Basi aina ya mitsubishi lenye namba T 895 BGE kama linavyoonekana mara baada ya kufanya utaratibu wa kuyaondoa barabarani pindi lilipogongana uso kwa uso na basi la Osaka Exective katika kijiji cha Komakocho,kilichopo Segera.

Basi la Osaka Excutive lenye namba T 417 AAG kama linavyoonekana mara baada ya kuondolewa barabarani.

Dereva wa gari aina ya mitsubishi lenye namba T 895 BGE lililokuwa likitokea Dar na kuelekea jijini Arusha akifanyiwa mpango wa kutolewa baada ya kubanwa miguu katika ajali iliyotokea leo maeneo ya Segera.ukiachilia dereva huyu kuna watu wengine watano ambao wamejeruhiwa vibaya katika ajali hiyo na kufanyiwa utaratibu wa kukimbizwa hospitali.

Abiria wakiangalia basi lililokuwa limepata ajali huku wakitafakari namna ya kuondoka eneo la tukio

msaada wa hapa na pale ukiendelea kutolewa na baadhi ya abiria wa mabasi mengine yaliyofika katika eneo hilo la ajali.

kwa picha zaidi

BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2010

    Mheshiwa Rais JK usisahau kwenda kutoa rambi rambi kama ulivyofanya wiki mbili zilizopita.

    Mdau USA

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2010

    Jamani inakuwaje mabasi yagongane uso kwa uso mchana?.Mimi nafikiri hawa madereva huwa hawapati usingizi wa kutosha,huwa hawapumziki,nafikiri dereva anapotoa basi leo toka dar mpaka mbeya(mf) kesho anachukua huyo huyo toka mbeya mpaka dar.

    Na hata akilifikisha gari yeye dereva huenda bar kugida ulabu mpaka manane kisha asubuhi anachukua basi.
    Nawasihi makampuni ya mabasi kuwa na utaratibu kuwa dereva anayelifikisha gari leo,kesho yake liendeshwe na mwingine ili kuepusha ajali za kizembe namna hii.Nafikiri wadau mtachangia.Daniel-Moshi

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2010

    Poleni sana.

    Kuna lolote linaloweza kufanyika ama kila siku tutakuwa tunamsingizia Mungu tu?!!

    Polisi anzisheni Police Marshall's wanaopanda mabasi bila ya madereva kujua na pale wanapovunja sheria muwe munawa arrest na kuwapeleka mahakamani.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2010

    Kaka Michuzi,

    I suggest you should open up a mini blogs, contained with pictures and maelezo yake as you currently post them on your blog.

    Call it ajalitanzania.blogspot.com, I am sure people of interest around the world and home alike will go back and study the statistics on these incidents in our country.

    Hopefully someday our government and those of interest, will come to a sensible conculusion that, this in itself an epidemic,

    and please do follow the stories of those affected just like this driver, and I am confident, those stories on itself will drive the story home, we are susceptible to emotions, I am sure vyombo husika vita react, and find a viable solutions regarding this AJALI EPIDEMIC on our public roads.

    Poleni wafiwa na mlioathirika na hili,

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 10, 2010

    Sasa wanaendelea kutuchanganya. Ikitokea ajali lazima aliyesababisha/waliosababisha wawajibike, full stop.Mhuu wa polisi Pwani ana story yake kuhusu ajali hiyo/hizo soma:http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=7294
    Ingawa kutokana na picha za hapa inaonekana basi la Osaka na Fuso(basi) yalikuwa yanakwenda opposite.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 10, 2010

    Hizi ajali zoooote sijawahi kumsikia Mh. Masha wala Mh. Dk. Kawambwa wakisema lolote wala kufanya lolote. Why would you spend millions in saving watanzania wasife na Malaria au Ukimwi and still let them die on the road au ndio tunasubiri Global Fund na Pepfa?? Najua waheshimiwa mtakuwa mnasema mnafanya alot but its all about perception and from where I stand I don't see you move a finger to minimise these accidents. Lawrence, Shukuru, this is your 8 to 5, DO SOMETHING!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 10, 2010

    Ajali za uso kwa uso mchana ni sababu ya mwendo kasi na overtake sizizoluwa makini kabisa (Uzembe) madereva wetu sijui elimu ndogo? Wanapenda sana ku-overtake milimani hasa madereva wa mabasi. Sijui wanakuwa na haraka ya nini wakati safari ya mkoani unafanya trip moja tuu kwa siku..Hii tabia sijui tufanyeje. Gavana ndio hivyo tena serikali imeshindwa kuzilazimisha kufungwa ili iue watu wengi zaidi. ITS A SHAME!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 10, 2010

    Unajua elimu ndogo ni kitu kibaya sana. Kanuni za mwendokasi hazina mjanja.

    Madereva wanaopiga safari za masafa marefu huwa wanajidanganya kuwa wao ni wataalamu zaidi. Wakati ukweli unabaki pale pale. Kanuni za mwendo kasi ni constant.

    Bara bara hii ni nyembamba sana. Kwa hiyo katika kupishana na katika ku overtake ni hatari mno.

    Halafu barabara zetu haziko "even" zina manundu manundu. Gari inaweza kuyumbishwa ghafla ikipita juu ya nundu na kuvutwa upande mmoja ghafla.

    Hii ni sayansi na haina ubishi wala mjanja zaidi. Kama alivyosema mchangiaji hapo juu. Kuzingatia sheria, uangalifu wakati wa kupishana na kuovertake. Kuchukua tahadhari kwenye miinuko na miteremko.

    Sehemu zote hatari ni vizuri kupunguza mwendo mpaka uvuke maeneo korofi (kama vile kwenye kona ambazo huoni mbele).

    Kimbiza gari pale ambapo unaona mbele vizuri. Kama vile sehemu tambarare huku uzingatia uwezo wa kumudu gari kama kitu kitatokea ghafla ikiwemo tairi kupasuka.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 11, 2010

    Ajali kama hajali wakati mwingine huwa si za makusudi lakini kwa kipindi cha hivi karibuni madereva wamezidi utakuta barabara kama ya mbezi kupitia kawe asubuhi saa kumi na moja au kumi na mbili madereva magari madogo wanakimbiza njia mbili hata wewe ambaye unakaa karibu na hiyo barabara unapoomba kupita nawe uingie kwenye hiyo barabara hakupi nafasi. Wanakutana na vichaa wenzao (madereva) wanasababisha ajali. Jamani tunaotumia hivi vyombo kuendesha au kupanda tujaribu kuangali mwendo na kuwa wastaarabu kidogo tupunguze ajali, nchi kupoteza nguvu kazi na kuongeza vilema wengi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...