Home
Unlabelled
audio za sehemu ya hotuba ya JK leo jioni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hadithi za sisimizi kammeza tembo. Akaenda weeeeee njiani akatokea tembo. Sisimizi akammeza tembo.
ReplyDeleteNa hadithi yangu imeishia hapo.
Mwalimu: Hadithi yako inatufundisha nini?
Tafakali chukua hatua!
Mdau
Hebu mnielimishe, waungwana. Hivi ushindi wa kishindo huwa unapatikanaje? Au hawa wazee wana uwezo wa kumpa mtu ushindi wa kishindo? Wao wenyewe bado hawajalipwa pesa za Jumuiya ya Afrika Mashariki ya miaka ya 70!
ReplyDeleteMalalamiko ya wafanyakazi ni ya msingi, lakini hoja za rais hazina msingi. Kama kweli hutaki kuwaibia wananchi milioni 39, punguza safari za nje, mishahara ya wabunge na matumizi ya serikali.
ReplyDeleteHuyo bwana uwezo wake wa kuongea lazima uukubali!!Yaani watu wanaingia na mkwala mkubwa wa kudai chao, lakini wakifika kwa huyo jamaa basi kwisha habari yao!!anawapiga kizaramo kidogo!!jamani kuweni na subira,oooh hela hakuna,oooh mambo hayaendi hivyo!!hahaha!!Bytetime anaondoka, unashtukia haaa!!kumbe jamaa hatulipi!!mkitaka chenu huyu jamaa lazima mumuingia mkiwa na dhamira moja tuu, tupe chetu ndio tuongee mengine!!
ReplyDeleteStory za Alinache!!!! Akaenda weee akaenda weeee mwisho akafika. Mnae huyo for another 5 years!
ReplyDeletenashindwa kuelewa hao wazee wanashangilia nini? yani unaambiwa mshahara hauongezwi unashangilia? ni uwendawazimu au..
ReplyDeleteMheshimiwa Rais Jakaya Kikwete. Ingia Studio utoe Album. Ulitoa ahadi nyingi sana 2005,katika mikoa yote uliyopita. Kwenye ukweli uongo hujitenga. Hata hivyo nakupongeza kwa kufanikiwa kudhibiti ujambazi katika miaka 5 ya mwanzo,ila ufisadi bado ...................
ReplyDeleteNa safari usipunguze,kuna nchi hujatembelea bado...
Leo nimeamini jamaa msanii, kwanza kawatukana viongozi wetu wa TUKTA kwamba ni WAJINGA, halafu katutishia ETI TUKIGOMA HATUSAMEHE yaani ni ubabe tuuuuuuu.
ReplyDeleteHivi tunaenda wapi?? na hao wazee kawapata wapi?? Maana wanaonekana ni CCM( yellow and Green the whole room)
Si angekaa tu peke yake kama hutuba ya mwenzi akatafuta wapambe wa kumpigia makofi ya NINI??
UKWELI UKO PALE PALE KODI NI KUBWA MNO na manufaa yake mimi mwanaichi wa kawaida siyaoni na tena nalipa kodi mara MBILI kwenye MSHAHARA na DUKANI(VAT) usawa uko wapi ???
Nirushe Ankal nimechoka maana huu mshahara naona NAMBA kwenye karatasi tu!!!!
ninapenda JK akiongea na wananchi. ila doh, waswahili tunapenda ushabiki, sasa vigelegele vya nini??
ReplyDeletemichuzi mkuu wa nchi aseme kama huwezi kufanya serikalini huwe mwana siasa naomba kuuliza wafutao wanalipwa tzs ngapi kwa mwezi
ReplyDelete1.wabunge
2.makatibu
3.mawaziri
4.katibu wa chama
5.wpiga debe wa cmm ua mkuu wa propaganda.
na Nesi, mwalimu wa kawaida tzs104,000 analipwa je kima cha juu ni shiling ngapi na posho ya wabunge ni tzs kwa siku.
Kikwete hana hoja hapo, uswahili tu,hiyo mishahara ya wabunge milioni kadhaa kwa mwezi inatoka wapi? mbona bajeti inatosha kwa wabunge na maafisa wengine wakubwa? 315,000/- ndio nchi ifilisike? hao wazee wasio na busara hata chembe sijui wanashangilia nini? NATANGAZA TENA, MGOMO UKO PALE PALE, MPAKA KIELEWEKE.. msg sent
ReplyDeleteEeeh Mungu tunusuru, huyu kweli ndo tumempa dhamana ya kutuongoza? anatuongoza au anatuangamiza? Ni speech gani ile ya maajabu (out of this world) aliyoitoa?. hivi kweli anaona mwalimu kulipwa 104,000 ni haki?? kwa siku yeye anatumia shilingi ngapi? mweeee!
ReplyDeleteNa hawa wazee walokuwa wakimshangilia, wanakijua walichokishangilia? au kwa vile wameshapewa fulana na kofia za kijani basi wamejisahau?
au ndio yale Mrisho Mpoto aliyosema kwamba "sio kila anayekupigia makofi anakushangilia???? kwanini amewaita wazee tu ilhali anajua wazee tu??
Yaani nachoka, bado sijaamini kama speech ile imetoka kwa raisi DR.
Lakini mheshimiwa mkuu wa nchi, mbona kuna madai ya msingi yaliyoanishwa humo kuhusu mgawanyo wa haki sawa kwa hicho kidogo tunachopata watanzania, lakini wala hakukizungumzia? Tunagawana kwa uwiano gani kati ya viongozi, wabunge, wafanyakazi na sisi wananchi kama kweli kuna haki? Hawa wabunge ambao ni juzujuzi tu wamejipandishia mishahara, wao pesa yao hutoka wapi, mabilioni wanayogawana watu wasiozidi 5oo?
ReplyDeleteMheshimiwa, watumwa wako (watumishi kazi yao kutumwa) wanalalamikia mgawanyo usio sawa, wachache tena wanaofanyakazi kwa vipindi tu hulipwa mamilioni kwa mwezi. Na inapofikia mwisho wa muda wao wa ubunge (miaka 5 tu) kiinua mgongo chao ni utajiri tosha. Sasa mwangalie Daktari anayekesha kila siku kuokoa maisha ya watu, anapata nini kwa mwezi? Halafu ngoja sasa akongoroke (kufikia kustaafu), hicho kiinua mgongo chake anachopata baada ya kufujika kwa miaka zaidi ya 30, hakifiki hata robo ya kiinua mgongo cha mbunge aliyekuwa anasinzia mbungeni kwa miaka 5!!! Haki iko wapi?
Ndiyo maisha bora uliotuahidia watanzania katika kampeni zako? Sasa naanza kupata ufahamu, kumbe haikuwa maisha bora kwa kila mtanzania, BALI NI MAISHA BORA KWA KILA KIONGOZI!!!
Yaani wazee wa Dar wanishangaza sana!! Yaani watoto wenu wanaambiwa hakuna mshahara kupanda, ninyi mnafurahia na kupiga vigelegele!! Mmhhh!!
Sitetei mgomo, na wala sifurahii kugoma na wala sipendi wafanyakazi kugoma. Lakini mkuu wa nchi, bado iko haja ya kutazama uwiano wa kipato na kurekebishwa. Msingi uko hapo. Sawa, hakuna fedha sambamba na madai ya kima cha chini kilichosemwa, lakini, basi hiki kidogo kigawiwe kwa haki. isiwe kuna wachache wananeemeka zaidi kuliko walio wengi.
Sasa swali, Kwani mamilioni wanayolipwa wabunge, mawaziri, makatibu wakuu pamoja na marupurupu, magari ya kutembelea, hawa wananchi washangiliaji watanzania, kwa viwango vya hawa wachache wanaopata mamilioni, wananchi hawa wanafaidika nini?
Na hata kwa hili, UKWELI UTAUMA.
HAWA SI WAZEE WA DAR BALI NI WANACCM, SI KWELI KUWA WAZEE WA DAR WOTE NI WANACCM HATA HIVYO WENGI WAO BADO NI VIJANA KWANI SURA ZAO ZINAONESHA. PIA JK HAKUJIAMINI KWANI HAKUWA NA UKWELI WOWOTE KANI HAKUTUONESHA USHAHIDI WA KARATASI ZA MAKUBALIANO ALIZODAI NA NDIYO SABABU ALIONA AUFANYE UWE NI MKUTANO WA KISIASA ILI KILA ATAKACHOSEMA ATASHANGILIWA NA WAFUASI WAKE. HAO SI WAAJIRIWA HIVYO HAWAHUSIKI NA SUALA ZIMA KWAO UPANDE USIPANDE NI SAWA TU, KWANINI HAKUWA NA UAJSIRI KUWAHUTUBIA WAAJIRIWA? JK KUSANYA KODI STAHILI KUTOKA KWA WAWEKEZAJI NA WAFANYABIASHARA WAICHANGIAYO CCM ILI PESA ZIINGIE SERIKALINI UTAWEZA KUWALIPA WATUMISHI. MHE. JK ULIPOZINDUA CHANGIA CCM KWA MUDA MFUPI TU WAFANYABIASHARA WALIICHANGIA CCM KIASI WENGINE TULIJIULIZA HAWA NI KWELI WANAKIPENDA CHAMA HICHO KULIKO ELIMU NA AFYA? MBONA HAWACHANGII KWA KASI HIYO, LAKINI JIBU NI SERILKALI HUWAPA NAFUU YA KODI HIVYO WANALIPA TAKRIMA.
ReplyDeleteMRISHO MPOTO- si kila akupigiae makofi anakupongeza inawezekana anataka umalize upesi hotuba yako.
ReplyDeleteWakati wa Mwalimu sera ilikuwa: UHURU NA UMOJA
Sasa hivi sera ni:
UFISADI NA KUJILIMBIKIZIA
HONGERA SANA CCM.
kikwete jana hakutenda haki kwanza tuite kachamba si kuongea ile ni ubabe akiwa kama rais si kivile kweli kanikatisha tamaa kama alivyosema tusimpigie kura na simpigiii
ReplyDeletewasalaaam
Mdau dsm
NDIO MAANA NCHI YETU IMEFIKA HAPA...SASA HAPA HAWA WAZEE WANASHANGILIA NINI?
ReplyDeleteMDAU, UK.
MHESHIMIWA, ULIPASWA KUONGEA HAYA NA WAFANYAKAZI WENYEWE, SIO WAZEE, TENA WA CCM WA DAR ES SALAAM.
ReplyDeleteHAO WAZEE WOTE TEGEMEZI TUPU, KAMA SI KWA WATOTO WAO WANAOFANYAKAZI BASI KWA KODI ZA NYUMBA TOKA KWA HAOHAO WAFANYAKAZI.
SASA KWA TAARIFA TU HAO WAZEE KUANZIA LEO HII WAMEANZA AJENDA YA KUPANDISHA PANGO LA NYUMBA, JAMOJA NA KWAMBA HATA HAYO MAJADILIANO NA TUKTA HAMJAMALIZA, SISI TUNAKWENDA KUANZA KULIPISHWA PANGO KUBWA NA KUAMBIWA, "MAISHA YAMEPANDA BABA, INABIDI NIPANDISHE KODI YA NYUMBA, SASA CHUMBA SHILINGI 50,000/=, MAJI NA UMEME TUTAKUWA TUNACHANGISHANA KILA BILI ZIKIJA"
MUNGU IBARIKI TANZANIA. MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.
I have never seen such a clap speech from any president in this world maybe dictators!!!
ReplyDeletenahisi kichefu-chefu na nitatapika
nilichoweza sikiliza ni ile kauli yake "...wanajifanya..." hivi hii ni kauli ya mtu tuliyempa dhamana ya kuongoza nchi???
halafu unataja eti gharama za sh 315,000/ jumla yake na serikali iitoe wapi,ilhali viongozi izo pesa zinapatikana,magari ya kifahari na matumizi ya ajabu ya serikali aaah pesa inapatikana,kodi inayokatwa katika mshahara wa mfanyakazi na kodi zingine zooote aaah ni lazima tu,kima cha chini sh 45,000 sijui ni sawa tu nk nk nk...ambayo siwezi ongelea hapa maana nitachafua hewa!!
maana jana JK kachamba tena kachamba na sio hotua ya mtu mwenye akili timamu aongee vile..kweli kuelimika shida!!
KIINI CHA KIKAO CHA JANA ILIKUA NI MOJA TU KUMTUKANA MGAYA NA WAFANYAKAZI WA TANZANIA NA MAISHA DUNI YA MTANZANIA!!
na kweli JK ata kama unasema kula na wasinipigie,ok unaweza kupigiwa izo kula na kuwa rais tena ILA KUMBUKA HILI MUNGUAONAYE SIRINI NA MUNGU ALIYE WA KISASI NA ATAJIBU KATIKA HILO....sawa????????????
Huyu jamaa hana jipya... TUCTA wana madai matatu
ReplyDelete1. Mshahara
2. Kodi
3. Mafao
mbona yeye anashikia bango mshahara tuuu.. halafu mfano anatoa wa house girl. "mama kamchukua mtoto wa kazi toka kijijini...tucta inataka naye agome. JK""".. Hivi Raisi wa nchi anaongea hivyo kweli?
kanisa na lisimame katika zamu yake...kila mamlaka iliyo chini ya jua ni Mungu ameiweka
ReplyDeletengojeni tu
Najuuuuuuta kumchagua.....kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa,mahali pakuongea kwa utaratibu kiongozi mkuu wa nchi ana lugha ya kukashifu,kazi tunayo watanzania ......
ReplyDeleteMachozi ya mnyonge yana malipo
ReplyDeleteHATA MIE NINGEKUWEPO NINGEPIGA MAKOFI SANA NA VIGELEGELE AHHAHAHAHAHAH ASANTE JK.... MAKALI UMESHIKA WEWE BABA.....
ReplyDeleteMtajiju Tucta na wafanyakazi wenu mwenzenu keshajichukulia chake moja wapo ni kujenga mlima mzimaaaaaaa pale msoga sasa saa ngapi atasikiliza njaa zenu??????hakuna jinsi endeleeni tu kuumia
ReplyDeleteLakini kwa kauli aliyo toa jana JK si nzuri na inaonekana hana washauri wazuri,kwa nchi zilizoendelea hasa europe huwezi sema vile na watu wakakuacha tu,lazima leo angejiuzuru,yaani hata mgome miezi mshahara hutapanda.kweli jk kawatudharau wa tz.
ReplyDeletejuzi tu hapa kawapa wabunge fedha kibao eti kwa ajili maendeleo ya majimbo,majimbo kwa ajili kampeni?
ReplyDeletejamani kwakweli mimi watanzania siwaelewi sasa hao wanaojiita wazee wanashangilia nini? hivi watu hawafikirii kikao kimoja mbunge marupurupu anayopata ni zaidi ya kima cha chini cha mwalimu,nesi askari nk lakini cha ajabu watu wanashangilia!!!! halafu wanapomshangilia yeye wanamjaza kiburi this is unfair jamani!! hao watu wafikirie kuna wajukuu wao na watoto wao baadae wanawaomba msaada leo hii wanashangilia haya bwana yetu macho
ReplyDeleteMHS ze President of TZ kama ulivyosema kwamba huitaji kura za wafanyakazi 350,000 wa serikali basi tunakuambia ni kweli hatukupigi kula wewe na CCM yako.
ReplyDeleteHAKI YA MUNGU
MUNGU NAAPA!!!!!!
JK KAMA NI MKWELI ANGELIZUNGUMZIA HOJA ZOTE ZA TUCTA, HIVI HOJA YA KODI KUBWA KWA WAFANYAKAZI NAYO SERILKALI HAINA PESA? JK KWELI NI MTU WA WATU KWANI ANAWEZA KUWAKUSANYA WASIO HUSIKA AKAWAPA VITENGE NA KOFIA, AKAWAHUTUBIA KWA MSEMO ULIO SAIZI YAO NA WAKAMPIGIA MAKOFI.
ReplyDeleteDa JK Kachemka Sana Fedha ya Kodi Inayoukusanywa na serikali inaishia matumboni mwao tu,100% kodi haimsaidii mwananchi,JK kubali au ukatae mishaara inabidi ibadilike acha blaa blaaa we mbona unamaisha mazuri? Mbona mafisadi uliokumbatia wana maisha mazuri? Punguza Kodi au futa kabisa iliyobaki hii ya VAT Inatosha!!!!! Malupulupu madogo,inabidi serikali ichangie kwenye kiinua mgongo cha wafanyakazi,na kupunguza gharama za huduma za jamii.mbona bajeti karibia asilia 60 ni msaada,Wher the F***k our kodi inaenda,Sichagui kiongozi yeyote!!
ReplyDeleteMdau Wa DSM....usije mjini
Safi sana JK. Wanaolalamika ndo wale wale waliokupigia kura baada ya kuwapa tshirt.Watukane then chapisha kanga na Tshirt, wape then kura zote zako.hii ndio asili ya WADANGANYIKA
ReplyDeleteMkuu naona katelez KIDOGO. Huyu Rais anakuja nchi za nje (UK), kuna kitu kinaitwa Minimum Wage. Hii ni protection kwa waajiriwa ili kupunguza "Labour Exploitation". Suala la mshahara lazima uangalie kama huo mshahara unakidhi mahitaji ya mfanyakazi. Sasa hicho kima cha chini hatitoshi hata kulipia Kodi, nguo za kuvaa na mengineyo. Hii nchi imeoza na inaongozwa na watu wasio na mawazo wala fikra. Hata marehemu bibi yangu alikuwa anaweza kupanga bajeti yake kwa mshahara wa Mkoloni. Halafu tunashangaa kuona Rushwa TRA, ARDHI, POLISI, HOSPITALI. Tunashangaa kuona UKWIMI unaongezeka, mimba kwa watoto wadogo! Watanzania amkeni, amkeni ndugu zangu. Masuala ya Policies yanabidi yaendeshwe na watu wengi mtazamo.....
ReplyDeleteAnkal kama utaibana poa. Lakini Mheshimiwa amechemsha na mtazamo duni. Hivi Rais anongea kama yuko Gengeni - Hii nchi ina wasomi au wendawazimu? Hivi kweli Rais wa nchi anaongea Pumba namna hii? Hana idea za Macro-economics; Labour protection; Child protection wala nini. Kwa hiyo yeye ana-support wafanyakazi wa ndani walipwe Elfu tano au Kumi? Kwa hiyo hajui Trade Unions negotiations? Maswali yapo mengine saana - Ankal kama ni hivi basi kweli hatuna Rais is tuna Rahisi!! Kama hutaitoa naomba mpelekee waraka huu.
ReplyDeleteKama mshahara ni mdogo ... si ukatafute kazi penye mshahara mkubwa??? ... ebo!! ... tatizo labda ni elimu tu!!! .... wenye elimu zao walishatimka siku nyingi ... wanabeba boxes huko na kupata mishahara minono ... na hawahitaji akina Mgaya kuwa middle-men katika kujadiliana maslahi .... Kaza uzi JK; ulilegea mno, sasa ona matokeo yake ... kila mtu anakukojolea kichwani ... hakuna katika historia ya nchi hii katika awamu zote za uongozi ambapo mishahara imeongezwa kuliko katika awamu hii ya nne, tena bila tija. Mwenzako, Ben Mkapa aliwagomea hao jamaa hadi waonyeshe tija,na hadi anaondoka madarakani watamkumbuka kama mwajiri kweli kweli ... sasa wewe ulianza kwa kulegea ... mtoto umleavyo, .... hizi nchi za Afrika ukijifanya kufuata demokrasia ya wenzetu hatuwezi kwenda mbele, kila siku itakuwa taabu tupu ... FFU hawajapasha misuli yao kwa zaidi ya miaka karibu mitano sasa ... inaonyesha jinsi gani uongozi wako ulivyo lege lege ... watanzania hawajaoea hayo mambo ... ebu wape kitu uone kama hawatatulia .... ebooooooooooooo!!! Natamani Mkapa arudi ili ainyooshe hii nchi, maana imepinda ile mbaya!!!
ReplyDeleteBob Marley aliimba,“You can fool some people sometimes, but you can't fool all the people all the time.” Wananchi sasa wamechoshwa , na upendeleo wa dhahiri unaofanywa na baba yao serikali.
ReplyDeleteInawezekana vipi, serikali ambayo ni masikini kununua ma-VX yanayogharimu mabilioni ya shs kwa viongozi wizarani hadi mikoani ? Kwa nini serikali itumie shs bilioni 2.5 kujenga nyumba ya Gavana na naibu wake ? Kwa nini wabunge wasikatwe kodi wakati wanalipwa hela nyingi? Kwa nini serikali inatumia mabilioni ya shs kwa semina zisizo na vichwa wala miguu ?
HII NI HOTUBA YA KISIASA. NA HAWA WAZEE VIJANI NI MASHABIKI TU WA CCM. USHABIKI NI KITU KIBAYA SANA KWANI HATA LIVERPOOL IFUNGWE MABAO MANGAPI ANKAL ATAENDELEA KUWA MSHABIKI TU.
ReplyDeleteLAKINI UKILETA USHABIKI KWENYE MAMBO NYETI YA NCHI UTAHARIBU NCHI
halafu tunaposema haturudi bongo mnaturushia madongo ati mkataa kwao ni mtumwa nyoo sasa sisi na nyie nani watumwa?? tena ndani ya nchi yako lol!!! huku watu wanakula bata sana tuu ukifanaya kazi yako aaahhh mbona unakula mlo wa obama kabisa bila zengwe! hivyo vimishahara watu lazima wapate kwashakoo manake mtakula dagaa weee aka misumari hadi utumbo uote kutu manake ukijidai kuweka bajeti ya maziwa mayai nyama matunda utashaa wakati hayo ni mavitu ya lazima kwa mwanadamu lakini si binadamu wa huko bongo wao ni ugali maharage na kauzu hayo ndo maisha bora kwa kila mtanzania kweli inatia uchungu na maudhi kweli GOD IS WATCHING IKO SIKU!!
ReplyDeletePunguza hao wafanyakazi ili uboreshe masalahi ya wale watakaobaki ... serikali gani inahitaji wafanyakazi wote hao 350,000? Kwa nini mnabeba mzihgo msiouweza??
ReplyDeleteNa hao wanaotafuta ma-house-girl, kama hawana uwezo wa kuwahudumia, basi wakazifanye hizo kazi wao wenyewe ... huna uwzo wa kulipa mshahara stahiki, basi huna sababu ya kumwajiri mtu. PUNGUZA WAFANYAKAZI. KWANZA NI WENGI MNO NA HAKUNA WANALOLIFANYA.
Halafu ondoa kabisa malipo ya likizo ya mwaka, n.k. maana mshahara utakuwa unatosha kwa hayo yote.
PUNGUZA WAFANYAKAZI, watakaobaki walipwe vizuri... hii haihitaji kwenda Diamond kuwahutubia wazee vijana wala nini!! Lazima viongozi serikalini muwe na mawazo kama vile mnaendesha sekta binafsi ili ufanisi uwepo ... Punguza wafanyakazi ... ili uwe na uwezo wa kuwalipa vizuri watakaobaki ... na ukishafanya hivyo boresha na maslahi ya kustaafu; maana hapo sasa uakuwa umebakiwa na mzigo mdogo sana wa watakaostaafu kila wakati.
yani hiyo hotuba imekaa kiswahili sana kama vile unamshushua mtu kweli kiongozi wa nchi anaongea namna hii aibu gani hii yani jazba na ubabe kwa kwenda mbele hizi jazba kina gordon, obama hawana kabisa utanyukwa na mayai na madaraka uvuliwe ndo mana nchi zao zina maendeleo makubwa africa viongozi ni madikteta na mbabavu tuu ndo maana umasikini hauishi africa kila siku misaada tuuu hadi Yesu arudi kwani laki 3 ni nini? mbona nyie mnajipendelea mishangingi mipya kila siku mijumba ya mabilioni mnapeana vyeo ambavyo humu duniani havipo ili tu mjikatie mapande yani nchi yetu imeoza utawala wote ni mbovu na kwa nini hamkai huko dodoma si ndio mji mkuu? kaeni huko manake hayo mashangingi yanajazwa mafuta na serikali otherwise amishieni bunge dar es salaam manake ndo mnakokupenda sana haina maana mnakwenda dodoma na kurudi kila leo ni mzigo kwa serikali mr president wahamasishe hao viongozi wa nchi waamie dodoma tena uwe mkali mithili hii hii tuone na uwaambie wazi asiehama ataachia ngazi tuone kama watatekeleza amri yani bongo ni nchi ya kisanii sanii tu kazi kubebana tuu na kuonea wanyonge
ReplyDeleteMzee tukana sana! Usiwapandishie hata senti tano ya nyongeza. Huo ndo mchezo wanaostahili wadanganyika... uwe na uhakika kuwa mwezi wa kumi utaondoka na asilima 99 ya ushindi kwenye uchaguzi. wabunge watachanguliwa kibao kutoka CCM. usihofu chochote! watanzanania wakiambiwa kujihadhali na Chama chako hawasikilizi... sasa watasikiliza matokeo ya ubishi wao! Asiyesikia la upinzani ataona la kikwete. kwani kuendelea kuikumbatia ccm ndiko kunaotufikisha kwenye vitisho vya kiongozi vya wetu. mnataka ushahidi gani tena?
ReplyDeleteKAMA HALI YA SASA NDIYO HII BASI MAENDELEO KWA TANZANIA NI NDOTO KWA KIZAZI HIKI.
ReplyDeleteKIONGOZI MKUU WA NCHI ANAONGELEA SUALA NYETI KABISA KIMASIHARA SIHARA TU HALAFU KUNA WATU WANAOITWA NI WAZEE WANAPIGA MAKOFI WAKATI WOTE!!!!.
Mkiambiwa mchague wapinzani hao wapumzike wamelewa madaraka,mnaanza kuchonga sana. Na ndo maana wanawadharau wanafanya wanavyotaka mtawafanya nini? Chadema Oyeeee!
ReplyDeleteMdau
AFADHALI TU JK ANGENYAMAZA KIMYA KULIKO KWENDA KUHUTUBIA HAWA WAZEE WAKATI SIO WALINGWA WA HII HOJA.
ReplyDeleteRais wa nchi anashindwa vipi kuwaita viongozi wa wafanyakazi Ikulu na kuwaeleza hali halisi ya nchi kama kweli ana hoja ya msingi badala ya kwenda kuhutubia watu ambao sio wafanyakazi?
ReplyDeleteHivi mheshimiwa anasomaga hii Glob ya Jamii??
ReplyDeletejamani nauliza hivi ndivyo mheshimiwa anotoa hotuba. heshima iko wapi?????? , what kind of presentation is this ? ni ya mtu na mke mwenzie au ni ya mambo muhimu ya nchi. Atakae sifia na asifie lakini ukweli unabaki palepale . watu hata point hatuoni kwa sababu presentation y is soo cheap !!!!!! mi kila siku nasema vyeti haviongezi upeo jamani angalieni hivyo vyeti mmnavyovipigania vinawasidiaje katika kupambana na mambo haya ya kidunia la sivyo mwanao anaweza kukutukana na wewe ukatukana , nani ataonekana mjinga???? Right approach matter jamani, tutaaibika mjini!!!!!!
ReplyDeleteMimi nafikiri JK ametoa points nyingi sana katika hotuba hii. Kama alivyosema mtu mzima..., Ila akae chini na kutafakari yafuatayo
ReplyDelete1. Serikali ni watendaji si wasimamizi (Yaani viongozi wasiwe wengi ili kupunguza matumizi, mawaziri 60, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wabunge kila jimbo, wakurugenzi wa halamashauri, makatibu wakuu Nafikiri umefika wakati sasa kuwa na serikali ndogo iliyo fanisi. Weka wizara 12 zenye mawaziri 12 tu ambao pia wafanyekazi kama makatibu wakuu. Tuwe na Masekratari tu kama marekani.
2. Kweli si jambo jema kuwaahidi watu kitu ambacho hakitekelezeki kama mishahara minono, Je huyu rais wetu si ndiye aliyeahidi maisha bora kwa kila mtanzania 2005? haya yalitekelezeka?
3. Unaposema kuwaongezea wafanyakazi laki tatu na nusu mshahara ni kuwanufaisha wao kwa kuwanyonya wengine Million 39, Hivi Rais wetu hajui kuwa uchumi wa Tanzania unaendeshwa na wafanyakazi?, Mfanyakazi akilipwa vizuri atweza nunua vitumbua au kula kwa mama ntilie. Kununua biadhaa mbalimbali za viwandani na kilimo. Je hajui kuwa hao Mil 39 wanawategemea hawa laki tatu na nusu kwa maisha?
4. Rais wetu anapoongeza masulufu kwa viongozi na wabunge na kuwaacha watendaji (Where rubber hit the roads) haoni kuwa anajenga Taifa la wanasiasa na watu wavivu?, Maana kapa hard working does not have good reward, je kila mtu akitaka kuwa mbunge si tutamalizana?
5. Haoni kuwa kwa kuwalipa watendaji vizuri(wafanyakazi kwa vitendo) atapunguza rushwa na kuongeza tija kwa taifa?
Mwisho kabisa, Rais wetu afanye mambo kwa vitendo kama serikali haina uwezo basi iwe kwa wote siyo watendaji wakati wabunge na mawaziri wanajilimbikizia mali kwa kulala na kupiga porojo tu mjengoni wanakuwa rewarded very high. Hata mtoto ukimwambia sina hela halafu akuone wewe unarudi kila siku umelewa unanukia bia na nyama choma atajua kuwa ni danganya toto.
Tuwe wakweli kuwa serikali ipo biased na ni kama ipo kwa manufaa ya kundi dogo la waliojipenyeza kwenye uongozi hata kama hawana commitment ya uongozi. JK aache vitisho atatue matatizo ya wafanyakazi, kwani kuwa kwao wafanyakazi si previledge bali ni wajibu na haki yao kwa nchi yao iliyo huru. Motivation ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi badala ya kukatisha watu tamaa na kuwatisha.
Kwa kweli hotuba ya rais kuhusu mgomo wa wafanyakazi ni ya kibabe mno.Rais alitakiwa kuwaelimisha wafanyakazi na siyo kutumia vitisho.Tuangalie ktk nchi zote zenye machafuko chanzo ni mambo kama hayo.Serikali inaona kuwa ni mzigo mkubwa kuongeza mishahara ya wafanyakazi mbona wabunge,mawaziri,diplomats,makatibu wakuu na manaibu wao,wakuu wa mikoa n.k wanapata pesa nyingi na wanatumia magari ya kifahari?Je,pesa wanazolipwa wao hazitoki katika serikali ya Tanzania?Hakuna sababu yoyote ya kujaza magari ya kifahari kwa hao watendaji wa serikali.Hivi mkienda nchi za wenzenu mnajifunza nini?Au mnakwenda kununua nguo na kurudi?Hii ni aibu kubwa na inasikitisha kwakweli.Kwa hali hii rushwa itaendelea na haitakoma kwasababu wale wote wanaojifanya kupinga rushwa ni WALE AMBAO MATUMBO YAO YAMETOSHELEZWA.Wale wenzangu na mimi wanaodai nyongeza kidogo tu mnafikiri wataishije?Serikali haioni kuwa yenyewe ndiyo chanzo cha hili tatizo la rushwa?Kugoma ni haki ya mfanyakazi endapo kile anachodai hakijatekelezwa.Hiyo kusema vyombo vya dola vitatumika NI UDIKTETA HUO.Je,mkitumia hivyo vyombo vya dola na waandamanaji wakaamua nao kujibu mashambulizi mnafikiri nini kitatokea?Je,Tanzania ni nchi ya demokrasia au ni nchi inayoongozwa kimabavu?SERIKALI IKAE IKIJUA KUWA JUMUIYA YA KIMATAIFA INAWAANGALIA.Wafanyakazi wote wote mshikamano daima.
ReplyDeleteKuna siku jamaa mmoja alinishangaza kwa malalamiko yake kuwa"BORA KULAZIWA NYAU ULAYA AU MAREKANI UTAPATA HAKI NA HUDUMA MUHIMU KULIKO BINADAMU BONGO" Nilishangaa sana ila nimegundua kuwa kweli Nyau na wanyama wa nchi zilizoendelea wana uhuru na protection kubwa sana kuliko binaadamu wanaozaliwa nchi za dunia ya tatu kama Tanzania. Wapi haki za wafanyakazi?
ReplyDeleteTatizo kubwa ni moja hatuna demokrasia ya kweli. Tume isiyo huru ya uchaguzi, vyombo vya dola vinavyotumikia matakwa ya viongozi badal ya sheria za nchi. Ama kwa hakika Tanzania ingekuwa na Chaguzi huru na haki basi huu si mwaka wa mwanasiasa anayetajia kuomba kura toka kwa wananchi kuongea aliyoongea JK.
Rubish,
ReplyDeleteSAA YA UKOMBOZI NI SASA - WHY WAIT
ReplyDeleteAnkal ulinibania au zamu yangu ilikua haijafika!?........Mheshimiwa huku huwa anarambaza? nauliza kaswali kadogo tu.....hivi mle mheshimiwa Wazee wa Jumuiya ya Afrika Mashariki walikuwemo? mweeeh!....MVUA INYESHE KWAO TU......KWETU ? nakulaaani kimoyomoyo!
ReplyDeletegloves off, but at least I think this is the beginning of the end of years of misrule, corruption and exploitation of the Tanzanian's poor. I'm impressed that 99% of comments posted have been in favour of the workers. God bless Tanzania and give us the strength to fight the establisment which is taking us nowhere.
ReplyDeleteSio kweli kuwa serikali haina pesa za kuwalipa wafanyakazi..wao(walio madarakani)wanalipana mamilioni ya shillingi kwa kazi wasizofanya..halafu wanakuja hapa ktk magari ya serikali kuleta dharau na kiburi kwa watu waliowapa ulaji(waliowachagua).Hotuba ya raisi imejaa vitisho,dharau na jeuri ya hali ya juu.mi nafikiri ni wakati umefika kwa hawa watu wa ccm kupata reality check;vote them out!
ReplyDeleteNilipata kusikia kwamba wakati fulani enzi za mwalimu kiongozi mmoja wa kenya alimwambia Nyerere ANATAWALA MAITI. Ndio haya ya sasa tunayaona.
ReplyDelete"Hata ikibidi kula nyasi watu wale lakini ndege ya rais inunuliwe"
"Watanzania ni mambumbu hawajui kitu"
"EPA keleleee wee mwishowe ziii"
"RICHMOND mayowe kibao mwisho wa siku jii"
"Mishahara ya wabunge isiongezwe mwisho wa yote imeongezwa"
"Posho ya jimbo isitolewe hatimaye inatolewa"
"Bei ya mafuta na bidhaa nyingine zinapanda kila siku hakuna anyethubutu kulalamika"
"Athari za mazingira north Mara kimyaa"
"madai ya walimu danadana"
"Mikataba mibovu ya uwekezaji hakuna anye jali"
"Ubinafsishaji wa mashirika ya umma usio na manufaa kwa taifa hakuna anayejali"
Pamoja na hayo yote uchaguzi ukija ushindi wa kishindo kwa CCM kwa nini mtu asijenge confidence ya kukudharau.
Du la salalee!! JK sasa hivi moto, tena wa kuotea mbali.
ReplyDeleteUmefanya good analysis ya problem,na good reporting na mwisho ukali unaotakiwa kuendesha serikali hii ya wabongo!
Tumekupa rungu kugonga wanofuruga nji hii.
Ukiendelea hivi hata kwa mafisadi hapanshaka kura yangu unayo mwakwetu!!!
Wafanyakazi 350,000. assume kila moja ana ndugu 10 wenye umri wa zaidi ya miaka 18 ambao wanamtegemea, kwa hotuba hii pumba, kama kila mfanyakazi atawaambia hao ndugu zake JK kawatusi na hataki kuongeza mshahara, maana yake JK atapoteza kuru 350,000 X 10 = 3,500,000 october au?.
ReplyDeleteHebu mie,alhamis nika vote chama cha labour
ReplyDeleteNyie mnasema tu,kama alivyochangia mdau hapo juu kuwa viongozi wa Tz wanaongoza maiti.
ReplyDeleteMtamwambia nini Jk wakati matokeo ya utafiti wa Redet anaongoza kwa asilimia 80. Bunge la bajeti anaongeza mshahara kidogo kama asilimia 1.4 na kupunguza kodi ya makato kwa wafanyakazi kwa asilimia 0.5. Baada ya hapo anaingia mtaani na kuwasahaulisha kwa kuomba kula. Watanzania tulivyorogwa na kujitapa ameshinda kwa kishindo. Sisi tuliwaambia wameona matokeo ya kuchagua sura.
Mungu ibariki Tz.
Mdau
MBONA WAZEE WENYEWE WOTE NI DINI MOJA? CCM ACHENI UDINI
ReplyDeleteHivi wewe hapo juu umetoka wapi? Watu wanzungumzia Mafao ya wafanyakazi wewe upo na udini? Kwani hujua siasa za TZ zilianzishwa na watu wa dini gani? Hujui kuwa TAA, TANU zimeanzishwa kwa hao wazee? Wewe babu zako walikuwa wanachunga Ng'ombe wakati watu wanatafuta Uhuru kutoka kwa wazungu. Amka na kasome historia ya nchi yako Bwege wewe!!
ReplyDeleteAnkal!
ReplyDeleteKwanza nikupongeze kwa kuwa 'mwanaume wa shoka' kwa kuuachia huu mjadala uedelee bila kubinya komenti wala nini. Big Up sana. haya ndio mambo. Unajua unamsaidia sana JK kujua hali ya hewa ikoje, kwani sidhani kama washauri wake wana mshipa kama wako wa kuacha mambo hadharani, ili na yeye mwenyewe JK apime upepo kama umejaa ama la. Hongera kwa hilo, na kama mimi ningekuwa JK ningekupa tunzo kwa kutotaka kusema uwongo kwa kuruhusu komenti za kusifia tu na za kuchana ubane. Hii ni feedback nzuri kwake yeye JK na washauri wake ambao wengi inaonekana wana nidhamu ya woga ile ya kumwammbia 'mkuu mambo yote poa, wananchi woooote wako nawe' wakati sivyo.
Baada ya hayo naomba unipe nafasi niwaulize woote walimponda JK kama wana njia mbadala wa hiyo aliyotumia kuwapasha TUCTA. Maana sie wamatumbi kazi ni kuponda tu, lakini toa wazo mbadala kifanyike nini ama kingefanyika kitu gani, utasikia ohh wenzetu Rwanda sijui mbona hawako hivi blah blah blah.. yaani hadi inakera!
Kwa maoni yangu hao TUCTA sio bure, iko namna. hata kama wanasema walikuwa wametoa ilani siku kibao zilizopita (mwaka jana sijui...)lakini hapa kuna harufu ya dili na mahesabu. TUCTA walikuwa wapi siku zote kama si unafiki kama aliosema JK? Eti wanadai Kapuya 'kaganga' maamuzi yao ya Lesco sijui nini, hii inaingia akilini kweli??? Nikiwa kama mmoja a mbayuwayu wa JK sioni mantiki kabisa TUCTA waseme Kapuya kagushi mazungumzo yao na kupeleka ya kwake. Huu ni uzanduki mwingine.
Vile vile nasikia wanatafakari ili wajibu mapigo ya JK hivi karibuni, sasa wajibu nini tena wakati mkuu keshasema? Rais, kama mahakama na taasisi zingine nyeti, ni mhimili wa Taifa. akishasema, kama ilivyo mahakamani Jaji akiamua, ama refa akiamjua hakuna wa kupinga. Waje na gia ingine bana! Wasitutibulie pozi hapa! We huoni nchi zote zinabroo na Bongo kiasi cha kung'angania kila mkutano ufanyike hbapa? kwa nini? mbona hawaendi huko Rwanda mnakosema mambo swafi? Kule bwana hakukaliki, msione vyaelea....JK akigeuza kibao cha kuwa mstaarabu na mfuata utawala wa sheria na kuwa kama Kagame hapa mtasema nini sijui. ACHENI HIZOOO!
Mkwere wa watu anapiga bao maraisi wote waliopita kwa kila kitu, ila basi tu nyie mnaompinga ambao wengi ni wa chama cha mtaa wa pili hamna jipya!
KIKWETE BABA MSHAURI WAKO HAKUFAI, NA KAMA HUNA MSHAURI BASI TAFUTA MSHAURI, USIKURUPUKE TU MWANANGU TAFUTA MSHAURI MWENYE BUSARA
ReplyDeleteNyie serikali punguzeni sana gharama zenu za uendeshaji na aachaneni na kutoa misamaha ya kodi isiyo na kichwa wala miguu ili msaidie wafanyakazi. Gharama za maisha zimepanda sana na wafanayakazi wanateseka, muogopeni Mungu pia japo kidogo.
ReplyDeleteMie wa TZ mnanishangaza. Kura mlimpa wenyewe kwakutojua kuwa mnadanganywa na flana na ttshirt vya thamani ya shs 5,000. Aliyesema tz ni maiti sidhani kama alisema uwongo. Kila mtu katika nafasi yake huwa kuna mtu nyuma yake kamuwezesha. Sidhani kama ni busara kutomtendea haki aliyekufikisha hapo ulipo. JK hapo sijampenda. Wafanyakazi anaowatishia kuachisha kazi maskini hao ndio waliomuweka IKULU. angeongea na viongozi wao aangalie namna ya kusevu hii ngoma. Na wazee siku hizi naona hawana hekima. Watoto na wajukuu wao wananyimwa ulaji nao wanashangilia. Ni watoto hao hao wanaowategemea. Nafikiri hivi vyakula feki viharibu akili. na wazee wameathirika zaidi
ReplyDelete