Michael Richard Wambura akiongea na wanahabari
baada ya mahakama ya Kisutu jijini Dar kusitisha uchaguzi wa Simba
MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI YA KISUTU JIJINI DAR LEO IMESIMAMISHA KWA MUDA UCHAGUZI MKUU WA KLABU YA SIMBA SC ULIOPANGWA KUFANYIKA JUMAPILI HII MEI 9, 2010 KUFUTIA KUKUBALIWA KWA MALALAMIKO YA MLALAMIKAJI MICHAEL WAMBURA KATIKA MADAI YAKE YA KUUSIMAMISHA UCHAGUZI HUO HADI KILE ANACHOKIITA HAKI ITENDEKE BAADA YA KUENGULIWA NA KAMATI YA RUFAA YA TFF KATIKA KINYANG'ANYILO HICHO WAKATI WA MCHUJO.

KATIKA KUOMBA HAKI, WAMBURA ALIITAKA PIA MAHAKAMA IMLINDE ASIJE CHUKULIWA HATUA YOYOTE KWA KUFIKISHA SWALA MAHAKAMANI HADI SHAURI KUU LITAPOAMULIWA. KWA MUJIBU WA KATIBA YA FIFA INAYOFUATWA PIA NA CAF, CECAFA NA TFF, NI MARUFUKU KUPELEKA SWALA LOLOTE MAHAKAMANI. SHAURI KUU LA KESI HII LINATARAJIWA KUSIKILIZWA MEI 31, 2010 NA HAKIMU MH. RITA TARIMO


HAPA CHINI NDIYO HUKUMU YA SWALA LA MICHAEL WAMBURA DHIDI YA MWENYEKITI WA SIMBA ILIYOTOLEWA NA MH. TARIMO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2010

    Ndo maana Mkuchika alisema mtumie kiswahili! Sasa "The applicant is PRAYING this Court..." ; The applicant has also PRAYED the Court... Jamaniii! Uwiiiiii! Na Mheshimiwa akasaini!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2010

    Nani kakuambia Simba ni mnyama wa kufungwa majumbani, Simba yake pori.

    Simba kwisha habari yake, tunasubiri kuwazika tu, Haaaaaaaaaaaaaaaaaaa, ama kweli adui yako mwomboe njaa tena balaaaaaa la njaa.

    Yanga Oyeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2010

    Hivi ninyi simba! kumfukuza huyo wambura mnaona ni kazi kuuuubwaaaa! mumpe red card ya kuwa mwanachama maana tutakosa starehe sasa hivi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2010

    Michael atawasumbua watu wa simba,wasidhani ni dhaifu kiasi hicho,yule mi namjua ni mpambanaji hakubali kuonewa kirahisi,atawatoa jasho.

    Sayz Haji a.k.a.MWAJIRI MKUU

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2010

    Nafikiri walivyoandika 'The applicant is praying this court' wanamaanisha kuwa mwombaji anaiomba mahakama hii..Hapo inaonekana huwa wanaandika kwa kiswahili kwanza kabla ya kuitafsiri kwa kingereza.Mimi nafikiri wangetumia neno 'ask'.'The applicant is asking this court to issue'.

    Bwana Michuzi nisaidie kuwafikishia ujumbe huu kwa wahusika.Neno pray linatumika katika kuomba dua kwa dini zote.Kweli mahakama zianze kutumia Kiswahili kwa kuwa kingereza bado kigumu kwa watendaji wake.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2010

    ..Halafu cha kushangaza hii barua imesainiwa tarehe 6/5/2009 Tehe tehe teh.Hivi hata hakimu amesaini bila ya kusima kilichoandikwa.Inabidi mawakili wa Simba Sports Club watumie udhaifu huu kwa kuwa uchaguzi ulishasimamishwa (mwaka jana te h teh te tehe )kabla hata ya watu kuchukua fomu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2010

    Huo msamiati wa 'pray' hutumika mahakamani kuonyesha kwamba mahakama ina nguvu za kiungu.
    Jamaa aliivuruga TFF, akaivuruga Simba kwa muda mfupi na sasa hivi ataenda kuimalizia kabisa iwe kama Liverpool ya Gillett na Hicks.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2010

    Na kweli bongo lipua lipua. Kidhungu hakipandi tarehe sijui twatumia za dini gani kwasababu wenzetu wako 2010 siye bado tupo 2009..

    bongooooo hiyooooooo

    ndio maana tunaingia mikataba tusiyoijua hata kuangalia tarehe tu ni kazi...

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 07, 2010

    Katika kuomba amri katika mahakama katika nchi za "Commomwealth", sijui katika maeneo mengine, neno linalotumiKa katika kuomba amri ya mahakama ni 'pray' wala si 'ask' neno hilo la pili ni la kuomba vitu vingine kama maji, wala si katika muktadha wa maombi katika mahakama. Naomba muwe mnaomba ushauri kwa wenye fani zao.
    Kuhusu neno 'praying this court, ni kuwa kuna herufi moja ya 'for' inayokaa kati ya 'praying' na na 'this' imesahaulika.

    kuhusu makosa ya miaka, nafikiri hii ni changamoto kwa idara ya Mahakama maana mnakumbuka mwezi wa pili mwaka huu nilipata amri moja ya Mahakama ya Rufani imesainiwa na Kaimu Naibu Msajili ikiwa imekosewa mwaka.

    Nkyabo

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 07, 2010

    Anon May 06, 10:47:00 hiyo siyo barua ila ni Ruling yaani uamuzi. Ni kweli tarehe kakosea. Inaashairia ukosefu wa umakini kwa upande wa Hakimu. Na hii ndiyo typical serikalini nyaraka nyingi hazihaririwi ndiyo maana mikanganyiko. Nakubaliana na wewe kuwa hiyo ruling ni batili. Juzi juzi nilipeleka barua DAWASCO. Walipoipokea wakapiga muhuri wenye tarehe ya mwaka jana. Mnakumbuka hundi aliyopewa JK mwaka jana maanidshi yameandikwa tofauti na figure iliyokuwa imeandikwa? Kazi kweli kweli. Hakuna umakini hata kidogo. Makosa ya spelling kibao, tarehe kukosewa na kadhalika.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 07, 2010

    Kweli kabisa tarehe ni ya mwaka jana. Mambo ya copy and paste hayo.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 07, 2010

    Anony wa 06, 06:35:00 PM, na 06, 10:44:00 PM, Hamjui mnachokosoa nawashukuru hamjaandika majina yenu maana mungejiaibisha sana inaonyesha katika elimu zenu hamjawahi kuhudhuria kozi yeyote ya sheria hata introduction yake, maana msingekurupuka kukosoa kitu msichokifahamu,naamini mgekuwa mmesoma au kupitia hata introduction ya sheria mgejua kitu kinachoitwa "LEGAL LANGUAGE" ndo maana kuna lijitu moja tena naliheshimu sana nililikuta lina ponda usemi huu "TO BRING SOME ONE BEFORE THE COURT" eti lilikuwa linaitafsri kwamba wamemaanisha ni kumpeleka mtu kabla ya mahakama hivyo wamekosea kiingereza, mwee! na hili jitu lina advanced diploma fulani na tunafanya nalo kazi.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 07, 2010

    Jamani watu tusiwe tunakariri kingereza ndug zangu..The aplicant is praying this court..kwa lugha za kisheria ndivyo inavyo takiwa hivyo...Akiwa ana maana mwombaji aliitaka mahakama.....siyo kwamba katafsiri kiswahili...otherwise letter ipo POA....Tambueni lugha inayotumika huko ni ya kisheria zaaidi..

    ManiDash

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 07, 2010

    Wambura ametumia mgawanyiko uliopo baina ya viongozi wa Simba wanaomaliza muda wao kupitisha anachokitaka kirahisi. Aliambatana na mwenyekiti ambaye ndiye mshitakiwa kwenda mahakamani na mwenyekiti alipoulizwa kama ana pingamizi akasema hana! kwa sababu amri ya kutofanya uchaguzi inamfanya mwenyekiti aendelee kuongoza simba kwa muda usiojulikana!! Wanasheria katika hali kama hii mnasemaje maana mimi nilidhani viongozi wanaomaliza muda wao wasingetakiwa kujihusisha na masuala ya klabu katika kuelekea uchaguzi kwa vile wengi wao hawana sifa za kuongoza baada ya katiba mpya. Kama ilivyojidhihirisha hapa, mwenyekiti hana tena interest yoyote na masuala ya simba na kama alivyo wambura wote wapo tayari kuona simba ikifungiwa!!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 07, 2010

    Sina uhakika na lugha ya kimahakama. lakini nafikiri neno sahihi ni demand na inapokuwa nje ya mahakama ni request lakini praying maana yake si kuomba kwa kumuomba mwenyezi Mungu jamani?

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 07, 2010

    ningekua mimi ndo ilo chama,ningeikana ilo tamko/barua ya mwaka 2009!!halafu tuende mahakamani maana haitambuliki this is 2010 for God's sake

    duh muwe mnawapa ma-administrators wapitie kwanza kabla sekretari hajadi-spatch

    upupu huu

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 07, 2010

    hao ndo washashi tipiko tabia zao!
    hawajali kama kuna faida au hasara

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 07, 2010

    Simba oyeeeee! Kama nimesikia kwenye redio leo asb kuwa wamemsimamisha Wambura uanachama?? Simba juu.. juu.. juu zaidi!

    ReplyDelete
  19. ObserverMay 07, 2010

    We anon 06,06:35:00 PM ondoa umbumbumbu wako, we unafikiri kila mtu duniani lazima apitie kozi za sheria ? Si wanasheria na maadvocate mngekufa kwa njaa. Jua kwamba kila mtu ana fani yake na sheria ni moja kati ya fani nyingi sana zinazoexist hapa duniani. Hakuna mwanasheria hata mmoja anayejua sheria zote na ndio maana lazima mfanye reference kwa kusoma vitabu vya sheria kabla ya kutoa judgment.

    ReplyDelete
  20. ObserverMay 07, 2010

    Baada ya game la Manchester United na Bayern Munchen au Munich kama wabongo wengi wanavyoiita, Sir Alex Ferguson alitoa maneno kadhaa but kwa leo nazungumzia kauli hii aliyosema,
    "...THIS IS TYPICAL GERMAN'S..."

    Haya anayoyafanya huyu jamaa Wambura nasema THIS IS TYPICAL TANZANIAN'S.

    Shame on you Wambura, wakati timu kesho inakabiliwa na mchezo mgumu sana Misri wewe badala ya kutoa support kama mdau unahangaika na mahakama, are you truly looking to help Simba as a club or Wambura as a family ? Kwani ni lazima wewe uwe mwenyekiti wa Simba ?

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 07, 2010

    simba ifungiwe ama isifungiwe aijalishi la msingi wambura ametumia haki yake kikatiba. haiwezekani watu wachache kwa faida yao wawe na sauti juu ya wengi na kupanga kila jambo wanalolitaka.
    Eti masuala ya michezo yasiende mahakamani kivipi!! uku mtu akidhurumiwa haki yake na wajanja wachache wasiotaka mtu makini awe kiongozi ili wao waendelee kufaidi jasho la klabu.
    mwaka huu tutajua mbichi na mbivu.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 07, 2010

    huyu wambura hafai kupewa uongozi ata wa kusimamia banda la kuku kwani ana busara ndogo hilo lilionekana wakati akiongoza tff..kuna taarifa za uhakika kuwa anajipanga kugombea udiwani baadae UMEYA wa jiji hilo asahau wenye mji tupo

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 07, 2010

    Wambura unaitikadi za watoto fulani Mysore kwamba wao ndio wanahaki ya kuwa na kila kitu lakini kila chenye mwanzo kiwe na mwisho,angalia mwisho usiwe mbaya.....waachie wenzako madaraka acha uroho..huo ndio udikteta.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 07, 2010

    Duuuh Yahya Hussein kweli kiboko!!!
    Nimeamini ni Gwiji la utabiri, nafikiri aliona uchaguzi huu ndio haukufanyika!Ila hakuna Kiongozi aliyekufa!!Kwa watu wenye maono wanafikiri anatabiri kifo

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 07, 2010

    MIMI NASHANGAA, WAMBURA, KWANI KUONDOLEWA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA UCHAGUZI WEWE UTALALA NJAA NA WANAO? HAPA NDIPO PANADHIRISHA KUWA WATU WANAFUATA KUCHUMA WALA SIYO KUONGOZA KWA DHATI!!!

    WATU WALIKUWA WANASEMA KUWA WAMBURA SIYO MPENZI HALISI WA SIMBA SC BATLI NI HASIDI MCHAFUZI, LEO NAAAMINI KABISA, NA NDIYO MAANA ANAICHAULIA SIMBA KTK HARAKATI ZAKE ZA KUTAKA USHINDI NA KUSONGA MBELE. AMEONA HATUA WALIYORUDIA WAO KTK ROUND YA KWANZA TU KUWA NI CHAFU, KUDHIHIRISHA KUTOWEZA MASHINDANO YA KIMATAIFA. LEO ANAAMUA KUTIA MCHANGA KITUMBUA CHA MWENZAKE.

    MTIMUENI HUYO, SI MWENZENU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...