barabara ya ali hassan mwinyi road ikiwa tupu baada ya kufungwa asubuhi kupisha misafara ya wajumbe wa mkutano wa uchumi huko mlimani city jijini dar
hapa ni karibu na barabara ya kawawa road zamani morocco
afande wa kituo cha oysterbay akitoa maelekezo kwa vijana wake
biashara inadodoa asubuhi hii kwa kijana muosha vioo vya magari
ni siku njema kwa wafagizi wa barabara






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2010

    World economic forum is halting Dar economy by disrupting daily traffic. How can we get our daily butter and bread on time! Men, they should have done this conference in Mikumi or somewhere near the jungle!
    Hata wapita kwa mguu wamekuwa haba barabarani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2010

    KUMBE INAWEZEKANA TANZANIA KUWA SAFI SIKU ZOTE. KWELI HII INAONYESHA HAKUNA VIONGOZI TANZANIA NA NI WAZEMBE KTK KUWEZESHA HILI JAMBO.

    ReplyDelete
  3. GodfatherMay 06, 2010

    That's not right!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2010

    Jamani hao wageni wapite na hii barabara inayounga Mlalakuwa na Africana.

    Yaani ni chafu, ni chafu, ni chafu. Haijawahi kufagiwa na mvua hii ndio imejaa matope.

    Thuluthi (moja kwa tatu) ya barabara imefunikwa na udongo na uchafu. YAK!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2010

    Hii si sawa kabisa..yaani unafunga barabara kwa sababu ya hao wageni hii inaonyesha ni jinsi gani viongozi wetu hawathamini raia wao..barabara zenyewe bongo ni za kuhesabu unategemea watu waende vipi kazini kama sio ujinga ni nini..Raisi wetu na yuko anatabasamu sababu adha hii haimkuti yeye wala familia yake...na kuhusu usafi yaani unafanyika wakija wageni tu maana nakumbuka alipokuja BUSH hapo bongo barabara zilipigwa deki..wabongo tuamke ikishindikana tufanye yanayofanyika huko ugiriki hivi sasa...yutakuwa wanyonge mpaka lini?..mungu ibariki tanzania...

    ReplyDelete
  6. Si walisema hakuna barabara kufungwa???????????Huo usafi ungekuwepo kila siku Dar ingependeza sana

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 06, 2010

    Anon May 6, 07:32, sio kwamba Serikali haiwajali raia wao, kufunga hizo barabara ni moja ya maamuzi magumu yaliyofikiwa katika kufanikisha mkutano huu, katika madhumuni ya kuwaletea wananchi hata barabara bora zaidi ya hizo, ikiwa ni moja ya matunda tarajiwa ya mkutano huu. Mwanzo huwa ni mgumu siku zote, ila tutafika tu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2010

    INASIKITISHA KUONA BARABARA BADO ZINASAFISHWA KWA MAFAGIO HADI KARNE HII YA 21,YAANI HUYO JAMAA ALOPOPEWA HIYO DHABUNI YA KUSAFISHA JIJI HAWEZI KUNUNUA HATA 2 TRUCKS ZA KUSAFISHA BARABARA?HUYO MAMA ATAMALIZA LINI KUFAGIA HIYO BARABARA?MAVUMBI YOTE ANAYOKULA,JE ANALIPWA KIASI GANI?MWENYE TENDA MIGUU JUU,KUKU KWA MRIJA NA HAKUNA HURUMA KWA HAO BINADAMU WANAOSOTA KWENYE JUA NA MAVUMBI.JAMANI NUNUENI MAGARI YA KUSAFISHA BARABARA NI AIBU HII

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 07, 2010

    DU Bado Tuko nyuma sana,mmm Aisee hatuko serious yaaani jamaa anafagia barabara na ufagio wa namna hiyo, tetehethe sina mbavu za kujicheka. Mjadala wa hao wakubwa ulitakiwa kujadili kuhusu huyo mfagiaji na namna ya kumkomboa, mengine ni propagandali. Tuache politiks kwani hazina maana, huyo jamaa atavunjika mgongo! Nani atamlipia matibabu yake?

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 07, 2010

    "maamuzi magumu?" my foot.
    unayajua maamuzi magumu wewe?

    kweli dar sio dili...maisha gani ayo sasa?na itawajengea nidhamu ya kuwahi alfajiri kazini saa 11 waenda ofisini...

    poleni

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 07, 2010

    Kaka michuzi habari, Kwanza kabisa nakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya. Nina jambo moja tu lakukushauri au linalonikera jinsi unavyochanganya lugha kwenye maneno kama barabara ya Kawawa road, barabara ya Ali Hassan mwinyi road, sidhani kama ni sawa kuweka neno barabara halafu ukarudia tena kwa kiingereza road. Itakuwa vyema kama ukisema barabara ya Kawawa na si barabara ya kawawa Road.

    Asante

    Paul
    Arusha

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 07, 2010

    We Paul wa Arusha...inaonekana jinsi gani ulivyo mgeni wa Globu yetu, karibu sana. Huku mwaya ndo lugha zetu, ndo style yetu.Ukikuta my wife wangu si kwamba mwandishi hajui la hasha, it's our chosen style na inanoga kinoma ukizoea utaona mwenyewe.Karibu wewe na mai friend zako lol!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...