Home
Unlabelled
ziara ya BBC world service mji wa kusoma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
wabongo bana!! mbona kiswahili chetu ni kizuri tu!! akuna ubaya kuongea kiswahili
ReplyDeleteAsante sana BBC, hususan Fredy Mtoi kwa kutuletea Interview safi ya Lovely Gamble...I can't wait to see it.
ReplyDeleteWABONGO MAMBO YETU UBWEGE UBWEGE TU!!
ReplyDeleteMAHOJIANO GANI HAYA YASO KICHWA WALA MIGUU
ANAEHOJI SHOMBO TUPU, NA BAADHI YA WANAOHOJIWA NDIO ZAIDI!
MTU KAZALIWA SIJUI NJOMBE HUKO, SIJUI TUKUYU, MKINGA FULANI, MZARAMO FULANI, ANAHOJIWA MASWALI KATIKA KISWAHILI SAFI, ANAROPOKA MAJIBU KATIKA KIZUNGU. NDIO NINI SASA?
HIVI MHESHIMIWA MKUU WA WILAYA KWA NINI UNARUHUSU UPUUZI KAMA HUU KATIKA UKURASA WETU WA JAMII?
KAMA MNAAMUA KUHOJI KWA KIZUNGU-KWA MASLAHI YA WANAOELEWA LUGHA HIYO, KUNA HAJA GANI YA KUCHANGANYA NA KISWAHILI?
NA KAMA NI KISWAHILI, KUNA UHUSIANO GANI NA HICHO KIZUNGU?
MBONA HAMCHANGANYI NA LUGHA ZA MAKABILA MLIZOZALIWA NAZO? MBONA HATUSIKII KIKINGA, AU KINYAMWEZI, AU KIBENA, AU KILUGURU, AU HATA KINYAKYUSA?
KAMA SI UBWEGE NA UNYANYAPAA NI NINI?
TAFADHALI JAMAA MTINDO HUU BORA UKOME.
WATZ WANAUTHAMINI UTZ WAO KULIKO UZUNGU USIO WAO.
KAMA MNAAMUA KUHOJIANA KWA LUGHA NYINGINE, MSIZICHANGANYE NA KISWAHILI CHETU KITAMU.
HIVI HAMNA HABARI KUWA HAKUNA LUGHA TAMU KAMA YA KISWAHILI?
Mndengereko, Ukerewe
kuongea kingereza si tatizo,ila kuongea kingereza cha kujifanya ndo tatizo na hicho ndo kingereza cha kujifanya sasa!
ReplyDeletehivi kwanini msiwe proud na lugha yenu!
najua kuna kuchanganya maneno ya lugha hiyo inatokea mara nyingi sana sana kwa watu wanaotumia lugha mbili tofauti lakini sasa sio ndo ujifanye kama hujui kiswahili fasaha huo ni ulimbukeni wa kutaka uzungu, kwanini we ujiweke chini nasi kwanini tusiipandishe lugha yetu kila mtu akaitamani. grow up Tanzanians, mnakuwa kama sio wasomi.
Hicho kiswanglish,kwa nini mnaharibu lugha yenu?au ndio watu wakikaa ulaya ndivyo wanavyoongea?
ReplyDeleteMbona mimi nimeiona interview iko bomba sana. Wewe Mndengeleko wa Ukerewe, ina maana hujui kuwa hii filamu haijachezwa na wabongo peke yao, imeshirikisha pia wasanii weusi lakini waingereza? wewe vipi hata hukusikia mwanzo wa interview wanasema imeshirikisha wasanii wa uk na tz? Labda tu huyo sister aliyeulizwa kwa kiswahili akajibu kiinglish lakini wengine unaona kabisa si wabongo. Huyo Fredy navyojua na kumsikia vipindi vyake si mtangazaji wa kubabaisha dogo sounds professional. Na hao waliotengeneza filamu jamaa nawapongeza sana sana kumudu kufanya filamu hiyo ughaibuni navyojua UK life tough sana. Acheni wivu jamani mtajinyonga buree!
ReplyDeletemdau-Belfast
Promo iko bomba sana nimeipenda. vijana mnatupa changamoto. Asante kwa kuitngaza bongo majuu. mwanzo mzuri.
ReplyDeleteIF YOU HAVE NOTHING TO SAY, SAY NOTHING..........HATERS!
ReplyDeleteSASA MDAU WA BELFAST MBONA UNAJIKANGANYA NA KUJIKANYAGA?
ReplyDeleteMARA UNANISHUTUMU SIKUONA MWANZO WA MAHOJIANO NDIO MAANA SIKUSIKIA KUWA FILAMU IMEIGIZWA NA WASWAHILI NA WASIO WASWAHILI.
KISHA UNAJIRUDI MWENYEWE KWA KUSEMA KUWA LABDA YULE SISTA NDIO AMECHANGANYA LUGHA KWA KUJIBU KWA MCHANGANYIKO WA KISWAHILI NA KIZUNGU.
YAWEZEKANA KUNA WATU WANA MARADHI YA KUIMBA KILA KINACHOIMBWA, KAMA WEWE MDAU WA BELFAST.
WIMBO WAKO HUU NI HATARI KWA JAMII YETU CHANGA INAYOKUA.
WIMBO HUU WA KWAMBA ETI WADAU WANAOJITOKEZA KUKOSOA WANA WIVU KWA WENGINE/
HUU NI WIMBO HATARI, KWA SABABU WAIMBAJI WAKE WANAJARIBU KUIPIGA VITA DHANA YA KUKOSOANA.
HAKUNA BINADAMU ALIYETIMIA, NA MARA NYINGI MAFANIKIO HUSAIDIWA SANA NA JICHO LA JAMII INAYOKUZUNGUKA.
WASANII WENGI HILO LIMEWASAIDIA, AMINI MANENO YANGU.
NA LABDA KABLA SIJAMALIZA, NIKUKUMBUSHE JAMBO MOJA MDAU WA BELFAST, KWAMBA USANII NA WASANII NI CHOMBO MUHIMU SANA KATIKA KUWAFUNZA WAGENI LUGHA. TUNAPOKWENDA KUTAZAMA FILAMU, SI TU KWAMBA TUNAKWENDA KUBURUDIKA NA MTIRIRIKO WA MATUKIO NDANI YA FILAMU, BALI PIA FILAMU HUTUSAIDIA KUKUZA MSAMIATI WA LUGHA.
HATA MAHOJIANO YA WASANII WACHEZA FILAMU HUWA NA MCHANGO SAWIA KATIKA KUBORESHA MSAMIATI. PIA WASANII HUUTANGAZA UTAMADUNI WA JAMII ILIYOWALEA NA KUWAKUZA. ENDAPO MATENDO NA MANENO YAO HAYAAKISI VIPENGELE VYA TAMADUNI ZAO, HASA KATIKA REAL LIFE SITUTION KAMA YA MAHOJIANO, WASANII HUONEKANA MABWEGE, HAWANA KWAO, HAWAHESHIMU UTAMADUNI WAO, AU VIBARAKA NA VITIMBAKWIRI.
MSANII NI KIOO CHA JAMII, SAUTI YAKE NI YA JUU KULIKO ZA WENGI, MATENDO YAKE YANAONEKANA MBALI SANA, NA TABIA YAKE AMA HUJENGA AU KUBOMOA.
MDAU WA BELFAST SAMAHANI KAMA HUELEWI NAZUNGUMZA NINI, LAKINI KWA SISI WANA FASIHI USANII HUUTAFSIRI NAMNA HII. AHSANTE,
Mndengereko, Ukerewe
wabongo tupendane na tupeane credits inapohitajika. wengine wanakandia, na hilo ni hatari sana. ona wazungu watakipamba kitu chao hata kama ni kibaya, lakini sisi wivu, kukatishana tamaa nk ndio wimbo wetu.
ReplyDeleteTubadilikeni jamani.
Lovely Gamble hoyeeeeeee!!!!
Anywe sumu asiyependa.
cant wait Lovely Gamble!!!
ReplyDeleteNimeipenda sana hii promo ya vijana. Nadhani nilishasikia pia BBC mahojiano. Vijana endeleeeni na moto, tunataka filamu zetu zijulikane kimataifa tumechoka na mambo ya kinaijeria kila siku,lol, mwenzangu!!!!!
watanzania uk tunazidi kuwa kama wazimbabwe kwa kuepuka kutumia lugha yetu ya taifa. Na wengine hata kujifanya eti wameshasahau kiswahili baada ya kuishi huku kwa miaka michache tu. HEKO wooote
ReplyDeletepumbavu...mzarau kwao ni mtumwa
ReplyDeletewakorea wamekaa ulaya/US kizazi adi cha 5 na wanaongea LUGHA YAO kwa ufasaha tu tena mahali walipo wachache kuanzia home au mtandaoni
ovyo kabisa