Michael Richard Wambura

Na John Bukuku
Michael Richard Wambura, aliyekuwa mgombea uenyekiti wa klabu ya Simba akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Malelezo juu ya kufungua kesi katika mahakama mbili Mahakama kuu na mahakama ya Kisutu kuhusu kukatwa jina lake kuwa mgombea wa nafasi hio.

Amesema Katiba ya Simba imekiukwa kwani Simba ilitakiwa kuunda kamati ya Rufaa ambayo ndiyo ingekuwa na mamlaka ya kushughulikia matatizo ya Simba juu ya uchaguzi.


Amesema kamati hiyo pamoja na kamati ya Uchaguzi iliyopo sasa zilitakiwa kupewa baraka ama kuthibitishwa na kamati ya utendaji ya Simba kitu ambacho hakijafanyika hivyo hata kamati ya uchaguzi ya Simba ya sasa ni Batili kwa mujibu wa katiba ya Simba.

Wambura amesema wamefungua kesi mbili katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Kisutu ili kutafuta haki.

Anasema kwa kutolea mfano wa hukumu moja iliyowahi kutolewa na Jaji Bubeshi wa mahakama kuu ya mwaka 1996 iliyokuwa ikimkabili Muhidin Ndolanga na Baraza la Michezo.


Akinukuu moja ya kifungu katika hukumu hiyo Wambura anasema "kifungu hicho kilieleza kwamba kama unanyang'anywa haki usingoje muda upite itafute hata mahakamani kwa kipengele hicho, anasema mahakama imemruhusu kutafuta haki yake huko, lakini pia anasema kwa kuwa katiba ya Simba inatambua Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania hivyo imeruhusu mwanachama yeyote kwenda mahakamani kudai haki yake".

Ameongeza kwamba ameliarifu Shirikisho la Soka Afrika CAF na Shirikisho la Soka la Dunia FIFA kuwa kuna mgogoro katika klabu ya Simba na TFF hivyo amekwenda mahakamani kudai haki yake. Pia, amewalaumu TFF kwa kuingilia kanuni za tararibu za katiba ya klabu hiyo na kwamba shirikisho hilo halikupaswa kuwa na kipengele cha pingamizi kukatwa kwenye Kamati ya Uchaguzi.

Alisema walipokiangalia kipengele hicho walipaswa kuwarudishia Simba ili wakirekebishe, lakini wao waliamua kuwafunga mdomo watu kwa kutokiondoa kipengele hicho.

Wakati huo huo, hakimu wa mahakama ya Ilala, Janeth Kinyage, ameitaka kamati ya utendaji ya klabu hiyo kukutana na kutafuta wakili baada ya mawakili watatu waliowekwa na watu tofauti kudai kila mmoja kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuitetea kamati hiyo dhidi mwanachama Juma Mtemi kutaka uchaguzi usifanyike.

Hakimu huyo alichukua hatua hiyo baada ya kamati ya utendaji ya Simba kuendelea kujichanganya kuhusu wakili ambaye anaitetea kamati hiyo ikitaka uchaguzi uendelee.

Alisema awali alipokea barua ya mawakili kutoka kampuni mbili kwa makundi mawili ambayo ni ya uongozi ambaye alipewa barua na katibu mkuu wa Simba, Mwina Kaduguda, ambaye ni wakili Majura Magafu na mwingine kutoka kwa wajumbe wa kamati ya utendaji wakiwakilishwa na wakili Peter Swai.

Alisema kuwa tangu aanze kazi ya kusikiliza kesi mbalimbali hajawahi kukutana na kesi kama hiyo ambayo ina mawakili watatu na kila mmoja hataki kushirikiana na mwenzake na kila mmoja kudai kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka ya kusikiliza na kuitetea kamati hiyo ya utendaji.

Hivyo, Kinyage aliitaka kamati hiyo ikutane na kukubaliana ni wakili yupi asimame na kuitetea kamati hiyo na wawasilishe kwanza mwakilishi huyo .

Alieleza kuwa bila kufanyika hilo atamsimamisha kizimbani mwenyekiti wa Simba (Hassan Dalali) mwenyewe bila mwakilishi kwa kuwa haki yao ya msingi ya kutetewa watakuwa wameipoteza,

Jambo lingine ambalo lilizuka mahakamani ni baada ya wakili wa Juma Mtemi ambaye amefungua kesi hiyo, Mh. Jerome Msemwa, kuikana barua iliyowakilishwa mahakamani hapo ya kufuta kesi.

Alisema kuwa barua hiyo haijaandikwa na mteja wake, hivyo kuitaka mahakama ichukue hatua kwa wale wote waliohusika na kughushi barua hiyo ikiwemo saini ya mteja wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2010

    Michael Richard Wambura!
    Kwa njia hiyo imeonesha unamapungufu makubwa ya kifikra na ubunifu wa mbinu za kukabilianana maisha.
    Unachotaka hapo ni kujisafisha. Lakini badala ya kufanya hivyo unajipaka uchafu ambao huenda kwa umri utakao kuwa umejaaliwa na mwenzi mungu HUTA KAA UTAKATE Fuata nyayo za mzee NDOLANGA umemtembelea na kupata nasaha zake kabla ya kukimbilia mahakamani???
    Hayati Mzee Richar wambura alikuwa mtu aliyejaaliwa busara nyingi. Wewe ni uzao wake kweli??? tunachelea kujiuliza hili.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2010

    Anony Wed May 05, 11:59:00 PM jiheshimu utaheshimiwa. Inaonyesha jinsi gani umetumwa kutuma ujumbe huu. Na kuhusu uzao wake, wewe ndio mkuu wa kitengo cha DNA?
    Wacha mtu atumie haki ya kidemokrasia mradi havunji katiba. Huyo aliyekutuma anataka atawale kwa mlango wa nyuma kuanzia TFF hadi Simba?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2010

    hivi haya ni mapenzi ya kweli na Simba au ndo kutafuta ulaji? its a shame kwa kweli.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2010

    Alichofanya WAMBURA nihaki yake tunataka klabu ya simba irudi kariakoo sio posta wewe unae mchambua WAMBURA hapo juu hujui mambo ya simba ndio maana unalingalisha haki ya michael na Baba yake mzee Richard Wambura hapa pana fitina mbona TFF hawaingilii uchguzi wa timu km JKT ruvu?

    ReplyDelete
  5. Kwa namna hii huyu jamaa hana lingine ila nikuharibu tukose wote, yaani Simba wafungiwe na yeye aendelee na shughri zake, nashindwa kumuelewa, anaju wazi kuwa FIFA si TZ wameweka sheria ifuatwe kwanini hajaenda kwenye mahakama ya michezo? analake ni mamuluki wa YAnga kama inawezekama anyang'anywe card atuachie sisi tunaejali sheria za michezo kwani hajui TUCTA wanamahakama zao? mbona hawajaenda kisutu? analake JAMBO.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2010

    Kuongoza Simba kuna nini hadi Wambura ang'ang'anie namna hiyo, nashindwa kupata majibu ya maswali yafuatayo:
    1. Kuandika barua FIFA wakati timu inacheza Misri wiki hii kulikuwa na madhumuni gani?

    2. Kwa nini Wambura alikubali na hakwenda mahakamani wakati uamuzi wa kutokuwa na "integrity" ulipotolewa kwa mara ya kwanza na jaji Mkwawa?

    3. Kwanini hakupinga katiba ya Simba kabla hajaenguliwa wakati kikao cha kuipitisha alikuwepo na aliiunga mkono?

    4. Hakuna kazi nyingine anayofanya maana anapoteza muda mrefu mahakamani?

    Kwa mtazamo wa haraka huyu mtu anachotaka ni yeye kuongoza simba kwa namna yoyote na yuko tayari kuona Simba ikiharibikiwa kama yeye hakupewa uongozi ndio maana ameandika barua FIFA huku akijua hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi ya Simba. Nadhani watanzania sasa wamemfahamu ni mtu wa namna gani sio katika simba tu hata nafasi yoyote ya madaraka. Ni vizuri historia yake ikachambuliwa toka akiwa mdogo ili watu wamfahamu vyema.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 06, 2010

    Wambura! kwani lazima uwe kiongozi wa 'football' ndiyo maisha yako yaende. Tafuta mbinu nyingine hapo ulishachemisha. Ndiyo faida ya kutafuna hela bila kufikiria baadaye itakuwaje.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 06, 2010

    Ukweli lazima usemwe: Watu kama hawa wakiendelea kuachiwa kufanya wanavyotaka hasara tunapata wote nchi nzima, sio Simba peke yao. Katika historia ya nchi hii hasa kwa wapenda soka, hakuna kipindi ambacho hali ya soka ilikuwa ya kutia kichefuchefu na ya ubabaishaji mno kuliko kipindi huyu bwana alipokuwa mtendaji mkuu wa TFF (FAT wakati ule). Wafadhili walikimbia kabisa kudhamini soka maana kulijaa kila aina ya ubabaishaji wa kiwango kilichokithiri. Sasa anaonyesha 'his true colours' Wana Simba mwangalieni huyu bwana kwa macho matatu, atawaliza na kuivuruga sana Simba. Hebu jiulizeni anachokifanya ni kwa faida nani??? Kwenda mahakamani ili iweje au kufanikisha jambo gani?????
    Ndugu yangu Wambura, naomba tu uukubali ukweli kwamba kipindi chako kimeshapita kwa wewe kuwepo katika masuala ya soka, waachie wenzako nao walete mawazo yao mapya, maana HUKUBALIKI KABISA, lakini la muhimu zaidi hayo mawazo yako kwanini usiyapeleke kwenye michezo mingine inayohitaji mawazo mapya kama, Kriketi, Mieleka, Kuongelea n,k?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 06, 2010

    Hata baba wa taifa hili wakati anagombea uhuru wengi walimuona kama wewe unavyomuona leo Wambura,anachofanya Wambura ni kukomesha uozo uliojaa katika jamii yetu hasa katika hivi vilabu vyetu sikulaumu sana wewe kwa vile nahisi huijui Simba historia yake ilipotoka na sasa ilipo, Simba kila kitu ukijuacho lakini leo masikini wa kutupwa na umasikini huu unaletwa na wajinga fulani wachache kama wewe kwa mfano leo kuna fulana zinanembo ya Simba na zimeuzika sana lakini klabu ya simba haijaambulia kitu ,kuna maduka ya klabu wachache wamepangisha kwa shilingi elfu hamsini kwa mwezi lakini tunavyosikia ni shilingi laki tano kwa mwezi sasa tunataka kuwaondoa wajinga hawa nyie hamtaki ,kuhusu kukatwa kwa wagombea wengine akiwemo Michael Wambura si kweli ya kwamba ati Wambyura ana uchu wa madaraka anachofanya yeye ni kumfunga paka kengele ili uozo huu usitokee tena kwa vizazi vijavyo haki itendeke Simba wanakatiba yao haiingiliani na TFF sasa wambura kafungiwa na tff anagombea simba Tff hawataki wanachama wa Simba wengine wanamtaka sasa aende kushitaki wapi? mbona yule aliyempinga hamumuoni ya kwamba ni msaliti wa Simba muhimu wangemuacha Wambura wanachama wa simba wamkatae na siyo TFF imkatae hii kwa kweli inatia kichefuchefu sana vilabu vyetu vinaendeshwa kama kampuni binafsi hao akina Kasim nawenzake wanaipeleka Simba Pabaya sana sisi wanasimba tuungane ili tupate uongozi imarana klabu yetu ifike mbali sana kwani mimi sioni tofauti ya Simba na MAN U,ARSENAL NK.
    moodsly

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 06, 2010

    KWANINI WAMBURA AWE NA HAMU YA KUKOMESHA 'UOZO' SIMBA LEO???? (KAMA KWELI KUNA UOZO!!) SIKU ZOTE ALIKUWA WAPI???? KWANINI HAKUENDA SIMBA, TFF AU FIFA WAKATI HUO, KAMA KWELI ALIKUWA NA HOJA ZA MAANA?? SIMBA SI WANA KATIBA NA VIKAO VYA HALALI VYA KUENDESHA MAMBO YAO?? KWANINI HAKUWASILISHA MASUALA HAYA WAKATI HUO KWA TAASISI HUSIKA ILI YAISHE WAKATI HUO??? MIPANGO YA UPANGISHWAJI WA MADUKA YA SIMBA, UUZWAJI WA FULANA HAIKUANZA LEO, IPO SIKU NYINGI TU!, SIKU ZOTE HIZO WAMBURA ULIKUWA WAPI???? HIVI WAMBURA UNAJUA KWAMBA: SIMBA IMEMALIZA LIGI IKIWA BINGWA KWA REKODI AMBAYO HAIJAWAHI KUTOKEA KATIKA NCHI HII??. HIVI UNAJUWA KWAMBA SIMBA INA MECHI MUHIMU YA KIMATAIFA KESHO KUTWA NA KUNA ATHARI KUBWA SANA SIMBA ITAPATA KWA UAMUZI WAKO HUO WA KWENDA MAHAKAMANI??!! HIVI UNAJUA KWAMBA SIMBA INA MWALIMU BORA WA MPIRA HAPA TANZANIA? HIVI UNAJUA KWAMBA HAYA YOTE NI MAFANIKIO YALIYOLETWA NA WATU WALIOFANYA KAZI KUBWA SANA KUFIKA HAPA?? KWANINI WEWE UNATAKA KUVURUGA MAFANIKIO HAYA?? KWANINI UNATAKA KUWARUDISHA WATU NYUMA KWA NJAA ZAKO? HIVI UNAWEZA KULINGANISHA UPUUZI WAKO HUO WA KWENDA MAHAKAMANI KWA MAFANIKIO HAYA???!!! ETI NINI UNATAKA KUSAFISHA UOZO KWA SABABU UNA UCHUNGU NA SIMBA???!!! HUWEZI KABISA NA NI BORA UNYAMAZE!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 06, 2010

    Anachofanya Wambura ni sawa na kugombana na mke halafu ukawaachisha shule watoto wenu ili mke asikitike, swali je wewe huwajutii watoto? Wambura alishaongoza Simba na sehemu mbali mbali na zote zilikuwa na migogoro mikubwa na kesi kila siku mahakamani. Inaelekea hii ndio namna yake ya uongozi, maneno anayosema ukiyasikiliza ni sawa na wana siasa wanaoahidi mabomba kutoa maziwa badala ya maji, anapaswa kuulizwa kwa nini hakutekeleza hata moja wakati akiongoza? Tusipochukua tahadhari mapema huju jamaa atavuruga mpira na mambo mengine ya nchi hii na kwa bahati mbaya wananchi wengi wa Tanzania kwa kawaida hawachambui mambo kwa kina na kuangalia mbali.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 06, 2010

    acha kutetea ushuz ati simba haina toafauti na mau or arsenal unaota mchana wewe haiko close hata na wigan tuliza mzuka kama wambura mjombaako hapati kitu anang'ang'ania nini ? si awe mjasiriamali ? aanze kwenda china kuleta mzigo atatoka tuu na sio mpira tuu au vile huko hela za mteremko bila jasho? safi saana tff TUPA KULEEE!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 06, 2010

    kutoa mawazo ni haki ya kila mtu,nimeyasoma maoni ya wengi lakini ninachoweza kusema ni kwamba klabu ya simba ipo msimbazi na siyo posta kama mchangiaji fulani na wote wanaompinga Wambura ni vibaraka wa simba posta kila kwenye ukombozi lazima wajitose watu wachache kama afanyavyo Wambura sioni tatizo hata kidogo mtu kudai haki yake hata kama atawaudhi wengine wachache nasema anachofanya Wambura ni sahihi kabisa hasa kwa vizazi vijavyo na siyo sisi tena.kuhusu utendaji wake wa wakati uliopita ati wafadhili walikimbia kuisaidia simba haya mawazo potofu ndiyo tuanayotaka kuyaondoa Simba haihitaji kuwa na mfadhili Simba inauwezo wa kuifadhili hata TFF kama uongozi utakuwa mzuri lakini kwa vile mnataka kuongozwa na Simba Posta hakika simba itaendelea kuwa ombaomba miaka yote cha msingi ni kwamba Wambura ni kiongozi mwenye misimamo naklabu zetu hizi kuna watu wanazitumia kuishi hivyo wanawahitaji viongozi longolongo wala rushwa,wezi wasiona huruma hata chembe anachofanya Wambura ni sahihi naunga mkono kwa asilimia miamoja

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 06, 2010

    Hivijamani kwani lazima mtu uwe Kiongozi wa mpira ? Au Mbunge ? Maana huyu jamaa yaani ana uchu wa madaraka kupindukia. Alikuwa baiskeli wakamwondoa. Akaibukia FAT aliyoyafanya pale kila mtu anayajua.

    Bado tu hajachoka anataka tena aingilie na Simba yetu kuididimiza? Hapana jamani...sisi si wajinga kiasi hicho. Mbona akina Hans Pope hawalalamiki? Yeye tu ndo anajifanya ana uchuingu kuliko watu wote? aaa bwan...ana lake jambo.

    Mi najiuliza kuwa kama kweli hamna namna ya kuibia Klabu, ni kwanini basi jamaa akope kiasi cha Milioni Thelathini na nane000,000)eti kwa ajili ya Kampeni ya uchaguzi wa Simba....hizi pesa zinarudi vipi kama si kwa kuiibia Klabu ?Hivi ni kweli kuwa Wambura anaipenda Simba kiasi cha yeye kukopa mamilioni ya shilingi ili tu achaguliwe? Tusiwe kama Kong'ota...huyu mtu si mwema kama anavyotaka kutudanganya....ni wa kuogopa kama UKOMA.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 06, 2010

    ni hivi jamani WAMBURA kabla hajachukua fomu alitangaza mikakati ya
    1 kusimamia mali zote zinzo husu klabu
    2 kusajili nembo ya klabu
    3kutafuta kiwanja cha kudumu cha klabu
    NAMENGINE MENGI SWEZI KUANDIKA YOTE.Sasa kinachoendelea hapa nikummaliza ili wale wanao tumia nembo ya klabu kwa faida yao waendelee kula,wale walio pangisha mayengo kwa maslahi yao waendelee na ulaji maliza klabu,Timu isajiliwe kwa michango ya watu au mtu mwenye mchezaji wake amsajili siku mkimnyima ulaji anamwambia mchezaji wakeacheze chini ya kiwango haya yote wambura aliahidi kuyamaliza ndio maana wanammaliza hana tamaa ya uongozi ila unaposema mtu hana maadili mpe sababu maana unamwaribia haakigombea ujumbe wa nyumba kumi hapati nimeandika kwakirefu ili nieleweke

    ReplyDelete
  16. ObserverMay 06, 2010

    Wote wanaomsuport Wambura na upuuzi wake ndio wale ambao Bonge wa Power Breakfast, Clouds FM anawaita Wapuuzi. Huyo Wambura ashaongoza miaka mingapi kwenye michezo na ni kipi anachoweza kujivunia aliwahi kukifanya katika kuleta mabadiliko ya michezo. Hv Watanzania tutabadilika lini sijui.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 06, 2010

    wanasimbaaa kuweni MBAYUWAYU!! kong'ota huyoooooooooooo

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 06, 2010

    Si lazima mtu uwe kiongozi wa chama fulani au club fulani, lakini unapoamua kuingia kwa hiari yako na ukaamini vigezo unavyo, kwanini watu wengine waibe haki ya wapiga kura? wanachama wa Simba ndio wangeamua! Unaposema kwa mfano ...Heshimiwa MAH**TA sio muadilifu kwa ndoa yake, watu wanakuelewa, ndio ! si mtoto wa nje ya ndoa amegundulika ni wake.
    Sasa Wambura sio muadilifu kwa USHAHIDI gani? kammegea nani mkewe?
    yaleyale ya DK SL*A, alipigwa zengwe akaenda CHADEMA. Ndio maana tunataka mgombea Binafsi na watu hawalali kujaribu kuzuia asiwepo kabisa, wakati kwa BASHIR juzi walikuwepo na mambo shwari tu.
    KWA KWELI, WAMBURA USINGECHUKUA UAMUZI HUU....NINGEKUSHANGAA SANA, DAWA YA ZENGWE NI HIYO TU!

    ReplyDelete
  19. willy mdauMay 06, 2010

    kama wengine walivyotangulia nadhani awaachie wengine waongoze kwani kipindi chake kilisha pita sasa mpaka kukimbilia mahakamani kwa ajili ya uongozi hapa njaa zake mwenyewe si kwa maslahi ya klabu ya SIMBA kuwa makini wanasimba

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 06, 2010

    Wambura kwani uongozi lazima???? hutakiwi na kila mtu toka apo simba hatukutakiiiiii....kama una mawazo mapya kwa ajili ya simba sjui pango sjui fulana kwani huwezi fungua kesi kushitaki bila ata ya kuwa kiongozi???? Toka bwanaaaaaaa!!!!washitaki kwamba wanapangisha kwa bei rahisi au nini sjui basi!!!umeona wafadhili wamerudi ligi ina hela wachezaji wanaenda trials ulaya unajua kuna pesa unataka kurudi, toka hatukutakiiiiii....

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 06, 2010

    Binafsi simsapoti Wambura lakini nasapoti wazo la kuizuia TFF isiingilie mambo ya ndani ya Clubs hasa kuhusu nani anafaa kua kiongozi na nani hafai, wao wanamambo wanayopaswa kuhusika nayo si kuingilia hadi kanuni za clubs. Hivi wanaweza kuingilia mfumo wa viongozi wa Azam na Afrikan Lions, au Kagera Sugar, Mtibwa, JKT Ruvu? kama haiwezekani kwa nini waingilie ya Simba na Yanga? Mbona hatuoni UK F.A kuingilia mambo ya uongozi wa Arsenal, Chelsea au Manchester Utd? Tujiulize kwanza hapo

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 07, 2010

    naomba wanachama na wapenzi wa simba sports club waelewe ya kwamba Wambura hana haja sana ya madaraka kama baadhi ya wengine wanavyodhani,na Wambura ni mwanachama hai wa Simba alichokifikisha mahakamani ni TFF kuingilia maswala ya simba nakuivunjavunja katiba ya simba leo hii wengi wetu tunaona kuchaguliwa kiongozi na TFF ni sawa ipo siku hao TFF watatuchagulia kiongozi yeyote wamtakao wao kwa maslahi yao sijui mtasemaje.sasa bila kuwa makini tuumia vibaya sana ,wengi wanaoandika maoni yao humu nahakika si wanachama wa Simba kwa maana hawana kadi ya Simba wao ni washabiki tu ndio maana hawaoni ni kitu gani kinachoendelea pale Simba nataka niseme ya kwa kwamba mageuzi duniani hayaji kama mvua ni polepole leo kaanzisha wambura kesho atakuja mwingine suburini tu mimi sioni tatizo hapa bora tufungiwe kuliko kuendeshwa na wachache ushindi wa Simba siyo kama ni uongozi Simba inawachezaji wazuri na wamejituma wanajua sasa wanatafuta nini kwani milango ya kutoka ipo wazi sasa tusidanganyane kuwa uongozi ndio umesababisha ushindi viongozi wote wababaishaji tu ili kuondoa uozo na kujenga vilabu vyetu viwe imara lazima tupate viongozi wenye kujua kama hawa akina wambura na wengine waliojificha waoga kujitokeza naomba wambura apewe sapport kwa jambo hili kuliko kuponda, najua wapo kama Wambura wengi tu lakini nwao wanasemea nje ya uwanja sasa hawa watu hawatusaidii jitokezeni timu yetu tusiwaachie mafisadi waendelee kuuza fulana zetu,kupangisha jengo letu kudhulumu wachezaji n.k

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...