Glamorous caters for any Organizational, Personal, Leisure and Culture Events.
For more info please visit www.glamorous.co.tz
Email: info@glamorous.co.tz
Tel: +255 22 2772230/0784 410254
Home
Unlabelled
ana kwa ana na nancy sayore wa glamorous company
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


moja kati ya watu wachache nilioona wakihojiwa na MR MICHUZI na kuelezea/kujielezea kwa ufasaha na kuonyesha anajua nini anafanya, hongera dada maongezi yako tu yanaonyesha ur a serious professional,im looking foward to work with u NANCY.
ReplyDeleteBig up Michuzi wa libeneke kwa hiyo video. Lakini mzee bado tunasubiri interview ya jamaa wa TRA tuelewe kulikoni??
ReplyDeleteMdau USA
huyu dada nancy ni mzuri kweli anafanana na Ini edo yule mcheza filamu bomba wa kinaigeria hongera dada kwa ujasiriamali sio kila mdada china.. china.. uko juu huo ndo ubunifu big up sana
ReplyDeleteNancy umesema point nzuri sana kwamba watu wengi wanafanya biashara bila ya kusomea. ni kweli kabisa na ndio maana huduma nyingi zina kuwa za hafifu sana hazina ubora. si vibaya kuiga wazo la biashara ila jifunze sana. Kwa upande wako kwanza hiyo website ipambe sana kwa sababu hiyo ndiyo ina-kutangaza na watu wanaiona hiyo kabla ya kukuona wewe. hivyo usiwe katika lile kundi la wababaishaji na jaribu ku-google makampuni ya nje ya event management uone wanavyo fanya vitu vyao. La pili zitenganishe biashara zako katika majina na shughuli zake ili watu wajue kwamba wewe ni specialist wa idara hii tu. wapi na wapi mambo ya event yakaienda pamoja na kutafutia watu kazi? na kufanya usafi wa majumba?. si semi usifanye hizo biashara zingine la hasha, fanya kwa jina lingine, si jina la glamourous, hai pendezi na wala haya endi sawa na biashara zako kwa maneno mengine havina uhusiano. una weza ukaongeza biashara ya cantering and party rental company hii vinaendana.
ReplyDeletehalafu soma website yako ili uone kama ina mvuto kwa wateja wako, jifanye wewe ni mteja na ufungue website yako usome na utaona mambo mengi sana ya kurekebisha.
basi na kutakia mafanikio.
Muhimu kabisa la Mwisho- kama unapo fanya mahojiano na michuzi mtengenezee mistari ya maswali ili akuulize kibiashara zaidi na isiwe kama hukujiandaaaaaa.
asante -mdau-USA
Nimempenda huyu dada hebu nipe nambari yake! Tunahitaji wajasiliamali makini kama hawa, watu wenye uwezo wa kufikiri kwa haraka na kufanya jambo likaeleweka.
ReplyDeleteBless her heart!!!
Hongera Michuzi kwa kumuweka huyo dada on the blog. Kuna jamaa tukiwa kwenye corporate launch ya bank fulani aliniambia kwamba ukiwa na brand then hujui ufanye je ili utengeze impact; in terms of promoting it via an event, alisema Glamorous wanaweza. alienda mbali nakusema, 'all they do is 1st, understand yo product, ask you unataka kufanya nini then wao wanakaa chini naku create event idea inayoweza best promote brand yako...'
ReplyDeleteSasa leo naangalia blog naona Glamorous, nikasema 'duh. kumbe wapo kweli.'
Basi wacha tujipange tutakutafuteni dada Nancy ili tuone mtakavyotusaidia ku promote bidhaa zetu.
Marketing Manager
Agreed with your points, your Company helped us to organise an event, and the job you did was excellent.
ReplyDeleteI would like to say thank you, and let you all know how much i appreciate your wonderful job.
Well done Glomorous.
Nancy ni mimi nilietoa maoni hapo juu. nimekutafutia hizi company website angalia wanavyo changanya huduma zao. utaona ni kwa nini nimesema kwamba ondoa au tenganisha biashara zako. hawa ni event planner kama wewe nani wadogo ila wapo kwa muda mrefu .chukua muda uangalie website zao na kazi zao ili ukitoka uwe umetoka ki kweli kweli. mfano wao wana chapisha kadi,wanapiga picha si lazima upige wewe unaweza ukawa na kampuni ambayo inapiga picha na isikuangushe kabisa na wakawa kama sub-contractor wako.
ReplyDeleteweb ni hiii hapa.www.galaevents.com
Enjoy....!
kama ume-appreciate nifahamishe kupitia hapa hapa kwa michuzi.
Big Up Nancy!! Umejieleza vizuri sana na unaonekana unajua nini unachoongea, kwa kweli kama nitakuwa na shughuli nitakutafuta. Pia kuna mchangia mada mmoja alishauri uzitenganishe huduma zako hata mimi na-support hiyo hoja naamini utafanya vizuri sana kuwa na kampuni au majina tofauti zinazotoa hizo huduma. Pia jitahidi kuipendezesha website yako kwani ni kitambulisho chako cha muhimu sana na ndiyo inayobeba sura halisi ya kampuni yako. mdau NZ
ReplyDeleteNawashukuruni sana kwa pongezi, ushauri, kwa kunipa moyo na kwa kutambua uwezo wa Glamorous.
ReplyDeleteNina wahakikishieni kwamba pindi tutapofanya shughuli pamoja, tutaifanya kwa viwango vinavyo kubalika.
Kwa wale wote mnaonipa ushauri, naahidi kuufanyia kazi kwa kuwa naelewa ushauri wenu ndio utasaidia shughuli zetu ziwe bora zaidi.
Ahsanteni sana.