Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya viongozi wa UVCCM wanohudhuria mafunzo mafupi ya uongozi huko eneo la Ihemi, nje kidogo ya mji wa Iringa leoMwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaongoza wanachama wapya wa CCM kutoka katika vyuo mbalimbali Mkoani Iringa kula kiapo cha utii kwa chama Cha mapinduzi muda mfupi kabla ya kuwahutubia viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana katika eneo la Ihemi nje kidogo ya mji wa Iringa.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti UVCCM Ndg. mBeno Malisa na kulia nia Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg. Shigela.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2010

    Ankal tutafutie niuwz hii.
    Tulisikia kuwa watu wamevuliwa uenyekiti na unaibu katibu toka jana kwenye huo mkutano huko Iringa. Mbona hiyo breaking nyuuuuuz hatujaipata. Tutafutie hiyo niuwz!

    Ankal au wewe ni sisi-em?

    Mdau ughaibuni

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2010

    Masauni amekosekana hapo!!!!!!!!!!!
    poleni sana UVCCM.
    Nape Nnauye ndo alikuwa mwenyekiti Bora kwa kipindi hiki muhimu cha siasa za CCM na Tanzania.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2010

    huu u CCM sasa adi una bore !!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2010

    jana nilisoma mwananchi kwamba JK amepata udhuru hivyo hata hudhuria mkutano na leo namwona au aliogopa mambo ya asili?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2010

    CCM hivi imeloga watu, wanafunzi wa vyuo ambao ni wafanyakazi wa kesho kweli wanajiunga na CCM wakati huu?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2010

    WANAFUNZI KUJIUNGA NA CCM NI ILE METHALI YA MTUMIKIE KAFIRI...;NADHANI MMESIKIA NINI KIMEWAPATA WANAFUNZI WA UDOM WALIOJIUNGA NA UPINZANI, MZUMBE PIA ILITOKEA NA UDSM VYIVYO HIVYO NA HATA WATUMISHI WA UMMA WALIOMO KWENYE UPINZANI YANAWAPATA LAKINI WALIOMO CCM HAYAWAPATI, KAWAULIZENI AKINA LAMWAI NA WENZAKEKE NINI KILIWAPATA NA BAADA YA KURUDI CCM MAMBO YAKAWA POA. IKO MIKASA YA WANAFUNZI KUNYIMWA MIKOPO KISA TU NI KUJIUNGA NA UPINZANI. TUJUE MOJA KUWA CCM SASA INATUMIKA KAMA SOMO WAPO WANAOPASI NA WANAOFELI NA MAMBO YAO YANAKUWA POA, WANAOFELI NI WALE WANAOJIUNGA NA CCM SI MKWA MAPENZI BALI NI KUONA KUWA HUKO SI LAZIMA UWE NA AKILI ILI UWE MBUNGE BALI MRADI UVAE NGUO YA KIJANI BASI LAZIMA UTAPITA HATA USIPOSHINDA UCHAGUZI KAMA ALIVYOSEMA JK KUWA HATA MSIPOMPIGIA KURA ZENU ATASHINDA!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 20, 2010

    SAFARI HII PIA KODI ZA WANANCHI ZINATUMIKA KAMA ILIVYO KWA SAFARI YA PINDA KWA SHUGHULI ZA CHAMA WANANCHI TUNAGARAMIA. INABIDI TUDAI KATIBA IZUIE VIONGOZI WANAPOINGIA MADARAKANI BASI WASIFANYE SHUGHULI ZA VYAMA ISIPOKUWA WAKATI WA UCHAGUZI TU, HII ITAZUIA KUDI ZA WANANCHI KUTUMIKA KWA SHUGHULI ZA CHAMA KINACHOKUWA MADARAKANI NA ITAMUWAJIBISHA KIONGOZI KUWA NI WA TAIFA BADALA YA SASA AMBAPO TUNASHUHUDIA WANACCM KUINGIA KATIKA ULINZI WA RAISI ANAPOKUWA KWENYE ZIARA NA SHUGHULI ZA KISERIKALI.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 20, 2010

    Brother MICHUZI tunataka kujadili issue ya MASAUNI kwenye blog yako tafadhali mbona huiweki?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 20, 2010

    Bro. Michuzi, tuwekee mambo ya maana ya kutuwezesha wengine tufanye jitihada gani kuiokoa Nchi yetu kutoka mikononi mwa wakoloni mambo leo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...