

siku chache baada ya kufunga ndoa huko Hamburg, Ujerumani, mwaka 1995
Da' Sherry ambaye alikuwa anatafutwa na mama yake mzazi baada ya kukosa kumsikia kwa takriba miaka sita, amepatikana, familia na aliyekuwa mume wake wamesema leo.
Akiongea na Globu ya Jamii kwa njia ya simu huku sauti yake ikiashiria anabubujikwa na machozi ya furaha, mama mzazi wa dada yetu huyu Bi. Fatuma Saidi Kajemba, amesema muda mchache uliopita kwamba amepokea simu toka kwa aliyekuwa aliyekuwa mume wa bintiye, Bw. OIiver Hammerling kwamba Da' Sherry yu buheri wa afya na anaishi Ujerumani.
Mama huyu amesema sio simu tu bali Bw. Oliver Hammerling ametuma hata namba ya simu ya Da' Sherry na amewataka wawasiliane naye. Yeye mwenyewe anasema aliongea na Da' Sherry jana jioni baada ya kuona habari hizi kwenye Globu ya Jamii na kuchukua hatua ya kuwasiliana na mkwewe mara moja ili kuondoa kiwingu cha wasiwasi kilichotanda kwa 'kupotea' kwa Da' Sherry.
Bi. Fatma Saidi Kajembe ametoa shukrani za dhati kwa wadau wote walioguswa na jambo hili kiasi cha kuanza kulihangaikia usiku na mchana, ikiwa ni pamoja na kumpigia simu kibao za kumtuliza na kumsaka Da' Sherry mitandaoni na mitaani. Mama anasema ameguswa sana na moyo wa usamaria mwema walioonesha Watanzania walioko sehemu mbali mbali kwa kumhangaikia na kumfariji. Anawaombea kwa Mola awazidishie baraka na Inshaallah atamuona tena Da' Sherry ambaye kukatika kwa mawasiliano naye kulikuwa kunamsononesha sana.
Globu ya Jamii imefarijika sana kwa jinsi jambo hili hatimaye limefikia tamati na inatoa pongezi na shukrani nyingi kwa wadau mlivyoonesha ushirikiano wa hali ya juu katika hili kwa namna moja ama ingine. Haya ndiyo mambo uyanayotakiwa katika kusaidiana pale penye raha na shida.
Asanteni sana wadau kwa moyo huo na tuendelee kusaidiana Watanzania ambao kwa jinsi maoni yalivyo mengi katika posti ya habari hii inaonesha wazi kwamba tunapendana sana Watanzania. Na hili liendelee katika shida zetu zote pamoja na raha. Shukrani za kipekee zimwendee pia shemeji yetu Bw. Oliver Hammerling kwa kuwasiliana na Mama Sherry na kumpoza.
Macho na masikio pamoja na juhudi sasa zielekee kule Los Angeles Marekani ambako nako tumepotelewa na dada yetu mwingine Da' Caroline Mmary
(Bofya hapa) ambaye hajaonekana nyumbani kwa muda.
Kwa habari ya awali ya Da' Sherry
BOFYA HAPA
Naona hii Blog inafanya kazi za Mabalozi.
ReplyDeleteWanablog pamoja na P.D.G wetu mkuu wa wilaya ya nanihii, tupo juu!
Kila la Kheri Mama Sherry na mwanao Sherry, pamoja na familia yenu yote kwa ujumla. Dada Sherry, usikae kimya sana kiasi hicho ndugu yangu.
Nimefurahi sana.
Nafikiri hii ni nusu ya habari njema, kwani badoo mama mzazi hajazungumza na mwanawe.
ReplyDeleteTunawapongeza wale wote waliojitahidi kumtafuta kwa njia mbali mbali mbali.
Ni vizuri zaidi kama ingelijulikana sababu za kukata mawasiliano na mama yake kwa muda wote huo.
Labda hiyo number wangelipewa wasamaria walio ujerumani wakajaribu kuwasiliana nae na kujua matatizo alio nayo na kama anahitaji msaada wowote.
Good news indeed!!!! lakini ni kwa nini huyu dada baada ya kujulishwa na ex-husband wake kama anatafutwa bado hajawasiliana na mama yake? au yuko jela? sorry i know it may personal lakini mwanzoni ilikuwa inasikitisha lakini kwa taarifa ya leo sasa inashangaza.
ReplyDelete...Naam...!!!! Nguvu ya Mtandao!
ReplyDeleteHii blogu inasomwa sana na watu wenye kujali sana jamii!! Hongera uncle kwa blogu hii kufanikisha jambo hili!!!!
ReplyDeleteI say! tunashukuru sana kwa habari hii, maana nasi tulikuwa tunaumiza vichwa labda hivi labda vile kumbe mtu anakula bata raha mustarehe lakini mimi naona kama bado kazi haijakamilika mpaka Sherry mwenyewe aongee na mama na mama kuhakikisha kweli aliyeongea naye ni bintiye, sababu maelezo yanasema shemeji kaongea naye mwenyewe Sherry hivi kwanini ushaambiwa kama mama yako anakutafuta miaka sita mpaka leo kaamua kukutoa mitandaoni bado tu kunyanyua simu kumpigia unasita? mpaka shemeji ndo anapiga yeye kujisafisha maana yeye ndo alikuwa anaonekana mtu wa karibu kuulizwa!
ReplyDeletePopote ulipo sasa hivi nyanyua simu uongee na mama yako bifu gani hilo lisiloishaa? sasa hivi akiaga atakuwa na furaha ya kujua kama uhai lakini atakwenda na kinyongo chako , dunia hii utaishi vipi?!
nimefurahi kwa kweli , asante sana michuzi wewe pia ndo mdau mkubwa kufanikishwa kwa jambo hili , mimi simjui da sherry lakini nimefurahi kama nimezaliwa nae tumbo moja , ila sasa utakoma wadau watakutumia watu waliopotea kibao.....
ReplyDeleteWote tumshukru Mungu.'' Tunakushukru Ee Mungu kwa kusikia kilio cha watanzania na cha mama mzazi wa dada yetu Sherry,wabariki wote walioweka nguvu zao katika kufanikisha zoezi hili,mbariki pia ndg yetu oliver kwa kujitokeza na kumaliza utata huu.Mungu mkumbushe sherry na oliver wasikae kimya tena,maana wameona usumbufu uliojitokeza,watanzania wengi wameweka muda wao katika jambo hili ,wakaweka kando kwa muda shughuri za ujenzi wataifa wengi wakaungana kama ndugu katika hili,hili litoshe kwa kuwafundisha.Ameeni"
ReplyDeleteIla kweli sisi wanadamu tunatofautiana sana, hivi mtu utakaaje miaka mitano hujawasiliana na mama yako mzazi jamani?? laana nyingine tunajitafutia wenyewe, mama anasononeka usiku na mchana kukuwaza mwanae, mpaka atangaze huku, kwa kweli inasikitisha, me nikimaliza siku 3 sijatuma hata msg kwa mama yangu silali vizuri. kuwa ulaya haimaanishi usahau wa kwenu, kwa wote wenye tabia kama hii mbadilike, wazazi ndo baraka za dunia na mzazi ni mzazi tu hata awe chizi.
ReplyDeleteDuh! Ex-Shemeji (Hammerling ?) aliopoa si kipole pole! Ama kweli 'Love' is Blind.
ReplyDeleteChinua Achebe kwenye kitabu cha 'No longer at Ease'.Alishawahi kuandika hivi "ukimwona kuku mwenye vifaranga anatembea tembea vichakani,na huko vichakani kuna mbeha,mfukuze kwanza mbweha,kisha mtoe kuku vichakani na muonye asirudi tena vichani".Nashukuru dada yetu kapatikana,nafikiri ni wakati mwafaka wa kumwita na kumkarisha chini,tumwonye asikae kimya tena kwa kipindi kirefu namna hiyo,maana atawaua wazazi wake kwa mawazo.Kama ni mbweha tumemfukuza mnaonaje tukikaa na kuku ili tumfunde?Au mnasemaje wadau?.Hili ndilo Neno la leo Mtoa nimenena.
ReplyDeletesasa huyo da'sherly yeye anaona ufahari kuwa hawasiliani na familia yake hadi anampa mama yake mzazi kazi ya kumtafuta?miaka 6 si haba,ana akili kweli au ana matatizo?kama ni buheri wa afya,namwambia asisahau home,home sweet home.unawapa watu presha wakati upo na unafanya shughuli zako vizur.usisahau wazazi hata siku moja hutafanikiwa.by the way nakutakia maisha mema.
ReplyDeleteDuh! Hongera mama Kajembe kwa kumpata mwanao. Hata hivyo...
ReplyDeleteHili liwe fundisho kwa watanzania ambao wakienda nje ya nchi wanaona hakuna haja ya kuwasiliana na familia tena.
WaTz mliopo nje kumbukeni kuna associations huko jiandikishe at least in one or two-hujui zitakufaa lini haa kama hauko active.
Mambo ya kujiweka facebook ni nusu ya kuonana-jitahidini mnetwork.
Tatizo:Watu walioondoka Tanzania enzi hizo za zamani bado akili zao zinawapa picha za Tanzania ile ya zamani. Hawajui kuwa Tanzania imebadilika sana. Watu wanaishi maisha mazuri wakiamua-tena it can be beter than majuu.
Kingine, hata kama kwenu kuna matatizo yalioje. Hii siyo sababu ya kutokurudi au kutokuwasiliana na wanandugu. Eti ukae hata miezi mingapi ndo usipige. Inatia aibu kwa sababu simu ulaya kupiga Africa ni very cheap!
Na msiposaidia kwenu who the hell are you working for out there? Mhmm. nawashangaa niko nje lakini kila siku i'm in touch and I feel good.
S
dah nimefurahi sana kusikia kwamba da shery hatimaye kapatika nilikuwa namwionea huruma sana mama yake kama mzaazi MICHUZI HOYEEEEEEEEEE WADAU OYEEEEEEEE HONGERENI KWA JUHUDI ZA HALI YA JUU NA USHIRIKIANO WA HALI YA JUU MLIOONYESHA.
ReplyDeletePole Da Sherry na matatizo ya mazingara ya ulimwengu,vipi hata simu ya mkononi kwa kutuma sms uliipoteza? shukrani kwa wanavyombo vya habari kwa kazi kubwa walioifanya kutuliza roho ya mama mzazi,nafikiri pia amewashukuru wana vyombo vya habari wote.
ReplyDeleteMickey Jones
Mpaka kumsahau mama mzazi! Ama kweli watu wana laana!!
ReplyDeleteHongera mama sherry kupata khabari za mwanao. Ndugu wa Ujerumani, anzisheni umoja wa watanzania waishio huko, na katika mambo muhimu ni kujuana na wenzenu na kudumisha Tamaduni zetu mfano kusheshimu, kuwajali na kuwasaidia ndugu na jamaa huko nyumbani hususan wazazi! Inasikitisha mtoto kutowasiliana na mzazi wake kwa miaka zaidi ya sita (ukiwa bukheri wa Afya) katika ulimwengu huu wa sasa, ambapo mawasiliano yamekuwa rahisi sana. Unaweza kumtoa uhai mama yako bure!
ReplyDeletedu tunashukuru kapatikana hata mimi nimefurahi sana yaani katika kumtafuta hadi nikawa namtilia shaka mwimbaji wa kongo jenerali def defao kuna kipindi nyimbo zake alikuwa nakibwagizo anaiba sherry i love...............nikazana asije kuwa alimtorosha.
ReplyDeleteBwana Michu, mimi hii habari haikai sawa masikioni wala akilini mwangu. Hasa ukizingatia mambo ninayoyaona na kuyasikia huku mtoni kuhusu visa ndani ya ndoa hasa kwa wenzetu wazungu hawa. Sipendi nieleweke vibaya, lakini watu hupotezwa huku wakasingiziwa wameondoka kwenda nje ya nchi au wamekimbia lakini kumbe walishatolewa uhai, hasa ukizingatia kuwa familia zao zipo dunia ya tatu na hakuna mtu wa kuwaulizia polisi za huku.
ReplyDeleteNaomba mnisamehe kwa kusema hivyo, lakini ndiyo hali halisi.
Unajua bwana, dada zetu wa kitanzania kwa asili yao tu hupenda sana kuhudumia wazazi wao, na hufanya juu chini wahakikishe kuwa wanawatunza na kuwajulia hali kila mara. Mimi mke wangu huongea na nyumbani kwao na kwetu kwa simu kila siku iendayo kwa mungu, pengine mara mbili hadi tatu kwa siku. Yaani hawezi kulala bila kujua huko bongo watu wameamkaje au kulalaje. Na madada wengi tu hizo ndiyo zao. Haiwezekani kwa mtu ambaye amekuwa ni wa mawasiliano kuamua tu kukata kuwasiliana na watu wa huku mtoni na wale ndugu zake huko hasa mama mzazi au hata ndugu wengine wa karibu.
Kinachonitia wasiwasi zaidi ni kuwa baada ya taarifa kutoka katika mtandao wako na watu wakaanza kuulizia juu ya habari za huyu mtu. Huyo Ex-Husband ndo awe wa kwanza kupiga simu na kuwahakikishia kuwa huyo ndugu yetu yupo hai na salama. Hii ni kuwanyamazisha tu. Then, baadaye mtu awasiliane na familia kwa simu kudai kuwa ndiye huyo dada.
Wandugu, hii haijakaa sawa. Mimi mpaka huyo dada aonekane kwa wenzetu wanoishi Ujerumani live ndo nitaamini kuwa yupo hai na salama.
Kwa nini huyu dada kama kweli hizi taarifa zimemfikia asiwatafute viongozi wa chama cha watanzania wanaoishi huko akaenda kuwaona uso kwa uso na pangine tukapata picha yake na hao viongozi humu kwa Michuzi?
Ninachokisema mnaweza kuona ni ujinga, lakini ndugu zangu, watu wengi sana wamedhurika hasa ndoa zinapovunjika na hadi leo hatujui waliko huku nje.
Tuendelee kumtafuta huyu mtu, wala tusiridhishwe na stori za huyo ex-husband. Hasa Mjerumani
michuzi oyeeeeeeeeeeeeeeeeeee. asante sana
ReplyDeleteMambo mengine ni kama tamthilia vile. Yaani utakaaje bila wasiwasi kwa miaka 5 bila ya kuwasiliana na wazazi? Siamini. Niko ughaibuni kila juma naongea na wazazi.
ReplyDeletewa kumalaumu sana huyu dada mtu gani huwa anakaa bila taarifa zozote kwa familia yake kwa miaka 5 hata kama mume ni mkorofi bado mtu huwa unatafuta njia ya kuongea na ndugu manake dada sherry kumbuka kitu kimoja katika maisha:
ReplyDelete"BARAKA ZOTE ZINAKUJA TOKA KWA WAZAZI"
hii tabia si nzuri kabisa tena iache lazima ufanye familia yako iwe ya kwanza. Manake unatutia wote presha kumbe umetulia huko. Ulaya huku watu wanauwawa kila leo mtu unaingiliwa na kila aina ya mawazo kumbe uko tu.
Sherry hivyo "SIVYO" na ungekuwa karibu ningeweza kukuchapa vibao mstzzzzzzz inamaana hata nyumbani huyu hatumi msaada. Tusidanganyane mamake anaonyesha si milionea, mi kaniudhi huyu dada, tabia hii ni chafu. unaambiwa kabisa baada ya mungu ni wazazi.... wazazi wako ndio mungu wa pili. Hata kama ndio umekuwa mzungu tena sio hivyo.
tumwache huyu tumshugulikie yule dada caroline mmari, huyu sherri hana mpango.
ReplyDeleteTuungane jamani kumtafuta mtu mwenye data zinazoeleweka
yaani katusumbua wote hata huo usingizi usiku ulikuwa unapatikana vipi kwa miaka 5? eeeh sherry tueleze? Miaka tano??? oooh please
ReplyDeleteKama ulaya kuna mbagala,basi shemeji yetu oliver alitoka mbagala ya uingereza.Maana huo mtoko wake du! hapo sherry ndo anaonekana katoka majuu.
ReplyDeleteGod is good. Jamani I do not want to judge but I struggle to understand how can you not communicate with your mother for all those years, even with the letter. It is real painful.
ReplyDeleteMheshimiwa Balozi Michuzi,
ReplyDeleteNimefurahi sana kuona mama ameweza kupata mawasiliano upya ya mwanae.
Nawapongeza wadau wote walihakikisha wanatafuita info na kuwasiliana na wahusika. Haya ndio maisha tunayotakiwa kuishi ambayo dini zote zinafundisha. Ni kusaidiana bila ya kuwa na maslahi nyuma yake. Ni kuhakikisha unamuwezesha mwenzako awe furahani, kumuondolea unyonge nk.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya na Balozi Michuzi, nakupongeza sana kwa moyo wako wote na kuliendeleza libeneke ipasavyo. Hii unasaidia pia kuondoa ile dhana potofu kuwa BLOGS ni upuuzi, uhuni nk.
MAKULILO, Jr.
www.makulilo.blogspot.com
www.scholarshipnetwork.ning.com
San Diego, CA
A HAPPY ENDING!
ReplyDeletesister huyu kweli amedata!!!yaani hata salamu kwa familia inakwishinda...?kweli hawa wazungu wengine wanatuharibia madada zetu.wakishafika ughaibuni wanasahau kila kitu.ssa sister funga safari ukaone familia usije ukakosa radhi za familia.
ReplyDeleteAlhamdulilah.
ReplyDeleteBwana asifiwe.
(US Blogger)
Pole mama,
ReplyDeleteIla huyo dada naye kwa nn akae muda wote huo bila kuwasliana nyumani??
Tutaua wazazi wetu jamani!!
Dada mpuuzi sana na mzembe kwa kusababisha hofu miongoni mwa familia yake na watu wengine.Sioni sababu ya msingi ya kutowasiliana na familia yako nyumbani kwa miaka kitano,na kuwatia watu hofu,hi nina uhakika katika nchi nyingine ingebidi upewe adhabu au kuomba msamaha kwa usumbufu.IDIOT !!!!!1
ReplyDeletemdau Mikocheni
WE DA SHERRY UNALEWA KUKU KWA MRIJA HADI UNAMSAHAU MAMIYO?
ReplyDeleteVIBAYA HIVYO MWAKWETU
Hongera Bwana Michuzi na Watanzania wote waliofanikisha kwa njia moja au nyingine kupatikana kwa dada yetu Sherry.. Najivunia kuwa Mtanzania na hili blogu liko juu ni matumaini yangu kuwa familia yake imefajirika kwa taarifa hizi nzuri.
ReplyDeleteMdau Ughaibuni
Salaam,
ReplyDeleteWa kushukuriwa ni Mola wa viumbe wote, aso mfano na kiumbe chochote.Alhamdullilah.
Wadau tufurahi kwa dada yetu kupatikana ila tusihoji kwa nini alipotea kwa masiku hayo.Hayo ni yeye na familia yake.Tunamshukuru mno kaka Michuzi kwa ushujaa wake Moyo wake kwa kuwasaidia familia hiyo ya Da Sherry.Tuwaombee wawe na mwisho mwema.Tunamuomba Mungu ampe mwongozo na Hidaya dada yetu na familia yake, Tnamuomba Mungu amnusuru na mabalaa yote na amuongoze kwa Nuru ya kweli na kudumisha umoja wa familia yake hususan wazazi wake na nduguze
Ewe Mola wabarike wote wliosumbuka kumtafuta dada Sherry na wale wote waliosadia kufanya Ibada na visomo maalum kusaidia kupatikana kwa dada Sherry.Mola wetu mpe Nguvu Kuu Al-Akh Issa Michuzi na wadau wote wa Blogu ya jamii
Amin Amin
Ustadh Khamis Hassan Batanyaga
Nakubaliana na wanaoshtukia habari hii.
ReplyDeleteMaana kweli lazima kuwe na jambo inakuwaje usiweze kuwasiliana na nyumbani kwenu wala rafiki zako muda wote huo kama kila kitu ni shwari?
Au ndo yale mambo ya reality show?
Kuna kitu hakijakaa sawa hapa!!
Nashukuru, kusikia hivyo na huu ni mwanzo mzuri wa kujiunga tena na familia dada Shery. nami naomba nichomekee maana yangu bado haijatolewa hadi leo kwa blog japo nimetuma, namtafuta dada yangu tulionana tukiwa wadogo sana mara ya mwisho 1995 nilisikia yupo mlimani, University of Dar es salaam ila sikupata habari zake, mtoto wa baba yangu J Mwaheleja nilivyokuwa najua, kama yeyote anamjua au yeye mwenyewe naomba tuwasiliane email yangu gtolondon@yahoo.com ninaishi london kwa sasa nategemea kurudi september 2010. wadau naombeni msaada wenu tafadhali. Natanguliza shukrani
ReplyDeleteHebu tuache kujipa moyo kwanza kama kapatikana , maana hawa wazungu hawaminiki, , isije kua huyu baba kamcharanga mapanga huyu binti na kumkata vipande vidogo dogo na kumweke kwnye trash bags na ku dumped her dismembered body in the middle of nowhere , mnakumbuka storyi ya yule demuw a huko USA alikua naaitwa Mwambashi Kupaza?
ReplyDeleteKama kweli anavyosema Shemeji kama yupo buheri wa afya na akaleta namba ya simu apigiwe, mimi nahisi huyu dada ana matatizo huko aliko nahisi yuko jela ndo mana kimya kingi na pengine aliona aibu kuijulisha familia ndiyo sababu familia wamepewa namba wampigie na si kusubiri yeye apige.
ReplyDeleteVyovyote vile tunamuombea kila la kheir InshaAllah Mungu atamfungulia njia aje aonane na mama yake kwa salama na naomba waTZ wa huko muwe na umoja kujuliana na kusaidiana wakati wa shida na raha maaana inaonyesha huyu dada hakuwa na mtz aliyekuwa nae karibu angeshaeleza kama yuhai au vipi?!
Nimewahi kusikia watz huko Germany hawapendani kazi yao mtu akipata matatizo ni kusemana na kupigana vijembe hata barabarani wakikutana yaani roho mbovu wamewekeana tu!
Hongera Dr.MANYAU NYAU, bila wewe kazi iluwa imeshakuwa ngumu sana.
ReplyDeleteNdugu zangu tusifurahie saana kupatikana kwa huyu dada huenda hata baada ya haya yote akaamua kukaa kimya bila kuwasiliana na mama yake kuna wengi tupo nchi hizi za ulaya tunaona tukifika huku tumefaula na hatuwahitaji tena ndugu na jamaa tuliowaacha nyuma. Sioni sababu ya huyu dada kukaa muda wote huo bila mawasiliano kama si walio katika kundi hilo.
ReplyDeleteULAYA NA USA BINADAMU YOYOTE ANAYEISHI KIHALALI NA HANA TATIZO LOLOTE SERIKALI LAZIMA INAMJUA JINA,MWAKA WA KUZALIWA ,MTAA ANAOISHI,NYUMBA ALIYOPANGA NA KAMA ALIHAMA KUNA KUMBUKUMBU ALIHAMIA WAPI,TOFAUTI KABISA NA BONGO HAKUNA MITAA WALA ANUANI ,MUNGU AMLINDE DADA YETU NA AWE NA MAISHA MAREFU
ReplyDeletemimi nahisi huyu Sherry atakuwa kama mimi niko ughaibuni lakini sina kazi nimeolewa nina watoto lakini sina kazi na mume hana kihivyo hivyo na maisha magumu inakuwa tabu kumtumia hata mama kisenti hivyo huona taabu kupiga piga simu mara kwa mara kumsikia mzazi wako analalamika maisha yalivyokuwa magumu na mimi siwezi kumsaidia wala kumshauri kitu naamua ninyamazage tu napiga mara moja moja mmpaka nnatafutwa naogopa namimi nisije nikafikia hiyo miaka 6, nitajitahidi at least mwezi mara mbili nimulize hali mama ndugu na jamaa hivo hivo kavu kavu. najua kuna atakae jiuliza kwanini sirudi nyumbani? ndo hivo kuolewa tena na niko nasomesha watoto huku najua nikirudi itakuwa mzigo zaidi pia wao si watz.
ReplyDeleteKwa hiyo naomba tusimlaumu sana huyu dada hatujui kakumbwa na nini kwani kitanda usicho kilalia haujui kunguni wake!
Bwana Michuzi, naona watu wanshangilia ushindi kabla ya mechi kwisha. Siwalaumu, wabongo tupo hivyo, ni watu wa vuhele hele na kutopenda kufuatilia mambo ya muhimu katika maisha.
ReplyDeleteKwa nini nasema hivyo? Jibu ni kuwa huyu dada hajapatikana, huyo shemeji kaahidi kuwa yupo hai na katoa namba ya simu. Huyo binti mwenyewe hadi sasa hakuna mtanzania au mtu mwingine yeyote aliyemuona kwa macho na kuhakikisha kuwa yupo hai na salama salimini, hajafungiwa sehemu wala kufanywa mtumwa. Narudia tena, hakuna kati yetu anayeweza kutuhakikishia kuwa huyo binti yupo salama.
Mbili, hivi ndugu zangu, ukioa binti wa watu, ukamtoa nchini kwao na kuja kuishi naye nchini kwenu, unapoachana naye kwa taraka, hata ndugu zake huwajulishi kuwa jamani mimi na nduu yenu tumeachana rasmi leo na kila mtu kaenda kivyake?
Hapa tumepigwa mchanga wa macho nawaambieni. Mimi huyu bwana wala siweji kumuita shemeji, kwa kuwa mashemeji wanajua wajibu wao ni nini kwa familia. Huyu hapana, si mtu kabisa.
Tuombeni jamani, huyu binti yetu shery aende yeye binafsi kwa uongozi wa watanzania huko anakoishi akajitambulishe na watuletee picha wamepiga naye au atupatie japo anuani yake ya yahoo mesenja au skype tuongee naye live, Ujerumani mtandao wa kumwaga, hata kwa jirani atapata au hata kama hana anuani hizo anaweza fungua za muda akawasiliana nasi.
Asipofanya hivyo mjue alishakufa na kuzikwa long kitambo, anzeni tu process za kufunua kesi polisi.
Hawa jamaa zetu kwa sanaa si mchezo, anaweza mtafuta mtu anayejua kiswahili akampa information za ndani kabisa ambazo pengine yeye na shery wanazijua huyo mtu akapiga simu na kujidai ni shery. Kwa wale mliowahi kutapeliwa bongo au sehemu yeyote ile duniani mtakuwa mmenielewa ninaongea nini.
Nasisitiza tu kuwa, huyu binti bado hajapatikana, taarifa tuliyonayo ni upande wa hadithi ya ex-husband, mpaka tumuone huyo binti live na ndo tutasema tumempata.
Acheni kulaumu laumu, huyu mtu hata kwao alikuwa akienda kutembelea, iweje apotee miaka sita bila taarifa akimchunia kila mtu hata mama yake na huyo mshenzi mnayemuita shameji, hata taarifa kwao asipeleke kusema kuwa ndoa yao ilishavunjika na kila mtu ameanza na ustaarabu wake.
MIMI siamini story ya huyu shemeji yenu mpaka nimuone binti yangu.
no atafutwe na aulizwe kwa nini kala bati for 5 goodyears bila hi kwa mama nooooooooooooo som is wrong
ReplyDeleteMichuzi, this case is still open, don't close it yet.
ReplyDeleteHuyu binti hajapatikana bado, kwa maelezo ya taarifa hii ni kuwa ex-husband kaongea na familia kuwahakikishia kuwa binti yao yupo hai. Kuweni macho wandugu mpaka huyu binti aonekane kwa macho akiwa hai na mzima wa afya ndiyo tuta-close hii kesi.
Hapa tumeuziwa mbuzi kwenye gunia, subirini tulifungue kwanza gunia ndiyo tujua kama tunambuzi au paka shume.
Hii si mara ya kwanza kuona, kaeni macho watanzania, hasa mnaopenda kuolewa kwa sababu za kuolewa tu
Jamani mbona manataka kondoka wakati movie halijaisha? Yaani hapa ndo kwanza ngoma inanza. Kuna mtu kashamuona huyo binti zaidi ya huyo mnaemwita shemeji? Kama hakuna, kaeni kimya kwanza mpaka huyo binti tumuone kwa macho, vinginevyo hiyo aliyowapa ni stori kama ya simba na sungura na ndugu yao bweha.
ReplyDeleteInatisha hii, mazimwi hayo kama ya thriler ya Michael Jackson, apumzike kwa amani
Michuzi, kichwa cha habari hii kinapotosha ukweli. Please, hii ni uhai wa mtanzania mwenzetu. Unasemaje kapatikana na hakuna mtu kamuona hadi leo hii zaidi ya taarifa za kujikosha za huyo mpuuzi mnayemwita shemeji yenu?
ReplyDeleteHaya ndo mambo ya kuamua kesi kwa kusikiliza upande mmoja.
Michuzi ninakuomba sana urushe tangazo lingine la kufanya huyu dada yetu akakutane na watanzania wanaoishi huko live na wamuone na kutuletea ushahidi kuwa kweli huyo ndiye.
Yaani mpaka sasa ni tup[o palepale. Kwani kabla si ni huyo jamaa mnayemuita shemeji ndo pekee aliyekuwa akijua alipo hasa, na je sasa kimebadilika nini? Si ni bado huyo jamaa ndo pekee anayejua hasa alipo. Isije ikawa huko kwao kawaambia kuwa shery alirudi bongo, na sisi huku anatuambia shery yupo hai, kumbe kitambo alishaaga dunia, naomba isiwe hivyo.
Haiwezekani kwa binti wa kitanzania kuamua kususa mawasiliano ghafla kwa kila mtu hadi wazazi wake baada ya ndoa kuvunjika, haiwezekani, lazima kuna jambo zito hapo.
Michuzi, kumbuka mpaka tumuone huyo binti kwa macho, picha halijaisha.
Hivi inakuwaje lakini watu kuanza kumshutumu tu Da' sherry bila kujua hata kisa cha yeye kuacha kuwasiliana na mama yake?. Mbona mnaanza lawama kabla hata ya kujua sababu. Hamumjui Sherry, mama yake, wala maisha yao kisha mnaanza kulaumu....watu wengine bwana!
ReplyDeleteDon't pass judgements people!!!. I just hope and pray that whatever came between them and separate them is over, and I hope all the best comes out of this. God Bless Sherry na mama yake, God Bless Tanzania, and may God bless the USA. Ameen!
;)
Nimesoma post zote mpaka nusu naona kila mtu anamlaumu Shery lakini mimi naona kazi bado haijaisha kabisa. Oliver kama unasoma hapa usimind sana ni mambo ya ulimwengu. Lakini huku kwetu kuna three way calling kama Shery hajamuita mama yake chukua simu upige na upige Tanzania mama yake hata asikie wewe ukiongea naye tu si anajua sauti ya mwanae? Sitaki kuwa mwanga lakini bado bado hujaniambia kitu...Mpaka mama yake asikie sauti ya mwanae ndio nitaamini unayosema. Na kama vipi mama weka hiyo number uliyopewa hapa tumpigie Shery. Au Oliver toa address yake ya sasa hivi tumfuate hapo anapokaa angalau tumtie machoni. Huyu mtu anaweza kujisafisha haraka haraka ili mama akae kimya haraka harak kumbe mmhhhhh
ReplyDeleteMnakumbuka yule mtu aliyemuua binamu yake. Sembuse huyu hawana undugu. Kule Wisconsin ilitoka kabisa kwenye Cold case show. Kila siku baba ya mtoto akipiga simu anawaambia yupo busy na masomo. Mara siku hizi kabadilika sana hata kuongea na nyie hataki na huku Marekani anawaambia watu wanaomuulizia kuwa ameamua kurudi Tanzania. Baba wa mtoto akawa anamlaaani mwanae kumbe keshauliwa. Na siye hapa tusimlaani Shery mpaka tujue kweli ameongea na mwanae au kama hataki kuongea na mama yake basi mama amesikia sauti ya mwanae kupitia mtu mwingine.
Mpaka mama aseme ameongea na mwanae ndio nitasema kazi imekwisha. La sivyo bado siamini mtu mimi.
Nikishasikia kuwa ameongea na mama yake ndio huyo Shery itabidi tumkalie kikao
Wewe wa hapo @ May 23 03;04 am Why God bless the USA na sio the world if not Africa..mambo ya kukariri haya taabu sanaaa...
ReplyDeleteSherry tunakusubiri...This Case is still open..Huko ujerumani twaomba mwende kwenye hiyo club kuulizia....Mama usisikilize mzungu ukaamini. Kwanza ngozi nyeusi hii wanaona kama manyani tu kwa hiyo kuitoa sio shida kwa...Ndio maana wanaitaga exotic bride jiulize kwanini
michuzi fanya hivi, huyu mama anayo number ya bintie, tumia umaarufu wako au huruma yako upande simu ampigie na kuzungumza na mwanawe, halafu utujulishe kama kweli ameweza kuzungumza nae na ni kweli alozungumza nae ni mwanawe. hatujali wala hatutaki kujua sababu za ukimya wake, tunachotaka kujua ni jee yu mzima.
ReplyDeleteHii itasaidia shutuma za baadhi ya wadau hapa kumshutumu ex-husband kuwa huenda amemdhuru huyu binti.
Please please michuzi nawe saidia hapa!!!
mimi ni full tomaso hadi nimuone sherry blogu ya jamii au mamake aje tena blogu ya jamii kudhibitisha kuwa kaongea na mwanaye na kisa cha kukaa kimya ni nini si bure iko mambo ndani yake! hata kama ni jela shemeji mzungu eeh mpe hela apige simu kwao ebo hapa ngoma bado mbichi
ReplyDeleteHaiingii akilini kabisa mtu kukaa mwaka ..sembuse miaka 6 bila kuwasiliana na nyumbani....nashangaa sana...watu wengine huko ulaya bora tu mngerudi nyumbani...
ReplyDeleteUzoefu nilioupata hasa ninapokuwa nje na kukutana na watanzania wenzetu ..wengi wanaishi maisha ya kubahatisha sana...na imefikia wanaona hata aibu kuwasiliana na wazazi au ndugu.....kwakuwa hawana msaada wanaoweza kutuma..lakini lazima kuelewa hisia za ndugu na wapenzi wenu...msiwatese...hata kama mammbo hayaendi sawa ni bora kusema ukaeleweka...na hata kama inabidi usaidiwe nauli urudi nyumbani uanze upya usione aibu vile vile....!!!...mimi binafsi nimeshawatumia marafiki zangu kama wawili walioshindwa maisha uk na usa....na michango ya kuwarusisha wale walioshindwa...maisha south afrika ni kawaida kabisa....na wengine wanarudishwa kwa lift za bure za serikali ya tanzania au south afrika....
badilikeni wadau...kwa mlio nje ya nchi wakati ni huu ...you have no reason to be out there if your stay is not benefiting you ...or your loved one...
kwa wale mlio nje na mnauwezo nawafagilia sana hasa wale ambao haata mkisikia msiba au sherehe kubwa kupanda pipa return ticket hata mara tatu kwa mwaka kwenu si tatizo......
....nimepata kushuhudia mzazi aliyefariki akiwa na watoto ...anazikwa kama mtu ambaye hakuzaa ...kila mtu alipata uchungu san...kisa ..eti watoto wake wako ulaya na amerika wamejilipua ...[walitupa passports]...na kuwafanya washindwe kumzika baba yao...acha wale ambao matatizo yakitokea hawana hata nauli ya kurudia nyumbani......
watanzania wenzangu mlio nje bila mpango nawadharau sana nawaona wajinga na malimbukeni....you must be there with reasons....ukishindwa karibu tupige KILIMO KWANZA !!!!
KUNA WATANZANIA WENGI TU WAKIFIKA ULAYA WANASAHAU HATA WAZAZI WAO MBAYA SANA HIYO
ReplyDeleteMIMI SIAMINI HADI MAMA MZAZI AZUNGUMZE KATIKA HII BLOG KUWA DADA SHERY YUKO ALIVE
ReplyDeleteKuongea na shery haitoshi, kwa kuwa hawa wazungu bwana wanatabia za kufungia watu jela za ndani ya nyumba zao, wanaziita basement, mtakumbuka kuna mzungu mmoja alishamfungia mwanae wa kumzaa mwenyewe chini ya nyumba wanayoishi na familia yake kwa miaka kadhaa na akawa akimzalisha watoto.
ReplyDeleteKuongea naye haitoshi kwa kuwa inaweza akawa kafanywa mfungwa ndani ya nyumba ya huyo shemeji yenu na kulazimishwa aseme yale shemeji yenu anayotaka msikie, halafu ndo ikawa tiketi ya kuendelea kudhalilishwa kwa kuwa hakuna atakayemtafuta tena kwa kuamini kuwa kaamua kuchuna. Hii ya simu si plani nzuri jamani, fikirieni maisha ya mwenzenu msipende kulaumu kipumbavu na kuamini hawa wazungu kwa kuwa ni ngozi nyeupe.
Lazima tujue shery yupo wapi anafanya nini na watu waweze kumtembelea na kujua anavyoishi.
Kama watu walionitangulia walivyosema, binti wa kitanzania hawezi kuwachunia watu wote anaowafahamu hadi ndugu zake ghafla bin vuu kwa miaka sita, hawezi, tuache ujinga jamani, tuzingatie maisha ya mwenzetu.
Na ni kwa nini hadi sasa hajaweza kumtembelea hata ndugu mmoja mtanzania huko ujerumani tangu tumeanza kumtafuta?
Huyu shemeji yenu matatizo sana.
Mpaka tumuone hai na kuhakikisha yupo salama na HURU, si mfungwa ndani ya basement yao ndo tuseme kapatikana.
Bwana Michuzi, waombe watanzania wanaoishi Hamburg na vitongoji vya karibu wakupatie anuani zao, emails, namba za simu tumpatie shery kama kweli yupo hai akaonanen nao na wao waweze kumtembelea wajue anapoishi na anavyoishi ili tuthibitishe kuwa yupo hai na hajafungiwa basement na kufanywa mtumwa.
ReplyDeleteDuh mie sielwei yaani mama yako mzazi unakaa miaka 6 hamwasiliani kulikoni. It is very very sad. Tusiwadharau wazazi hata kama hawanacho ndio waliotuleta duniani. Unless bibie alikuwa jela maana "SIPATI PICHA"
ReplyDeleteYAAN MICHUZI HAPA HUJATUAMBIA KITU NA HUYO MAMA YAKE NAE PIA ANATUZUGA SIO, YEYE KUAMBIWA NA HUYO MNAOMUITA SHEMEJ YAKE ANASEMA NDIO KAPATIKANA MIMI KWA UPANDE WANGU NASEMA HAJAPATIKANA NA HUWEZ KUCHUKULIA MANENEO YA UPANDE MMOJA YAAN UPANDE WA HUYO MZUNGU SIO MICHUZI WEKA NUMBER HAPA HADHARAN TUJUE VP MTANZANIA MWENZETU YUKO WAP AU MPIGIE WEWE RECORD MAZUNGUMZO HALAF TUWEKEE HUMU,TUSILETE MAMBO YA MZAHA SIO
ReplyDeleteWatu mnaongea ongea hovyo tu bila kufikiri. Mnasemaje kuwa hana makaratasi na wakati aliolewa na huyo mnayemuita shemeji yenu kihalali kabisa? Ninyi ni watanzania wapumbavu msiojali maisha ya wenzenu, mnakalia umbeya wa kijinga usiotuletea maendeleo. Mtanzania mwenzetu hajulikani aliko mpaka leo hii, halafu ninyi mnaleta mambo yenu ya kishenzi shenzi tu, sijui mmezaliwa na nani ninyi.
ReplyDeleteKwa nini mmekuwa watu wa kufikiri kwa kutumia makalio badala ya vichwa?
Mnasemaje kuwa shery kapatikana wakati hadi leo hii, sijui siku ya ngapi tangu tangazo hili litoke hakuna mtu amemuona kwa macho?
Ninyi ni watu wa namna gani jamani? Mnaacha kuzingatia maisha ya mwenzetu mnakalia uonga msiokuwa na uhakika nao, eti mnasaidia watu nauli za kurudi bongo, shenzi sana ninyi.
Nyie wote mnaomlaumu Sheri wacheni hizo.
ReplyDeleteMnajuaje kama alijilipua na kusema ye MNYARUANDA je bado mlitaka aseme ye mtanzania akamatwe?
Nyie vipi nyie? Wenzenu huku tunaJILIPUA kisawasawa!
Michu na wadau, nimejaribu kutafuta kwa google Karamala band in German na nimeweza kupata link hii:
ReplyDeletehttp://dioplaye.oyla16.de/cgi-bin/hpm_homepage.cgi?skip=23378871|||dioplaye
Nimeandika email kwao kuulizia kama wanataarifa zozote juu ya huyu binti Sherry.
Kwa kweli mimi binafsi nashindwa hata kulala vizuri kwa kuwaza juu ya suala hili, unajua kama ni mchezo mchafu umetendeka, unaweza kumtokea yeyote yule, hivyo tumtafuteni mpaka tumpate live, si kwa simu wala kuamini maneno ya shemeji yenu. Jamani mimi huyu si shemeji yangu. Mtu hawezi oa dada yanu halafu aachane naye kienyeji miaka kumi bila kutoa taarifa kwa wazazi alikomchukua. Mshenzi sana huyu.
Jamani habari mbaya zimetufikia dada carolyn amepatikana akiwa marehemu,inasemekana huyo aliyekua anakaa nae ndio mhusika mkuu!
ReplyDelete