Pichani ni Sherry Kajembe ambaye mama yake mzazi, Bi. Fatm Saidi Kajembe, amefika leo ofisi za Globu ya Jamii akiwa na mwanae mkubwa Rashidi Kajembe kudai kwamba bintiye huyo amekata mawasiliano toka mwezi Juni mwaka 2004 na hadi sasa hajulikani aliko. Miaka yote hata kabla ya kukata mawasiliano Da'Sherry alikuwa akiishi Hamburg, Ujerumani
Mama Mzazi wa Da' Sherry Kajembe akiwa ofisi za Globu ya Jamii kuleta waraka wa kutafuta binti yake Sherry ambaye hawajawasiliana tokea Juni 2004. Mama anasema Sherry ama yeyote anayemfahamu aliko ampigie kwenye namb +255 714 757 418. anasema ana hamu amsikie japo sauti yake tu na kujua kama yu mzima. Kaomba waraka huu chini tuutoe kama ulivyo..







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 54 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2010

    Jamani mliokio huko mnaofahamu chochote kuhusiana na habari hii saidieni hii familia , chukua muda kidogo kuangalia kama unaweza ukapaparazi habarizake , maana mambo ya nchi za watu YANATISHA tujitahidi tujue what happened kwa dada sababu habari hii inaonyesha ni mtu aliekuwa na mawasiliano na nyumbani sasa kukaa kimya muda wote huu kweli INATISHA NA INASUMBUA.
    Asanteni.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2010

    sio huyo mama tu bali hata mimi nimekuwa nikimtafuta bro tangu mwaka 2005 hadi leo hii hatujawasiliana nae... yeye amekuwa akiishi australia tangu mwanzoni mwa mwaka 1980 hadi sasa na alikuwa pirot .. anitafute kwa francylumbo@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2010

    hata mimi imenigusa sana maskini mama pole sana pia jaribuni kumtafuta kwa njia ya mtandaoni imenigusa sana

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 20, 2010

    Dah.. machozi yana ni-lenga na sijui kwa nini.
    Wadau from Umoja House na German msaidieni mama yetu, Authorities always have records especially on migrants where about.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2010

    Imenigusa sana! Huyu dada kama sikosei anafanana na binti ambaye alikuwa anasoma na mdogo wangu Kilakala Secondary miaka ya tisini. Sherry alikuwa Form Six 1990 wakati mdogo wangu alikuwa form Five. Nilimfahamu kwa kuwa mabinti wengi wa Dar walisoma Kilakala walikuwa wanatembeleana sana.

    Nashauri kama kuna mtu anaweza kuwasiliana na Ubalozi wa Ujeruman hapa halafu wawape connection kule Ujeruman itaweza kusaidia. Kwa kweli ni muda mrefu tena kwa binti kukaa kimya hivyo inatisha, na kama mzazi imenigusa sana.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2010

    jamani hizi kesi ni nyingi mno,mtoa maoni wa tarehe 20 may 4:20 ,bona hujasema jina la bro wako sasa watu watamjuaje?poleni sana jamaa wa huyu dada najua inavyoumiza hata mimi nina mjomba anngu anaitwa samuel nicholas kimwaga aliondoka miaka mingi sana kama sio 92 basi 93 ni miaka takribani 17-18 sasa na toka aondoke aliwahi kuwasiliana na sisi mara mbili au tatu kama sikosei mpaka leo hii,ameondoka toka mimi niko primary school mpaka nimekuwa na mimi nimekuja nje sijawahi kumuona tena toka mika hiyo,mimi inaniuma kwa kuwa ni mjomba angu ila cousins zangu ambao ni watoto wake wanaumia sana,mara ya mwisho alituaga kama anakwenda msumbiji kibiashara then akatuandikia kwamba ameamua kukaa aangalie maisha huku ndio ikawa mwisho wa mawasiliano mpaka leo.kama kuna mtu yeyote anayejua awasiliane na mimi kwenye e-mail ssambukile@yahoo.com..asanteni

    ReplyDelete
  7. Mpalang'ombeMay 20, 2010

    Tatizo wabongo MIZINGA imezidi ukiona mtu yupo nje ya bongo na hasa Ulaya na Marekani basi haupigi simu au kumuandikia barua pasi na kutoa shida. Yeye akikupigia kukusalimia unaanza "Tena bora umepiga, na nyumba yetu hapa ukuta umedondoka kwa mvua".

    Ni kweli hali ya bongo ngumu sana, ila wakati mwingine tunaharibu kwa kuweka uwongo, kiasi kwamba mtu mambo yake yakimuendea Kombo huko nje ya nchi anaona njia pekee ni ku "MUTE" tu maana akijifanya mawasiliano mzinga, akisema hana hali ngumu yaanza majungu "FULANI KAISHIWA KWELI KWELI SIKU HIZI, UNADHANI ULAYA MCHEZO!".

    Wakati mwingine huwa tunatengeneza wenyewe mazingira ya watu kukata mawasiliano nasi. Tupunguze mizinga, mtu akikupigia leo kukujulia hali, ukampiga MZINGA akakwambia sina kitu, siyo simu ijayo akipiga tena unampiga tena mzinga, subiri hata miezi sita iishe ndiyo ukumbushie tena!.

    Ni matumaini yangu kuwa Da'Sherry atajitahidi kumtafuta mama, kwani mzazi ni mzazi tu, na kama kuna lililomkuta "say yupo jela, au hatma yake ya uhai ilifika ukingoni, god forbid" basi wenye taarifa wamjuze bimkubwa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 20, 2010

    Nimegoogle sherry hammerling, sherry kajembe haiji kitu lakini kwenye facebook kuna mtu anaitwa Oliver Hammerling ...wangeanzia na hapo

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 20, 2010

    Germans are hardcore racists. Very sorry Mama Sherry.

    Ila 2004, hadi hii leo ni muda mrefu, japo sio nia yangu kulaumu mtu, nadhani ingetakiwa muanze kumtafuta tangu hiyo hiyo 2004, ama baada ya mawasiliano kuanza kupungua. Poleni sana, ila msikate tamaa.

    Jaribuni pia kuulizia kwa marafiki zake wa huko Ujerumani, ama kwa vile mna address yake tayari, jaribuni kuulizia kwa majirani zake (kama watakuwa na muda huo), ama kwa mwenyeji wake wa huko Ujerumani, ama hata pia kwa marafiki zake wa huko huko Bongo, na leads zinginezo kadha wa kadha kama hizo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 20, 2010

    Mdau wa pili, unamaanisha alikuwa huyo brother wako alikuwa PILOT? Ama PIRATE? Lol! Maana umeandika alikuwa PIROT!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 20, 2010

    Nimegoogle tena huo ukumbi ni kweli upo kwanza bado unafanya mambo huko Germany na unaweza kuwacontact pia kiurahisi tu...kama huyo mwanadada alitumia jina lake la ukweli lazima watakua na kumbukumbu kwenye vitabu vyao vya watu walioimba hapo. Na hata kama hakutumia jina lake wakisema mtu kutoka Tanzania obvious wanaweza kumkumbuka...

    God forbidden kama hakuna baya lilikomkuta maisha ya ughaibuni tunayajua wenyewe tunaoishi huku. Ukikuta mtu anayependa fast life Utashangaa na roho yako...Unaweza kusikiliza wazazi walichoambia lakini kumbe na upande mwingine mtu kaamua kujaribu maisha ya life style nyingine kabisa na kuamua kumuacha huyo mume wake aliyekua anampa stable life. Wakianza kazi wazijuazo hawatumii majina ya kweli ha huko kuna hatari sana. Na kama alikuwa anaimba kwenye maukumbi ni rahisi sana kuvutiwa na hizo kazi zingine na kuacha kuimba na kujaribu kumake fast money lakini hizo kazi za kukupa fast money huwezi kuifanya bila kula unga. Na ukishaingia kwenye unga ndio hivyo tena unaishi day by day...

    Hope she's alright and better.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 20, 2010

    Kaka Michuzi,
    Mimi nimejaribu ku-google(google germany) jina la huyu dada sikupata chochote ila nikagoogle tena Oliver Hammerling " the x-husband" inakuja Jan-Oliver Hammerling kama ndio mwenyewe basi yuko hata Facebook. Labda umuulize mama kama anaweza kujua Oliver jina lake kamili ni Jan-Oliver; if that's the case, basi angalau anaweza kumwambikia huyu jamaa kamuuliza kama ana habari zozote za Sherry.

    Hope this will help

    Thanks

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 20, 2010

    Habari hii inatia huruma kupoteza mawasiliano na ndugu yenu mpendwa,nadhani katika hizi nchi za nje tunazoishi Watanzania mmojawapo kama mimi huwa kuna ubalozi,jumuia zetu ambazo ziko well organized na zinawatambua karibu Watanzania wote waishio katika nchi husikana huwa zinasaidia kwa mambo mengi hasa ya misiba hata inayotokea huko nyumbani na kufanya visomo kwa pamoja bila kubagua dini,ushauri wangu ni kutumia ubalozi au hizo jumuia kama zipo au Watanzania wote waishio nchi hiyo,hiyo inaweza kuwa njia nzuri ya kujua pahali alipo huyu dada yetu.Kitu kingine ni kwa sisi tuishio majuu ni vizuri kujiunga na umoja wetu ili kuweza kushirikiana na wenzetu na kusaidiana kwenye matatizo kama haya,maana kuna kuumwa,kukamatwa nk.kuna Watanzania wenye mawazo na mtazamo finyu wa mambo pia wapo huku majuu,la ajabu ni kukataa kata kata kujiunga na jumuia ihusuyo nchi yako,unapopata shida ndiyo unaaza kulaumu watu,sidhani kama kuna sababu ya msingi ya kukataa kujiunga na jumuia au chama kinachowahusu Watanzania.kwa hiyo nashauri watu wawe pamoja ili kuweza kusaidiana katika matatizo kama haya.poleni ndugu wahusika.
    mdau Tokyo Japan.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 20, 2010

    Nafikiri interpol ingesaidia au wadau mnasemaje?
    GJK

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 20, 2010

    Anzeni kutafuta na Ubalozi wa Ujerumani hapo DAR maana anaweza kua ni raia wa huko kwa sasa. Ni rahisi kwao kufahamu

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 20, 2010

    Woooow. Very sad!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 20, 2010

    wewe mdau wa Thu May 20, 04:53:00 PM mbona unaudhi sasa! huoni kama hii issue ni serious na huyu mama anatia huruma, au hujui uchungu wa mwana?

    sasa kama wewe unamtafuta huyo kaka yako anaeishi australia ni kwa nini hujamtumia michuzi huko nyuma akakuanzishia post yako mwenyewe? na hivi kama kweli nawe umepoteleana na kaka hukupata idea ya kuomba msaada hapa mpaka umeona haya ya mama huyu?

    Inaudhi jamani, kuna wakati inabidi kuwa serious na kuweka jokes upande.

    Jamani wenye kumjuwa huyu dada au waliowahi kumuona sehemu yeyote ile ni vizuri wachangie hapa. I doesn't matter ni miaka mingapi nyuma umemuona ni vyema ikajulikana mara ya mwisho alionekana wapi.

    Na labda kati ya watanzania waliopo huko ujerumani atatokea msamaria mwema mmoja wa kuweza kuweka tangazo katika magazeti na hata kuomba ubalozi wetu umsaidie huyu mama.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 20, 2010

    jamani imenigusa sana hii habari.kweli mlioko huko Germany saidieni familia hiii kumtafuta mpendwa wao.inaelekea mama inamumiza sana.yaani imenigusa mnoo,nimeona ni kaka mimi nitoweke then mama yangu anitafute.mama na familia yote poleni kwa kukosa mawasiliano naamini Mungu atawasaidia mtampata mpendwa wenu akiwa salama kabisa.hii inabidi ipelekwe kwenye sauti ya kiswahili Ujerumani itangazwe kabisa.atapatikana tu.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 20, 2010

    That is sad! Mungu atamsaidia na atampata mwanae! she gave out as much information as she could! ngoja tusaidie kusearch! penye nia pana njia!
    ashangedere

    ReplyDelete
  20. Pole sana mama!
    Nashauri nendeni ubalozi wa ujerumani,wanaweza kuwasaidia kama bado atakuwa anaishi ujerumani.Muwapatie majina yote matatu natarehe yake ya kuzaliwa.Pia kama mnakumbuka jina kamili la mumewe itakuwa vizuri pia labda anaweza kusaidia pia.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 20, 2010

    Watanzania wanaoishi Ujerumani huwa wana community yao na wana mawasiliano ya karibu sana. Nina hakika taarifa hii ikiwekwa kwenye network yao Sherry anaweza kupatikana.

    Kwa wasiomfahamu, ni kwamba amesoma Songea Girl's (1985 - 1988) na baadaye akaenda kusoma Kilakala (July 1989 - May 1991). Mwaka 1993 alikutana na Oliver hapa Dar es Salaam. Oliver alikuwa ni mwanafunzi wa Hamburg University, alikuja UD kwenye Exchange Program. Hapo ndipo walipoanza mahusiano na hatimaye mwaka huo huo 1993 Sherry aliondoka na Oliver kwenda Ujerumani na walikuwa wakiishi Humburg. Kabla Sherry hajaondoka kwenda Ujerumani nilikutana nae Goethe Institute na ndipo nilipofahamu kwamba alikuwa na mahusiano na Oliver. Oliver alikuwa hajatulia tangu zamani, kwa hiyo siwezi kushangaa nikisikia walitengana sababu ya ulevi na ukorofi.

    Baada ya kufika Hamburg, Sherry alikuwa na mawasiliano na watanzania waliokuwa wakiishi hapo. Kwa hiyo nina uhakika ni mtu ambaye anaweza kujulikana yuko wapi. Niliwahi kumuona kwenye videos tatu za matukio tofauti ya minuso ya watanzania waishio Hamburg.

    Mama Kajembe anaonekana anaongea kwa uchungu sana, watanzania mlio Ujerumani nina uhakika mnaweza kuwa mnafahamu yuko wapi, msaidieni mama japo amsikie binti yake ili aweze kujua kama mwanae ni mzima au la. Kimya cha miaka 5 ni muda mrefu sana, watu wanaweza kuhisi vibaya na kufikiria mabaya.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 20, 2010

    Jamani hata mimi imenigusa sana. Naungana na anonym. hapo juu aliyesema inaonesha wazi dada huyu alikuwa na mawasiliano ya karibu na ndugu huko nyumbani. "INATISHA SANA" Chonde chonde mlio Ujerumani na hata yeyote mwenye details za kutosha atoe taarifa kwa mama. Huu ndio umuhimu wa kablog ketu ka jamii na sio habari za vikao vya chama nanihino mji wa kusomaa.

    MPG BX UK

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 20, 2010

    Mpalang'ombe, I like your writing style, man. Ha, Ha!

    ReplyDelete
  24. Pole sana mama.sasa ndugu zangu mnae is ujerumani tafadhali tafuta siku moja ambayo hauta kua na kazi nyingi,halafu chukua hii adress mama ametupa hapa weka kwenye JPC katika gari lako JPC itakufikisha na unaweza kuonge na yeyeto ambaye utamkuta katika adress hii,na muulize habari za huyu

    dada,naimani kubwa sana kua yeyeto atakae enda hapo atapata habari yeyote ile ambaye itasaidia kujua wapi huyu dada alipo.

    Jamani tuachane mambo ya utani .Naimani kubwa sana Mtz yeyeto ambae yupo ujerumani akijitolea tutajua wapi dada yetu ameenda.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 21, 2010

    mdau wa tarehe 20.may 10;07:00 pm
    wewe ndio umetupa kijimwanga kidogo kuhusu huyu da'sherry, kwa kweli hawa wazungu wanamatatizo sana haswa wakiwa walevi na ukorofi mwingine namaanisha ugomvi, si jambo la kulipuuzia naamini mama mzazi wa sherry hakuwa kimya kwa kipindi hicho chote kwa mzazi mpaka kuja katika blog ya jamii na kuomba msaada basi atakuwa amepita sehemu nyingi kuulizia au kumtafuta bila mafanikio, basi tujitahidi kwa kila tuwezalo na haswa wale walioko ujerumani ili kumjusha mama mzazi wa sherry nini kimempata hata kama atakuwa amepata matatizo nikimaanisha yupo jela msisite kumfahamisha mama,ili ajue ukweli kuliko kuwa na majonzi au mashaka juu ya mwanae,kama tujuavyo wengi wetu tulioko huku nje hawa wazungu kuua kwao ni kitu kidogo sana lakini hilo hatuliombi litokee tushirikiane watanzania kuujua ukweli
    asanteni mdau italia

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 21, 2010

    Kaka mtu na mama mngeenda Goethe Insitute na ubalozi wa Ujerumani mkatoa taarifa hizi.Jmaa za Ujerumani nao(sijui kama wana blogu yao) pia wasaidie kumtafuta huyu dada.Ujerumani na Ulaya imeharibika, kuna mtu alikuja Ulaya toka miaka ya 60 hajarudi mpaka sasa na hana mawasiliano na dnugu zake!Alikuwa baharia huyu Mzee sasa yuko hapa Viena, hana mke wala mtoto na ni mzee kuliko !

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 21, 2010

    Kaka yangu mkubwa aliondoka nyumbani toka mwaka 1982 akazamia wazazi wakawa na huzuni kubwa mno mpaka ilipofikia mwaka 2000 ikabidi wamuelekee Mola kumuomba kwa kukesha na visomo na tunamshukuru sana Marehemu Sharif Juneid ambaye alikuwa anatupa muongozo katika maombi na kufunga mpaka jamaa yetu akaja toka huko mafichoni(Alexandria ,Misr) na ameoa na kuzaa huko.Na sasa tuna mawasiliano naye yeye na mkewe na watoto na mwaka jana walikuja kutembea na aliwahi kuonana na marehemu baba kabla hajafa
    Mustafa Badiri Musa
    Narung'ombe
    Kariakoo

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 21, 2010

    Twende taratibu wadau, maana jina la KAJEMBE lina watu wa Kenya, Malawi na Tanzania, hivyo ni jina lenye maelfu ya watu. Je jina lake SHERRY- linatokana na SHERIFA ? Labda itasaidia wadau pa kuanzia. Pia jina Hammerling ni kubwa lenye watu maelfu, hivyo waliokuwa kipindi hicho Chuo Kikuu UDSM wanafunzi /Goethe Institute wangesaidia zaidi.

    Hivyo sote tusomao hili tangazo la mama kumtafuta mwanae SHERRY SAID KAJEMBE, tusiposti comments ambazo hazikufanyiwa kazi, ila tuposti comments zilizofanyiwa kazi (mfano: nilimwona dada huyu mwaka fulani Germany, au anuani hiyo ipo na jengo halijavunjwa n.k)

    Ama sivyo tutaishia kutoa comments sympathy zaidi badala ya nini umefanya kusaidia dada yetu apate ujumbe. Ni wazi tumeguswa na hali hii iliyowatokea familia ya SHERRY SAID KAJEMBE.


    Mdau
    Ughaibuni

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 21, 2010

    I've tryed to search using Google-Deutschland and I came across one name "Shery Said Hämmerling" If You look at the first name, there is a single s instead of double s. So, I am not sure if is the same person. And, also I keep googling the name Shery by using crues "Karamali" And I found a page with a lead singer of the band goes by the name "Laye" . Diging deeper in his "Myspace pages" I found a couple pictures in which one of them, "Laye" noted "Lana and Shery". So, It is best if they can contact the lead singer I will provide the link later

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 21, 2010

    Pole sana mama kwa kukosa mawasiliano na mwanao kwa muda mrefu hivyo. Nakushauri uende Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatiafa Dar es Salaam, uwape hayo maelezo wao watajua namna ya kukusaidia kwa kupitia ubalozi wa Ujerumani hapo bongo au kuwaandikia Ubalozi wa Tanzania Ujerumani nao watalifanyia kazi. Pole sana.

    ReplyDelete
  31. Mtoa NenoMay 21, 2010

    Sina taarifa zozote juu ya SHERRY,ila nimefurahishwa na moyo wa upendo ulioonyeshwa na wengi.Nina jambo moja tu la kufanya juu ya mada hii ni kuwaombea wote weliochukua hatua kufanikisha zoezi hili.''EE MUNGU WA MBINGUNI,WABARIKI WOTE WALIOGUSWA NA KUTOA MICHANGO YAO ILI KUSAIDIA KUPATIKANA KWA NDG YETU SHERRY,NAJUA WAMETUMIA MUDA WAO NA WENGINE PESA ZAO ILI KUPIGA SIMU ,WAPE MOYO WA UPENDO NA UBARIKI KAZI ZAO,KAMA KUNA SIKU WATAPATA MATATIZO YEYOTE YALE, WAINULIE WATU WA KUWASAIDIA KAMA WAO WALIVYO SIMAMA NA MAMA SHERRY.WABARIKI HATA WALE WANAODHIHAKI ,ILI SIKU MOJA WAWE NA HEKIMA YA KUPAMBANUA MAMBO.MGUSE SHERRY POPOTE PALE ALIPO ILI AJITOKEZE AJUE KUWA UKIMYA WAKE UMEWALIZA WATANZANIA WENGI.ABARIKIWE PIA ISSA MICHUZI KWA BLOG HII YA JAMII ,MAANA IMEKUWA MSAADA KWA WATANZANIA WENGI.AAAAAAAAAAMENI".Hili ndilo Neno,Mtoa Neno nimetoa.

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 21, 2010

    jamani hii itabidi iwe police case, kwani wazungu wengi huku ughaibuni(kama mnaangalia "forencic") sio waaminifu kama wanavyooneka hasa wakiwa katika nchi zetu. God forbid, isije ikawa da sherry aliamua kumuacha, na ulevi aliokuwa nao na ukorofi akamfanyia kitu kibaya, you never know. kwa hiyo nafiriki hii ni very serious case, tujaribu kusaidia hii familia

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 21, 2010

    pole sana mama mwenyezi akusaidie mumpate mwanao

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 21, 2010

    Pole sana mama. This is sad. Sasa kama wakienda kumuulizia ubalozini then kumbe Sherry hakuwa na makaratasi si ndio wanakuwa wameshamchomea ama? anyways kwavile aliolewa, lets hope aliyapata. Na huyo husband mie hata simuamini. Waliachana coz alikuwa mlevi, I wont be suprised kama amehusika na kutoweka kwa Sherry. Tunaona hayo mambo huku all the time.Au kam-kidnap kamuweka somewhere anamfanyisha all sorts of nasty jobs. Mie nashauri wam-consult kwanza huyo mume au hata huyo mchungaji( Baba wa mume). Lazima watakuwa nahints to where Sherry is.

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 21, 2010

    KWELI KWA TAARIFA ZOTE ZILIZOTOLEWA HAPO JUU MIMI NAONA WATANZANIA WA UJERUMANI WASIJIKAUSHE WANAJUA SANA HUYU DADA TAFADHALI MSAIDIENI MAMA ACHENI MANENO KWAMBA "SIWEZI KUINGILIA MAMBO YA WATU" SAUTI YA UJERUMANI- BWANA LYONGO NA YULE MAMA BETTY MACHANGE HATA KAMA UMESTAAFU, CHARLES HILLARY HATA KAMA UPO BBC TAFADHALI TUMIENI RAFIKI ZENU MSAIDIENI HUYU MAMA.

    MICHUZI NAOMBA WEKA TRANSLATION YA ENGLISH ILI NIMTUMIE MAMA MMOJA WA KIJERUMANI ANAISHI HUMBERG ILI AMTANGAZE KWENYE LOCAL MAGAZINE NI POSSIBLE APATIKANE HATA KAMA AMEFUNGWA AU AMEKUFA LAZIMA TUJUE NDUGU YETU AMEPATWA NA NINI??
    WATANZANIA UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU... TUANZE NA HILI

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 21, 2010

    Niliwahi kuwapo Humbug hiyo sehemu sio ya kawaida kwa msichana kutoka bara la afrika mara nyingi unaingia katika mambo ya kuuza mwili au kufanya movie za ngono kutokana na hali ya maisha na wazungu wake hasa wajarumani wanapenda kuwatumia kwa kiasi wanachoweza wasichana weusi naimani huyu dada yupo mzima lakini pia nahofia kuna mambo anajaribu kuhifadhi mwenywe ili familia isiabike pole mama

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 21, 2010

    wewe mdau wa Fri May 21, 11:04:00 AM unadhani wazazi wake wanajali wakati huu kama mtoto wao ana makaratasi au la? watu wanawasi wasi tele hawajamuona wala kumsikia miaka yote hiyo na wewe unaleta kasumba zako hizi, kwa nini ni lazima watokee watu kama wewe mnaojifanya kujuwa kila kitu ilhali ni mambumbumbu?

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 21, 2010

    na wasiwasi sana na huyo husband iko namna akichunguzwa ukweli utajulikana tuu mkorofi plus mlevi lol! kichaa kilimpanda nimlete mimi majuu then animwage duuh kweli huyo mume ana majibu ya huyo bibie alipo mdau hapo juu nakubaliana na wewe kwenye forencic tunaona sana hii mijitu mkewe akisema tuu kuwa anamuacha kinachofatia ni mtu anatoweka kwenye mazingira ya kutatanisha hadi abanwee na kufatiliwa ndo siri nje kwa kweli huyo mume anajua alipo tuu vinginevyo bibie alihama mji kuogopa vitisho nk akabadili na jina ndio ukute hata anaogopa kuwasiliana na nduguze who knows tumuombee uzima popote alipo

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 21, 2010

    Wakuu nimejaribu ku-google jina la mumewe, sijui kama ni hili ila nimepata taarifa zifuatazo pamoja na picha yake ndugu zake Sherry wanaweza kutizama kama ni huyo shemeji yao. Japo nimeipata ndani ya http://www.xing.com/profile/Oliver_Haemmerling kama ni huyo basi ndugu zake wafuatilie taarifa ya huyu bwana sehemu anazofanyia kazi hasa kupitia watanzania waishio ujerumani. Naamini wana umoja wao na Shery atakuwa ameshiriki matukio na wao. Soma profile hii:

    (PIcha nimeweka hapa imekataa ila ukifungua hiyo link utaipata)

    Oliver Hämmerling Premium Member
    Personal information
    Wants
    Geschäftliche Kontakte zur persönlichen Weiterentwicklung neue und alte Kontakte
    Haves
    Finanzbuchhaltung, Lohnbuchhaltung, Personalplanung, Budgetierung, Controlling
    Interests
    Skifahren, Biken und Familie


    Professional experience
    2003 - present
    Freiberufler
    (The company name is only visible to registered members)
    Industry: Accounting, Finanzen und Controlling
    Nov 2007 - present
    (2 years, 7 months)
    Finance & Personal & Controlling
    EuroAvionics Navigationssysteme GmbH & Co. KG
    Industry: Others
    ________________________________________
    Jan 2004 - Oct 2007
    (3 years, 10 months)
    Freelancer
    Interim, http://www.haemmerling.org
    Industry: Accounting, Finanzen und Controlling
    Aug 1992 - Dec 2003
    (11 years, 5 months)
    Geschäftsführer
    Lackierung Hämmerling
    Industry: Automotive

    Educational background
    Languages
    German

    http://www.xing.com/profile/Oliver_Haemmerling

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 21, 2010

    Namwomba Mungu huyu Dada yetu apatikane salama inasikitikisha sana..Na mdau wa pili naomba awake jina la bro yake aliye Australia kwani kuna baadhi ya ma-PILOT walizama na ndege za kijeshi enzi za mwalimu na walipewa hifadhi Australia. Sijui kama kesi zao bongo zimefutwa..nilisikia walikuwa wanaishi Melbourne..

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 21, 2010

    nimemuona facebook jamani ngoja nimfuatile tatoa jibu

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 21, 2010

    Najivunia kuwa Mtanzania, nimefuatilia kwa ukaribu sana comment za watu wengi hapo juu,nimefurahishwa na moyo wa upendo na kujali matatizo ya wengine na kuyapa umuhimu kana kwamba sisi wote ni watu wa familia moja, naomba msichoke kufuatilia habari za huyu dada jamani, halafu ningependelea Bwana Michuzi azidi kutuhabarisha endapo kama huyu dada atapatikana huko aliko, thank you all

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 21, 2010

    Nimepiga simu 0714757418,akajitambulisha kuwa yeye ni mama yake na sherry,kasema jana alioongea na mume wa sherry akasema sherry yuko hai.Leo jioni ataongea na herry mwenyewe.
    Michuzi fatilia hii.Mtoa Neno

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 21, 2010

    Mama yake sherry kasema anaishi Dsm,Tandika,Kanihakikishia Sherry yuko hai maana kaongea na mume wake kwa simu.Kasema anaahadi ya kuongea na Sherry mwenyewe jioni hii,nimeongea naye kwa namba aliyoitoa kwenye barua yake inayoonekana kwenye blog 0714757418.Tuendelee kufuatilia mpaka kieleweke,Damu ya mtanzania hiyo ni ndg yetu.Jina la Bwana libarikiwe

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 21, 2010

    Sikusudii kuzidi kuwatia homa na mashaka familia ya huyu binti, ila ninashauri wanaopenda kusaidia basi hatua ya mwanzo ni kumchunguza huyo ex-husband wake. huenda anajuwa alipo au lilompata.

    Hapa uk kuna mzungu alimuua mkewe mwenye asili ya south africa na kumuweka katika freezer miaka mitatu na huku akawadangaya familia yake na marafii zake kuwa amekufa ghfla na ameshachomwa moto (cremated). kumbe ni uongo muda wote huo alikuwa yumo ndani ya freezer. Ukweli haukujulikana mpaka alipoamua kuhama nje na akauwacha mwili katika dust bin.

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 21, 2010

    Kaka Michuzi,
    Kama mdau hapo juu na mimi nilipata info za Oliver. Kama ndio yeye anafanya kazi Kwenye kampuni inaitwa Freiberufler. So far nimeona wana locations tano in Germany, ladba mama na kaka yetu wangejaribu kumtatuta huyu kijana ladba anainfo za dada sheri. Namba za kazini kwa Oliver( again; kama ndio yeye) ni
    49-71178285310

    49-924149000

    49-6105454821

    49-8936086169

    49-911587830

    Mungu atasalidia... Sheri atawasiliana na mama soon

    Thanks

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 21, 2010

    aende ubalozi wa ujerumani hapo dar na data zifuatazo tarehe ya kuzaliwa,rangi,mara ya mwisho kuondoka dar kwenda ujerumani anuani zake wakati akiishi huko kwani ulaya na usa serikali zinawafahamu watu wote wanaoishi ndani ya hizo nchi kihalali hata nyumba wanazoishi mitaa nk

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 21, 2010

    Mimi ni O Haemmerling, Shery na mimi tuliachana miaka kumi iliyopita. Jana jinoi mwanamke mzuri kutoka Tanga aliniona katika internet, alinigusa katika facebook na aliniambia kama mamake wa Shery anamtafuta mtoto wake. Nilifuraha sana kwa sababu tulitafuta anwani wake sana na miaka mingi. Usiku sawasawa nilimpigia simu Shery na mamake wa Shery na nilimwambia Shery ni sawa. Mamake alifuraha sana. Miaka sita Shery alipotea. Sijamwona muda ndefu, lakini miaka miwili iliyopita nilimkuta tena, bado sisi ni rafiki sana, kama ndugu. Kwa sababu hii nilicheka sana kusoma maneno hapa – waswahili wanapenda kupuza ;-)

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 21, 2010

    Mimi ni O Haemmerling, Shery na mimi tuliachana miaka kumi iliyopita. Jana jioni mwanamke mzuri kutoka Tanga aliniona katika internet, alinigusa katika facebook na aliniambia kama mamake wa Shery anamtafuta mtoto wake. Nilifuraha sana kwa sababu tulitafuta anwani wake sana na miaka mingi. Usiku sawasawa nilimpigia simu Shery na mamake wa Shery. Nilimwambia mamake kama Shery ni sawa. Mamake alifuraha sana. Miaka sita Shery alipotea. Sijamwona muda ndefu, lakini miaka miwili iliyopita nilimkuta tena, bado sisi ni rafiki sana, kama ndugu. Kwa sababu hii nilicheka sana kusoma maneno hapa (ulevi ...) – waswahili wanapenda kupuza ;-)

    ReplyDelete
  50. AnonymousMay 21, 2010

    i wrote a message to a few Oliver Hammerling.. will let you know if i hear anything. Poleni

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 21, 2010

    story hii inahuzunisha sana,isije kuwa aliuliwa na huyo mumewe.maana hawa wazungu kuuwa, kwao si kitu cha ajabu hasa ukitaka kumuacha wakati bado anakupenda.mangapi tushaona ktk tv.hizo story za kuuwa wake zao kisa kaachwa.tumombee!

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 22, 2010

    all in all tuongee kama binadamu huyo mwanamke kweli ana akili timamu au zimeshamfyatuka? mzazi wako hata kama atakuwa anakulilia shida kila unapoongea nae isiwe sababu ya wewe kukata line kwa mzazi wako. lakini kuna kijimsemo mkomo ukishika mavi huwezi kuukata. anatakiwa kumuomba radhi mzazi wake japo kuwa hawezi kumlipa mama yake kwa vyovyote vile.

    ReplyDelete
  53. hahah bora kapatikana na shemeji pia kazuka kwa michu mmemwita mlevi hakuna mtu anaekunywa pombe anapenda jina la ulevi kwaniaba ya watanganyika waote waliokuita mlevi tunakuomba msamaha mie pia nakunywa lakini sitopenda mtu aniite mlevi sory shemeji yetu na wewe ndio umefanikishwa dada huyu kupatikana tena powa powa mchizi weut

    ReplyDelete
  54. AnonymousMay 23, 2010

    Asalaam aleikum,
    Wa kuhimidiwa ni Allah pekee yake, kama nilivyotanguliza habari hapo juu mwanzo.Haya mambo tuwaachie familia wao ndio wanajua nini kilimsibu mtoto wao.Tumefanya msaada tuliofanya na familia inashukuru nasi turidhike na hilo na tuendeleze moyo huo ila tusiingie ndani zaidi kujua familia kwa nini imekuwa hivyo hii si kazi yetu.
    Nimeongea na mama Sherry ameishawasiliana na mwanawe na wameongea.Ni kweli Ulaya mambo si mazuri wakati mwingine lakini haya tuwaachie familia, Msaada tuliowapatia ni wa kuigwa na yeyote atakayepotea tusichoke kumtafuta.Malipo yetu tumuachie Allah ndio mlipaji mwema na tusianze kutafuta shukurani za mama huyu kwa kuingilia undani wa kupiotea binti yake
    Mola awalinde na awasimiamie mambo yao yote Inshallah.
    Natanguliza shukurani
    Khamis Hassan Batanyaga
    babuu79@hotmail.co.uk

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...