEZA MENGI NIKABAKI NA MASWALI MENGI KICHWANI MWANGU.
    CHA MSINGI NAWASIHI WAONGO KUISHI KWA KUANGALIA MAMBO YA MAMBO YA MSINGI NA HASA KUWEKEZA KATIKA ZAIDI KATIKA MALI ZISIZOHAMISHIKA BADALA YA KUWEKA MAMILIONI KWENYE MALI ZINAZOWEZA KWEPULIWA NA WAJANJA

    ReplyDelete
  12. Mdau Konso kwanza pole kwa kizaa zaa hicho, Ningependa kukuambia kwamba if you go ahead and sue the Agha khan you're going to waste your money and time cause you don't have a solid case here to press your charge..you digg? Kwa hiyo next time take this as a wake up call kwamba never trust no one but you and GOD, Petty thieves wako kila sehemu mpaka makanisani na misikitini and the bottom line hapa always watch your back and stand your ground however, those phones are just materials and can be replaced anytime even upgrading to the better ones and also the good news here that i'm impressed with is no one got hurt.So thank Goodness for not getting hurt.
    WABEJA KURUMBA....MASANJA HAPA-SHY TOWN

    ReplyDelete
  13. Wizi everywhere jamani sio Aga Khan tu acheni unafiki. Mpaka nyumba za ibada watu wanaibiana. Msichafue majina ya sehemu.

    Mwambie shem akununulie BB nyingine, maana ungenunua mwenyewe usingekua mzembe mzembe na manyama uzembe.

    Pwagu kweli wewe!

    ReplyDelete
  14. Konso pole sana, ukweli hata mimi nilishaibiwa simu yangu na huyo mama, nilienda pale clinic ya watoto, yule mama akaja anauza bra tena za mitumba na vijinguo vingine, basi akanisemesha kuwa anauza nguo, nikamjibu kuwa sihitaji. sasa mtoto alikuwa kapata chanjo so alikuwa analia sana na simu sikuwa nimeweka ndani ya handbag as nilikuwa nasubiri mume wangu anipigie kwa bahati mbaya sana ilikuwa kwenye silent mode. Basi mi nimeconcetrate kumbembeleza mtoto nashtuka mbona mr hanipigi nakuta yule mama ashatoka na simu haipo. Wakati nashangaa naulizia kwa manesi wakasema hawajaiona mara yule mama haonekani kina mama wengine wakasema yule mama katoka lazima anahusika maana sisi wenye watoto wote tulikuwa hatujatoka tunasubiri chanjo. Nikaenda kwa askari getini wakasema yule mama katoka, nikawaeleza issue yangu wakasema watafuatilia, kesho yake nilivyoenda wakasema yule mama kaja lakini kakataa hivyo wamempiga marufuku kuingia pale ndani kwani siyo eneo la biashara, lakini cha ajabu hadi leo hivi yupo yule mama mule mule aga khan ni mnene ana tumbo kubwa halafu yupo rough na ana harufu ya kikwapa. Yule mama baada ya wiki moja nilikutana naye na usoni alioneka kabisa anajua alichonifanyia. Si vyema kumshuhudia mwenzako wizi ila yule mama ni mwizi kwani akifika tu pale anaanza kuangalia mtu ambaye yupo desparate au stranded ndo anamvaa na mara nyingi huwa anafanikiwa. Pole mwaya!!! Lakini siku moja aga khan watashuhudia yule mama anapewa kipondo na mimi ni lazima nije nimtegee yule mama nitazubaa na simu na akichukua simpi muda ya kuificha namkamata.

    ReplyDelete
  15. Konso, kwanza pole sana.
    Pili Trust your instincts, kama huyo mama unaamini ndiye aliyeiba na kama unaamini nje alikwenda kuficha basi ndiye huyo huyo mwizi wako ila ujue kama hapo hayuko peke yake kuna genge wataokula hela baada ya simu kuuzwa hapo kuna hao walinzi, watu wa camera na hata manesi. kosa ulilofanya ni kumuachia aende zake.
    Ushauri wangu kama unaweza umkamate mpeleke polisi na waombe polisi wakusaidie na waambie kabisa kama ikipatikana watafurahi aseme ukweli kama simu kachukua na kaipeleka wapi? nakwambia atasema mwenyewe na aliyemuuzia! muhimu hao watu wazima wakishakusaidia uwafurahishe kweli!
    ndugu yangu aliangusha simu uchwara tu ndani ya taxi, dereva akatutoa hajaiona! ndugu yangu alikuwa na imani kabisa kaiangusha kwenye gari, tulimpeleka polisi tukawambia kabisa watafurahi! akajidai kukataa mbona mwisho aliwapeleka polisi mpaka alipoificha buguruni kwa manyanya, hilo lilikuwa dume zima limesema itakuwa huyo mwanamke! nakushauri mtafute mumtegee hapo hapo hospitali kama unauchungu na simu zako!

    ReplyDelete
  16. Simu ya milioni moja ya nini TZ. Huitumii kwa shuguli za kikazi kama email, au navigator au microsft au podcast na vitu kama hivyo sasa ya nini wewe dada.
    Unatumia kumpigia simu mume wako tu kwa jili ya kununua vijisidiria vya mitumba na vijuguo vya barabarani, acha waikwapue tu wakafaidike mbele.

    ReplyDelete
  17. tanzania ni nchi ya amani jamani msitake kututisha ila tahadhari inatakiwa. ikiwa mtu nyumbani kwako unaacha vitu ovyo lazima zitapotea. sasa wewe unafikiri hawo walinzi wanakuchunga wewe? hao dada wamewekwa kulinda mali ya shirika.ikiwa mpaka umefikia umri huo hujaijua kuchunga mali yako basi utapoteza sana maana hakuna wa kukusaidia.jilinde dada vizuri

    ReplyDelete
  18. mambo yakuzubaa yamepitwa na wakati. jamani changamkeni. wakati ndio huu . watu kila siku wako kwenye mitihani ya kila aina ya maisha sasa tutafute jinsi yakutatua na kupata ufumbuzi wa masuala tulioulizwa na huyu dada. je hospitali na walinzi wake wangemsaidiaje dada huyu wakati aliporipoti?

    ReplyDelete
  19. Wewe Konso ni bishoo toka unafanya kazi hapo receiption Aga Khan receiption.How come unaweka valuable belongings ovyo ovyo sehemu ya public kama hiyo?Huo ni uzembe wa hali ya juu pamoja kuwa hapo Hosp kuna matatizo yao pia.

    ReplyDelete
  20. Hey dada that is your personal belonging, you are solely responsible for its safety,and care, and not the hospital authority responsibility.Come on you people. Kuna siku mtu ataibiwa pants aliyovaa kwa wakati huo alafu aanze kulalamika humu ndani..!!

    ReplyDelete
  21. Wizi wa simu upo kila mahali Dar es Salaam. Usipokuwa makini hata Ikulu unaweza kuibiwa simu. Nadhani si haki kuulaumu uongozi wa Aga Khan kwa vitendo vya wizi wa simu hospitalini hapo kwa kuwa si rahisi kujua kama mtu ni mwizi kwa kumuangalia usoni. Kitu muhumu ni kwa wamiliki wa simu kuwa makini, sio to wanapokwenda hospitalini hapo, bali sehemu yoyote Dar.

    ReplyDelete
  22. NENDA KWENYE VYOMBO VYOTE VYA HABARI KATEME MACHUNGU YAKO YOTE, NENDA TVs, MAGAZETNI, RADIO. NA KAMA UNAPATA MWANASHERIA MZURI UNAWEZA KUWASHITAKI NA WAKAKULIPA. WANA HOJA NYINGI TU ZA KUJIBU KWANZA WANAMRUHUSU VIPI MTU AJE AFANYE BIASHARA HOSPITALI KWANI HILO NI DUKA AU SOKO. HUWA WANALIPA KODI KWA KUTUMIA JENGO LAO KAMA SEHEMU YA BIASHARA? THEY HAVE RESPONSIBILITY AND DUTY OF CARE TO THEIR CLIENTS. TATIZO WANASHERIA WA BONGO NDO HAO WA KUKARIRI SI WAELEWA WA KUCHAMBUA MAMBO KIUNDANI. ZIPO SHERIA ZINAZOHUSU MAJENGO NA RESPONSIBILTY YA MWENYE JENGO SI KUANDIKA TU VITU VYA THAMANI VIKABIDHIWE KWA UTAWALA NA UKIKAA NAVYO BASI VIKIPOTEA NI JUU YAKO, HIYO WALA SI DEFENCE.

    ReplyDelete
  23. Inaelekea wafanyakazi wa Aga Khan hospital wanamjua huyo mama mwizi na wana ushirikiano nae. Kwa nini wanamruhusu auze vitu pala kama si mgonjwa, au si mfanyakazi wa hospitali?

    ReplyDelete
  24. DADA HILI SUALA LIMEFIKA MAHALI PAKE.. MESSAGE SENT. TUPE WIKI MOJA TUU UTASIKIA MWENYEWE YULE MAMA TUMESHASIKIA HABARI ZAKE NA TUNAJUA ANASHIRIKIANA NA WATU WENGI PALE WAKIWEMO WALINZI WEW SIO MTU WA KWANZA. DAWA YAKE TUNAIANDAA NA HATOTOKA AKINASA KWANI TUTAKUWA NA USHAHIDI TOSHA. TUTAKUWA NA KESI YA MUDA MFUPI SANA YA KUTOLEA FUNDISHO.
    SINA MANENO MENGI. HUU NI WAKATI WA SAYANSI NA TEKNOLOGIA.

    ReplyDelete
  25. Hivi ni wapi kwenye mkusanyiko wa watu hakuna wezi? Hivi Konso tanataka kuulaumu uongozi wa Aga Khan kwa uzembe wake? Hivi unawezaje kuibiwa simu mbili ndani ya pochi bila ya kuwa aware. Nina hakika,huyo dada ni mzembe na hastahili huruma. Hata style ya uandishi wake ni ya kuonyesha zaidi nini anacho badala ya kuelezea kwa undani jinsi alivyoibiwa. Kutuambia ni BB au nokia ya ukweli haimsaidii msomaji, kwani hata kama simu ni ya elfu tano, haimanishi ndiyo inafaa kuibiwa......

    ReplyDelete
  26. KWA KWELI NINGEPENDA KUUNGA MKONO WADAU WANAOTOA USHAURI KWA KUSISITIZA WANANCHI WAWE WAANGALIFU KULINDA MALI ZAO, LAKINI KUNA WADAU WANAODAI KWAMBA KUWA NA SIMU YA MILIONI NI UFISADI AU HUPATIKANA KWA UFISADI, HIVI NI KUSEMA NCHI YETU HAINA WATU WALIOFANIKIWA FINACIALI KWA KUCHAPA KAZI YA UHALALI? NA HATA KAMA NI WACHACHE SI WAPO? SASA HAWA HAWANA HAKI YA KUPATA USALAMA WAO AU MALI ZAO KWA SABABU HUWEKWA KATIKA KUNDI LA MAFISADI? LAKINI PIA YULE MDAU WA MAJUU ALIERUDI VEKESHEN NA KUPIGWA NA BUMBUWAA! ITAKUWA AMEONDOKA ZAMANI MNO MAANA HAYA MAMBO YA WABONGO NAKUJIONYESHA YAPO SIKU ZOTE ISIPOKUWA YANAONEKANA ZAIDI HIVI SASA KULIKO ILE MIAKA YA NYUMA , NI KWABAU MAENDELEO YA NCHI KAMA ZETU HUJA KWA MANUFAA YA WACHACHE NA UKICHANGANYA NA MAFISADI NA WAFANYA BIASHARA HARAMU WENGI WAO WAKISHAIRIKIANA NA WAGENI, BASI NDIO MAANA BONGO INAZIDI KUWA TAMBARARE.....
    KWA HIYO KONSI KAMA NI VIGUMU KUVIPATA TUNZA KWA UANGALIFU AMA SIVYO NUNU VYENGINE, "AFTER ALL SI NI MLLIONI TU"
    MDAU NUTRO, KANADA

    ReplyDelete
  27. HIVI MTU ANAHITAJI SIMU MBILI ZA MKNONONI KWA SABABU GANI? UNAWEZA KUONGEa na simu mbili kwa wakati mmoja???>

    ReplyDelete
  28. Dada Conso pole nafikiri nilikuwepo siku uliyoibiwa (kama si wewe basi the same tukio lilitokea) Huyo mshukiwa alikuwa amevaa blouse ya yellow na suruali nyeusi. Nilikuona (kama si wewe nisamehe) ukiulizia pale kwenye reception ya first floor kwa wale wadada wakakuelekeza uende kwenye camera room. Pole mamii na aksante kwa taarifa.

    Ila napenda kukujulisha kuwa ungekuwa mhindi wangekusaidia wale lakini kwa kuwa u black mh pole mamii.

    ReplyDelete
  29. Pole dada kwa kuibiwa simu zako. Hili ni fundisho kwetu sote kuwa simu sio kwa ajili ya show off. Simu siyo kwa ajili y display. Ni vizuri kuitoa hadharani wakati wa matumizi ukishamaliza weka ndani. kazi ya simu kubwa ni kupiga na kupokea simu kwa wengi wetu hizo zingine vikorombwezo na mikogo tu. Ni vizuri sana kurudi kwenye basics za kwanini simu? Why do you need a phone? Simu siyo show kama wengi tufanyavyo. Chochote cha thamani when displayed it tempts na ndicho kinachowapata dada na kaka wengi wanaopenda show off. Halafu yawezekana pia wewe hizo simu ulipata za dili kwani kumiliki simu mbili za zaidi ya sh. millioni wengi wenu mnaletewa na hao hao wanaokwapua kama walivyofanya kwako. But kwa vyovyote vile inauma, badala ya kununua simu nyingine za milioni, nunua za laki tano halafu hizo balance wape hata ndugu zako wenye mahitaji wapate mitaji ya biashara. laki tano unaweza ukawpa watu watano kazi.

    ReplyDelete
  30. Hi,

    Wadai matumai ni wazima wa kheri. Mimi nafikiri hayo maelezo ya Konso haya ground kabisa. Halafu naona kuna mahali ameandika nilikuwa nafanya Aga Khan b4 kwa hiyo anajua fika pale palivyo sasa sioni sabab ya yeye kuona Aga Khan imekuwa ni hovyo baada ya yeye kuondoka au ilikuwa na wizi kama alivyoibiwa yeye? Pole ila napenda kukuambia jinsio ulivyotoa maelezo yako kwa kweli sijayaelewa kabisa ni kwamba tu kama ulimshuku ni yeye ni bora ungepiga hata kelele ili hata aogope na kama kweli angekuwa ameiba angeshtuka na kukimbia sasa wewe umetoa maelezo marefu kuwa alizunguka nyuma kwenda kumpa mtu sasa ulijuaje kama ameenda kumpa mtu simu. Sasa inatuonyesha ni jinsi gani na wewe ulivyokuwa unafanya kazi Aga Khana na kushirikiana na watu kama hawa kama alizunguka kwenda kumpa mtu hizo simu zako kwa nini na wewe usingeenda kuangalia anampa nani ili uweze kupata ushahidi wa kutosha?? Wewe jaribu kwenda mbele kushtaki ndio utajua Aga Khan ni kina nani kama hatujatoa siri zako za ndani kuhusu hapa Aga Khan na huyo unaejidai ni mume wako mpendwa kama hajakuacha. Mambo mengine lazima utumie akili ukiwa unaandika huku kwanza nina wasiwasi kama hizo simu umeibiwa hapa Aga Khan. Shame on you.

    xxxxooooo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...