Asalaam Aleikhum,
Bwana Asifiwe,
Tumsifu Bwana,
Shalom,
Namaste,
konnichiwa,
Nihao,
olá
Shikamooni
Mambo?

KWA heshima na taadhima nawaamkia wadau wote popote mlipo ulimwenguni. Salamu nilizotoa hapo juu naomba ifahamike kuwa hizo nilizozimudu ni kama kielelezo kwamba nia ni kumuamkua kila mmoja kwa nafasi yake popote alipo. Mie sijambo na naendelea vyema na Libeneke kama kawaida.

Waama, baada ya salamu, napenda kuwafahamisha kwamba Globu ya Jamii hivi karibuni itaingia kwenye awamu mpya ya dot com. Hii ni katika jitihada za kuboresha Libeneke liendelee mbele zaidi.

Imechukua muda kuchukua hatua hii kutokana na mazoea kwani toka September 8, 2005 hadi leo si kidogo ati. Hivyo mabadiliko kama yapo inabidi yafanywe kwa uangalifu wa hali ya juu ili kutoleta usumbufu wa aina yoyote kwa wadau wa Globu ya Jamii ambao kwangu ndiyo waajiri wangu wakuu.

Naam, wakati wowote kuanzia sasa libeneke la issamichuzi.blogspot.com litaingia katika awamu ya www.imichuzi.com. unakaribishwa kujaribu na kutoa maoni yako.

Mabadiliko haya tayari yameshafanyiwa kazi na sasa yako katika hatua za nchani. Kilichosalia ni kuhamisha 'mzigo' wote wa miaka takriban mitano toka issamichuzi.blogspot.com na kuutua katika www.imichuzi.com ili libeneke liendelee vile vile kama ilivyo siku zote - ukaicha mabadiliko kiasi ya muonekano.

Ni kweli jina litabaki lile lile la 'MichuziBlog' na 'Globu ya Jamii' lakini si uwongo kwamba hivi sasa itakuwa tovuti kamili ila katika sura ya globu kama siku zote. Hii yote ni katika juhudi za kuongeza ufanisi, tija na vionjo vingi zaidi pamoja na kuondoa kero ya kusaka mitundiko iliyopita. Nadhani sasa itaeleweka kwa nini kulikuwa na kwikwi katika kutafuta posti za zamani.

Mdau usihofu kwamba labda utapata shida kusaka www.imichuzi.com. La, hasha. hautopata shida kwani hata kama utaingia Globu ya Jamii kwa kutumia issamichuzi.blogspot.com ama hata kwa kutumia 'michuzi' pekee utapelekwa moja kwa moja kwenye kurasa mpya bila matatizo. Isitoshe, posti zitabakia kwenye ukurasa wa mwezi husika na kuingia kwenye 'archive' baada ya mwezi huo kwisha.

Hivyo basi, kwa unyenyekevu mkubwa naomba niwashukuru wadau wote popote mlipo kwa kampani yenu wakati wote huu ambayo kwa kweli bila nyie Libeneke lisingefikia hapa lilipo, hususan katika wakati huu wa kulifanya bora zaidi. Na kwa unyenyekevu huo huo naomba tuendelee kushirikiana kwa hali na mali, sera ikiwa ile ile ya "sibagui, sichagui; atayenizika simjui"

Maoni, ushauri na mawazo vinakaribishwa kwa mikono miwili, pasina kusahau kukosoana kwa kujenga na mawazo mbadala ili kieleweke na Libeneke liendelee mbele kwa ufanisi zaidi zaidi na zaidi.

Kwa kuwa nawapenda wadau wote, nitakuwa mtovu wa fadhila endapo kama sintowaonjesha Libeneke litalokuja kwa muonekano mpya. Hivyo basi ni ruksa kubofya http://www.imichuzi.com/ na kuangalia ni nini kinaendelea.

Hapo hapo naomba radhi kwa usumbufu wowote utaotokea kwani kama inavyofahamika si rahisi kwa binadamu kuwa sahihi kwa kila jambo. Hivyo n penye kwikwi na tusameheane na tushtuane haraka iwezekanavyo kupitia anuani ile ile ya issamichuzi@gmail.com ambayo nayo itabadikika mambo yakikaa sawa muda si mrefu ujao itakuwa info@imichuzi.com


Angalizo: Wakati tukielekea huko kwenye http://www.imichuzi.com/ libeneke hapa litaendelea kama kawaida na hakutakuwa na mabadiliko yoyote hadi siku utapokuta unapelekwe huko. Na hii itafanyika wakati wowote kuanzia sasa.
Na wale Wadau 100 walioshinda katika ule mtanange wa mdau wa milioni 8 na mnaotakiwa kupata ze fulanazzz za Blobu ya Jamii kaeni mkao wa kula, maana zilisitishwa kusubiri anwani mpya. Wala Msikonde email zenu zote zipo kibindoni na nyote mtafurahi. Fanyeni subira kidogo na samahani kwa kuchelewa kwa hilo
Shukrani za pekee zifike kwa
wanaowezesha yote haya na memngine mengi tu.
Asante sana MK
Wenu mtumishi mtiifu,
Muhidin Issa Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. MstaarabuMay 18, 2010

    Ankal Hongera sana. Ila kabla hujahama kwenda dot com tunaomba ripoti ya ugawaji wa zile fulana ulizoahidi kwa wadau wa Milioni nane kwa maana wengine tunahisi kama umetudhulumu vile. Hatujaona fulana ilihali tulistahili, tukiulizia hatujibiwi yaani mashaka matupu. Nawasilisha.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2010

    Mdau umesahau ya huku kwetu "shimoni na mchichaa"

    Big UP!! good step ahead!! wadau tupo kama kawa.hope tutazid kupata mabrek newzz na udaku zaidi zaidi..

    Congrats !!!

    Mdau Dziim

    ReplyDelete
  3. hongera kaka kwa hatua nyingine katika libeneke mungu akujalie mafanikio mema

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2010

    MICHUZI TUNAKUTAKIA HERI NA FANAKA KATIKA KUHAMISHA BLOGU YAKO KUWA DOT COM. ILA TUNA WASIWASI KWA KUWA KAMA MIAKA MIWILI AU MITATU ILIYOPITA ULIJARIBU KUFANYA KITU KAMA HICHO MATOKEO YAKE IKAWA KWIKWI KILA WAKATI NA WAKATI MWINGINE IKAWA HAIPATIKANI KABISA. HIVYO BASI TUNAOMBA SANA JARIBU KUZIENDESHA ZOTE SAMBAMBA KWA MUDA MREFU KIDOGO KABLA YA KUHAMISHA KABISA. HII BLOGU NI KAMA YA TAIFA KWA SASA KWANI WATU TUKISHAIKA COMPUTER TUU KITU CHA KWANZA KWENYE BLOGU YA JAMII. TUNAOMBA SANA USITUANGUSHE MZEE KWANI MAISHA YATAKUWA MAGUMU KAMA KWIKWI ZITAANZA KAMA WAKATI ULE.
    NAKUTAKIA MAFANIKIO MEMA.

    MZOZAJI.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 18, 2010

    Ankal,
    Natumai hiyo imichuzi.com itakuwa customer friendly, maana Globalpublisherstz dot com walivyoenda Globlpublisherstz dot info, webusaiti imekuwa 'clutter' (makororo kibao) hata hainogi kama blogu.
    Mdau1

    ReplyDelete
  6. Imetulia, lakini nadhani ingependeza zaidi kama ingekuwa imichuzi.co.tz ili iwe ya kitanzania zaidi! Uzalendo mbele!

    ReplyDelete
  7. Mdau, BloomsburyMay 18, 2010

    Michuzi,

    Wazo zuri. Ila lingekuwa zuri zaidi kama ungetumia domain inayoashiria Tanzania, yaani www.imichuzi.co.tz.

    Nawasilisha. Tuitangaze Tanzania yetu, ingawa kuna mijamaa inatuharibia

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 18, 2010

    Kila la heri mimi ningependekeza jina liwe Issamuchuziblog dot com

    Ila huko unakohamia usije ukaincooperate na kuanza kuissue public stocks...LOL... Wenzako wasomaji wako wala hatutaki mizwenge we are easy goer tu...Wengine hata kusoma email tunatumia wajukuu zetu watusomee...sasa ukiengeza michakato utatupoteza

    Wishing you luck....
    Abuela

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 18, 2010

    Kama mawaziri wetu wangetambua kwamba na wao ni watumishi wetu tena wanatakiwa kuwa wanyenyekevu kwetu kama alivyo ankal wasingethubutu kutukejeli eti hata tukila majani wao dege watalinunua tu!!

    Ankal usibanie hii, sisi wengine hatufungamani na upande wowote.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 18, 2010

    Ankal who cares .com, .org. .net who cares!!!!!! what we are caring ni michizu blog na habari kwa picha kila saa! That is it!
    Ukituambia unafunga blog hapo ndo tutalia na kusaga meno. Lakini kama tutaendelea kupata habari kwa picha na zinapostiwa kila baada ya dakika 10 ndani ya masaa 24 siku 7 za wiki na siku 365 na nusu katika mwaka! Libeneke hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 18, 2010

    hongera mjomba kwa dot com .
    mimi nimekuja na marekebisho kidogo juu ya muonekano wake.
    kwanza ukiangalia kwa makini utaona melezo ya post comment yamebebana fulani,kuna white and blac bolded.. jaribu kuliangalia hli kwa makini.
    pili, utumiaji wa javascript uwe wa kiwango cha chini sana, kwani kinafanya website kufunguka kwa taratibu.
    ama mwisho kabisa jitahidi ku-separate video na habari za kawaida..kwa sababu video pia zina peleka bandwidth chini na kufanya website kufunuka taratibu sana.

    ni hayo tu mkuu !

    Mdau No 5 .

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 18, 2010

    Safi sana sasa ulinzi wa google wote umeisha, itakuwa rahisi kuku hack, sasa kazi kwako.
    Tutakumomesha mshamba wewe.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 18, 2010

    HONGERA SANA. ILA KWANINI SIO .CO.TZ? PROUDLY TANZANIAN???

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 18, 2010

    Hongera kwa kazi kubwa ya kuelimisha jamii,

    Kaka michuzi kwa wakristu salam inatakiwa kuwa Bwana YESU asifiwe na sio Bwana asifiwe kwani mtu yeyote anaweza kuwa bwana pia Tumsifu bwana sio hivyo ni TUMSIFU YESU KRISTU. ili salam kukamilika lazima YESU awepo.

    tunashukuru kwa kazi nzuri ya kusaidia jamii kwa mawasiliano na taarifaa mbalimbali.

    ReplyDelete
  15. Marahaba kijana,hongera sana. Huko ndio 'kukimbia' na dunia. Ni lazima walau kujaribu. Kila la heri.

    ReplyDelete
  16. Mdau K.VMay 18, 2010

    Michuzi kila siku unasema unahamia .com ila hiyo site hauiupdate kama unavyoupdate hii blog yako, bora weka tangazo hapa na link ili watu wahamie huko... hiyo site ni nzuri na rahisi zaidi kwa wadau kufuatilia post za zamani....
    Hongera sana.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 18, 2010

    Ankal,
    Tunashukuru kwa mabadiliko hayo, ni hatua nzuri sana. Mie najazia mapendekezo km wenzangu hapo juu.
    1. Tumia domain ya .co.tz, au .or.tz
    2. Ningependa iwe 'issamichuzi.co.tz au issamichuzi.or.tz


    NB: Ombi langu la kuomba kukutana nawe lipo palepale

    Ni hayo tu
    Mdau Mtiifu wa Mwenge.

    ReplyDelete
  18. MDAU KV

    ASANTE KWA MAONI YAKO. KAMA NILIVYOBAINISHA HAPO JUU NI KWAMBA HIYO YA imichuzi.com IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO KUPOKEA POSTI ZOTE ZA SASA NA ZA NYUMA, HIVYO BADO KAZI HIYO HAIJAKAMILIKA. IKIKAMILIKA UPDATES ZOTE ZITAENDA HUKO. HIVYO USIWE NA WASI FANYA SUBIRA KIDOGO KWANI MZIGO KUUHAMISHA WA MIAKA TAKRIBAN MITANO SI KODOGO. INACHUKUA MUDA.

    ReplyDelete
  19. US BLOGGERSMay 18, 2010

    BREAKING NEWS....KAKA MICHUZI NIMEPOKEA KWA FURAHA NONO THIS MORNING KWAMBA THE YOUNGEST EVER BILLIONAIRE OF EAST AND CENTRAL AFRICA MUHASHAMU HASHEEM THABEET HAS SUCCESSFULLY BOUGHT KIMPENSKI HOTEL MAJORITY SHARES THE DAY BREAK NEWS HAS MADE ME FEEL SO PROUD OF THIS SON OF AFRICA IF ALL PEOPLE ESPECIALLY THOSE FEWEST BILLIONIRES AVAILABLE IN THE CONTINENT COULD FOLLOW HIS HEART THEN AFRICA COULD HAVE REACHED ITS PEAK, AGAIN MR. THABEET I SALUTE YOU WITH ALL MY HEART BROTHER, IF IT IS POSSIBLE PLEASE BUY NEW AFRICA TOO, YOU HAVE ENOUGH MONEY TO BUY ANYTHING IN DAR ES SALAAM, TENA NINGEFURAHI SANA KAMA UNGEAJIRI WAZUNGU WATUPU TENA WENGI ILI KAZI IFANYIKE VIZURI SISI NGOZI NYEUSI WAZEMBE SANA, ALSO DON`T FORGET MISS USA MALIDADI SANA ANAFAA SANA KUWA MWALI KAKA HASHEEM JITOSE TARATIBU TU HANA MTU SASA HIVI NI USHAURI TU HUO.

    ReplyDelete
  20. Hongera sana Ankal,

    Nilikuwa naona ungetumia www.issamichuzi.co.tz kwa sababu tushazoea jina hilo hata kabla ya dot com pia kuwa proud na .tz yetu.

    Ni hayo tu.

    Mdau Voda

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 18, 2010

    Congrats x millions.Carry on thats the way to go slow but sure. SAFI SANA.

    ReplyDelete
  22. Hongera Ankal!!

    Hayo ni maendeleo mema!

    Mungu akubariki!

    Mdau wa www.uksokainbongo.blogspot.com
    [www.sokainbongo.com]

    Storming

    ReplyDelete
  23. Hongera sana kaka michuzi.ila kama ukipata wakati ingekua vema ukaweka imichuzi.co.tz kama kaka samweli alivo sema hapo juu.ni lazima tujivunie nchi yetu bwana,

    mdau toka
    Washngton stat
    Usa

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 18, 2010

    Us Blogger hizo ni habari njema lakini mbona kama hazina ukweli umezitoa wapi uncle, Michuzi tupe fununu kama hizo ni habari njema na za kweli?

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 18, 2010

    Mabrook
    Congrats
    Safi hiyo .com na ingawa binafsi napendelea ile kongwe, inshallah hali hii mpya tutaizoea.
    Naona umeondoa word verification, that will allow smart computers adding comments,wasema email address hutaitangaza, jee jina
    Kwa ufupi good job and congratulations BUT
    Tahadhari maji yasizidi unga
    (I learnt that in Mpanda)
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 18, 2010

    Ankal, hii ni hatua moja muhimu sana kuelekea mafanikio ya kweli. Mola aendelee kukuangazia njia.

    Hongera!!

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 18, 2010

    ANKAL HONGERA SANA KWA KUFIKA HATUA HII KUBWA MIMI NATAKA KUMUELEWESHA MDAU HAPO JUU MTU PAKA ANAPO AMUA KUCHAGUA DOMAIN YA .NET .CO.TZ AMA .INFO NI KWAMBA .COM INAKUA HAIPO SASA ANKALI KABAHATIKA KUPATA HII.COM MIMI NAKUPA BIG UP SAANA ANKAL.NA NAHISI TAYARI IMELIPIWA HII .COM,MAANA NIMETEST NIMEONA IKO HEWAN HONGERA ANKALI

    TUKO PAMOJA KILA KONA NA KILA WAKATI

    LIBENEKE HOYEEEEEEEE
    ANKALI JUUUUUUUUUUUU
    WANA LIBENEKE TUNANGOJA TUU APA ZE FULANAZ

    MDAU
    BABUU

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 18, 2010

    Asalaam alaykhum Ankal,

    Hongera sana komaa sisi wote tunaiga mfano wa hatua zako wewe ulietutangulia. Nakutakia kheri na mafanikio libeneke liendelee kusonga kwa kasi ilele.

    Chef Issa

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 18, 2010

    ANKAL NASHUKURU. MAAANA MM KRO YANGU ILIKUWA NI KUPATA POST ZA ZAMANI.
    huyu Us Blogger ni kichaa. tuko kwenye topic ya maana anatuletea habari za hashim sijui bilionea .... acha ushamba bwana mdogo.

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 18, 2010

    Naungana na wale wote waliosema dot co dot tz. Dhamini nchi yako na jenga nchi yako, rudisha uchumi Tanzania.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 18, 2010

    Anonymous wa May 18, 07:27 (Mdau No. 5, kama unavyojiita mwenyewe).

    You remind me of a Guy, that I once knew! Na huo sio wimbo tafadhali! Ni ukweli ukweli.

    That guy (Mtu wa zenji nadhani) yupo mwake sana na masuala ya computer, nadhani alisomea Computer Science ama kitu kama hicho pale Chuo (kwa maana ya mlimani - UDSM). Mara ya kwanza na ya mwisho tulipoonana ulikuwa umejikalia zako tuli nje ya lecture room (kule karibia na Chemistry Laboratory), nami nilikuwa nashuka ngazi kuja lecture room (Nimejivalia ki-peddle cheusi na kishati chekundu ndani kuna kitop cha draft, na kikuku mguuni). TUKAANGALIANAAA weee. Then mwalimu hakuja, nikatoka nje na kuanza kupandisha ngazi huku nahema. Ukaniangaliaaa weee. Nadhani umeshajifahamu enh? Tuwasiliane basi.

    Aisee, Ankal Michuzi, fata ushauri wa huyo mtaalam, maana ni specialist haswa. Pia Ankal usilazie damu kideti cha Mwenge!

    ReplyDelete
  32. Dingi NokoMay 18, 2010

    Muono wangu:-
    1) Hongera sana Ankal unapaswa kupata pongezi.
    2)Kwa sisi watu wa IT kubadili kutoka .com mpk .co.tz ni issue ndogo sana so wasikilize wadau ili uzalendo uwe mbele hata mtu akiingia aone TNZ imetajwa, na km alikuwa haijui .co.tz ndo chanzo cha kuijua tnz.
    3)lakini si mwisho kwa umuhimu ZE FULANAZZ BADILI, yani uje na ZE FULANAZ ingine kidot dot(yani .co.tz). Kumbuka tunaachana na Kiblog so mambo mapya ss.

    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 18, 2010

    mi naona umeamua kutupotezea tusipate habari tena.
    hakuna mtu asiyependa maendeleo ni hatua nzuri kwa kweli ila unataka utuache hewani. akina dot com wako angapi na mizinguo tu ukienda habari unazokuta ni za maka juzi. mie naona kama we unaenda dot com, basi hii blog waachie wenye moyo kama wako wakujitolea ili watusaidie kwa habari namaanisha hii blog iendelee kuwepo. pia nafikiri kama unafuatilia habari za websites na blog za kiamataifa utagundua nazungumzia kitu gani. blog hii ina hadhi yake tena kubwa sana ila.
    tupotezee kama vipi.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 19, 2010

    Ankal hii ni ya yakimataifa zaidi so ibaki .com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...