mdau Fabian Aloyce Jerome akiwa na mai waifu wake baada ya kumeremeta jioni ya leo kanisa la Mt. Joseph jijini Dar
Maharusi na wapambe wao kwenye mnuso hoteli ya Lamada
Maharusi na madada wa maua...



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2010

    Kupendeza wamependeza maharusi wote, ila mbona inaonyesha kuwa ni "Awamu ya pili pambamoto" as umri wa maharusi wote wawili unaonyesha saa tisa kasorobo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2010

    Anony wa kwanza hapo juu. Siku hizi watu wanaoa wanapokuwa tayari. Si mambo ya kuwa na miaka 20 halafu babu au baba wanasema lazima uoe ili waone wajukuu kabla hawajafa. Wadau wamejisikia kuoana muda huu, na hiyo inatosha. Wewe haikuhusu.

    Hongereni wadau kwa kumeremeta.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2010

    Hii sasa ndio HARUSI YA MWAKA si ile iliyopita. Hongereni bwana na bibi harusi. Mmependeza.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2010

    Hongereni maharusi kweli mnameremeta. Mungu awabariki katika ndoa yenu takatifu mkaishi maisha marefu na kuzaa watoto wengi na wazuri!!! Hongereni sana kwa hilo!!! Huyo anonymous wa hapo juu asiwapotoshe maana ndoa ni wakati wowote. Unaweza kuwa na miaka hata 60 bado unaweza kufunga ndoa. Kwani tatizo liko wapi? Rais mstaafu wa Africa Kusini Mzee Nelson Mandela alifunga ndoa na Grache Macheli akiwa na miaka 85 leo hawa vijana wabichi kabisa?
    Mzauuuuuuuuzzzzzzzzzz

    ReplyDelete
  5. Matari, New Albany, OHMay 23, 2010

    Huyo anony.. wa kwanza hapo juu amedata kichwani na anataka kunikatisha tamaa, mimi nina miaka 47 na mchumba wangu ana miaka 52 na tumepanga kuoana July 2011.
    Nani alimwambia kuwa kuna ukomo wa umri katika kufunga ndoa.

    ReplyDelete
  6. Mrozari, Westerville OhioMay 23, 2010

    Hallow Hallowoooooooooo!!!!!
    Maharusi mmependeza kisawasawa.
    Mwanya wa Bi harusi umeongeza ladha katika taswira hizi.
    Mola awajaalie kizazi cha kutosha na tushirikiane kuijaza Dunia.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2010

    Hii bwana ndiyo ndoa yenyewe haswa, maana inaonyesha wazi kabisaa kuwa ni ya kutimiza maandiko matakatifu ya misaafu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 23, 2010

    Hongereni sana maharusi, cha msingi ni mmeamua kuhalalisha, haijalishi kama ni awamu ya pili ama mmeamua kubariki ndoa.

    Anon wa kwanza, pilipili ya shamba yakuwashia nini? Au ndio yale mambo ya , ... Kuachwa kuachwaaa, kuachwa ni shughuli peevuuu ...?.

    Maharusi maisha mema ya ndoa, alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe.

    Hayo mambo ya sijui watoto nini hayo ni majaaliwa, na ni kama nyinyi wenyewe mnataka watoto. Watu hawaoani ili wazae watoto ati! Wanaoana kwa ajili wanapendana (ukiachilia mbali zile ndoa za makaratasi na nini).

    Kila la kheri. Mmependeza kwa kweli.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 23, 2010

    HARUSI YA MWAKA bisha usibishe.

    Huyo anayesema hawa ni saa tisa kasorobo sio kosa lake anahitaji kutoka hapo nje ya anzania akatoe matongotongo. Pole kama bado una hayo mawazo ya kizamani kuoana wakati huna hata hela ya kununua ufagio.
    Watu siku hizi wanaoa na kuolewa wakishajua wamejikimu. Na wanawake wa siku hizi wanajua kujitegemea na kuolewa sio kutafuta kitega uchumi. Wanawake wakubwa wanaolewa kwa mapenzi ya kweli tu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 23, 2010

    hii blog ina mambo katika kumi lazima mmoja aende nyuma saa tisa kasoro haya mwingine tena atafyatua lake lkn ndio tunapata hamu ya kuchungulia kila saa mithupu ubarikiwe

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 23, 2010

    hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
    hawa nao tena heheheeeee
    mmependezapo mweeeeh

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 23, 2010

    Aisee hongereni maharusi, mjue kuwa mmekuwa kitu kimoja sasa, harusi ni kitu kikubwa katika maisha yenu, Bwana awabariki sana katika maisha yenu ya ndoa, mmeamua na kufikia hatua ambayo wengi sana wanatamani kufikia, so .. big ups na kila la kheri, na mmependeza sana!! hehe, mmoja kanifurahisha, eti mwanya wa bi arusi!...

    ReplyDelete
  13. Nawatakia kila la kheri katika ndoa yenu,hii sasa ndio harusi,kwani naimani kua itadum kwa shida ama kwa raha.kikweli kweli.

    ile ya awali mzungu ata done mda wowote
    sasa huyo mdau hapo juu anae sema hawa watu ni saa tisa kasoro?

    ama kweli hajatoka anzania,oo masikini angetakiwa atoke atoe matongo tongo machoni.

    mdau
    usa

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 24, 2010

    binafsi niliolewa nikiwa 35 kwamara ya kwanza baada ya kudanganywa sana na wanaume, wengine mpaka walikuwa tayari na familia zao ila walinilaghai sana. Niko sawa nina kazi nzuri, nyumba ni yangu gari ni langu so jamaa alivyokuja kutaka kunichumbia alinikuta tayari niko sawa. mpaka sasa yeye ni "head of the household" lakini vitu vyote tunaamua wote. mishahara yetu tunachanganya na kufanya vitu pamoja... ndugu kaeni mbali.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 24, 2010

    ...Sio vibaya kuoa/kuolewa kumi na moja kasorobo!
    Jamani mtanitoa roho, ni kweli ngoma ishakuwa jioni!
    Kimtindo naona ngoma "imeswiii"...tayari!
    Uzazi upo!

    ReplyDelete
  16. Hongera maharusi mmependeza.Mdau unayesema watoto ni majaaliwa nakuelewa, ila kusema kuwa inategemea kama wenyewe mnataka na kuwa hamuoani ili mzae eti mnaowana sababu mmependana.Wewe kama upo bongo na bado hujaoa au kuolewa nakushauri uende nje ya nchi kajitafutie zungu tu utulie ndio hizo statements zao zitakuwa sawa,lasivyo UPENDE USIPENDE, bongo jamii bado kabisa na haitaacha kamwe kusisitiza kuwa baada ya ndoa ni WATOTO.Ole wako wasipokuja, mwanamke utasakamwa wewe hadi dunia utaioa chungu.Kama unaweza andika kitabu uwafunze watu kuwa watoto sio lazima muhimu mapenzi, au itisha mikutano, maseminar huo uwajuze watu,kama wasipokuona umechanganyikiwa tu.Otherwise UTAMADUNI wetu hautakufa kamwe, kila ndoa inategemea kutoa mtoto, isipotoa ni shida kubwa SANA na ndoa nyingi sana zimevunjika sababu ya hilo.Tumuombe mwenyezi mungu atujalie watoto na uelewa ikitokea tunakosa watoto.
    Maana wewe unaweza kuwa muelewa, ukavumilia kwenye ndoa yako lakini ndugu zako na jamii yote hawawezi kukubaliana NG'OOOO utaangaliwa macho ya ajabu wewe utadhania una UKOMA.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 24, 2010

    wewe anony wa kwanza umeniboa. Kivyako tu bora wanao-oana jua limekuchwa wakapendana kuliko wanao oana miaka ishirini kisha wakajuta maana hawakuwa ready. Kila mtu ana maisha yake, kama wewe umejaaliwa kuoa/kuolewa mapema kheri tuu, wengine ndo Mungu kawaandikia wafunge ndoa muda huo. Watoto ni matokeo, tena bora kuomba watoto wa kheri na wachaMungu, usije kuishia na majambazi...! Si bora ukose... Ni mtazamo tu!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 24, 2010

    Haya malizieni kusifiwa.....karibuni rasmi kwenye FRUSTRATED TEAM!.......HABARI NDIYO HIYO!!......Haijalishi MMEPENDEZA KIASI GANI.......Hiyo ni formality tuu....sasa kila BAYA na ZURI litajulikana kati yenu....

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 24, 2010

    ...Ngoma watu wazima hawa!
    Washaonja kila kitu!
    Watatulia! Hakika!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...